Hotuba ya Waziri Kabudi Umoja wa Mataifa - UN, kwa niaba ya rais Magufuli - 27 Septemba 2019

middo lulyheart

JF-Expert Member
Mar 18, 2014
260
98
Leo Mh Paramagamba Kabudi amehutubia mkutano wa 74 wa Umoja 2a Taifa jijini NewYork marekani.

Tanzania tumedhamiria kubadili maisha ya watu wetu: Kabudi​

Palamagamba Kabudi, Waziri wa Mambo ya Nje  na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania akihutubia Mjadala Mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, mkutano wa 74, mjini New York Marekani, 27 Septemba 2019

Palamagamba Kabudi, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania akihutubia Mjadala Mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, mkutano wa 74, mjini New York Marekani, 27 Septemba 2019

Malengo ya Maendeleo Endelevu
Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania Profesa Palamagamba John Kabudi amesema Tanzania imedhamiria kubadili maisha ya wananchi wake ikijitahidi kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu SDGs.

Akihutubia mjadala Mkuu wa Baraza Kuu laUmoja wa Mataifa kikao cha 74 mjini New York Marekani Ijumaa usiku Profesa Kabudi amesema Tanzania imeweka ajenda kuu za kuzitekeleza ambazo ni pamoja na “kutokomeza ufisadi, kurejesha haki na heshma katika sekta za umma, na kuimarisha ukusanyaji kodi kama mbinu ya kufikiwa kwa haraka ukuaji wa kiuchumi."

Mengine wanayoyapa kipaumbele ni “elimu bora kwa wote, huduma za afya, na uwajibikaji.”

Waziri huyo amesema hivi juhudi hizo pia zinalenga kuboresha kiwango cha elimu nchini , kutokomeza umasikini, na kukabiliana na kushughulikia tatizo la ajira, uandikishaji watoto wanaoingia shule kimepanda kwa asilimia 35.2 ikiwa imechangiwa na hatua ya serikali ya kutoa elimu bure kwa shule za msingi hadi kitato cha nne.
Hatua zinazochukuliwa

Waziri Kabudi amesema serikali imechukua hatua madhubuti kukabiliana na ufisadi ambazo ni pamoja na “kuanzisha kitengo cha kupambana na uhalifu na ufisadi katika mahakama kuu, na kuimarisha suala la uwajibikaji na uwazi katika serikali. "

Katika miaka minne iliyopita Profesa Kabudi amesema serikali imetekeleza mabadiliko kadhaa yanayojumuisha kudhibiti utajiri na mali asili ya nchi hiyo kwa kupitia mikataba mbalimbali na hatua hizo zitasaidia kuongeza pato la taifa kwa ukusanyaji mapato, pia sheria mpya za madini zimeisaidia Tanzania kukusanya mabilioni ya fedha ambayo yameisaidia serikali kuongeza kiasi cha bajeti yake hadi asilimia 40 mwaka 2019 ukilinganisha na asilia 25 mwaka 2016.

Profesa Kabudi ameongeza kuwa mapato hayo yamesaidia kuboresha miradi mbalimbali ya miundombinu na kuinua hali ya wananchi kuanzia katika afya, maji, na usafi. Hatua hizo pia zimesaida kutoa elimu bure kwa shule za umma za msingi na sekondari akitolea mfani shule za msingi uandikishaji Watoto umeongezeka kwa asilimia 35.2.

Amesema serikali pia inahakikisha uhifadhi mazingira na kujumuisha kila mwananchi katika mchakato wa SDGs ikiwemo makundi yasiyojiweza.

Na katika upande wa nishati ambayo awali ilikuwa ni bidhaa adimu sasa takriban asilimia 67 ya wananchi wa Tanzania wana nishati ya umeme kutokana na mradi maalum wa kusambaza umeme vijijini, REA .

Pia kuna ujenzi wa bwawa kubwa kabisa la kuzalisha umeme unaoendelea ambao utakuwa mkombozi sio tu kwa wananchi wa taifa hilo bali hata nchi jirani.
Pia amesema mbali ya uhifadhi wa mazingira kuna masuala mengine yanayozingatiwa ikiwemo nishati endelevu na kuhakikisha teknolojia hiyo inawasaidia mengi.

