Hotuba ya Rais ya mwisho wa mwezi Agosti 2012- Watanzania tuchukue lipi kwa sasa juu ya Ziwa Nyasa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hotuba ya Rais ya mwisho wa mwezi Agosti 2012- Watanzania tuchukue lipi kwa sasa juu ya Ziwa Nyasa?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MpangoA, Sep 2, 2012.

 1. MpangoA

  MpangoA JF-Expert Member

  #1
  Sep 2, 2012
  Joined: Jul 27, 2012
  Messages: 363
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Nimemsikiliza Mhe. Rais wakati wa hotuba yake ya mwisho wa mwezi. Ameongelea kwa kirefu masuala mawili: sensa ya watu na makazi na pia mgogoro wa mpaka kati ya Tanzania na Malawi. Mi naomba niongelee suala la mpaka wa Tanzania na Malawi.

  Kufanikiwa kwa Rais:​
  • Ameelezea vema historia ya mpaka huu.
  • Amekuwa muwazi kwamba mtangulizi wake, Rais Mkapa, alijali zaidi kukabidhi madaraka na hivyo kuacha kushughulikia suala la mpaka hata baada ya Rais Mutharika kukubali mazungumzo yaanze.
  • Amekuwa msomaji mzuri, au pia wasomaji wake wamejitahidi, kutafuta mifano ya mipaka kati ya nchi inayopita katikati ya mito au maziwa.
  • Sababu za kwa nini mpaka uwe katikati ya ziwa pia nazo zimeelezwa vizuri.

  Aliposhindwa Rais:

  • Ameshindwa kutoa maamuzi ya Rais. Hajakitendea haki kiti ya Uamiri Jeshi Mkuu. Malawi wanakataa mpaka kuwa katikati ya ziwa; sasa wananchi wa Tanzania hususani walioko mpakani wafanyeje? Waache kutumia ziwa au waendelee na maisha yao wakati mazungumzo kati ya nchi mbili yanaendelea. Sijasikia kauli juu ya hili na bahati mbaya msomaji hawezi kumshauri juu ya hili!
  • Ni bora kauli ya Mhe. Benard Membe kuliko hotuba ya Rais juu ya hili. Mhe. Membe alisema, anaiamuru nchi ya Malawi kusitisha utafiti wa mafuta upande wa Tanzania mara moja wakati mazungumzo yanaendelea.
  • Mbali na kumshutumu mtangulizi wake, hajatupa uhakika kama yeye suala hili atalimaliza kabla ya kuondoka madarakani.

  Maoni yangu:

  • Rais amekuwa msomaji zaidi badala ya kuwa Rais juu ya suala hili. Unajua katika shule za awali tulizoea kusoma historia mbalimbali na kukariri nadhalia (theory) mbalimbali. Katika ngazi ya utaalam, sifa kuu inayoangaliwa si jinsi ya kukariri na kukumbuka nadhalia bali ni jinsi gani unaweza kutumia nadhalia hizo kutoa maamuzi. Mhe. Rais sijaona maamuzi yake juu ya mpaka zaidi ya kusema hana nia ya kuingia vita na Malawi. Mimi mwenyewe siombei vita lakini nilitamani kusikia suruhisho walau la muda mfupi.
  • Ujinga wa waafrika na hasa Wamalawi juu ya hili. ‘Wazungu’ bado wanatawala akili zetu mpaka leo hii. Kosa la ‘mzungu’ ni hukumu ya haki kwa Waafrika, inashangaza sana! Yaani Wamalawi wamefunga akili zao na dhamira zao na kushikilia Heligoland Treaty 1890. Hivi, mpaka wa Sudan na Sudan Kusini ameweka ‘mzungu’ gani?
  • Hata Malawi wakatae vipi, suala la mpaka kupita katikati ya ziwa haliepukiki!
   
Loading...