Hotuba ya Upinzani iliyozuiwa Bungeni leo Aprili 01, 2020 hii hapa (Full Text)

Hiyo hotuba ambayo spika kasema ni ya upotoshaji ana maana ukweli wote anaujua yeye tu.

Angeacha isomwe, kipindi cha mjadala na kwa kuwa wabunge wa CCM ni wengi wangeipigia kura ya kuikataa kwa huo unaoitwa upotoshaji.

Sioni hata mantiki ya hao wabunge wa upinzani kuendelea kushiriki hivyo vikao. Labda tu ni kwa kuwa kuna vipaumbele zaidi ya kimoja kuwa bungeni.

Fikiria umealikwa kikaoni halafu huruhusiwi kuongea.

Ina maana wabunge wa upinzani hawapaswi kutoa maoni yao kwa mtazamo wa kiupinzani.

Kwamba watoe maoni yao kwa mtazamo wa CCM hilo linawezekana vipi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata mie ningekuwa spika nisingeruhusu hiyo hotuba kusomwa bungeni, naona imejaa mipasho wampe Aisha mashauzi au waimba singeli na vigodoro wawasute watu huko mwananyamala.
Ndio shida makao makuu ya ofisi kuyaweka uswahilini
Unaita mipasho sababu masahibu yao hayakuhusu. Moyoni unakiri ukweli lakini mdomoni na kimaandishi unaponda.

Ungekuwa spika bila shaka ungewafukuza nje ya bunge hadi uchaguzi.

Siku zote aliyeshika mpini ndiye mjanja, aliye shika makali ajiandae kuumia tu.

Lakini jiulize pamoja na kujeruhiwa kwanini washika makali wanaendelea kuwepo?

Yahitaji kuona mbali sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dungai anaona wapinzani wanakuwa maarufu sana kuliko yeye kwa hotuba zao kwahiyo yeye anaona yeye anatamani angekua maarufu kuliko upinzani ndio maana anaubania.Dungai anafanya mambo kwa utashi wake tu na sio kwa kufwata sheria za bunge.
 
Katika hali isiyokuwa yakawaida Spika amezuia hotuba ya msemaji mkuu wa kambi ya upinzani bungeni
Spika amesema hotuba hiyo imejaa upotoshaji

Spika ndugai amesema...

Hotuba hii ya Kambi Rasmi ya Upinzani imejaa makosa karibia kila ukurasa, ina matumizi mabaya sana ya jina la Mhe. Rais na kulituhumu Bunge la 11. Nadhani wangeshirikiana kuiandika pamoja isingefika hapa, mimi siko hapa kutetea chochote.

Kulifanya Bunge kuwa mahala pa uzushi haifai, kwa hiyo kwa mamlaka niliyonayo, sitaruhusu hotuba ya Kambi ya Upinzani kusomwa Bungeni kwa sababu inavunja kanuni kadhaa na hotuba zinazokuja huko mbele zikiwa za aina hii itakuwa hivyo hivyo.

UKIMWI alionao na Kisukari +Magufulism ndo Tatizo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jana kulikuwa na member humu. Alileta hoja ya "BUNGE KUWA MTUMWA" Aliyaeleza vizuri kuhusu utumwa huu, wa bunge kuacha majukumu yake na kuanza kazi ya kujikomba kwa watawala. Bunge tena si wawakilishi wa wananchi bali iko pale kwa niaba ya serikali dhidi ya wananchi.

Odhis *
kama nitakosea kwa hiki nitakacho kiandika hapa naomba mnisahihishe,sijawahi kusikia kipindi cha JK hotuba ya kambi rasmi ya upinzani kutopokelewa Bungeni hali kadharika hata katika uongozi wa BWM.Kwanini iwe sasa na hii siyo mara ya kwanza nakumbuka katika Bunge lililopita kuna wabunge wa CCM waliichana hotuba ya KUB pale pale Bungeni na hawajachukuliwa hatua yoyote.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Duru za kimataifa zinaeleza kwamba mpaka muda huu hii hotuba imefika kila kona ya dunia
 
kama nitakosea kwa hiki nitakacho kiandika hapa naomba mnisahihishe,sijawahi kusikia kipindi cha JK hotuba ya kambi rasmi ya upinzani kutopokelewa Bungeni hali kadharika hata katika uongozi wa BWM.Kwanini iwe sasa na hii siyo mara ya kwanza nakumbuka katika Bunge lililopita kuna wabunge wa CCM waliichana hotuba ya KUB pale pale Bungeni na hawajachukuliwa hatua yoyote.

Sent using Jamii Forums mobile app
hujakosea .
 
Mkiambia kuwa Magufuli ni dictator muelewage basi, hizo ndo dalili, kamwe hatojitangaza kuwa yeye ndiye!
 
Spika Ndugai amesema...

Hotuba hii ya Kambi Rasmi ya Upinzani imejaa makosa karibia kila ukurasa, ina matumizi mabaya sana ya jina la Mhe. Rais na kulituhumu Bunge la 11. Nadhani wangeshirikiana kuiandika pamoja isingefika hapa, mimi siko hapa kutetea chochote.

Kulifanya Bunge kuwa mahala pa uzushi haifai, kwa hiyo kwa mamlaka niliyonayo, sitaruhusu hotuba ya Kambi ya Upinzani kusomwa Bungeni kwa sababu inavunja kanuni kadhaa na hotuba zinazokuja huko mbele zikiwa za aina hii itakuwa hivyo hivyo.

ISOME HOTUBA ILIYOKATALIWA HAPA

HOTUBA YA KIONGOZI WA UPINZANI BUNGENI (KUB) MHESHIMIWA FREEMAN AIKAELI MBOWE (MB), AKIWASILISHA BUNGENI MAONI YA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KATIKA OFISI YA WAZIRI MKUU KWA MWAKA WA FEDHA 2020/2021

(Inatolewa chini ya Kanuni ya 99(9) ya Kanuni za Kudumu za Bunge,

Toleo la Januari, 2016)

____________________________

A. UTANGULIZI:

Mheshimiwa Spika,
kwa niaba ya Kiongozi wa Upinzani Bungeni, naomba kuwasilisha Maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, kuhusu makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha katika Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Mwaka wa Fedha 2020/2021. Kwa kuwa huu ni Mkutano wa Mwisho katika Kalenda ya Mikutano ya Bunge ya miaka mitano (2015 – 2020); hii itakuwa ni hotuba ya mwishoya vilevile ya Kiongozi wa Upinzani Bungeni kwa Bunge hili la 11.

Mheshimiwa Spika, pamoja na heshima niliyopewa na Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Mheshimiwa Freeman Aikaeli Mbowe (Mb) kusoma hotuba hii kwa niaba yake, lakini binafsi, na kutoka sakafu ya moyo wangu, nina kila sababu ya kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunilinda kwa miaka yote mitano ya Bunge hili, na kunipa nguvu na ujasiri wa kukabiliana na dhoruba nyingi zilizonikabili mimi binafsi kama Mbunge na Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake katika Chama Kikuu cha Upinzani hapa nchini - Chadema.

Mheshimiwa Spika, dhoruba na mbinu chafu za kisiasa dhidi yangu binafsi, dhidi ya viongozi wenzangu wa chama na dhidi ya chama zilikuwa nyingi. Hata hivyo, kinachosikitisha zaidi ni pale ambapo vyombo vya sheria vyenye wajibu wa msingi wa kulinda haki za wananchi vinapotumika kuhalalisha mbinu hizo chafu. Ni katika muktadha huo ninadiriki kusema kwamba, hukumu ya tarehe 10 Machi, 2020 dhidi Kiongozi wa Upinzani Bungeni na viongozi wengine wa Chadema, mimi nikiwa mmojwapo, ni mbinu nyingine chafu iliyokuwa inatafutiwa uhalali wa kisheria. Kimsingi hukumu ile imeutia doa mfumo mzima wa utoaji haki nchini Tanzania; na imeingia katika rekodi mbaya kwa kulenga kuharamisha na kuzifanya shughuli za kisiasa ambazo ni halali kwa mujibu wa Katiba na Sheria za nchi, kuwa makosa ya jinai.

Mheshimiwa Spika, uko Mwongozo wa Maadili, ambao umeweka utaratibu wa kushughulikia uvujifu wa maadili na kanuni za uchaguzi wakati wa Kampeni. Na mwongozo huo huandaliwa na kusainiwa na vyama vyote vinavyoshiriki katika uchaguzi husika. Ikiwa mgombea mmoja atatoa maneno ambayo kwa namna moja ama nyingine yataathiri sifa, utu na heshima ya mgombea mwingine na hivyo kuathiri matokeo ya kura zake; basi mgombea aliyeathirika anaweza kulalamika katika Kamati ya Maadili ambayo huundwa na vyama vyote vinavyoshiriki uchaguzi na shauri hilo hutolewa uamuzi. Ikiwa mtu hataridhika na uamuzi uliotolewa basi ana haki ya kukata rufaa kwenye Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

Mheshimiwa Spika, kitendo kilichofanyika cha kupeleka masuala ya kiuchaguzi mahakamani (tena bila wadau wa uchaguzi kulalamika),na kuyabatiza maneno yaliyotumika kwenye kampeni kuwa ni ya kichochezi, na hivyo kuyafanya masuala ya kichaguzi kuwa jinai, ni mwendelezo wa nia ovu ya Serikali ya kudhoofisha vyama vya upinzani na viongozi wake. Mimi ninaamini kuwa kesi ile ilikuwa ni kesi ya kisiasa; na kwa sababu hiyo ilistahili kupatiwa ufumbuzi ama suluhu ya kisiasa. Kama Serikali ilikuwa na nia njema; ingekuwa imeshamkamata na kumfungulia mashtaka Askari Polisi alifyetua risasi iliyomuuwa Akwilina Akwilini.

Mheshimiwa Spika, pamoja na madhila yote hayo; nina faraja kubwa moyoni mwangukwa kuwa wananchi wa Tanzania walisimama kidete kuupinga uonevu huo kwa vitendo, na hivyo wakaamua kujinyima kula,na kuchanga fedha zao kiasi cha shilingi milioni 320 ambazo zilitumika kulipa faini iliyokuwa inatukabili, na hatimaye tumetoka. Tuko huru! Asanteni sana Watanzania kwa michango yenu, lakini asanteni zaidi kwa ujumbe mlioutuma kwa watawala kwamba Umoja wetu ndio nguvu yetu; na kwamba hakuna jambo gumu linaloweza kuishinda nguvu ya umma.

Mheshimiwa Spika, ili kuthibitisha kuwa Serikali ilikuwa na nia ovu tangu mwanzo, kitendo cha Wananchi kututoa Gerezani kiliwaudhi sana watawala; hivyo waliamua sasa kujichukulia sheria mkononi kwa lengo la kutaka kutuuwa au kutuachia vilema vya maisha. Ni Tanzania peke yake ambapo Mbunge wa Wananchi – tena Mwanamke anadhalilishwa kwa kupigwa hadharani tena na Polisi wa Kiume, hadi kufikia hatua ya kuvunjwa mkono au kutenguliwa uti wa mgongo!

Mheshimiwa Spika, kwa nguvu na kudra za Mwenyezi Mungu, sikufa! Nimebaki hai ili nitoe ushuhuda wa jinsi Serikali hii ilivyo katili, na katili zaidi kwa wanawake. Wabunge wenzangu waliojeruhiwa pamoja nami hawakufa! Wamebaki ili wawaeleze Watanzania jinsi ambavyo Serikali hii haijali haki za Binadamu na jinsi ambavyo maisha ya wananchi wake si kitu muhimu. Sina kisasi cha kulipa! Isipokuwa ninamwomba Mungu ajipatie utukufu kwa njia hii tunayopita.

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa uhai wa Bunge hili la 11 unaelekea ukingoni, na kwa kuwa huu ni mwaka wa Uchaguzi Mkuu, hotuba yangu itajikita zaidi kwenye masuala ya Uchaguzi Mkuu na haja ya kuwa na maridhiano ya kitaifa ili kuliandaa Taifa kupata uongozi mpya unaotokana na matakwa ya wananchi likiwa na umoja na mshikamano. Aidha, hotuba hii itaeleza namna ambavyo Serikali hii ya awamu ya tano ilivyoshindwa kutekeleza bajeti zake zote na hususan katika sekta zinazogusa maisha ya wananchi. Nitazungumzia kwa kifupi sana majanga yanayolikabili taifa kwa sasa, na uwezo na utayari wetu kama Taifa wa kukabiliana na majanga hayo. Mwisho, nitahitimisha hotuba yangu,kwa kutoa tathmini ya miaka mitano ya shughuli za Serikali shughuli za Serikali na ufanisi wa Bunge na kutoa wito kwa Wananchi kuiondoa Serikali hii madarakani kupitia Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, 2020 kwa kuwa imeshindwa kukidhi matarajio ya wananchi. Masuala mengine yote ya kisekta yatazungumzwa na Wasemaji Wakuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni katika Wizara wanazozisimamia.

UTEKELEZAJI DUNI WA BAJETI KATIKA SEKTA ZINAZOGUSA MAISHA YA WANANCHI

Mheshimiwa Spika,
hii ni bajeti ya tano na ya mwisho kwa Serikali hii ya awamu ya tano inayotarajiwa kuondoka madarakani mapema mwezi Oktoba mwaka 2020 baada ya kumaliza mhula wake wa miaka mitano ya uongozi.Hata hivyo, ukifanya tathmini ya Utekelezaji wa Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano 2016/17 - 2020/21 utagundua kwamba Serikali hii ya awamu ya tano iliyokuwa ikijinasibu kwa Kauli Mbiu ya Hapa Kazi na inayotetea wanyongehaijawahi kufikia asilimia 50 ya utekelezaji wa Bajeti za Maendeleo katika sekta zinazoguza maisha ya watu moja kwa moja kama vile afya, kilimo, elimu nk.

Mheshimiwa Spika, hii ni hatari kubwa sana kwa ustawi wa watu na ukuaji endelevu wa uchumi. Ili uchumi uwe endelevu ni lazima uwe shirikishi na ili uwe shirikishi ni lazima watu wawezeshwe kupitia uwekezaji katika sekta zinazogusa maisha yao moja kwa moja, ili na waweze kuchangia ukuaji huo wa uchumi.

Mheshimiwa Spika, ukichukua sekta ya Kilimo mathalani, ambayo inakadiriwa kuajiri takriban asilimia 80 ya watanzania, bajeti ya maendeleo imetekelezwa kwa wastan wa asilimia 17.55 kwa miaka yote minne ya utawala wa Serikali hii. Hii ni kwa mujibu wa Randama za Wizara ya Kilimo ambapo, mwaka 2016/17 bajeti ya maendeleo kwenye Kilimo ilitekelezwa kwa asilimia 2.22; mwaka 2017/18 asilimia 11, mwaka 2018/19 asilimia 42, na mwaka 2019/2020 asilimia 15.

Mheshimiwa Spika, ikiwa Serikali imetekeleza bajeti ya maendeleo kwenye kilimo kwa wastani wa asilimia 17.55; hii ina maana kwamba, asilimia 82.45 ya bajeti ya maendeleo kwenye Sekta ya Kilimo haikutekelezwa! Kwa maneno mengine, asilimia 82.45 ya miradi ya maendeleo ya Kilimo haikutekelezwa! Hapa utajua ni kiasi gani cha ajira kwa wananchi wanaotegemea kilimo zilipotea. Aidha, unaweza pia kufanya hesabu ni kiasi gani cha hasara kilichopatikana kutokana na kutotekeleza miradi hiyo kwa kuzingatia mnyororo wa thamani ya mazao ya Kilimo ( Value chain in Agro Economy)

Mheshimiwa Spika, ukienda kwenye Sekta ya Afya – ambayo ndiyo sekta inayoshikilia sekta nyingine kwa maana kutoa hakikisho la nguvu kazi yenye afya (healthy labourforce); hali ni mbaya zaidi. Kwa mfano, Bajeti nzima ya Afya ilipungua kutoka shiingi trilioni 1.07 mwaka 2017/18 mpaka kufikia shilingi billion 866.233 mwaka 2018/19 ikiwa ni anguko la shilingi bilioni 211.468 sawa na asilimia 19.622.

Mheshimiwa Spika, ukiachilia mbali kuporomoka kwa bajeti ya afya; bado utekelezaji wa bajeti ya maendeleo kwenye sekta ya afya umekuwa kizungumkuti! Kwa mujibu wa Taarifa ya utekelezaji wa Bajeti ya Sekta ya Afya ni kwamba kwa mwaka wa fedeha 2019/2020 fedha za miradi ya maendeleo kwenye sekta ya afya zilizowa zimetolewa hadi kufikia Machi, 2019 zilikuwa ni asilimia 16 tu! Hii ni sawa na kusema kwamba bajeti ya maendeleo katika sekta ya afya haikutekelezwa kwa asilimia 84 kwa mwaka husika.

Mheshimiwa Spika, Kwa mwaka wa fedha 2019/20 wizara ya Afya ilitengewa jumla ya shilingi 544,137,902,597. Hadi kufikia mwezi Machi, 2020 kiasi cha fedha kilichokuwa kimetolewa ni shilingi 83,066,202,217.19 tu sawa na asilimia 15.3%na kati ya fedha hizo fedha za ndani ni asilimia 9.2 na za nje ni asilimia 21.

Mheshimiwa Spika, Tumwombe Mungu apitishe Corona mbali, kwa kuwa kwa utekelezaji wa bajeti ya afya namna hiyo, ni dhahiri kuwa tutakufa wote! Kimsingi Serikali haiko makini kabisha na maisha ya watu, inahangaika na vitu bila kujali kwamba bila ustawi wa watu, vitu hivyo havina tija yoyote! Na uthibitisho kuwa Serikali hii inashughulika na vitu zaidi kuliko ustawi wa watu ni namna inavyotekeleza bajeti za miradi ya vitu kwa ukamilifu.

Mheshimiwa Spika, kwa mfanoWizara ya Ujenzi, Uchukuzi na mawasiliano kwa mwaka wa fedha 2016/17 na 2017/18 ndiyo wizara iliyokuwa na miradi ya kipaumbele katika mgawanyo wa bajeti ya maendeleo na hiyo ndiyo wizara iliyopewa sehemu kubwa ya fedha za walipa kodi. Mwaka wa fedha 2016/17, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano – sekta ya Ujenzi fungu 98 iliidhinishiwa shilingi 2,176,204,557,000.00 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo. Sekta ya uchukuzi fungu 62 ambayo iliidhinishiwa shilingi 2,495,814,130,000.00, na sekta ya Mawasiliano fungu 68 zilitengwa jumla ya Shilingi 92,730,110,000.00 na hivyo kuifanya sekta nzima ya miundombinu kutengewa fedha za maendeleo jumla ya shilingi 4,764,748,797,000.00 kiasi hiki kilikuwa ni sawa na asilimia 40.3 ya bajeti nzima ya miradi ya maendeleo kwa mwaka huo ya shilingi bilioni 11,820.5

Aidha, Mheshimiwa Spika, kwa mwaka 2017/18 Sekta ya Ujenzi fungu 98 imetengewa jumla ya shilingi 2,411,026,062,496.00 kwa ajili ya miradi ya maendeleo ambayo ni ya kimkakati na isiyo ya kimkakati. Uchukuzi fungu 62, fedha za miradi ya maendeleo zilitengwa Shilingi 2,477,931,183,000.00 na fungu 68, mawasiliano zilitengwa jumla yaShilingi 14,000,000,000 na hivyo kufanya bajeti nzima ya maendeleo kwa wizara hii kuwa shilingi 4,902,957,245,496.00. Kiasi hicho kilikuwa ni sawa na asilimia 40.85 ya fedha zote za maendeleo kwenye bajeti ya Serikali ya shilingi bilioni 11,999.6

Mheshimiwa Spika,
kwa mwaka huo wa fedha 2018/19 Sekta ya Ujenzi fungu 98 kwa miradi ya maendeleo ilitengewa jumla ya shilingi 1,822,093,269,360.00, Sekta ya uchukuzi fungu 62 kwa mwaka huo wa fedha zilitengwa jumla ya shilingi 2,300,739,000,000.00 kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo, aidha kwa sekta ya Mawasiliano fungu 68 ilitengewa jumla ya shilingi 15,000,000,000.00 kwa ajili ya miradi ya maendeleo. Hivyo kufanya kuwa wizara kwa mwaka huo kutengewa fedha za miradi ya maendeleo yenye jumla ya shilingi 4,137,832,269,360.00 sawa na asilimia 34.46 ya bajeti nzima ya shilingi bilioni 12,007.3 matumizi kwa miradi ya Maendeleo kwa mwaka huo wa fedha.

Mheshimiwa Spika, kutokana na takwimu hizo ni rahisi sana kuona kuwa kwa kipindi cha miaka mitatu yaani 2016/17, 2017/18 na 2018/19 wizara hii imetengewa jumla ya shilingi 13,805,538,311,856.00 au (trilioni 13.806). Vyanzo vikuu vya fedha hizo vilikuwa ni mikopo ya masharti ya kibiashara na misaada ya kibajeti.

Mheshimiwa Spika, Sekta ya ujenzi fungu 98 iliidhinishiwa shilingi 1,385,270,955,497.52 za miradi ya maendeleo, hadi mwezi Februari 2020 zilikuwa zimetolewa jumla ya shilingi 862,410,826,456.20 sawa na 54% ya fedha zote za maendeleo zilizoidhinishwa na Bunge. Fungu 62 sekta ya Uchukuzi iliidhinishiwa jumla ya shilingi 2,543,722,242,895 kwa ajili ya miradi ya maendeleo. Hadi februari 2020, zilikuwa zimetolewa jumla ya 1,009,049,881,683. Aidha, kulikuwa na fedha zilizokuwa zimebakia katika bajeti ya 2018/19 ya shilingi 455,623,760,000. Na hivyo kufanya jumla ya fedha zilizotolewa kuwa shilingi 1,464,673,641,683.00 sawa na asilimia 41.3.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani inapenda kupatiwa takwimu za ajira za kudumu au za muda zilizotokana na uwekezaji huo kwa kipindi tajwa hapo juu, ili watanzania waweze kupima kama fedha za walipa kodi zinaenda kwenye miradi ambayo inaleta matokeo chanya kwa watanzania wote au ni matokeo chanya kwa kundi fulani katika jamii ya watanzania.

Mheshimiwa Spika,mbali ya kupatiwa takwimu za ajira iliyotokana na uwekezaji huo, ni vyema tukafanya ulinganisho wa jinsi fedha za vipaumbele zinavyotolewa. Afya na kilimo fedha zilivyotolewa kwa kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Tano kulinganisha na fedha za zilivyotolewa kwenye sekta ya Ujenzi na Uchukuzi. Watanzania ni muda wao mwafaka wa kufanya maamuzi kulingana na jinsi kodi zao zinavyotumika. Sambamba na hilo itakuwa ni vyema tukapewa hali halisi ya ujenzi wa mitambo ya kuzalisha umeme huko Stiegler katika kipindi hiki cha masika ambapo takriban 80% ya wilaya wilaya ya Rufiji imeathirika na mafuriko.

MAPENDEKEZO YA MABADILIKO YA KATIBA NA SHERIA MBALIMBALI ZIHUSIANAZO NA UCHAGUZI KUWEZESHA UPATIKANAJI WA TUME HURU YA UCHAGUZI

Mheshimiwa Spika,
huu ni mwaka wa Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani. Ikumbukwe kwamba, chaguzi zimekuwa zikiacha madonda na mpasuko katika Taifa kutokana na mifumo mibovu ya usimamizi wa chaguzi jambo linalofanya chaguzi hizo kukosa uhalali kutokana na kutokuwa huru na za haki. Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni imekuwa ikitoa angalizo kwa Serikali mara kadhaa la hatari ya nchi kuingia kwenye machafuko ya kisiasa kutokana na kukosekana chombo huru (kwa maana ya Tume Huru ya Uchaguzi) ambayo itafanya kazi bila mashinikizo kutoka upande wowote ili iweze kutenda haki kwa wadau wote wa uchaguzi na hivyo kuondoa malalamiko au manung’uniko yasiyo ya lazima baina ya vyama vya siasa vinavyoshiriki uchaguzi.

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa muda uliobaki kuanza kwa mchakato wa Uchaguzi Mkuu (kwa maana ya utoaji wa fomu za kugombea na uteuzi wa wagombea) ni mfupi - takriban miezi minne kutoka saa; na kwa kuwa hakuna Mkutano wowote wa Bunge zaidi ya Mkutano huu wa Bunge la Bajeti utakaokaa kujadili muswada wa Sheria ya Tume Huru ya Uchaguzi; Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, imeona ni busara kutumia fursa hii ya Bunge la Bajeti kutoa mapendekezo ya marekebisho madogo (minimum reforms) ya Katiba na Sheria mbalimbali zinazohusu uchaguzi ili mosi, kuipa Tume iliyopo uhuru wa kuendesha na kusimamia Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, 2020 kwa haki; lakini pili, kuliepusha Taifa kuingia kwenye machafuko ya kisiasa kutokana michakato mibovu ya kiuchaguzi isiyofuata sheria. Maeneo yanayopendekezwa kufanyiwa marekebisho ni kama ifuatavyo:-

Tume ya Taifa ya Uchaguzi

Mheshimiwa Spika,
Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeundwa kwa mujibu wa ibara ya 74 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977. Aidha, kwa mujibu wa Sheria ya Uchaguzi; Wakati wa Uchaguzi, mamlaka ya Tume hutekelezwa na Wakurugenzi wa Majiji, Manispaa, Miji na Halmashauri za Wilaya na watendaji mbali mbali walio chini yao.
Mheshimiwa Spika,kwa kuwa vipo vifungu vya Katiba na Sheria ya Uchaguzi vinavyoifanya Tume ya Uchaguzi ikose uhuru wa kuendesha chaguzi huru, za haki na halali; Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, inapendekeza maeneo yafuatayo ya Katiba na Sheria ya Uchaguzi, yafanyiwe marekebisho ili kuipa Tume ya Uchaguzi uhuru wa kiutendaji.

Ibara ya 74(1) ya Katiba inayompa Rais wa Jamhuri ya Muungano mamlaka ya kuteua Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Wajumbe wa Tume.

Ibara ya 74(5) inayompa Rais mamlaka ya kumwondoa madarakani mjumbe yeyote wa Tume kwa sababu ya kushindwa kutekeleza kazi zake, ama kutokana na ugonjwa au kwa sababu yoyote au kwa tabia mbaya au kwa kupoteza sifa za kuwa mjumbe.

Ibara ya 74(12) inayonyang'anya Mahakama mamlaka ya kuchunguza jambo lolote lililofanywa na Tume katika kutekeleza madaraka yake.

Ibara ya 75 (1) na (2) inayoizuia Tume kugawa majimbo ya uchaguzi na kuweka mipaka yake bila kupata kibali cha Rais.
Ibara ya 75 (6) inayokataza Mahakama kuchunguza jambo lolote lililofanywa na Tume katika kutekeleza madaraka yake ya kugawa majimbo ya uchaguzi na kuweka mipaka yake.

Ibara ya 74(7) ikisomwa pamoja na kifungu cha 6 (1) cha Sheria ya Uchaguzi inayompa Rais mamlaka ya kuteua Mkurugenzi wa Uchaguzi, ambaye ni Mtendaji Mkuu wa Tume, kutoka miongoni mwa watumishi waandamizi wa Serikali watakaopendekezwa na Tume.

Kifungu cha 7(1) cha Sheria ya Uchaguzi kinachowapa Wakurugenzi wa Majiji, Manispaa, Miji na Halmashauri za Wilaya mamlaka ya kuwa wasimamizi wa uchaguzi unaofanyika katika majimbo ya uchaguzi.

Kifungu cha 7 (2) na (3) cha Sheria ya Uchaguzi kinachoilazimisha Tume kuteua mtumishi mwingine yeyote wa serikali kuwa msimamizi wa uchaguzi.

Mheshimiwa Spika, Kwa kuzingatia vifungu vya Katiba na Sheria ya Uchaguzi nilivyovitaja hapo juu utagundua kwamba, Mfumo wetu wa Uchaguzi sio huru; na kwa maana hiyo,hauwezi kuendesha uchaguzi huru, wa haki na wa halali. Hii ni kwasababu:-

Mosi, Kwa mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma, Wakurugenzi wa Halmashauri za Serikali za Mitaa ( kwa maana ya Wakurugenzi wa Wilaya, Miji, Manispaa na Majiji) ni wateule wa Rais. Aidha, Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Wajumbe wa Tume ya Utumishi wa Umma, kama ilivyo kwa Tume nyingine zote, ni wateule wa Rais kwa mujibu wa ibara ya 36 (3) ya Katiba.

Pili,Wakurugenzi wote wa Halmashauri za Serikali za Mitaa waliopo madarakani kwa sasa wameteuliwa na Rais.

Tatu, Mkurugenzi wa Uchaguzi na wasimamizi wa uchaguzi wote wanaweza kuondolewa madarakani wakati wowote na Rais mwenyewe chini ya ibara ya 36 (4) ya Katiba; au na Tume ya Utumishi wa Umma ambayo imeteuliwa na Rais.

Nne, Wasimamizi wa uchaguzi wa ngazi zote sio watumishi wa Tume kwa maana ya uteuzi na uwajibikaji wao kiutendaji na kinidhamu. Ni 'watumishi wa Tume' kwa matakwa ya Sheria ya Uchaguzi na kwa wakati wa uchaguzi
tu.

Tano, Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Wajumbe wa Tume hawana ulinzi wowote wa kikatiba wa ajira zao. Hii ni tofauti kabisa na ulinzi wa kikatiba wa ajira walionao Majaji wote wa Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufaa ya Tanzania; Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Wajumbe wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.

Mheshimiwa Spika, maeneo mengine ya Katiba na Sheria ya Uchaguzi ambayo Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inapendekeza yafanywe marekebisho ni pamoja na :-

Ibara ya 41 (7) ya Katiba;ili kuruhusu Matokeo ya Rais yapingwe Mahakamani na Rais asiapishwe mpaka shauri lililofunguliwa kwa hati ya dharura liamuliwe.

Ibara ya 74 (1) ya Katiba irekebishwe ili kuviwezesha vyama vya siasa na asasi na taasisi za kiraia, ambao ni wadau wakuu wa uchaguzi, kupendekeza majina ya Wajumbe wa Tume ya Uchaguzi kwa ajili ya uteuzi wa Rais, baada ya kukidhi masharti ya kitaaluma na kiutendaji yaliyowekwa na Katiba.

Ibara ya 74 (5) ifanyiwe marekebisho ili kuwapatia Wajumbe wa Tume ulinzi wa kikatiba wa ajira zao, sawa na Majaji, Wajumbe wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.

Ibara ya 74 (7) na kifungu cha 6(1) cha Sheria ya Uchaguzi virekebishwe ili kuwezesha Mkurugenzi wa Uchaguzi kuteuliwa na Tume, bila kujali ni mtumishi mwandamizi wa serikali au la, ili mradi ametimiza masharti ya kitaaluma na kiutendaji yaliyowekwa na Katiba au Sheria ya Uchaguzi.

Ibara za 74 (12) na 75 (6) zirekebishwe ili kuondoa kinga dhidi ya mashtaka kwa Tume kutokana na utekelezaji wa madaraka yake na ugawaji wa majimbo ya uchaguzi kwa mujibu wa Katiba na Sheria ya Uchaguzi.

Kifungu cha 7 cha Sheria ya Uchaguzi kirekebishwe ili kuipa Tume mamlaka ya kuteua wasimamizi wote wa uchaguzi wenye sifa za kitaaluma na kiutendaji bila kujali ni watumishi wa serikali au la. Tume iwe na mamlaka pekee ya uteuzi wa watumishi wake wote.

Mheshimiwa Spika, kuhusu Mchakato wa Kutoa na Kurudisha Fomu za Uteuzi wa Wagombea; Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni imebaini mapungufu yafuatayo:-

Kifungu cha 38 (6) cha Sheria ya Uchaguzi kinawaelekeza wasimamizi wa uchaguzi kutoa na kumpatia mgombea au mpiga kura yeyote idadi ya fomu za uteuzi wa wagombea atakazohitaji.

Kifungu cha 38 (7) kinamtaka kila mgombea au mdhamini wa mgombea kuwasilisha fomu za uteuzi kwenye ofisi ya msimamizi wa uchaguzi kabla ya saa 10 jioni ya siku ya uteuzi wa wagombea.

Hakuna masharti yoyote ya kisheria yanayomlazimu msimamizi wa uchaguzi kuwepo ofisini kwake wakati wote wa kutoa na kurudisha fomu za uteuzi. Aidha, hakuna masharti yoyote ya kisheria ya kumlazimisha msimamizi wa uchaguzi kutoa au kupokea fomu za uteuzi za wagombea wa vyama vyote vya siasa vinavyoshiriki kwenye uchaguzi.

Kumekuwa na matukio mengi ya wasimamizi wa uchaguzi kutoa au kupokea fomu za uteuzi kwa wagombea wa CCM na kisha kukimbia ofisi zao ili wasitoe au kupokea fomu za uteuzi kwa wagombea wa vyama vya upinzani.

Kumekuwa na matukio mengi yaliyoshuhudiwa wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa, 2019 ya wasimamizi wa uchaguzi kuongeza herufi au namba kwenye fomu za wagombea wa upinzani kwa lengo la kuziharibu na hivyo kuwafanya wakose sifa za kugombea.

Mheshimiwa Spika, kutokana na mapungufu hayo, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, inapendekeza vifungu kadhaa vya Sheria ya Uchaguzi vifanyiwe marekebisho ili Mchakato wa Kutoa na Kupokea Fomu za Uteuzi wa Wagombea uweze kuendeshwa kwa namna bora zaidi ili vyama vyote vinavyoshiriki uchaguzi viweze kuridhika na mchakato huo.

Kifungu cha 38 (6) cha Sheria ya Uchaguzi kirekebishwe ili kumlazimisha Msimamizi wa uchaguzi kutoa fomu kwa wagombea wote wanaoshiriki uchaguzi husika. Aidha, Sheria iweke adhabu kwa Msimamzi wa Uchaguzi atakayetoa fomu kwa ubaguzi (kwa maana ya kuwapa fomu baadhi ya wagombea na kuwanyima wengine kwa sababu zozote zile iwe ni kwa kufunga na kukimbia ofisi au kukataa kutoa au kupokea fomu kwa sababu zozote zile. Sheria pia iweke sharti la kutoendelea namchakato wa uchaguzi ikiwa msimamizi wa uchaguzi atakakuwa hajatoa fomu kwa wagombea wote wanaoshiriki uchaguzi husika.

Hii itaondoa tabia mbaya ya wasimamizi wa uchaguzi kukimbia ofisi zao ili kukwepa kutoa fomu za uteuzi kwa wagombea wa vyama vya upinzani.

Kifungu cha 38 (7) kirekebishwe ili pale ambapo msimamizi wa uchaguzi hayupo ofisini kwake wakati wote wa zoezi la kurudisha fomu za uteuzi kwa sababu yoyote ile; au anapoondoka ofisini baada ya kupokea fomu za uteuzi za mgombea mmoja au baadhi tu ya wagombea, basi zoezi zima la kurudisha fomu za uteuzi na hatua nyingine zinazofuata zisimame hadi hapo msimamizi wa uchaguzi atakapopokea fomu za uteuzi za wagombea wote waliochukua fomu hizo. Hii itaondoa tabia ya wasimamizi wa uchaguzi kukimbia ofisi zao ili kukwepa kupokea fomu za uteuzi za wagombea wa vyama vya upinzani.

Kifungu cha 38 kirekebishwe kwa kuongeza kifungu kidogo kitakachowalazimisha wasimamizi wa uchaguzi kutoa au kupokea fomu za uteuzi za wagombea wa vyama vyote vya siasa vinavyoshiriki kwenye uchaguzi kwa pamoja au kwa wakati mmoja. Hii pia itaondoa tabia ya wasimamizi wa uchaguzi kutoa au kupokea fomu za uteuzi kwa wagombea wa CCM tu na kisha kukimbia ofisi zao ili kukwepa kutoa au kupokea fomu za uteuzi za wagombea wa vyama vya upinzani.
Kifungu cha 38 kirekebishwe kwa kuongeza kifungu kidogo ili kuwezesha wagombea waliopoteza au kunyang'anywa fomu za uteuzi kupatiwa fomu nyingine za uteuzi ili waweze kushiriki kwenye zoezi la uchaguzi.

Hii itaondoa tabia inayojitokeza kwa kasi ya wagombea wa vyama vya upinzani kutekwa nyara na kisha kunyang'anywa fomu zao za uteuzi na hivyo kushindwa kuzirudisha kabisa, au kuzirudisha nje ya muda uliopangwa kwa ajili hiyo na hivyo kukosa sifa ya kugombea.

Tunapendekeza kuwepo kwa marekebisho ya sheria ili kuiwezesha Tume kuweka kwenye mtandao fomu zote za uteuzi wa wagombea na hivyo kila mgombea kuwa na fursa ya kupakua fomu hizo kuzijaza na kuzirejesha. Fomu irejeshwe kwa msimamizi wa uchaguzi ikiwa na uthibitisho wa Chama cha Siasa kilichomteua na nakala ya fomu hiyo itumwe Tume Makao makuu kwa njia ya mtandao kama uthibitisho wa fomu kurejeshwa na Mgombea. Hatua hii itaondoa tabia ya wasimamizi wa uchaguzi kukimbia ofisi zao siku ya kutoa na kurejesha fomu za uteuzi.

Mheshimiwa Spika, Sifa na masharti ya Kugombea ni eneo jingine linalohitaji kufanyiwa marekebisho. Kwa namna ilivyo sasa; Kifungu cha 36 cha Sheria ya Uchaguzi kinakataza mtu yeyote kuteuliwa kuwa mgombea wa uchaguzi wa Ubunge mpaka awe na sifa za kuchaguliwa hivyo kwa mujibu wa ibara ya 67 ya Katiba. Sifa zilizowekwa na ibara ya 67 (1) na (2) ya Katiba ni uraia wa Tanzania; umri wa miaka 21 au zaidi; kujua kusoma na kuandika Kiswahili au Kiingereza; kuwa mwanachama na kupendekezwa na chama cha siasa; kutokuwa na hatia ya kosa la kukwepa kodi; kutokuhukumiwa adhabu ya kifo, au kufungwa kwa zaidi ya miezi 6 kwa kukutwa na hatia ya kosa lolote la utovu wa uaminifu; kutokuhukumiwa na Mahakama kwa kukutwa na hatia ya kosa la utovu wa uaminifu au kwa kuvunja Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma; kutokuwa na maslahi na mkataba wa aina yoyote uliowekewa miiko na kukiuka miiko hiyo; kutokuwa afisa mwandamizi wa serikali; na kutokuzuiliwa kujiandikisha kama mpiga kura katika uchaguzi wa Wabunge.

Mheshimiwa Spika, nje ya masharti haya ya Katiba, kifungu cha 38 cha Sheria ya Uchaguzi kimeweka masharti mengine ya ziada yafuatayo:

Kupata udhamini wa wapiga kura 25 waliojiandikisha kupiga kura kwenye jimbo husika. (Kifungu cha 38(1).
Kutokukatazwa na Tume ya Uchaguzi kuwa mgombea kwa mujibu wa Sheria ya Gharama za Uchaguzi. (Kifungu cha 38(2).

Jina, anwani na kazi ya mgombea; majina, anwani za wadhamini na namba za kadi zao za wapiga kura, na hati ya kiapo ya mgombea kuwa yuko tayari na ana sifa za kugombea uchaguzi. (Kifungu cha 38(3).

Hati ya kiapo iliyosainiwa na mgombea mbele ya hakimu kwamba ana sifa na kwamba hajazuiliwa kugombea uchaguzi; picha za mgombea zilizopigwa ndani ya miezi mitatu kabla ya uteuzi, na maelezo binafsi ya mgombea. (Kifungu cha 38(4).

Kifungu cha 38 (5) kinatamka wazi kwamba pale ambapo fomu za uteuzi hazijaambatanishwa na nyaraka zilizotajwa na kifungu cha 38 (4), basi uteuzi wa mgombea husika utakuwa batili. Hata hivyo, Tume inaweza, endapo itaona inafaa, kuelekeza kwamba fomu za uteuzi za mgombea huyo zikubaliwe kuwa ni halali endapo nyaraka zikizokosekana zitawasilishwa kwa msimamizi wa uchaguzi ndani ya muda wa nyongeza uliowekwa na Tume. (Proviso ya kifungu cha 38 (5).

Mheshimiwa Spika, masharti yote hayo kuhusu sifa za mgombea yamekuwa kikwazo kikubwa kwa wagombea kuyatimiza kwa ukamilifu jambo ambalo hupelekea wagombea wengi kuonekana hawana sifa na hivyo kuenguliwa na kutoshiriki uchaguzi. Ili kuondoa sintofahamu hiyo; Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inapendekeza kwamba; Kifungu cha 38 (5) cha Sheria ya Uchaguzi kirekebishwe ili fomu za uteuzi zenye mapungufu ya nyaraka zilizotajwa na kifungu cha 38 (4) zisiwe batili. Badala yake, kifungu kipya kielekeze kwamba mgombea husika atapatiwa muda wa kurekebisha mapungufu ya nyaraka yaliyoonekana. Faida ya pendekezo hili ni kwamba, sababu pekee ya kubatilisha fomu za uteuzi wa wagombea itakuwa ni kukosa sifa za kugombea au kuchaguliwa zilizotajwa na ibara ya 67 ya Katiba. Mapungufu mengine yote yasiyohusu kukosa sifa za kikatiba yataweza kurekebishwa na hivyo kuwezesha wagombea wote wenye sifa za kikatiba kushiriki kwenye uchaguzi.

