Hotuba ya Tundu Lissu aliyotoa baada ya kupokea tuzo ya kupigania uhuru, haki na utawala bora (Bush - Thatcher awards for freedom) kutoka IDU

snow snow

Senior Member
Sep 12, 2014
118
225
HOTUBA YA MH. TUNDU LISSU ALIYOTOA BAADA YA KUPOKEA TUZO YA KUPIGANIA UHURU, HAKI NA UTAWALA BORA ( BUSH - THATCHER AWARDS FOR FREEDOM) KUTOKA UMOJA WA VYAMA VYA KIDEMOKRASIA DUNIANI (IDU).

Hotuba hii imetafsiriwa kutoka lugha ya kiingereza na Hosea Ikubisabu.

Mh. Mwenyekiti Rt. Stephen Harper; Mh. makamu mwenyekiti David McAllister; Mwenyekiti wa jina tu Lord Ashcroft; Mh. Katibu mkuu Christian Kattner; Mh. Katibu mkuu msaidizi Miss Tina Mercep; Mwenyekiti msaidizi na makamu mwenyekiti; Wajumbe na maofisa wa familia ya IDU kote duniani; Mabibi na Mabwana; Itifaki imezingatiwa.

Mh. Mwenyekiti, wanasema kuwa 'mwaka mmoja katika siasa ni mapito ya muda mrefu' kama ndiyo hivyo, miaka mitatu ni lazima iwe ni safari ndefu; imeonekana hivyo kwangu binafsi na chama changu chadema vilevile kwa nchi yangu pendwa Tanzania. Muda kama huu miaka mitatu iliyopita nilikuwa hospitali ya Nairobi Kenya nikipigania uhai wangu kutokana na jaribio la kuuawa kwangu ambapo nilipigwa risasi 16 mwilini mwangu. Nilikaa bila kujitambua (nusu mfu) kwa siku 6 ndipo nilizinduka na kupata fahamu.

Na baada ya wiki na miezi kadhaa mfululizo nilifanyiwa upasuaji mara 24 na kupelekea kuwa na mkono ambao siwezi kuunyosha sawasawa na mguu wangu mmoja kuwa mfupi kwa pungufu ya sm 7.

Miaka mitatu baadaye nimeweza kufanya kampeni za urais kwa kuungwa mkono na kwa matumaini makubwa sana ya mamilioni ya watanzania; Mimi pamoja na chama changu Chadema tumeungwa mkono na mamilioni ya watanzania ambao walikuwa na matumaini makubwa sana na sisi.

Baada ya takribani siku 5 uchaguzi kuwa umefanyika, nililazimika kutafuta hifadhi ya usalama wangu katika ubalozi wa Ujerumani nchini Tanzania; nikiwa kama mwathirika wa vitisho vya kuuawa, ukilinganisha mazingira ni yaleyale ya vitisho vya kuuawa kulikotokea septemba 2017 hivyo sikuweza kupuuza vitisho hivyo ikabidi nikimbilie ubalozi huo wa Ujerumani.

Na sasa ni rasmi niko uhamishoni (ukimbizini); na mimi leo ni mpokeaji wa Tuzo ya Bush-Thatcher katika kupigania uhuru, haki na utawala bora. Ni heshima kubwa sana kwangu binafsi na chama changu Chadema kupokea tuzo hii kutoka kwa familia ya IDU na duniani kote, tuzo yenye majina ya viongozi mashuhuri wawili yaani Bush na Thatcher katika kupigania uhuru, haki na demokrasia.

Ni furaha kubwa sana kwangu kupata bahati hii ya kutunukiwa tuzo hii. Nimekuwa nikipata bahati zingine kama kuchaguliwa kuwa Rais wa chama cha Mawakili Tanganyika (TLS) kwa taaluma yangu; na kabla ya kuchaguliwa (nikiwa katika mchakato wa maandalizi ya kampeni) niliwekwa kizuizini na Jeshi la polisi na siku ya uchaguzi niliibuka mshindi wa kiti hicho cha urais wa TLS.

Nimekutana na vizingiti vingi sana katika harakati zangu, nimelala sana katika mahabusu za polisi. Nimekuwa katika kilele cha giza na mabonde ya uvuli wa mauti; na nimepitia kilele angavu cha maisha na radha ya utamu wake; hivyo ndo kwa namna miaka mitatu ya siasa nikiwa mgonjwa kutokana na kunusurika kifo cha mabunduki.

Mh. Mwenyekiti, kwa miaka mitano, chama chetu chadema kama ilivyo kwa nchi yetu kwa ujumla tumepitia nyakati ngumu sana kama ambavyo taasisi zozote zinazopigania demokrasia katika tawala za kidikteta zinavyoweza kupitia katika hatari na ugumu. Viongozi wa chama chetu, wanachama, wafuasi, wanaharakati; wameuawa kinyama, wametekwa, wamepotezwa kama ambavyo Utawala wa kiimla wa Latin America katika miongo mingi (makumi mengi ya miaka) iliyopita ulivyokuwa ukifanya; wengi wameteswa mikononi mwa mapolisi na katika majumba maalumu ya mateso yanayoongozwa na usalama. Wengine kama mimi wamekutana na vitisho vya uhai na wengine wamekamatwa na kuwekwa kizuizini kwa muda mrefu kinyume na sheria za nchi na kupewa mashitaka ya uongo.

Na hivyo, nasema hakuna chochote ambacho kinaweza kufanywa na utawala huu kukiua au kusambaratisha chadema zaidi ya kutishia, kukamata, kutunga sheria kandamizi, kuwagawa viongozi na maafisa wa chama chetu. Kwa ufupi, chama chetu kimepitia katika shambulio la kisaikolojia na kimwili ambavyo haijawahi kutokea katika historia ya vyama vingi nchini Tanzania; na pamoja na mazingira hayo tumeendelea kuwepo na kuendelea na mapambano.

Kutokana na zuio la miaka mitano ya kufanya siasa katika utawala huu hasa kwa vyama vya upinzani, ilibidi kujenga msingi wa chama chetu nchi nzima na kufanikiwa kwa kiasi kikubwa sana.

Hivyo, kutokana na kuimarika kwa chama chetu, katika uchaguzi wa serikali za mitaa Novemba 2019, wagombea wetu zaidi ya asilimia 90% walienguliwa kwa kisingizio kuwa hawajajaza fomu zao kwa usahihi, kwa mara ya kwanza karibu miongo mitatu (karibu miaka 30) ya chama chetu wagombea wetu walishindwa kujaza fomu zao; udikteta uliotumika kwa kutumia vyombo vya dola kuwaengua karibu wagombea wote wa chama chetu hivyo kwa mazingira hayo hapakuwa na uchaguzi wa serikali za mitaa Novemba 2019 nchi nzima; kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi yetu. Mazingira kama hayo yalitumika pia katika uchaguzi mkuu wa 28 oktoba 2020; wagombea wa chadema udiwani zaidi ya asilimia 95% na ubunge zaidi ya asilimia 92% walienguliwa eti hawajajaza fomu zao za kugombea kwa usahihi.

Pamoja na kuenguliwa kwa wagombea wetu wengi nchi nzima wakati wa uteuzi; tuliweza kufanya kampeni kubwa na kwa kuungwa mkono na mwitikio mkubwa sana wa mamilioni ya watanzania, haijawahi kutokea ukilinganisha katika chaguzi zilizopita; kauli mbiu yetu kwa watanzania wakati wa kampeni ilikuwa "Uhuru, Haki na Maendeleo ya Watu". Na hivyo ilipelekea rufaa ya udikteta kutumia vyombo vya dola kuvuruga uchaguzi ili kuhakikisha utawala huo unabaki madarakani. Kwa maana hiyo kama ilivyotokea katika uchaguzi wa serikali za mitaa Novemba 2019 hatukuwa na uchaguzi mkuu Oktoba 28, 2020 kulingana na mazingira ya namna hiyo.

Mh. Mwenyekiti, naomba uniruhusu kumshukuru mke wangu Alicia na vijana wetu wapendwa Augustino Lissu na Edward Bulali ambao hawakuweza kuwa na mimi leo hapa kulingana na masharti ya kujikinga na COVID 19; kwa upendo na uvumilivu wao katika miaka hii migumu kwangu na kwa familia yangu. Nitoe mwnga kidogo kwa ambavyo familia yangu imeenenda tangu septemba 2017; mwezi huu wa Disemba tutakuwa tunasherehekea kwa pamoja kama familia sikukuu ya Krismasi kwa mara ya kwanza katika miaka minne tangu septemba 2017.

Naomba uniruhusu niwapongeze viongozi wenzangu, wanachama wa chadema na mamilioni ya watanzania ambao wamekuwa nasi na kushirikiana pamoja katika kipindi cha miaka hii migumu; Kwa mafanikio hayo ya kihistoria, Tuzo hii ni ya kwao kama ilivyo ya kwangu.

Mh. Mwenyekiti, Tuzo hii ni ishara ya mapambano ya watu wetu katika kupigania demokrasia na kujitoa mhanga kwangu na viongozi wenzangu wa chama, wanachama, wanaharakati na wafuasi wanaotuunga mkono ambao wamelipa gharama za uhai wao na mali zao.

Ujumbe wangu nauelekeza kwao wote kama Alphonce Mawazo aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Geita ambaye aliuawa kikatili mchana kweupe, Ben Saanane aliyekuwa msaidizi wa Mwenyekiti wa Chadema Taifa ambapo alitekwa na kupotezwa Novemba 2016 alilipa gharama ya uhai wake kama ambavyo malengo ya Bush-Thatcher Awards for freedom yalivyoasisiwa.