Uhuru wa vyombo vya habari​

Prosesa Kabudi amesema Tanzania imepiga hatua kubwa katika suala la uhuru wa vyombo vya habari na kuongeza kiwango cha utoaji leseni akitolea mfano kwamba taifa hilo lina jumla ya vituo vya redio 152 na ni vitatu tu ndivyo vinamilikiwa na serikali, huku vituo vya televisheni vikiwa 34 na viwili tu ndivyo vinavyomilikiwa na serikali. Kwa upande wa magazeti serikali imetoa jumla ya leseni 172.

Na mwisho ametoa wito kwa nchi zote wanachama kukumbatia ushirikiano wa kimataifa sio tu kwa ajili ya kutomoza umasikini, kuboresha kiwango cha elimu, kukabiliana na mabadiliko yatabianchi na kufikia uwajibikaji bali pia katika kudumisha amani na usalama lakini pia katika kuleta haki na kuwa na dunia bora.
 
Prof Kabudi ni mzuri sana kwa lugha na ushawishi tatizo ameongea uongo sana kwenye ishu eti Tanzania inajitahidi kutoa AJIRA hili ni uongo hakuna ajira pili amelidanganya UN kua Tanzania Democrasia na uhuru wa vyombo vya habari apa napo serikali haifanyi vizuri kwani hakuna Democrasia wala uhuru wa vyombo vya habari anaona ufahari kua Tanzania kuna vyama vya siasa 11 na ata apa UN tuko nao wapinzani lakini hajui hao wapinzani ambao anaona fahari kuwataja uko UN ni sera madhubuti za awamu ya 4
 
Shida n kuwa ameandaa hotuba ya UN kama ya bunge letu huku , sifa zinachukua dk tatu ambazo zingetumika kuitambulisha tz KWA yale ambayo hayakuhusu ujumbe wa mkutano hasa Usalama wa nchi despite matishio ya Ebola na ugaid ambayo yanaichafua nchi.

Pia mwisho anaomba juu ya majirani badala ya yeye binafsi achilia mbali suala LA biashara kwa nn asingetoa ajenda ya un kuanzisha viwanda has a vya madawa afrika au awakaribishe nchi wanachama kuja kuwekeza kupitia viwanda kama Sera ya nchi inavyosema.

Kimsingi hiyo hotuba n ya kabudi na sio ya nchi.
Hivi angeenda rais angeongea Hayo
Tazama speech ya kenyata ilikuwa inadress mafanikio ya nchi kama ya afrika na dunia hata correlation ya mafaniko yetu na dunia hakuonesha had I ikafika hatua nikawa najiuliza huo ndio mfumo wa hotuba za un na za matangulizi wake?
Naendelea kujifunza
 
Ameenda kumsifia magufuli un
badala ya kuadress matatizo tunayopitia
That's exactly what this asshole was busy doing, eti Dr Pombe personally alitaka kuhudhuria hicho kikao huko UN lakini kabanwa na udhuru blah blah blah....(I felt like vomiting). Tangu lini huyo Dr Pombe akahudhuria vikao vya nje? lol.......!
 
Hotuba ya Prof Kabudi UN ni ya hovyo kuwahi kutokea.

Nimesikiliza speech ya Kabudi ambayo 90% inamtetea Sisonje. Speech inataka kusema huko nyuma as a country hatukufanya chochote.

Ameenda kueleza vitu ambavyo vilitakiwa vielezwe kwenye Baraza la madiwani huku Missenyi na sio kwenye UN Assembly.

Mambo ya kusema serikali imejenga vyoo vya shule za msingi wakati huo ni wajibu wenu sio poa kabisa.

UN we adress global issuea.. serikali inasimama upande upi?

Nashauri next time, tujipange.

 
Naona unang'ata na kupuliza.



Unforgetable
 
Kwa vyovyote vile speech yake ni ya hovyo.
Naona unang'ata na kupuliza.



Unforgetable
 
Nimeshangaa mno kusikia, wanacho kifanya kwa Watz sio ukweli 100% na wanachokisema UN.Dunia inawaona hawa.

Itakuwaje mda wote unasoma kama unaamini unacho kisema? tuanzie haoo kwanza.

Alichoongea cha muhimu ni rasilimali za Afrika kunufaisha mataifa tajiri, Afrika ibadilike. "hii ni kutokaana na viongozi wetu wenyewe, rejea mikataba isiyo kaguliwa.

Eti, Zimbabwe iondolewe vikwazo, ni mpango wao kufanya wapendavyo harafu dhambi i siwatafune?

"Adhabu nyingine zimo ndani ya kitengoo, hazisubiri" Mwl. Nyerere 1995.
 
Back
Top Bottom