Mheshimiwa Spika, eneo jingine lenye changamoto katika uchaguzi, ni mchakato wa kuweka mapingamizi dhidi ya uteuzi wa wagombea na kuyatolea uamuzi. Kifungu cha 40 cha Sheria ya Uchaguzi kimeweka sababu za fomu za uteuzi wa wagombea kuwekewa mapingamizi, na utaratibu wa kusikiliza na kuamua mapingamizi hayo. Aidha, Kifungu cha 50A kimeweka utaratibu wa ziada kuweka mapingamizi wakati wa kampeni za uchaguzi. Katika muktadha huohuo wa kuweka na kuamua mapingamizi; Kifungu cha 40 (3) kinawataja watu wenye haki ya kuweka mapingamizi dhidi ya uteuzi wa wagombea kuwa ni wagombea, msimamizi wa uchaguzi, Mkurugenzi wa Uchaguzi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Msajili wa Vyama vya Siasa.

Mheshimiwa Spika, Mapingamizi yote katika hatua hii yanapaswa kuwasilishwa kwa msimamizi wa uchaguzi sio zaidi ya saa 10 ya siku inayofuatia uteuzi wa wagombea. (Kifungu cha 40(2). Baada ya uteuzi wa wagombea kufanyika na mapingamizi yoyote kuamuliwa, kifungu cha 50A (1) kinamruhusu Msajili wa Vyama vya Siasa kumwekea pingamizi kwenye Tume mgombea yeyote anayekiuka masharti ya Sheria ya Gharama za Uchaguzi, wakati kampeni za uchaguzi zikiwa zinaendelea. Baada ya kusikiliza pingamizi hilo, Tume inaweza kumfuta mgombea husika kwenye orodha ya wagombea na kumzuia kuendelea na mchakato wa uchaguzi. (Kifungu cha 50A (2).

Tofauti na utaratibu wa mapingamizi ya awali chini ya kifungu cha 40, hakuna utaratibu wowote wa rufaa kwa mapingamizi yanayowekwa au kuamuliwa chini ya kifungu cha 50A. Tofauti na utaratibu wa mapingamizi ya awali chini ya kifungu cha 40, utaratibu wa mapingamizi chini ya kifungu cha 50A umeondolewa kwenye mikono ya wasimamizi wa uchaguzi na kupelekwa kwenye mikono ya Tume moja kwa moja. Kwa maneno mengine, mapingamizi chini ya utaratibu huu yatawasilishwa, kusikilizwa na kuamuliwa kwenye ofisi za Tume; badala ya kuwasilishwa, kusikilizwa na kuamuliwa kwenye ofisi za wasimamizi wa uchaguzi walioko majimboni.

Mheshimiwa Spika, kwa sababu ya mkanganyiko huo wa mchakato wa kuweka, kusikiliza na kuamua mapingamizi; Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inapendekeza kuwa,Kifungu cha 40 (3) kinachohusu watu wenye haki ya kuweka mapingamizi kirekebishwe, ili pale ambapo mweka pingamizi ni msimamizi wa uchaguzi, au Mkurugenzi wa Uchaguzi au Msajili wa Vyama vya Siasa au Mwanasheria Mkuu wa Serikali, basi pingamizi hilo lisikilizwe na kuamuliwa na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya au Mahakama ya Hakimu Mkazi ya eneo ambalo Jimbo la Uchaguzi husika lipo. Hii itaondoa hatari ya watu wanaohusika na uchaguzi kuwa waweka mapingamizi na waamuzi wa mapingamizi hayo. Itaondoa pia uwezekano wa Mkurugenzi wa Uchaguzi anayeweka pingamizi kumshinikiza msimamizi wa uchaguzi ambaye yuko chini yake kimamlaka kuamua pingamizi hilo kwa upendeleo. Aidha, pendekezo hili litaondoa uwezekano wa wateule hawa kula njama za kuwaengua wagombea wa vyama vya upinzani.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inapendekeza pia marekebisho ya kifungu cha 40kwa kuongeza kifungu kingine kidogo kitakachoweka wazi kwamba sababu pekee ya kubatilisha uteuzi wa mgombea aliyewekewa pingamizi ni kama fomu zake za uteuzi zinaonyesha kwamba hana sifa za kugombea au kuchaguliwa zilizotajwa na ibara ya 67 ya Katiba. Tunapendekeza pia Kifungu cha 40 (6) kirekebishwe ili kuondoa kinga dhidi ya mashtaka kwa Tume kutokana na uamuzi wake juu ya rufaa za mapingamizi ya uteuzi wa wagombea mara baada ya kutolewa uamuzi huo, badala ya kusubiri uchaguzi husika kukamilika kwanza. Pendekezo hili litawezesha uamuzi wa Tume kuengua wagombea wa vyama vya upinzani kubatilishwa kabla ya uchaguzi kufanyika na hivyo kuwaruhusu kuendelea na kampeni na kushiriki kwenye uchaguzi.

Mheshimiwa Spika, uzoefu unaonyesha kwambani rahisi zaidi kwa mashauri ya mapingamizi kusikilizwa na kuamuliwa kabla ya uchaguzi kuliko kesi za uchaguzi zinazofunguliwa baada ya uchaguzi kufanyika na washindi kutangazwa. Sambamba na marekebisho ya mchakato wa mapingamizi; Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inapendekeza Kifungu cha 50A kifutwe kabisa kwa sababu kinaweza kutumiwa vibaya kwa kuwaonea wagombea, hasa wa vyama vya upinzani, kwa kuwaengua kabisa kwenye mchakato wa uchaguzi, au kwa kuvuruga kampeni zao za uchaguzi.

Mheshimiwa Spika, Sheria nyingine ambayo inabidi kufanyiwa marekebisho ni Sheria ya Gharama za Uchaguzi hususan kifungu cha 12 (1), (2), (3) na (4) kinachotaka vifaa vya uchaguzi kuingizwa siku 90 kabla ya uchaguzi. Tunapendekeza masharti ya kifungu hiki yafutweHii ni kutokana na ukweli kwamba katazo hilo halijazingatia uteuzi unaofanywa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwani Tume inateua wagombea ikiwa imesalia siku moja kabla ya kampeni kuanza, inawezekana vipi kwa chama cha siasa kuagiza vifaa bila kuwa na mgombea aliyeteuliwa na Tume. Aidha katazo hili la kisheria halijazingatia ugumu wa kuagiza, kuzalisha na kusafirisha vifaa hivyo kutoka nje ya nchi. Mapendekezo haya ya marekebisho ya sheria yaende sambasamba na kuboresha Sheria ya uchaguzi wa Madiwani “The Local Government (Elections) Act Ca. 292” kwa sababu uchaguzi huo pia ni muhimu na unafanyika sambasamba na uchaguzi wa Rais na Wabunge.

UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA ULIOFANYIKA NOVEMBA 2019

Mheshimiwa Spika,
Kwa ajili ya kuliunganisha Taifa tunapendekeza uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika tarehe 24 Novemba, 2019 ufutwe na urudiwe chini ya Tume huru ya Uchaguzi baada ya kufanyika kwa marekebisho kama tulivyopendekeza hapo juu. Hii ni kutokana na sababu kwamba uchaguzi huo kwa ujumla wake ulishindwa kuwapatia wananchi viongozi ambao wamepatikana kidemokrasia kwa sababu ya mapungufu makubwa ya kiusimamizi kama ambavyo chama chetu Chadema kilivyomwandikia Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI.

Mheshimiwa Spika, Uchaguziwa Serikali za Mitaa umeacha sintofahamu kubwa na mpasuko mkubwa miongoni mwa jamii yetu huko Vijijini na Mitaani. Huko ndipo Umoja na Mshikamano wa Taifa unapozaliwa. Ni wajibu wa Bunge hili ambalo ndilo linalowawakilisha wananchi na lenye wajibu mkuu wa kuisimamia na kuishauri Serikali kusimama katika nafasi yake kuitaka Serikali kuufuta uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa Novemba, 2019 ili kuepusha kusambaratika kwa Umoja na Mshikamano wetu kama Taifa. Ninatambua kuwa haya ni maamuzi magumu lakini hayana budi kufanywa ili taifa lipone. Aidha, kufutwa kwa uchaguzi huu kutathibitisha nia njema ya Serikali kupitia kwa Kauli ya Rais kuwa atahakikisha kuwa uchaguzi mkuu unakuwa huru, wa haki na halali.

TUME YA TAIFA YA MARIDHIANO

Mheshimiwa Spika,
Kutokana na matatizo mbalimbali ndani ya nchi kwa sasa ni imani yetu kwamba kuna malalamiko mengi kutoka kwa wananchi ambayo yanahitaji kufanyiwa kazi ili kuliunganisha Taifa. Masuala ambayo kwa sasa tunashauri yafanyiwe kazi na Tume ya Maridhiano itakayoundwa ni pamoja na haya yafuatayo:

Kupotea kwa baadhi ya watu na wengine kuuwawa kikatili na miili yao kuokotwa kwenye fukwe za bahari ya Hindi kwa nyakati tofauti na mpaka sasa hakuna taarifa zozote.

Kufuta kesi zote zenye sura ya kisiasa na zile zinazohusiana na makosa ya uhujumu uchumi na utakatishaji wa fedha zenye sura ya kisiasa, uonevu na au zinazolenga watu ambao wanaikosoa Serikali kwa mujibu wa Katiba na sheria zetu.

Kufuta makatazo yote ya kisiasa yanayozuia vyama vya siasa kufanya shughuli zake za kisiasa ikiwemo mikutano ya hadhara na maandamano.

Kutafuta muafaka kati ya wananchi na baadhi ya Wakuu wa Wilaya na Mikoa nchini ambao wamekua wakitumia vibaya mamlaka yao ya kuwaweka kizuizini wananchi bila kufuata taratibu, kutoa maagizo mbalimbali kuhusu mali au uwekezaji wa watu binafsi waliofuata misingi ya sheria na au kufukuza Watumushi wa umma bila kuzingatia taratibu na Kanuni za Utumishi.

Kukamata na kutaifisha mali za wawekezaji nchini bila kufuata taratatibu za kisheria

Uwepo wa mfumo wa kodi ambao sio rafiki kwa wawekezaji na au matumizi mabaya ya madaraka yanayofanywa na Mamlaka ya Mapato (TRA) kwa kusaidiana na vyombo vya ulinzi na usalama.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaamini kwamba mihimili ya Bunge, pamoja na Serikali itaona mantiki na nia njema ya mapendekezo haya na kuyafanyia kazi kwa msingi wa haraka na dharura kwa ajili ya mustakabali mwema na uendelevu wa nchi yetu.

JANGA LA VIRUSI VYA CORONA NA TISHIO LA KUANGUKA KWA UCHUMI NCHINI

Mheshimiwa Spika,
kila mtu sasa anafahamu kwamba dunia imepata janga la shambulio la Virusi vya Corona ambapo idadi kubwa ya watu wamefariki dunia huku mamia kwa maelfu wakiendelea na matibabu kutokana na maambukizi ya COVID 19. Kutokana na kusambaa kwa kasi kwa virusi hivyo katika nchi mbalimbali duniani;Tanzania nayo imekumbwa na janga hilo.

