Hotuba ya Rais ya Kufunga Mwaka 2013

Bonson

Senior Member
Apr 20, 2013
183
250
Mh. Rais wetu Kikwete, taarifa hii ikufikie unapoandaa hotuba ya kufunga mwaka. Ni matazamio yangu kwamba utakemea kwa nguvu na kwa uso wa hasira mambo yafuatayo:
1. Udini na Ukabila: Mh. Rais, inasikitisha sana kuona mbegu za udini na ukabila zinapandwa kwa kasi TZ. Mbaya zaidi ni kwa baadhi ya Viongozi wa CCM wanafurahia matendo haya.

2. Ulinzi na Usalama wa Raia: Kuna wa TZ wengi wamepoteza maisha, kuteswa na kudhalilishwa na wachache wenye nguvu. Tafadhali zungumzia hili na ni kwa jinsi gani utasimamia haki itendeke.

3. Kuporomoka jwa Elimu: Mheshimiwa, hii ni aibu kubwa jwa Taifa. Hivi viwango vipya vya ufaulu ni janga kwa Taifa. Plz chukua maamuzi.

4 . Kupanda kwa Gharama ya Maisha: Hali ni mbaya huku mitaani. Life ni ngumu sana.

Mheshimiwa Rais naomba uzungumzie mambo hayo kwa uzito unao stahili.

Mungu Ibariki Tanzania.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom