Hotuba ya raisi kwa walevi na wavuta sigala wa tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hotuba ya raisi kwa walevi na wavuta sigala wa tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mnyikungu, Jun 19, 2012.

 1. mnyikungu

  mnyikungu JF-Expert Member

  #1
  Jun 19, 2012
  Joined: Jul 26, 2009
  Messages: 1,441
  Likes Received: 582
  Trophy Points: 280
  Enji wavuta sigala wa tanzania, tafadhali tunawasihi sana ongezeni kasi ya kuvuta sigala, tuko chini ya miguu yenu tafadhali,chondechonde fanyeni juu chini mhakikishe kuwa kila mmja japo anatumia hata pakti hamsini kwa siku, ni kweli tunajua kuwa ni hatari kwa afya yenu ila tutafanyeji hatuna jinsi lazima mvute ili tupate mapato mengi yatayotuwezesha kuendesha nchi. ni kweli taifa linawategemea hasa ukizingatia kuwa migodi yetu yote ipo kwenye misamaha ya kodi na pia si mnajua sisi watanzania ni wakarimu hivyo tumeamua wanyama wetu tuwazawadie wageni wetu ili kuendeleza sifa ya ukarimu wetu.

  ENYI WALEVI:pia na nyie mimi kama mkuu wa nchi kwa niaba ya wadanganyika nina waomba muongeze kasi ya kunywa ili atlest hata mkinywa kila mmja kreti moja kwa siku mtakuwa mnatusaidia sana.najua ulevi wenu ni hatari kwa familia zenu maana hamuwezi kuwahudumia watoto wenu wala hata wake zenu na pia ni hatari kwa usalama wenu na afya zenu, lakini hamna jinsi lazima mnywe ili tupate fedha ya kuendeleza miladi ya nchi.kwanza mimi kama rais nimekuwa nikiwajali sana nyinyi walevi, je mmeishawahi kupata mgao wa pombe? na nataka niwahakikishie kwenye bajeti ya mwaka huu kuna kipengele cha kuwapa ruzuku wote wanaotaka kufungua baa ili kufanikisha mpango huu na kuhakikisha kuwa hii huduma mnaipata jirani.

  Ndugu zangu walevi na wavuta sigara, najua kuwa nawahatatarishia maisha yenu ila nawahakikishia kuwa selikali kwa kuwajali imeishanunua majeneza na sanda kwa ajiri yenu, pia kama selikali itatoa ubani wa sigara kwa wavuta sigala na creti za bia kwa wanywaji. pia nawahakikishia hata mkifa mtaingizwa kwenye kumbukumbu ya mashujaa wa nchi hii kwa maana mtakuwa mmekufa kwa ajiri ya nchi yenu.

  Mbali ya yote, kuanzia leo napiga marufuku kwa redio na terevisheni kuacha mara moja kutangaza matangazo yenye kuwakashfu walevi na yenye kupiga vita ulevi kwa kuwa kufanya hivyo ni kinyume na sheria na kanuni za chi.pia kuanzia leo natoa maagizo kwa wizara ya afya kuwaagiza madokta kuacha kutoa ushauri wa kuacha kutumia vilevi hivi kwa wagonjwa wao maana kufanya hivi ni kuhatarisha usalama na uhai wa taifa.

  Na pia kama selikali tunatafakali kwa kina juu ya kuongeza chanzo kingine cha mapato ambapo tunafikiria kuhalalisha matumizi ya bangi ili tuongeze wigo wa upatikanaji wa mapato ya taifa yatayotuwezesha viongozi wenu kula na kusaza na kwenda kupunga upepo ulaya maana tumegundua kuwa idadi ya wavuta ndumu inaongezeka,najua hatua hii itaongoza idadi ya vichaa nchini ila haijalishi maana nchi inahitaji mapato
  mungu ibariki afrika na mungu ibariki tanzania
  by raisi wa danganyika
   
 2. Maishamapya

  Maishamapya JF-Expert Member

  #2
  Jun 19, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,280
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Malo mmmh! Hili neno
   
 3. O

  Otorong'ong'o JF-Expert Member

  #3
  Jun 19, 2012
  Joined: Aug 17, 2011
  Messages: 31,110
  Likes Received: 10,461
  Trophy Points: 280
  Tumekupata wadanganyika.
   
 4. M

  Mussa Loth Member

  #4
  Jun 19, 2012
  Joined: Apr 13, 2012
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  RAISI KUFANYA MAAMUZI KWA MASLAHI YA UMMA

  Katka sheria nyingi zilizotungwa na Bunge, pamoja na katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania,baadhi ya ibara katika katiba na baadhi ya vifungu vinampa mamlaka Raisi kutekeleza baadhi ya maamuzi kwa maslahi ya Umma. Naomba kufahamisha mahali popote ambapo naweza kuyapata maslahi ya Umma yaliyoanishwa ilinifahamu msingi wake.
   
 5. M

  Mussa Loth Member

  #5
  Jun 19, 2012
  Joined: Apr 13, 2012
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  RAISI KUFANYA MAAMUZI KWA MASLAHI YA UMMA

  Katika sheria nyingi zilizotungwa na Bunge, pamoja na katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania,baadhi ya ibara katika katiba na baadhi ya vifungu vya sheria vinampa mamlaka Raisi kutekeleza baadhi ya maamuzi kwa maslahi ya Umma. Naomba kufahamishwa kama kuna mahali popote ambapo naweza kuyapata maslahi ya Umma yaliyoanishwa ilinifahamu msingi wake na endapo maslahi hayo ya Umma yatakuwa na mipaka wakati wa kutekelezwa.Kama kuan kamusi ambayo nitaweza kupata maana yake kwa urahisi.
   
 6. mnyikungu

  mnyikungu JF-Expert Member

  #6
  Jun 20, 2012
  Joined: Jul 26, 2009
  Messages: 1,441
  Likes Received: 582
  Trophy Points: 280
  bila shaka wadau watakujuza tu
   
 7. Communist

  Communist JF-Expert Member

  #7
  Jun 20, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 5,391
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Aiuwe ccm kwa manafaa ya umma.
   
 8. mnyikungu

  mnyikungu JF-Expert Member

  #8
  Jun 20, 2012
  Joined: Jul 26, 2009
  Messages: 1,441
  Likes Received: 582
  Trophy Points: 280
  ndo kwanza anatamani kuiuwa cdma kwa manufaa ya mafisadi
   
 9. Donnie Charlie

  Donnie Charlie JF-Expert Member

  #9
  Jun 20, 2012
  Joined: Sep 16, 2009
  Messages: 6,575
  Likes Received: 842
  Trophy Points: 280
  are men.
   
 10. kizomanizo

  kizomanizo Member

  #10
  Jun 20, 2012
  Joined: Jan 26, 2010
  Messages: 59
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Uandishi mzuri wa 'kejeli' (satire) lakini kwa jinsi unavozichanganya hizo 'l' na 'r' unaharibu maana yote ya hao maoni yako. Mara sigala mara sigara, kwa ajiri nk.
   
 11. mnyikungu

  mnyikungu JF-Expert Member

  #11
  Jun 20, 2012
  Joined: Jul 26, 2009
  Messages: 1,441
  Likes Received: 582
  Trophy Points: 280
  nisamehe mkuu nafikiri ujumbe umekufikia japo kwa tabu
   
 12. M

  Mkira JF-Expert Member

  #12
  Jun 20, 2012
  Joined: May 10, 2006
  Messages: 425
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35


  KWANZA HAO AMBAO SERIKALI YA CCM INAWATEGEMA KUWAPATIA KODI NI ``WALEVI'' KWA HIYO NI MUHIMU MNO KWETU ILA cha ajabu wassira ALIWAITA WALEVI TU WALIOMZOMEA AKIWA BUNDA KUMBE WALEVI WALIKUWA NA HAKI YA KUMZOMEA KWA SABABU NDIO WALIPA KODI WAKUBWA TANZANIA PAMOJA NA WAFANYAKAZI!!


  ILA KUNA KITU HAPA MKUU WA KAYA MWISLAMU NA WASHAURI WENGI WAISLAMU ISIJE IKAWA KWA KUWA WAO POMBE KWAO NI HARAMU BASI WANAONA WAWEKE KODI KUBWA ILI KUPUNGUZA WANYWAJI? ILA PIA HOJA HII INAWEZA KUWA SI MUHIMU MAANA WAO WANATEGEMEA WATU WANYWE ZAIDI ILI KODI ZAIDI IPATIKANE!

  NINAMALIZIA KWA KUSEMA WASSIRA KUZOMEWA NA ``WALEVI'' KULE BUNDA ILIKUWA NI SAWA NA HAKI YAO
   
 13. I

  ISIMAN Member

  #13
  Jun 20, 2012
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 72
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kufika tutafika ila tutafika tukiwa tumechoka sana mungu saidia
   
 14. mnyikungu

  mnyikungu JF-Expert Member

  #14
  Jun 20, 2012
  Joined: Jul 26, 2009
  Messages: 1,441
  Likes Received: 582
  Trophy Points: 280
  hapo nakumbuka ule wimbo wa:
  aiyolele amba,
  aiyolele amba,
  tunakotoka amba,
  ni mbali sana amba,

  tunakokwenda amba,
  ni mbali sana amba,
  mola saidia,
  twaomba tufike salama,
   
 15. mnyikungu

  mnyikungu JF-Expert Member

  #15
  Jun 20, 2012
  Joined: Jul 26, 2009
  Messages: 1,441
  Likes Received: 582
  Trophy Points: 280
  kaka kinywaji hakina dini ni kitimoto tu ndo chenye dini,lakini pia hawa jamaa huwa hawaangalii dini zao zinasema nini kwenye maslahi yao.kama wangekuwa wanafanya mambo kwa kufuata imani ya dini zao hata mafisadi wasingekuwepo
   
Loading...