Mh. Mwenyekiti kama nilivyosema wakati nilipofanya mkutano na vyombo vya habari vya kimataifa kwa njia ya mtandao wiki iliyopita kuwa kuibiwa (kuhujumiwa) kwa uchaguzi mkuu wa 28 Oktoba 2020 kunaweka rekodi ambayo haina afya ya kidemokrasia.

Utawala huu hauwezi kutufanyia lolote la kutuondoa zaidi ya ukandamizaji na kutunga sheria kandamizi; hivyo ni lazima tujiombee wenyewe kwa kipindi kigumu na kichungu sana kinachokuja juu yetu, ni lazima tuwaandae wanachama na watu wetu kupinga matumizi ya nguvu na ukandamizaji. Kwa kumnukuu Fredrick Douglass, mpigania mabadiliko ya kijamii na mpinga utumwa wa ki-Amerika; alisema, "Mwisho wa madhalimu huwa inategemeana na uvumilivu wa wale wanaonyanyaswa", uwezo wetu wa kupinga ukandamizaji wa utawala huu utategemea zaidi jinsi ambavyo tumejenga msingi wa chama chetu katika kipindi cha miaka hii migumu ya ukandamizaji na zaidi itategemea mshikamamo wa kimataifa kama ilivyo katika malengo ya kuanzishwa kwa IDU mwaka 1983, ambapo IDU yenyewe inajikita katika masuala ya kijamii na kisiasa ikiwa jamii za kidemokrasia zinaanzishwa ambapo ni pamoja na uhuru wa kujieleza; haki ya kukutana, kukusanyika, kupinga uvunjifu wa haki za binadamu; haki ya kuwa na chaguzi zilizo huru na uhuru wa kuundaa Kambi rasmi za upinzani bungeni (serikali mbadala); uhuru wa vyombo vya habari, uhuru wa kuabudu; haki ya kuwa sawa mbele ya sheria na haki ya kutumia fursa. Haki hizo zimekuwa chini ya mateka katika miaka mitano ya utawala huu.

Katika taarifa za IDU na Democratic Union of Africa (DUA) zilikuwa wazi kuwa uchaguzi wa Oktoba 28, 2020 haukuwa wa haki na huru na haukuwa halali na kupendekeza namna nzuri ya kuwa na uchaguzi wa kiwango kinachokubalika kimataifa ni kuwa huru, haki, shirikishi kwa pande zote, wazi, unaokubalika na halali.

Sasa tunaviomba vyama rafiki na serikali rafiki na chama chetu duniani kote kusimama na watanzania katika mapambano ya kupigania demokrasia katika nchi yetu.

Tuzo hii ni utambulisho wa kimataifa katika mapambano hayo na kutambua michango yao ya kujitoa mhanga kuwa ni hatua muhimu katika mwelekeo huo na haiwezi kuwa mwisho wa mapambano; hivyo zinatakiwa kuchukuliwa hatua madhubuti, mshikamano wa chadema na watanzania wote.

Kwa kumnukuu Fredrick Douglass kwa mara nyingine tena "Hisia ya taifa ni lazima iharakishwe, dhamira ya taifa ni lazima iamushwe; stahiki ya taifa ni lazima ishituliwe". Kwa hiyo, naomba uniruhusu kwa niaba ya familia yangu na kwa niaba ya wanachama wote wa chadema na watanzania kwa ujumla wao kuwashukuru IDU.

Asanteni sana.
 

Magema Jr

JF-Expert Member
Apr 22, 2020
1,299
2,000
We kijana kwa mwenendo wako huu wa kupost habari zenye uchochezi na zisizo na tija kwa taifa letu ,utaiona jf kama jehanam.
Who is Lissu by the way??🤔
 

MEXICANA

JF-Expert Member
Nov 16, 2014
1,492
2,000
Lissu utalaumu wanadamu bure tu,
Wewe ulichagua fungu baya Sana la kuiasi nchi ya Tanzania ambayo kwa bahati nzuri mkono wa Bwana Mungu uko juu ya nchi hii,kila atakayejaribu kuigusa kwa namna yoyote ile lazima akione cha moto
 

KISIWAGA

JF-Expert Member
Oct 22, 2015
2,352
2,000
Kuna tetesi Lissu alikabidhiwa rasmi Pete ya Freemason iliyokuwa kidoleni kwa Mkapa
 

Jozi 1

JF-Expert Member
Aug 16, 2015
6,494
2,000
Mbona hajawaambia kuws baada ya ucguzi ACT wameenda kujiunga na serikali na kula nata
 

snow snow

Senior Member
Sep 12, 2014
118
225
We kijana kwa mwenendo wako huu wa kupost habari zenye uchochezi na zisizo na tija kwa taifa letu ,utaiona jf kama jehanam.
Who is Lissu by the way??🤔
SORRY KAMA HUNIJUI ILA MIMI NI MCHAMBUZI TU POPOTE ILIPO SIASA TUTAICHAMBUA WEWE HUNA AKILI YA KUJUA LIPI NI LIPI MPAKA UCHOCHEWE....WEWE NI KUNI.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom