Wembe ule ule uliomnyoa kanga manyoya. Kama walifikiri kuenguliwa bungeni Godbless Lema kutaleta unafuu kumbe wimbi la mageuzi si mtu fulani bali ni msukumo wa mazingira na wakati, ukiruka kuhunzi hiki unakutana na kingine hadi kieleweke.
Ndio hadaa ya kiti cha spika kutoruhusu baadhi ya vipengere visisomwe, lakini ukisoma hutoba hii yote yaliyoandikwa ni ukweli mtupu, na ukweli unauma ndio maana kiti cha spika kinajiumauma katika kuyumbisha kauli za kambi ya upinzani.
Mheshimiwa, Pale hakuna spika wala naibu spika, nakumbuka siku moja Dogo janja ( Mbunge wa Arumeru mashariki) alisema " ...ni kama mechi ya Simba na Yanga, halafu shabiki mmoja wa simba au Yanga anakuwa reffer ..." pataeleweka hapo ?