Mheshimiwa Spika, si nia yangu kuelezea kiini na athari za kiafya za gonjwa lenyewe isipokuwa ningependa kuzungumzia athari za gonjwa hili katika uchumi wa Taifa na utayari wetu kama Taifa kukabilina nalo.

Mheshimiwa Spika, kutokana na kuenea kwa gonjwa la COVID 19 ambalo mpaka sasa halina chanjo wala tiba, nchi mbalimbali duniani zimefunga mipaka na kuzuia mikusanyiko ya aina yoyote kama njia mojawapo ya kujihadahari na maambukizi ya Virusi vya Corona. Kutokana na hali hiyo, biashara nyingi zimesimama kutokana na kufungwa kwa maduka na viwanda vya uzalishaji pamoja watu kuwa chini ya zuio la kutoka nje (quarantine).

Mheshimiwa Spika, jambo hilo, limesababisha upatikanaji wa bidhaa na huduma kuwa wa tabu na hivyo kusababisha kupanda kwa bei za bidhaa na huduma husika. Katika maeneo mengine, ambapo ununuzi wa bidhaa ulitegemea wageni kutoka nje wanaoingia nchini, bei za bidhaa hizo zimeporomoka kutokana na kukosekana kwa wanunuzi ambao wamesitisha safari zao kutokana na hofu ya Corona. Aidha, uuzaji wa bidhaa kwenda nje ya nchi utakuwa umeathirika kutokana na nchi wanunuzi wa bidhaa zetu kufunga mipaka. Ni dhahiri pia kwamba, Sekta ya Utalii itaathirika sana na janga hili kwa kukosa watalii. Kwa ujuma sekta ya biashara na uwekezaji imeumizwa sana na janga hili.

Mheshimiwa Spika, kutokana na tishio la Virusi vya Corona katika uchumi; nchi nyingi Duniani zimechukua hatua madhubuti kuzia chumi zao zisianguke. Mathalan Nchi Jirani ya Rwanda Katika kukabiliana na hali hiyo, mamlaka ya nchi hiyo imetangaza hatua kadhaa kukabiliana na kupanda kwa bei kiholela. Kwa mujibu wa tovuti ya Rfi[1]Benki Kuu ya Rwanda imetangaza kupunguza masharti ya ulipaji wa mikopo ya benki kwa kampuni na watu walioathirika na ugonjwa wa Covid-19. Ili kufanikisha mpango huo, Karibu Euro milioni 50 pia zimetolewa kwa benki za biashara, ambazo zitahitaji ukwasi zaidi. Aidha, Ili kuzuia maambukizi ya virusi kupitia biashara ya fedha (kutoa na kupokea fedha), mamlaka pia imesitisha ada ambayo ilikuwa ikitozwa kwa kutoa fedha kupitia mfumo wa kidijitali.Hatua hizo zinalenga kupunguza athari za Covid-19 kwenye uchumi wa Rwanda. Mojawapo ya sekta zilizoathiriwa zaidi ni sekta ya utalii. Angalau matukio 20 yaliyokuwa yamepangwa kufanyika mwezi Machi na Aprili yamesogezwa mbele, kwa hali hiyo Rwanda itapoteza euro milioni 7, kulingana na Mamlaka ya Mapato ya Rwanda.

Mheshimiwa Spika, Serikali ya Kenya nayo imetangaza hatua za kunusuru uchumi kipindi hiki cha janga la Corona. Kwa mujibu wa taarifa ya Rais Kenyatta kwa wananchi wa Kenya ni kwamba ili kulinda ajira kwa wananchi na kuwapa waajiri uhakika wa kutopata hasara; Serikali ya Kenya imetoa nafuu ya kodi ya mapato kwa asilimia 100 kwa wafanyakazi wote wenye pato ghafi lisilozidi shilingi za Kenya 24,000/= kwa mwezi( kwa hapa kwetu ingekuwa takribani shilingi za kitanzania 240,000/=) . Hii imekwenda sambamba na kupunguza kodi ya mapato (Kulingana na mtu anavyopata – Pay As You Earn) kutoka ukomo wa kiwango cha juu cha asilimia 30 hadi asilimia 25 na kodi nyingine za mapato.

Mheshimiwa Spika, hatua nyingine kubwa iliyochukuliwa na Serikali ya Kenya ni kupunguza Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kutoka asilimia 16 hadi asilimia 14 kuanzia mwezi Aprili, 2020. Hatua hii imekwenda sambamba na Mamlaka ya Mapato ya Nchi hiyo (KRA) kutakiwa kuharakisha kulipa kiasi kilichohakikiwa cha shilingi za Kenya Bilioni 10 zamadai ya marejesho ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT refund claims) kwa wafanyabiashara ili kuhakikisha kwamba kuna mzunguko wa fedha wa kutosha katika biashara.

Mheshimiwa Spika, pamoja na hatua nyingine nyingi za kiuchumi ambazo Kenya imechukua kukabiliana na janga la Corona, Rais Kenyatta amependekeza punguzo la mishahara kwa hiari kwa viongozi wakuu wa Serikali kama ifuatavyo:- Rais na Makamu wa Rais asilimia 80, Mawaziri asilimia 30 na Makatibu Wakuu wa Wizara asilimia 20.

Mheshimiwa Spika, si nia yangu kuishawishi Serikali yetu kuiga hatua walizochukua wenzetu, lakinini Wajibu wa Serikali kulihakikishia Taifa usalama wa uchumi hasa kipindi cha janga hili. Serikali inatakiwa kuwa na‘interest’ kwenye jambo hili zaidi kuliko hata jumuiya ya wafanyabiashara; kwa kuwa endapo kutatokea anguko la kiuchumi, Serikali ndiyo itakayokuwa ya kwanza kushindwa kuendesha nchi.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaitaka Serikali kulieleza Bungeni hili, imepoteza mapato kiasi gani hususani katika sekta ya uwekezaji kufuatia mlipuko wa Virusi vya Corona? Aidha, Serikali imechukua hatua gani za kiuchumi ili kuzuia anguko la uchumi wa Taifa linaloweza kutokea kutokana biashara nyingi kusimama kufuatia nchi nyingi tunazofanya nazo biashara kufunga mipaka yake?

UWEZO WA NCHI KUKABILIANA NA MAAFA/MAJANGA

Mheshimiwa Spika,
nchi yetu kwa sasa inakabiliwa na majanga mawili makubwa yanayohitaji kushughulikiwa kwa dharura ili yasizalishe majanga mengine. Majanga hayo ni Virusi vya Corona na Mafuriko katika maeneo mbalimbali ya nchi.

Mheshimiwa Spika, Mvua za masika zinazoendelea kunyesha maeneo mbalimbali nchini, zimeshababisha mafuriko makubwa ambapo wananchi wengi wamepoteza maisha kwa kusombwa na maji, familia nyingi zimebaki bila makazi kutokana na nyumba zao kusombwa na maji, miundombinu ya barabara na madaraja imeharibiwa vibaya na hivyo kuathiri sekta nzima ya usafirishaji. Aidha kuna tishio la baa la njaa kutokana na mazao mengi ya chakula mashambani kusombwa na maji.

Mheshimiwa Spika,ili kukabiliana na majanga haya, kwa vyovyote vile Serikali inatakiwa iwe na bajeti ya dharura ya kushughulikia majanga hayo. Imekuwa ni desturi mbaya sasa kuwa kila tunapopatwa na majanga unakuta hatuko tayari kibajeti kukabiliana na majanga hayo. Mfano mzuri ni wakati wa tetemeko la ardhi kule Bukoba ambapo ilibidi wananchi wachangishwe fedha za kunusuru maisha ya wananchi walioathrika na janga lile.

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa hivi sasa tunakabiliwa na majanga mawili makubwa kama nilivyosema awali; na majanga hayo yana athari za moja kwa moja kwenye uchumi wa nchi na ustawi wa wananchi; Kambi Rasmi ya Upinzani inaitaka Serikali kulieleza Bunge hili kuhusu mambo yafuatayo:-

Ina mpango gani wa dharura wa kutoa fedha za kukabiliana na corona na mafuriko na fedha hizo ni kiasi gani?

Ina mpango gani wa dharura wa kutoa fedha kuzisaidia taasisi za fedha na makampuni ya biashara ili kunusuru anguko la uchumi kutokana na corona na mafuriko, na fedha hizo ni kiasi gani?

Ina mpango gani wa dharura wa kutoa mafunzo kwa madaktari na wauguzi kwa ajili ya kukabiliana na janga la corona
Kuna wilaya na mikoa mingapi yenye maabara zenye uwezo wa kupima corona hapa nchini?

Imeandaa vituo vingapi vya zuio (quarantine centers) kwa ajili ya kuwaweka watu wanaoshukiwa kuwa na maambukizi ya corona?

Ina hifadhi ya chakula kiasi gani, ikiwa italazimu watu kubaki majumbani ili kuzuia maambukizi ya corona?

Miradi mikubwa ya Reli ya SGR na Stiegler’s Gorge imeathirika kiasi gani kwa mafuriko na tishio la corona?

Ni hasara kiasi gani imepatikana katika mfumo mzima wa uchumi kutokana na majanga ya corona na mafuriko?

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani imelazimika kuuliza maswali haya, kwani majibu yake tatoa tathmini nzuri ya uwezo wa nchi kukabiliana na majanga. Aidha, kupitia majibu ya maswali hayo, Serikali inaweza kujipanga upya na kubuni mbinu madhubuti na mikakati endelevu ya kukabiliana na majanga.

VIASHIRIA VYA KUZUKA KWA UKABILA NA HATARI YAKE KWA UMOJA NA MSHIKAMANO WA KITAIFA

Mheshimiwa Spika, hakuna
mtu mwenye mashaka kuwa Baba wa Taifa, Mwalimu Nyererealikuwa mwasisi wa Taifa hili na alikemea ukabila kwa nguvu zake zote. Licha ya Mwalimu Nyerere kuupiga vita ukabila na udini; na licha ya wosia wake huo kuendele kutolewa na Redio ya Taifa (TBC Taifa) kupitia kipindi cha Wosia wa Bana kila saa kumi na moja alfajiri na saa mbili na robo usiku; lakini nasikitika kwamba kuna na kauli za kikabila ambazo zimeanza kuchipua katika nchi yetu.

Mheshimiwa Spika, kwa takriban mwezi mmoja uliopita, kumetokea kikundi cha watanzania chenye ajenda 3. Moja, Kujenga umoja wao, Pili, kuendeleza lugha yao ya asili, na tatu tatu wanasema lazima wamlinde kwa nguvu zao zote kwenye mitandao, kwenye vyombo vya habari na hata kuanzisha vikundi vya kupambana na yeyote anayempinga Rais Magufuli. Hii ajenga ya tatu ndiyo yenye shida!

