Hotuba ya Waziri Gwajima wakati wa mapokezi ya chanjo ya sinopharm Uwanja wa ndege tarehe 1 novemba, 2021

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,801
11,961
HOTUBA YA MHE. DOROTHY O. GWAJIMA, WAZIRI WA AFYA, WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO WAKATI WA MAPOKEZI YA CHANJO YA SINOPHARM UWANJA WA NDEGE TAREHE 1 NOVEMBA, 2021.
  • Mhe.Liberata Mulamula (Mb) Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
  • Mh Mwigulu Lamek Nchemba, Waziri wa Fedha
  • Mh. Chen Mingjian, Balozi wa China hapa Tanzania
  • Msemaji wa Serikali,Mr Gerson Msigwa,
  • Prof. Abel Makubi, Katibu Mkuu, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Wazee na Watoto,
  • Balozi Joseph Edward Sokoine, Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
  • Dkt. Aifello Sichalwe, Mganga Mkuu wa Serikali,
  • Mh Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam
  • Mstahiki Meya ,Jiji la Dar Es Salaam (Ilala)
  • Katibu Tawala, Mkoa wa Dar Es Salaam
  • Mkurugenzi Idara ya Kinga,
  • Wafanyakazi wa Sekta ya Afya, Mambo ya Nje na Wizara mbalimbali,
  • Wadau mbali mbali wa maendeleo,
  • Ndugu wanahabari, Mabibi na Mabwana.

Ndugu Wananchi,

Kwanza kabisa napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujaalia uzima na afya hadi kufikia siku ya leo na kuweza kujumuika tena hapa katika tukio hili muhimu la mapokezi ya Chanjo dhidi ya UVIKO-19.

Pili, shukrani za pekee ziwaendee serikali China hususani katika kujali afya za Watanzania kwa kutupatia Chanjo hizi aina ya Sinopharm Dozi 500,000 ambazo zitatusaidia kuwakinga watanzania 250,000 dhidi ya mapambano ya Ugonjwa wa Virusi vya Korona (UVIKO-19).

Vilevile nachukua fursa hii kuwashukuru uongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam, na uongozi wa airport kwa kukubali jukumu la kuandaa mapokezi ya chanjo hii.Hongereni sana kwa maandalizi mazuri mliyofanya.

Nawashukuru viongozi wote mliofika mahala hapa leo kushuhudia upokeaji wa chanjo hizi za Sinopharm na huku mkiwawakilisha wengine wengi ambao wangependa kuwepo hapa leo lakini kwa sababu ya majukumu mengi haikuwezekana.

Ndugu Watanzania,

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inathamini sana afya za Watanzania. Ndiyo maana tumeendelea kuchukua hatua mbalimbali za kuboresha huduma za kinga nchini. Kwa chanjo za UVIKO-19, Tanzania tulipata jumla ya Chanjo Dozi 1,058,400 aina ya Janssen (Johnson and Johnson) Dozi 1,065,600 aina ya Sinopharm kutoka shirika la COVAX ambazo zimeendelea kutolewa katika vituo vyote nchini na kupitia huduma ya mkoba. Ni vyema wananchi wote,wenye miaka 18 na kuendelea wakafika kupata huduma hii ya Chanjo.

Ndugu wananchi hadi sasa, takwimu zinaonyesha kuwa tumeshafikia wananchi waliochanjwa 972,476 kwa chanjo ya Janssen sawa na asilimia 91.9 ya chanjo hizo. Aidha nichukue fursa hii kusema kuwa chanjo ya Jenseni ilikwisha tangu tarehe 19.10.2021 na sasa tunaendelea kutoa chanjo ya Sinopharm. Kwa takwimu za hadi kufikia tarehe 31.10.2021 jumla ya watanzania waliopata chanjo ya Sinopham ni 88,546 sawa na asilimia 8.3 ya chanjo 1,065,600 zilizotolewa na kusambazwa kwenye vituo vya huduma kote nchini. Mwamko ni mkubwa na wananchi wanaendelea kujitokeza kwa wingi. Napenda kuwapa pongezi wananchi wote waliojitokeza kupata huduma hii kwani wamechukua uamuzi sahihi ya kulinda afya zao na wananchi wengine. Aidha naipongeza mikoa mitano ambayo inaongoza kwa kasi ya utoaji wa chanjo ya Sinophama hadi kufikia jana tarehe 31.10.2021 ambayo ni Ruvuma, Mbeya,Mtwara,Dodoma na Kagera.

Aidha, nitoe pongezi zetu za dhati kwa Mheshimiwa Rais wetu, Mama Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kujali taifa letu na kutuletea huduma hii ya chanjo dhidi ya UVIKO-19.

Ndugu Watanzania,

Leo tunapokea chanjo dozi 500,000 aina ya Sinopharm kutoka Serikali ya China kwa ajili ya kuendelea kuwapatia wananchi aina nyingine ya chanjo dhidi ya UVIKO-19, hii itawapatia wananchi fursa ya kuchagua chanjo anayotaka. Chanjo hizi zimethibitika ni bora na salama na wataalamu na vyombo vyetu. Mara baada ya kuzipokea leo, mpango wa usambazaji upo tayari na mara moja zitapelewa katika vituo vyetu kwa ajili ya kuwapatia wanachi.

Ndugu Watanzania,

Serikali itaendelea kutoa Chanjo dhidi ya UVIKO-19 katika vituo mbalimbali vya Afya hapa nchini kwa mujibu wa miongozo iliyopo hivyo, niwaombe wanaohusika na zoezi hilo kuwajibika kwa kasi kubwa ili kuwawezesha watanzania wengi kupata chanjo mapema iwezekanavyo. Aidha, Wizara ilitoa Mwongozo wa Chanjo unaofafanua vyema taratibu za utoaji wa chanjo hizi wenye lengo la kufikia uchanjaji wa asilimia 60 ya watanzania. Tunaendelea kusisitiza chanjo zinatolewa kwa watu wote wenye umri wa miaka 18 na kuendelea nchi nzima.

Ndugu Watanzania,

Chanjo zinatolewa katika vituo vya kutolea huduma za Afya nchini kwa hiari na bila malipo. Hii ni pamoja na vituo maalumu vilivyoundwa kwa ajili ya kuwezesha kusogeza huduma hii karibu zaidi na jamii (huduma mkoba). Natoa wito kwa Jamii nzima ya Watanzania kujitokeza kupata chanjo hii dhidi ya UVIKO-19 kwani jamii ikipata Chanjo itasaidia sana kupunguza milipuko ambayo inaweza kutokea mara kwa mara na ikijitanabaisha kwenye ugonjwa mkali unaohitaji matibabu ya muda mrefu ikiwemo kulazwa wodini na kufikia kufariki.

Ndugu Watanzania,

Ninachukua fursa hii kuwaagiza Viongozi na Watendaji wa ngazi zote kutoa ushirikiano wa hali ya juu ili kuhakikisha kuwa wananchi mnahimizwa kwenda kwenye vituo vya huduma za afya ili wakapate elimu kuhusu umuhimu wa chanjo. Aidha, nawahimiza wananchi kuchua hatua mbalimbali za kujikinga dhidi ya UVIKO-19 ikiwa ni pamoja na uvaaji wa barakoa, kunawa mikono kwa maji na sabuni, kutumia vitakasa mikono (sanitizer) na nyinginezo ambazo wataalamu wa afya wamekuwa wakiendelea kuzisisitiza.

Ndugu Wanahabari,

Mwisho, Nitumie fursa hii kuwaomba wadau wengine wote wenye nia ya kusaidia eneo hili kwa namna moja au nyingine kujitokeza na kufuata utaratibu wa mwongozo wa serikali kuhusu suala la kuwezesha msaada huo. Dunia ni yetu sote kila mmoja analo jukumu la kujilinda kwa ajili yake na kwa ajili ya vizazi vijavyo.

ASANTENI SANA KWA KUNISIKILIZA
 
Attachments

  • HOTUBA_YA_MHE_DOROTHY_GWAJIMA_MAPOKEZI_YA_SINOPHARM_01_11_2021.docx
    33.3 KB · Views: 8

We do not buy such craps
 
Hii ni chanjo ya mwisho kabisa kwa ubora. UAE walipiga haijafanya kazi vizuri. Ya Russia na Cuba ni bora sasa sana kuliko hii sijui kwanini Tanzania wameikubali. Vilvile Saudi Arabia hawaikubali hii kwa watu wanaotaka kwenda Hija kule Mecca kwa sababu hizo hizo
 
Back
Top Bottom