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inataka umma wa watanzania kujua kuwa, Rais Magufuli sio Rais wa Wasukuma; ni Rais wa Watanzania wote. Ingekuwa Urais wa nchi hii unapiganiwa kwa ukubwa wa kabila lake Bila shaka Mwalimu Nyerere asingekuwa Rais, Marais wastaafu Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete wasingekuwa Marais. Hao wasukuma waliosema wanampigania Rais kimsingi wanamharibia Rais.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inayoongozwa na Chadema inawapenda Watanzania wote na wa makabila yote. Chadema haitampenda mtu wala kumchukia mtu kwasababu ya kabila lake. Sheria za uchaguzi zinazuia kuchagua kiongozi kwa misingi ya ukabila. Ninatoa wito kwa Serikali kukemea kwa nguvu zote viashiria hivi hatarishi kwa amani na umoja wetu kama Taifa. Majirani zetu Rwanda walianza kwa mzaha kuendekeza ukabila matokeo yake wakauwana zaidi ya watu milioni moja.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani inamtaka Rais Magufuli, kama anakerwa na ukabila, atoke hadharani na awakemee hao watu wanaonzisha mtandao wa kumlinda, kumtetea na kumpigania kwa kuwa yeye ni Msukuma mwenzao. Ikiwa atakaa kimya, maana yake ni kuwa, vikundi hivi vina baraka zake, na kwa maana hiyo atakuwa ameuthibitishia umma kuwa anaendekeza ukabila.

TATHMINI YA UTENDAJI NA UFANISI WA SERIKALI NA BUNGE KWA KIPINDI CHA MIAKA MITANO

Mheshimiwa Spika,
tunamaliza miaka mitano ya uhai wa Bunge la 11 tukiwa tumeacha rekodi mbaya ya utendaji wa Serikali na ufanisi wa Bunge kuliko awamu zote za Serikali zilizopita. Ni kipindi ambacho Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni imeteswa na kunyanyaswa kwa kutumia kila aina ya mbinu licha ya Kambi hiyo kuwepo kwa mujibu wa Katiba, Kanuni za Bunge na Sheria nyingine za Nchi.

Mheshimiwa Spika, ni katika Bunge la 11 ambapo Kambi Rasmi ya Upinzani imedharauliwa na kunyimwa haki zake za kikatiba na kikanuni kuliko mabunge yaliyopita. Mimi binafsi kama Kiongozi wa Upinzani Bungeni nimenyang’anywa nyumba na pia nimenyimwa gari ambalo ni stahili yangu ya kisheria; na hata pale nilipoamua kutumia gari yangu binafsi, nimenyimwa mafuta pia. Aidha, ni katika bunge hili la 11 ambapo Sekretarieti yangu (kwa maana ya wasaidizi wangu) wamefukuzwa kazi bila kupewa stahili zozote kwa mujibu wa sheria.

Mheshimiwa Spika, baada ya kuinyong’onyeza Ofisi Binafsi ya KUB; mkakati uliofuata ulikuwa ni kuwafunga midomo wabunge wa upinzani kwa kuwapa adhabu kali kwa mambo waliyoyasema Bungeni licha ya Ibara ya 100 ya Katiba ya nchi kuwapa uhuru wa kusema Bungeni. Adhabu kali zilizotolewa katika Bunge hili la 11 ni pamoja na wabunge wa Upinzani kufungiwa kuhudhuria vikao vya Mikutano mitatu hadi minne ya Bunge – adhabu ambayo ni nje kabisa ya adhabu zilizotajwa na Kanuni za Bunge. Wabunge waliopata hukumu hiyo ya kionevu ni pamoja na Gobless Lema (Mb), Halima James Mdee (Mb) na Ester Amos Bulaya (Mb). Aidha, waliopata adhabu za kutohudhuria vikato vitatu hadi kumi vya Bunge ni pamoja na Mhe. Suzan Lyimo (Mb), Mhe. Conchesta Rwamlaza (Mb), Mhe. Anatropia Theonest (Mb), Mhe. Joseph Mbilinyi (Mb), Mhe. Saed Kubenea (Mb), na Mhe. John Heche (Mb).

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani haipingani na Kanuni za Bunge zilizoweka utaratibu wa adhabu kwa Wabunge wanaovunaja Kanuni kwa makusudi; ila inataka kuona haki ikitendeka kwa pande zote. Ni jambo la kustaajabisha na ambalo haliingii akilini kuamini kwamba kwa kipindi chote cha miaka mitano kati ya Wabunge takriban 270 wa CCM; hakuna Mbunge hata mmoja aliyewahi kufanya kosa na kupewa adhabu hata ya karipio!

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni italikumbuka Bunge la 11 kama Bunge lililodumaza Demokrasia ya Kibunge (Parliamentary Democracy) kwa kuminya uhuru wa mawazo kwa wabunge wa upinzani. Hili limefanyika kwa namna mbili. Mosi, ni kwa kuhariri hotuba za Wasemaji Wakuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kwa kufuta baadhi ya hoja za upinzani kwa “Maelekezo ya Kiti” jambo ambalo ni kinyume na Kanuni za Bunge na pili; kutupilia mbali hoja binafsi za wabunge wa upinzani zilizokidhi vigezo vya kikanuni kuingia Bungeni, huku maazimio ya kuipongeza Serikali yakipewa nafasi ya kujadiliwa Bungeni.

Mheshimiwa Spika, Kanuni za 54 na 55 za Kanuni za Kudumu za Bunge (Toleo la Januari , 2016) zimetoa fursa kwa wabunge kupitia Hoja Binafsi kupendekeza jambo lolote lijadiliwe Bungeni kwa kuwasilisha hoja na kwa kutoa pendekezo lililokamilika ili lipate uamuzi wa Bunge. Tofautina mabunge yaliyopita ambayo Bunge, kupitia hoja binafsi za Wabunge lilipata fursa ya kujadili na kuyatolea maamuzi mambo mbalimbali nyeti na muhimu kwa mustakabali wa nchi; Bunge la 11 limeingia kwenye rekodi ya kutoruhusu hata hoja moja binafsi ya Mbunge kujadiliwa na kuazimiwa na Bunge.

Mheshimiwa Spika,Wabunge waliopeleka Hoja Binafsi zikawekwa Kapuni ni pamoja na hawa wafuatao:-
Mhe. Paschal Haonga: Kuhusu Mfumo wa Ununuzi wa Zao la Kahawa.

Mhe. Devotha Minja: Kuhusu Migogoro ya Wakulima na Wafugaji Mkoa wa Morogoro

Mhe Hussein Bashe: Kuhusu Kutaka kuundwa kwa Tume Teule itakayochunguza matukio mbalimbali yanayoonyesha kutishia Umoja, Usalama na Mshikamano wa Taifa letu.

Mhe. Upendo Peneza: Kuhusu Kuitaka Serikali kutoa Bure Taulo za kujihifadhi wakati wa Hedhi kwa Wanafunzi wa Kike

Mhe. Ernest Silinde : Kuhusu Tume ya HURU ya Uchaguzi

Mhe. Saed Kubenea Kuhusu:

  • Muswada wa Marekebisho ya Katiba ili kuruhusu kuwepo wa Tume Huru ya Uchaguzi
  • Uuzwaji wa Nyumba za NHC zilizokokwenye maeneo ambayo siyo ya biashara.
  • Mheshimiwa John Mnyika (Mb) – Muswada Binafsi kuhusu Marekebisho ya Sheria ya Barabara 2017.
  • Mheshimiwa Sophia Hebron Mwakagenda: kuhusu Haki Miliki ya Mlima Kilimanjaro;
  • Mheshimiwa Jesca Kishoa: kuhusu Deni la Taifa,
  • Mheshimiwa Esther Amos Bulaya kuhusu Kikokotoo cha Mafao ya Wastaafu (Pension)

Mheshimiwa Spika, Wakati hoja za wabunge zenye maslahi makubwa kwa wananchi zikiwekwa kapuni, licha ya kukidhi vigezo vya kikanunu; tumeshunudia maazimio ya bunge kuipongeza serikali yakipewa nafasi ya papo kwa papo kujadiliwa bungeni. Na mfano mzuri hapa ni hoja ya Mheshimiwa Elibariki Kingu aliyetoa pendekezo kwa Bunge Kupitisha Azimio la kumpongeza Rais juu ya ununuzi wa Korosho. Bunge lilipongeza; lakini sote tunafahamu namna wanachi wa Mikoa ya Kusini walivyonyanyasika na korosho yao na wengine mpaka leo hawajalipwa fedha zao.

Mheshimiwa Spika, tutalikumbuka Bunge la 11 kama Bunge ambalo halikulinda hadhi na heshima ya Wabunge wake. Ni katika Bunge la 11 ambapo Wabunge waUpinzani walikamatwa na Polisi wakiwa katika maeneo ya Bunge na kushtakiwa mahakamani kwa masuala waliyosema Bungeni kinyume na ibara ya 100 ya Katiba inayowapa kinga ya kutoshtakiwa kwa mambo waliyosema Bungeni. Wabunge waliokumbwa na sakata hilo ni pamoja na Waheshimiwa Suzan Kiwanga, Godbless Lema, Saed Kubenea, Cesilia Paresso na Paschal Haonga,

Mheshimiwa Spika, hujuma dhidi ya Upinzani ziliendelea na kuchukua sura mpya ya kuwinda uhai wa wabunge ambao walionekana kuwa mwiba kwa Serikali. Mnamo tarehe 7 Septemba, 2017, Mbunge wetu Mahiri wa Jimbo la Singida Mashariki, Mwanasheria Mkuu wa Chadema na Mnadhimu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Mheshimiwa Tundu Antipas Lissu, alipigwa risasi mchana kweupe nyumbani kwake Area D - Dodoma, kipindi ambacho Mkutano wa Bunge ukiwa unaendelea. Ni tukio ambalo halitasahaulika kwetu kwani ni tukio la kwanza la kinyama dhidi ya Mbunge kuwahi kutokea katika historia ya nchi yetu. Licha ya kelele nyingi ndani na nje ya Bunge kuitaka Serikali kuwabaini na kuwachukulia hatua wahalifu hao waliokuwa na nia ovu ya kudhulumu uhai wa mbunge wetu; Serikali iliamua kukaa kimya na kutofanya chochote ikiwa huu ni mwaka wa tatu tangu tuko hilo litokee.

Mheshimiwa Spika, pamoja na Mhe. Tundu Lissu kunusurika kifo, pamoja na kutopewa huduma za matibabu na Bunge, pamoja na Bunge kuzuia mshahara wake na stahili zake nyingine za kibunge, bado amevuliwa ubunge eti kwa sababu ya utoro Bungeni na kwamba Bunge halina taarifa kuwa yuko wapi! Hii inweza kutokea tu Tanzania!

Mheshimiwa Spika, tutalikumbuka Bunge la 11 kama Bunge ambalo halikukemea Ukiukwaji wa haki za binadamu unaofanywa na vyombo vya dola. Mara kadhaa Waheshimiwa Wabunge walitumia Kanuni ya 47 kuhusu hoja za dharura, miongozo mbalimbali kwa Spika pamoja na hoja binafsi kuhusu ukiukwaji wa haki za binadamu unaofanywa na vyombo vya dola kama vile mauaji ya Kibiti, kuzagaa kwa maiti katika fukwe za Bahari ya Hindi na Mto Ruvu, kupigwa risasi kwa Mbunge Mhe. Tundu Lissu, kupotea kwa Ben Saanane na Mwandishi wa Habari Azory Gwanda, kutekwa kwa Wasanii mbalimbali nchini; halikusimama kwenye nafasi yake kuiwajibisha Serikali na matoke yake ukiukwaji wa haki za binadamu bado unaendelea.

Mheshimiwa Spika, kwa kifupi, wabunge wa Upinzani wamefanya kazi katika mazingira magumu sana katika Bunge la 11 ukilinganisha na mabunge yaliyopita. Hii ni kwa sababu Serikali ya awamu ya tano imeuingilia mhimili wa Bunge kiasi kwamba badala ya Bunge kuisimamia Serikali kama ibara ya 63 ya Katiba ya Nchi inavyoelekeza; kinachoonekana dhahiri ni Serikali kulisimamia Bunge. Kwa mfano, wabunge wamezuiliwa kusafiri nje ya nchi mpaka wapate kibali cha Rais, Bunge halijaona kama limeingiliwa uhuru wake na limekaa kimya na kukubaliana na hali hiyo. Wabunge wanakamatwa hovyo na polisi na kushtakiwa wakiwa katika maeneo ya Bunge bila Spika kutaarifiwa, Bunge halioni kama limeingiliwa uhuru wake; Rais anatoa vitisho vya kuwafukuza wabunge wa kusini waliochaguliwa na wananchi kwa kuwasemea wananchi wao kuhusu biashara ya korosho Bunge linaona kuwa ni sawa. Haya na mengine mengi yanalitofautisha sana Bunge hili la Kumi na Moja kiutendaji na kiufanisi na Mabunge yaliyopita.

Mheshimiwa Spika, Tofauti nyingine kubwa ambayo Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni imeibaini ni kwamba; kipindi cha Bunge hili la Kumi na Moja ndio kipindi ambacho Serikali imesusiwa na Jumuiya ya Kimataifa kuliko wakati mwingine wowote wa mabunge yaliyopita. Kimsingi mahusiano yetu ya kidiplomasia na Jumuiya ya Kimataifa yamedorora ukilinganisha na vipindi vya mabunge yaliyopita. Ni katika kipindi hiki ambapo Denmark ambayo ni mshirika wetu mkubwa wa maendeleo, imesitisha misaada yake ya kibajeti; Umoja wa Ulaya umepunguza baadhi ya misaada yake sasa unajadili kusitisha kabisa; Bunge la Marekani nalo linajadili kusitisha misaada yake; na sababu kubwa zinazotolewa na washirika hao wa maendeleo ni kwamba; Tanzania kuna ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu na ukandamizaji wa demokrasia.

Kusitishwa kwa misaada ya kibajeti na washirika wa maendeleo kutaathiri sana ukuaji wa uchumi wetu jambo ambalo litaadhiri moja kwa moja maisha ya wananchi wetu. Hata hivyo, pamoja na hatari hiyo, Bunge kama chombo cha uwakilishi wa wananchi halijachukua hatua yoyote dhidi ya Serikali ili irekebishe masuala hayo yanayolalamikiwa ili nchi isiingie kwenye mkwamo wa kiuchumi.

Mheshimiwa Spika, Bunge la 11 limeingia pia katika rekodi mbaya ya kupambana na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ambaye kimsingi analisadia Bunge kuisimamia Serikali na huku likijua kuwa nafasi yake ni ya kikatiba na utaratibu wa kumwondoa madarakani pia umewekwa kikatiba.

Mheshimiwa Spika, Matukio yote ya ukiukwaji wa haki za binadamu; ukandamizaji wa demokrasia, kuminywa kwa uhuru wa habari, na uvunjaji wa sheria yanayofanywa na Serikali ambayo yalipaswa kukemewa na Bunge; Bunge limekaa kimya! Badala yake tunashuhudia Mkuu wa Nchi akimwagiza Spika wa Bunge kuwafukuza wabunge wa upinzani wanaosema Bungeni ili yeye (Mkuu wa Nchi) awashughulikie huko nje!

Mheshimiwa Spika, ili kuondokana na mkanganyiko huo wa mahusiano kati ya Mhimili wa Bunge na Serikali na kuhakikisha kuwa kuna mgawanyo wa dhahiri madaraka na mipaka (clear separation of powers cheks and balances); Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni,inaendelea kuitaka Serikali kuhuisha Mchakato wa Katiba Mpya ambao ulishafikia hatua ya kwenda kwenye kura za maoni ili Nchi iwe na Katiba Mpya inayotokana na maoni na mapendekezo ya wanachi.

HITIMISHO

Mheshimiwa Spika,
miaka mitano ya utawala wa Serikali ya awamu ya tano imetosha kuifahamu Serikali hii jinsi ambavyo haijali demokrasia, uhuru wa wananchi wa kutoa mawazo na kueleza fikra zao, uhuru wa wananchi kufanya shughuli za siasa, haki za binadamu, utawala wa sheria nk. Hakuna mwananchi ambaye hajaonja machungu ya Serikali hii. Katika uchumi, miaka mitano ya utawala wa Serikali hii imewaacha wananchi katika hali ya umasikini zaidi kuliko awamu nyingine zote. Ni kipindi ambacho Serikali imejitarijirisha kwa kunyang’ang’anya vyanzo vya mapato vya Halmashauri zetu na kuziacha zikishindwa kujiendesha; Ni kipindi ambacho Serikali imewabambikia kesi za uhujumu uchumi wafanyabiashara na wafanyakazi na kudai fedha nyingi kwa masharti ya watuhumiwa kukiri makosa; ni kipindi ambacho Serikali imewabambika viongozi wa upinzani kesi za uchochezi na kuwapiga faini ya kiasi cha hadi shilingi milioni 350 – faini ambayo haijatajwa na sheria yoyote; ni kipindi ambacho Serikali inatumia vyombo vya dola kukusanya mapato kwa nguvu kutoka kwa wafanya biashara na ni kipindi ambacho Serikali imeweka mazingira magumu kwa sekta binafsi kukua.

Aidha, ni kipindi ambacho Serikali inawekeza kwenye maendeleo ya vitu na sio kwa ustawi wa watu. Kwa mfano ni aibu kwa Taifa, kwamba wakati mataifa mengine yanapambana na janga la Corona kwa kutenga bajeti ya kushughulikia afya za wananchi wake, hapa kwetu Mkuu wa Nchi anasema watu waendelee kuchapa kazi na Mamlaka ya Mapato TRA ikatangaza kufanya kazi mpaka jumapili ili Serikali ikusanye mapato ya kupeleka kwenye miradi yake ya vitu na sio kunusuru afya za wananchi na janga la Corona!Afya ya wananchi kwa taifa hili sio kipaumbele cha Serikali hii; ila reli, na Stiegler’s Gorge ndio vipaumbele. Ninapata shida kuelewa kuwa miradi hiyo itawanufaisha akina nani ikiwa watu wote watakufa kwa Corona!

Mheshimiwa Spika, yapo mambo mengi mabaya yaliyofanywa na Serikali hii ambayo yameacha madonda kwa wananchi; lakini itoshe kusema kuwa miaka mitano ya utawala wa Serikali ya awamu ya tano ilikuwa ni miaka ya maumivu makubwa kwa wananchi. Kuipa Serikali hii muda mwingine wa kuongoza nchi ni sawa mtu kusaini hati ya kifo chake mwenyewe. Kwa hiyo, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inatoa rai kwa Watanzania kuchagua mabadiliko katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, 2020. Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kupitia Chadema inawaahidi wananchi neema tele, ikiwa itapewa ridhaa ya kuunda Serikali mara baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, 2020.

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo naomba kuwasilisha.

Halima James Mdee (Mb)
Kny. KIONGOZI WA UPINZANI BUNGENI (KUB) NA
MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI, KATIKA OFISI YA WAZIRI MKUU

1 Aprili, 2020.

[1]Rwanda yachukua hatua za kiuchumi kukabiliana na ugonjwa wa Covid-19
Unataka tukubali kuwa hiyo ndiyo kweli hotuba iliyoandaliwa na kambi ya upinzani bungeni na kuwasilishwa bungeni? Laiti ungetuwekea nakala badala ya wewe kuchukua jukumu la kuichapisha upya humu JF, angalau tungeamini kwa kiasi fulani na madai ya Spika wa Bunge kuyapa mtizamo mpya.

Sinalo la kuongeza zaidi ya kuhitimisha kuwa nia ya kuileta humu jamvini imekosa nguvu ya uhalisia wake, kujadiliwa.
 
Mhe. Ndugai ni mtumiaji wa kinywaji gani? Inawezekana anatuiaga mjani?
 
Ukisoma makini kwa kipindi cha simba wa Yuda huwezi ungana na KUB,Ila ukisoma baada ya uchaguzi na simba wa Yuda kusafiri kwa gharama kubwa utaelewa kuwa hotuba ilitulia na inapaswa kuheshimika kwamba maendeleo ya watu kwanza then maendeleo ya vitu.
 
Hiyo haikuwa bajeti ni porojo

bajeti upinzani hawajui Bajeti ya upinzani hukosoi iliyopo unatengeneza ya kwako kuwa Sisi tungeshika nchi hii ndio bajeti yetu

Hiyo hotuba inaitwa ya bajeti ya upinzani sio bajeti ni porojo naunga mkono Spika aliyeizuia kusomwa hakuna bajeti kwenye hiyo hotuba
 
Ukisoma makini kwa kipindi cha simba wa Yuda huwezi ungana na KUB,Ila ukisoma baada ya uchaguzi na simba wa Yuda kusafiri kwa gharama kubwa utaelewa kuwa hotuba ilitulia na inapaswa kuheshimika kwamba maendeleo ya watu kwanza then maendeleo ya vitu.
For sure
 
33 Reactions
Reply
Back
Top Bottom