Hotuba ya Rais ya Kikwete kwenye baraza la Idd-Mawazo yangu

@Mkandara
Mkuu wangu katika majibu yako yote, naomba ibara au kifungu cha sheria kinayoruhusu uliyoyasema. Ni wapi kwenye katiba imeandikwa serikali haitashirikiana na taasisi yoyote katika kutoa huduma kwa wananchi wake? Hivi Bugando ni kanisani? Au kwenye visima vya maji ni sehemu za ubatizo?

Halafu unazungumzia mambo ya Sadaka, hivi wewe kinachofanyika kanisani ndio unataka kifanyike Msikitini?.. why not?. if it works kanisani why not try msikitini? Ni dhambi? Na kumbuka pamoja na kuwa na MOU sio kwamba hizo taasisi hazina gharama nyingine. Serikali inachangia sehemu tu kama ilivyo kwenye ruzuku za mbolea etc. Hivyo kanisa linagharamia uendeshaji. Nyie kwenye mahakama ya kadhi mlikuwa mna-propose 100% funding au less? sijawelewa MOU yenu kwenye mahakama mlitaka ikaaje.

sadaka zetu zinakwenda kwa maskini watu wasiojiweza na sio kuendesha shule na zahanati, mkuu kila dini ina mpango wake haya ni maswala ya kiroho.. how convinient? Na maskini wa ki-kristo wanasadiwa na nani? Let me tell you something, ukitaka kumsaidia mtu unampa uwezo wa kuvua samaka na sio samaki. Ukupe ni janga la Africa nzima let alone Tanzania. Na ndio sababu bara hili limekumbwa na hii fedheha ya Libya. NATO, Qartar, UAE are doing their things Africa wamebaki kulalamika na kuchunguza bendera. Back to the topic, kama kweli mnatumia sadaka kusaidi maskini bila kuwejengea uwezo i.e. elimu then mnaanda janga ya kitafa. I hope ulikuwa unatania:)

Mimi siwezi kukuuliza wewe mshahara wako unakwenda wapi - Sijaulizi mambo binafsi hapa nauliza 'institutional development' Huwezi kuendesha kitu kama mahakama kwa misaada kwa sababu mahaka sio shughuli ya siku moja. Kanisani kwangu kila jumapili mwenyekiti (sio mchungaji) anasimama na kusoma michango yote ya week pamoja na sadaka, matumizi, na balance! every damn sunday!. Siwezi kukuambia msururu wa michango tuliyonayo kwenye jumuiya kwa ajili ya kusadia (a) wasiojiweza (b)kujenga/kuendeleza seminari (c) majengo ya kanisa na matumizi mengine. Sasa hivi tuna matembezi ya hiari tunachanga kujenga ukumbi wa sherehe ili tukudishe (sio ruzuku).

Mkandara maadam unaonekana kujuwa dini ya uislama vizuri naomba unielimishe, ni dhambi msikiti au Bakwata kubuni mradi utakaoengeza kipato? Kwa mfano Bakwata wakaamua kujenga hospotali then wakapata ruzuku na huku wagonjwa wakawa wanalipa? Hii inaruhusiwa?

Kwani wewe mipango yako iwe sawa na yangu kwa sababu tu sote ni binadamu au mimi nimefanikiwa ktk swala fulani basi lazima nawe ufuate yangu!.. mbona mnachosha wakuu zangu ktk kufikiria kwenu. Kinachochosha watu Mkandara ni kutokuelewana kuhusu equal opportunity. Katika halio ya kawais=da mzazi huwezi kumpa mtoto mmoja ubwabwa na nyama ya kuku na mwingine chips mayai. Wakristo wana MOU na serikali kwenye hospital, shule etc. Waislam wameambiwa na Rais wa nchi kwamba hii OFA haiko tu kwa wakristo, wanachotakiwa ni kupeleka maombi yao na mambo yatakuwa safi tu. Lakini kumbuka MENU ni moja. Kama ni ubwawa na kuku ni wote, na kama ni chips mayai ni wote.
 
ʞontɹact Sniper;2444491 said:
Endeleeni kutofautiana, ila tu msisahau kuwa kuna mwisho unaoutuhitaji twende muelekeo mmoja kwa maslahi ya Jamii yetu.
Mkimaliza mtuambia
Nimeipenda signature yako... Mkuu wangu nachofurahi mimi naweza bishana na watu 100 wenye fikra huru na pana lakini hushindwa kubishana na mtu mmoja mwenye ufinyu wa kufikra na akili za kabatini..
 
Kamundu, mkuu wangu kama huelewi kitu ni bora ukae kimya itakusaidia sana kusilikiza...

1. Huwezi kuchukua ya Uislaam ukayaweka sawa na wakristo, haiwezekani na ndio maaana tunaamini dini hizi tofauti. Kwanza kubali kuna tofauti baina ya dini hizi hivyo huwezi kulazimisha haramu ya upande mmoja kuwa halali pande zote au kinyume chake..Wewe huna sababu ya kua na mahakama ya kadhi kwa sababu kesi nyingi za madai zinaamuliwa kutokana na sheria tangulizi za kikristu (canon law) na zimefanyiwa marekebisho ya hapa na pale lakini bado utaona mahakimu wetu wakivaa wig na majoho ya sawa na yale ya waasisi wao.

2. Huko Marekani kuna shule za watu weusi zinatoa matokeo mabaya sana ukilinganisha na zile zilizopo sehemu ya wazungu na sababu inajulikana wazi..watu weusi ni kama second citizen na wazungu wengi hawaelewi kabisa weusi wanalalamika nini wakati huo huo wakiwaita with a - N word!..

Unachozungumza hapa huna tofauti kabisa na kaburu wa Zimbabwe au South Afrika na nasikitika sana kuona mtu kama wewe umeingia ktk kuamini ukweli unaotanguliwa na tatizo kubwa la matabaka ambalo limejengwa na hawa viongozi wetu mara tu baada ya Nyerere kujiuzulu.. Kama unaamini Tanzania ni nchi yetu sote inakuwaje wewe unasema Waislaam wako hivi ama vile kama sii kujiona wewe ni mbora na tofauti na hao Waislaam?..

Maadam tumeona kuna tatizo katika baadhi ya shule zetu ni muhimu zitafutiwe ufumbuzi wa kitaifa kama tunavyoona shule za kata huwezi kusema hizo ni shule za maskini walalahoi - so it's their problem!

Mkandara umekamatwa pabaya kaka .Mie nawashauri waislam wote Tanzania tuandamane kupinga hotuba ya Mh.Dr.Kikwete juu ya Uislam na Waislam .JK anatunyanyasa mbele ya Wakristo hatukubali kwikwikwikwiwkiw mie nasoma tu ila nimesha zoea kulia lia kwa waislam kula kukicha wanadai haki sijui ni haki zipi hizo .JK alikuwa sahihi acha awanyame waache chokochoko.Kama ni Kanisa leo JK angalikuwa wapi ? So he knows better
 
Nakubaliana na wewe sana. Nimeshikwa pabaya bro na hii hotuba ya JK ambayo imeonyesha wazi jinsi Wakristo walivyokuwa na nguvu ktk utawala huu na imekuwa bora kwangu niko Chadema ambako nakubaliana na sera zao za Kijamaa even though I'm Conservative na naendesha maisha yangu kibepari.. Na kweli nilikuwa sijui mengi ya utawala huu lakini kila siku zinavyokwenda ndivyo vitu vingi vina make sense kwangu kuwa kuna Siri kubwa ambayo mimi sikuwa nikiijua..Hakuna aliyesema kweli kama Mwanakijiji alipouliza toka lini CCM ikawa rafiki wa Waislaam?...Ndio haya yanajitokeza jipu linapopasuka.

Waislaam hawaishi kulialia kwa sababu mfumo uliopo haujengi jamii zetu isipokuwa unawakwaza zaidi halafu watu wanashindwa kuelewa...Umemsoma FJM akisema serikali kama mzazi haiwezi kumpa mtoto mmoja ubwabwa na nyama halafu ikampa mwingine Chips na mayai. Mzazi si anapika chakula kwa watoto wote kisha kinatengwa mezani ili wote wale kwa pamoja!. Iweje serikali ipike ubwabwa na nyama kisiri kwa wakristu lakini waislaam washtukie waambie hamkuomba ili hali serikali ndiye mzazi alitakiwa kuwapikia wote chalula hicho?... Hii akili kweli babu!. Kisha mitoto yenyewe mikubwa inayoweza kujitegemea lakini bado innalia lia na sahani mkononi kuomba ruzuku..Inatia kichefuchefu..I'm not for Bakwata wala Kanisa bro na stand kuitahadhalisha serikali kuchukua jukumu lao na kuwa responsible na accountable - nobody else!

It's all good na nimeshikwa pabaya lakini ndio ukweli usiotakiwa kuzungumzwa na ndicho waislaam huita mfumo kristo. Serikali inatakiwa kuunda policy yenye uwazi kwa mashirika na taasisi zote za uwekezaji iwe hata hizi taasisi za kidini. Wanataka kuwekeza kwenye shule hatua A,B,C zifuatwe lakini sio kisirisiri mnaweka mkataba bila hata kulihusisha bunge letu na kuifanya sheria wala haikuwa sera wala ilani ya kiongozi yeyote isipokuwa usiri leo jipu lilmetumbuka wanatafuta pa kuchomokea..

It's wrong kwa serikali kuingia mkataba na taasisi yoyote ya kidini nje ya policy zake ktk uwekezaji kisha kuwapa kodi zetu bila ridhaa ya wananchi kupitia bunge na fedha hizo zikajulikana zinatoka kifungu gani - Haya ni makosa! na sintayapa nafasi kabisa kuyatetea hata kidogo. Kinachotakiwa ni policy moja kwa wawekezaji, tena hizi NGO kwa kupewa ruzuku ndio wanatakiwa kutoa huduma bure au karibu na bure na kama hawawezi wasitumie jina la dini wala NGO kwa sababu kutoza wanafunzi au wagonja gharama kubwa kuliko private companies nyingine ni wizi wa wazi wazi halafu bado wanavuta ruzuku zetu on top of profit wanayoitengeneza..

Tazama bajeti yetu ktk elimu na Afya kisha nambie hiyo ruzuku waliyopewa makanisa kutoka sehemu gani ya bajeti (was it 6bil -Tsh?)- Je, ni asilimia ngapi ya bajeti ktk wizara hizo..Again all walimu na madaktari ni wananchi wetu wenyewe ambao wangeweza kuifanya kazi hiyo under any conditions.

Serikali inaweza kabisa kuendesha huduma za shule, Hospital na Zahanati kinachotakiwa ni sera nzuri tu na Chadema wameweza kutumia nafasi hiyo kuwaambia wananchi isipokuwa CCM na wadau wenye interest zao wakasema haiwezekani hali serikali inapoteza fedha nyingi katika maswala yasiyokuwa muhimu..
 
Say NO MORE CCM.

thumbnail.aspx
 
Waislaam hawaishi kulialia kwa sababu mfumo uliopo haujengi jamii zetu isipokuwa unawakwaza zaidi halafu watu wanashindwa kuelewa...Umemsoma FJM akisema serikali kama mzazi haiwezi kumpa mtoto mmoja ubwabwa na nyama halafu ikampa mwingine Chips na mayai. Mzazi si anapika chakula kwa watoto wote kisha kinatengwa mezani ili wote wale kwa pamoja!. Iweje serikali ipike ubwabwa na nyama kisiri kwa wakristu lakini waislaam washtukie waambie hamkuomba ili hali serikali ndiye mzazi alitakiwa kuwapikia wote chalula hicho?... Hii akili kweli babu!. Kisha mitoto yenyewe mikubwa inayoweza kujitegemea lakini bado innalia lia na sahani mkononi kuomba ruzuku..Inatia kichefuchefu..I'm not for Bakwata wala Kanisa bro na stand kuitahadhalisha serikali kuchukua jukumu lao na kuwa responsible na accountable - nobody else!
..

ha ha ha haaaaa....lakini hapo umenichekesha haswa mkuu wangu. Mtoto mzuzuraji huyo lazima. Akifika nyumbani anakuta watu wanaosha vyombo. But now you know dinner time na menu. Usicheze mbali!
 
ha ha ha haaaaa....lakini hapo umenichekesha haswa mkuu wangu. Mtoto mzuzuraji huyo lazima. Akifika nyumbani anakuta watu wanaosha vyombo. But now you know dinner time na menu. Usicheze mbali!
Hakuna cha dinner time, Kanisa ndio baba serikali inawekewa chakula sasa hivi. Makanisa yakigoma JK yupo hatarini na hivi sasa yuko hatarini baada ya kuitoa ile siri ktk mkutano alioalikwa.. wengine hapa mnafikiria ni swala la wauza unga lakini ile siri aloitoa JK of how much kanisa katoliki hupewa ruzuku na kupandisha mori ya Waislaam ndiyo inawasumbua sana kina Pengo.

Labda niwe open zaidi, mimi nina hakika hata Bakwata wanavuta toka serikalini, mchezo huu upo tena nje ya bunge letu tukufu. Ni kiasi gani wanavuta ndicho hatujui lakini siku Bakwata waliposikia Kanisa Katoliki linavuta bil 6 au sijui ilikuwa 600 ndipo ugonvi mkubwa ulipojitokeza lakini zamani haikuwa issue kwa sababu kanisa limekuwa likivuta toka enzi za Mwinyi. Ilikuwa janja ya JK kuhakikisha kanisa halimfuati fuati lakini ndio kaharibu kabisa kuitoa siri ya kwamba mbali na dinner mnayokula wenzenu huwekewa menu nzito! (that was a message directed to muslims - Udini)) Sasa game likaharibika na ili kulipoza tena kanisa ndio kaingia na gear hii mpya akijua Waislaam hawana ubavu.
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Nimesoma kwenye magazeti na kusikiliza kwenye vyombo vya habari. Kwa kweli wengi wamemsifia kwamba ametoa hotuba nzuri. Lakini mimi kwa kweli nimekuwa na mtazamo tofauti. Naomba niseme wazi kwamba Raisi Kikwete amekuwa mean with the truth kwenye hii hotuba yake. Kwanza kwenye suala la Mahakama ya Kadhi, ni yeye na CCM yake ambao waliwaahidi waislamu mwaka 2005 kuwa watalipatia ufumbuzi.

Sasa kwa waislamu wengi ufumbuzi ilikuwa serikali itaanzisha hiyo Mahakama. Lakini cha ajabu nadhani mwaka 2008, Kikwete huyo huyo mbele ya Maaskofu wa KKKT alikanusha kuhusika na suala la mahakama ya kadhi. Akasema lilianzishwa na Mrema na Sheikh Ramia. Kwa maana nyingine yeye asiulizwe.

Leo anasema kuwa ni suala la waislamu wenyewe lakini hapo hapo anakiri kuwa Waziri Mkuu anaratibu. Waziri Mkuu ataratibu vipi suala la ibada. Kwangu mimi nadhani Kikwete angekiri walipoteleza na kueleza kuwa walifanya makosa kuingiza suala la dini kwenye siasa.

Suala la pili ni kuhusu suala la MOU ambapo waislamu wamelalamika kuwa wakristo wanapewa fursa zaidi. Kikwete amesema kwa sababu wao hawaombi. Hapa kwa kweli panatia shaka. Kikwete kama mara mbili akiwa kwenye mikutano na viongozi wakristo alinukuliwa akitoa takwimu kuonyesha pesa ambazo taasisi za kikristo wamepata kutoka serikalini.

Hivi alishindwa nini kutoa takwimu kuonyesha ni kiasi gani taasisi za kiislamu zinapokea kutoa serikalini? Kwa nini hakutoa hata mfano kuwa Muslim University kilitolewa na serikali? Je pia alishindwa kuonyesha kuwa hizo shule za makanisa kama zinazuia kusoma watu wa dini nyingine? Na pia kwa sababu alikuwa Waziri wakati Mzee Mwinyi atakuwa anajua kwanini MOU ilisainiwa, je alishindwa nini kutoa hiyo institutional memory ili kuondoa upotoshaji unaoendelea.

Alichozalisha hapa ni kuonyesha kuwa wakristu wamekuwa wakipendelewa kwa sababu wanaomba na waislamu wamenyimwa kwa sababu hawaombi kitu ambacho nadhani si sahihi. Kama kwenye wamenyimwa serikali haitakiwi kusubiri hadi kuombwa, kwani Nyerere aliombwa na nani kutaifisha shule?

Kwa kweli kwangu nadhani ni hotuba inayopalilia udini badala ya kuumaliza.

NAWASILISHA
kasikilize tena hotuba vizuri, majibu kwa karibu ya naswali yako yote yako kwenye hiyo hotuba
 
Jamani itafuteni elimu kwa udi na uvumba. Mtu ukiwa na elimu ya kuelewa mambo wala haya mambo hayawezi kukuchanganya. Mtu ukiwa na elimu utajua tu hiyo MOU manake nini na utagundua kwamba hiyo MOU imewasaidia wakristo na waislamu. Wakristo kwa waislamu twendeni shule tukasome. Elimu ya siku hizi ni rahisi ushindwe wewe tu. Mikopo ya elimu ya juu ipo kwa mtu asiyeweza kujitegemea. Tuache kulalamika.
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Jamani itafuteni elimu kwa udi na uvumba. Mtu ukiwa na elimu ya kuelewa mambo wala haya mambo hayawezi kukuchanganya. Mtu ukiwa na elimu utajua tu hiyo MOU manake nini na utagundua kwamba hiyo MOU imewasaidi wakristo na waislamu.
Alaa sasa kwa nini ilikuwa siri?..na wanapewa kodi zetu bila ridhaa ya wananchi. Na mbona OIC ni ya Waislaam na Wakristu na imekataliwa kwa sababu watu wanasoma katiba ya OIC lakini hawasomi katiba ya kanisa katoliki inapokuja swala la MoU..
 
Labda niwe open zaidi, mimi nina hakika hata Bakwata wanavuta toka serikalini, mchezo huu upo tena nje ya bunge letu tukufu. Ni kiasi gani wanavuta ndicho hatujui lakini siku Bakwata waliposikia Kanisa Katoliki linavuta bil 6 au sijui ilikuwa 600 ndipo ugonvi mkubwa ulipojitokeza lakini zamani haikuwa issue kwa sababu kanisa limekuwa likivuta toka enzi za Mwinyi. Ilikuwa janja ya JK kuhakikisha kanisa halimfuati fuati lakini ndio kaharibu kabisa kuitoa siri ya kwamba mbali na dinner mnayokula wenzenu huwekewa menu nzito! (that was a message directed to muslims - Udini)) Sasa game likaharibika na ili kulipoza tena kanisa ndio kaingia na gear hii mpya akijua Waislaam hawana ubavu.

Hapo pa Bakwata nakubaliana na wewe kabisa. Na nahisi wanachokifanya hawa Bakwata ni kupalilia malumbano hivyo kuwafanya waislam wachooonge sana kuhusu wakristo kupata ruzuku na kusahau kuwauliza wao Bakwata wanapata kiasi gani na wanafanyia dini? Kila jambo lina mwisho wake, na sitashangaa siku za hizi hizi waislam wakawageukia Bakwata na kuwauliza 'show us the money'. Kama mtu anapewa kidogo na hakuna cha kuonesha, kuna uhakika gani kwamba wakiongezewa watafanya la maana? MAKRTISTO yako makini kidogo ha ha ha haaa.
 
Haa haa haa! Hapana Makristo ni wale wanapenda sana kutukana, kushabikia Udini na sii wale wanaotaka kuelimishana..Siku zote nawasifia kanisa na mpango wake ktk jamii lakini kwangu mimi Muislaam hilo sii jukumu na kazi ya kiimani kwa sababu Yesu kasema ya Kaizali tumwachie Kaizali.. Uislaam haupingani na Ukristu hata kidogo isipokuwa sehemu moja tu nayo ni pale mnaposema - Yesu ni Mungu!..

Hili ni swala la imani ambayo imetutenganisha lakini wenzetu siku hizi hata Ukristu mnautoka maana kunywa pombe, nguruwe, kufunga, na kadhalika ni mambo ya Waislaamkwenu hakuna haramu siku hizi, wakati huo huo waislaam nao kitimoto, pombe ni haramu lakini wanatembea nje ya ndoa, na wake/waume za watu, ushoga na kadhalika sii hoja tunafukuzana. Dini sii rahisi mkuu wangu binadamu wa leo sisi ni wanafiki watupu na hakika kama kweli ipo peponi basi sijui nani ataingia ktk Umma huu!
 
Haa haa haa! Hapana Makristo ni wale wanapenda sana kutukana, kushabikia Udini na sii wale wanaotaka kuelimishana..Siku zote nawasifia kanisa na mpango wake ktk jamii lakini kwangu mimi Muislaam hilo sii jukumu na kazi ya kiimani kwa sababu Yesu kasema ya Kaizali tumwachie Kaizali.. !..
QUOTE]

Sasa mtaishije kama uwekezaji katika miradi hata ya kijamii halipewi kipaumbele? Shida nyingine ninayoona ni kwamba hivi vitabu vya dini (biblia or koran) havifanyiwi update obviously kwa sababu kila kilichoondikwa kinaaminika ni holly and will remain so. Sasa challenges za nyakati zinapoingia kunakuwa na limitation kwenye response strategy. Wakatoliki walipata shida sana na talaka maana biblia ina kasheshe zake when it comes to marriage! hata hivyo wakubwa wamesoma kwa kutumia mawani mazito na sasa talaka ipo ila process yake is no small matter!. Kama ni sababu za hivi hivi sijui pua imeelekea kushoto au mara kanenepa sana utajikuta unamrudia mke na pua hiyo hiyo kutokana na process ilivyo complex. msalaba wako watakuambia!

Anyway, goodluck na crusade and I hope mgao ujao mpo! but watch out the menu ...coming out soon! Na kama hutupata wala usijali, karibu Bungando Hospital. hatubagui sisi:)
 
Myself nimekuwa sipendi these discussions za discrimination kwa sababu hazina umuhimu wowote ule na pili ni kwamba most people don't have a clue how and why are we really having these discussions in the first place.

Only thing I see here ni jinsi ya kikwete yeye mwenyewe kuonyesha jinsi gani wananchi kweli hawakumchagua na jingine ni kwamba tunajua this so called speech wa prepared by his people ili aonekane he's relevant to Tanzanians nchini kote. Why are we discussing mahakama za kiislamu kwenye forum za serikali? Why we want to drag issues from the past to our history today. It's true serikali ya Tanzania kama serikali zingine zimefanya makosa katika nation building but society yetu leo inaonyesha kabisa majority wamefika mbali na kuona solution ni sisi kama wananchi kujenga na kushirikiana and this is only way to move forward. Hakuna sababu yeyote ile ya kuendelea ku-visit hizi issues na only thing here ni jinsi gani kikwete anavyotumia hizi issues za udini kugawa watanzania na kudanganya wakati akijua the facts.

Tukichunguza utendaji wa serikali na majukumu yake, hakuna sehemu yeyote ile kuna nafasi ya mahakama za kidini. Serikali inaongozwa na Katiba (ingawa Tanzania haina katiba kwa sasa) na kazi ya serikali ni kufuata sheria na hakuna alie juu ya sheria ikiwemo kikwete mwenyewe na viongozi wa dini. Sioni sababu zozote za dini mbambali kuendelea kujadili haya maswala. Tulishasema tangu awali, kama waislamu wanataka kuanzisha vitu vyao wafanye hivyo na wakijua wazi hivyo vitu vipo chini ya katiba na havivuki katiba na wakristo wakitaka kuanzisha vitu vyao wafanye hivyo na wasifike na kuingilia mipaka ya katiba ya nchi. Constitution is the only law of the land period!

Hayo maswala ya misaada na utendaji wa serikali juu ya institutions mbalimbali nia maswala ya bunge na kama kuna wananchi hawatendewi haki au kubaguliwa kwa namna yeyote ile ni swala la kupelekwa bungeni na mapendekezo yapelekwe ili suluhisho lipatikane na hizi njia zinazotumika za kutaka ofisi za serikali zitetea dini fulani inaonekana yote haya ni ignorance ya positions za watu waliopo humo serikalini.

People lets focus na maswala muhimu ya kulikwamua Taifa letu kutoka kwa ccm na ujambazi wao. Sioni sababu yeyote inatufanya kuacha kujadili policies mbovu za kikwete na uchumi wa kimaskini. Inflation inakwenda 20%, tatizo la umeme ndio bado linakolea na bidhaaa muhimu zinazidi kupanda bei. Sijui kama mahakama za kidini au misaada ya kidini itatatua haya matatizo, lets stay away kwenye hizi distractions za kikwete!

Nimesoma kwenye magazeti na kusikiliza kwenye vyombo vya habari. Kwa kweli wengi wamemsifia kwamba ametoa hotuba nzuri. Lakini mimi kwa kweli nimekuwa na mtazamo tofauti. Naomba niseme wazi kwamba Raisi Kikwete amekuwa mean with the truth kwenye hii hotuba yake. Kwanza kwenye suala la Mahakama ya Kadhi, ni yeye na CCM yake ambao waliwaahidi waislamu mwaka 2005 kuwa watalipatia ufumbuzi.

Sasa kwa waislamu wengi ufumbuzi ilikuwa serikali itaanzisha hiyo Mahakama. Lakini cha ajabu nadhani mwaka 2008, Kikwete huyo huyo mbele ya Maaskofu wa KKKT alikanusha kuhusika na suala la mahakama ya kadhi. Akasema lilianzishwa na Mrema na Sheikh Ramia. Kwa maana nyingine yeye asiulizwe.

Leo anasema kuwa ni suala la waislamu wenyewe lakini hapo hapo anakiri kuwa Waziri Mkuu anaratibu. Waziri Mkuu ataratibu vipi suala la ibada. Kwangu mimi nadhani Kikwete angekiri walipoteleza na kueleza kuwa walifanya makosa kuingiza suala la dini kwenye siasa.

Suala la pili ni kuhusu suala la MOU ambapo waislamu wamelalamika kuwa wakristo wanapewa fursa zaidi. Kikwete amesema kwa sababu wao hawaombi. Hapa kwa kweli panatia shaka. Kikwete kama mara mbili akiwa kwenye mikutano na viongozi wakristo alinukuliwa akitoa takwimu kuonyesha pesa ambazo taasisi za kikristo wamepata kutoka serikalini.

Hivi alishindwa nini kutoa takwimu kuonyesha ni kiasi gani taasisi za kiislamu zinapokea kutoa serikalini? Kwa nini hakutoa hata mfano kuwa Muslim University kilitolewa na serikali? Je pia alishindwa kuonyesha kuwa hizo shule za makanisa kama zinazuia kusoma watu wa dini nyingine? Na pia kwa sababu alikuwa Waziri wakati Mzee Mwinyi atakuwa anajua kwanini MOU ilisainiwa, je alishindwa nini kutoa hiyo institutional memory ili kuondoa upotoshaji unaoendelea.

Alichozalisha hapa ni kuonyesha kuwa wakristu wamekuwa wakipendelewa kwa sababu wanaomba na waislamu wamenyimwa kwa sababu hawaombi kitu ambacho nadhani si sahihi. Kama kwenye wamenyimwa serikali haitakiwi kusubiri hadi kuombwa, kwani Nyerere aliombwa na nani kutaifisha shule?

Kwa kweli kwangu nadhani ni hotuba inayopalilia udini badala ya kuumaliza.

NAWASILISHA
 
Niliogopa kujibu kabla sijatazama hotuba nzima

Nimeshangaa sana kuona FORUM iliyosheheni mashabiki wa CHADEMA ambao kila kukicha hawaishi kumtukana JK matusi ya kia aina wameamua kumsifia kwa kila sifa

Kumbe alichokifanya JK ni kwenda Dom

1. Kawakandia waislam kuulizia kulikoni kuhusu MOU

2. Kawaambia wasithubutu kuomba shule kama wakristo kwani wamechelewa

3. Kawaambia kuwa alikutana na viongozi wa Kanisa (ambao walimpa hotuba ya siri juu ya mustakbali wa Nchi)

4. Na katika mambo ambayo yaliyoku(walimpa instructions ) ni hili la WAISLAM na MAHAKAMA ya KADHI

5. Amekutana na waislam kisha kawaambia kuwa serikali imekubaliana na matakwa ya viongozi wa Kanisa (kama walivyomwambia kwenye hotuba yao)

Couple of things labda JK ningemkumbusha:

A) BAKWATA ni just another NGO kama vile klabu ya Yanga, Namisado, Blackwizard, Mama na Mwana, Mtoto kwa mtoto, zoma zoma evalengicals etc

B) BAKWATA haiwakilishi maoni ya waislam wote Tanzania

C) MAJORITY ya waislam kisheria za dini ya kiislam ni HARAM kuongozwa na viongozi ambao hawana QUALIFICATION za kueleweka kama the likes of Mufti etc

D) JK asisahau kuwa kuna MISTRUST toka kwa Waislam kwa serikali ambayo in almost 50 years imekuwa ikiwakandamiza systematically waislam na haikutaka kuwasilkiliza kwa lolote mpaka Rais Mstaafu Mkapa alipoamua kulia approcah hili jambo kwa undani na kukaa nao chini na alikubali kuwa kulikuwa na uhuni uliofanywa na zealots walioposerikalini

E) Waislam HAWANA ugomvi na Kanisa wala wakristoi ila tatizo la waislam ni mfumo kristo

Waislam na hoja ya Shule:

Ni kweli Nyerere aliamua ku taifisha shule zote za kidini mwaka 1969 lakini kuna baadhi ya mambo manne makuu lazima niyaweke wazi kwa hiyo kijana aliyemwandikia JK hii speech.

1. kati ya mwaka 1961-1969 Nyerere huyo huyo ambaye JK juzi alimsifia kule Dom ndiye aliyekuwa kinara wa kupinga utaifishajiwa hizi shule za kidini na hasa za kikiristo. Hili lilitokana na ukweli kuwa waislam walikuwa nyuma sana kielimu sasa kutatua tatizo la waislam na elimu akaona bora kufanya short cut ya kutatua tatizo la waislam na Nyerere alitoa order kuwa shule za wakristo zisitaifishwe ila serikali ijenge zingine ili ziwa accommodate waislam

Kama mnataka ushahidi someni kkitabu kilichoandikwa na David Westerbud Ujamaa na Udini : A study of some aspects of society and religion in Tanzania-soma ukurasa 122.

2 Kabla ya uhuru mpaka mwaka 1969 shule zote za kanisa zilikuwa zinaitegemea serikali kipesa na hii ilithibithishwa na kauli ya Father Robinson wa TEC ambaye alisema kuwa serikali ikithubutu kutoa misaada basi hizi shule zote zitafungwa au zitakufa. Na pesa hizi ambazo wa kristo walikuwa wanapata zilitokana na KODI za waislam! Infact asilimia 66 ya bajeti ya kuendesha shule hizi ilikuwa ni grant toka serikalini.

3. Baada ya kutaifisha hizi shule za Kanisa, bado shule hizi zilikuwa zinaendelea kuendeshwa na watu wale wale! yaani effectiveness ya hii policy ya utaifishaji katika operational level was largely dependent on the goodwill ya wale wale waliokuwa wanapinga huu utafishaji kwa nguvu zote in the first place. No wonder almost 50 yrs baada ya uhuru JK, policy advisor's wake, speech writers wake na maaskofu aliokutana nao wanaona taabu kukubali na kusema wazi kuwa if anything Muslims are far worse today than Christians.

4. Kwa wanaojua historia ya Tanzania ni kuwa ukweli usiopingika ni kuwa by 1969 serikali ya Nyerere ilijaa wakristo na haikuwa na nia ya kukaa na kuangalia namna ya kutatua issues zinazohusu waislam. Baada ya hapo (KAMA ALIVYOAGIZA JK juzi kule Dodoma) waislam wakaamua kujitegemea kwa nguvu zao (japo leo wanakebewa kuwa hawana self efforts) na kuunda jumuiya yao chini ya East Africa Welfare Sosiety (EAWS) ambayo ilikuja kupigwa marufuku na Nyerere baada ya kupewa instructions na viongizi wa kanisa (Msome Sivalon 1992) na baada ya hapo Nyerere akaja kuunda chombo kinachoitwa BAKWATA mwaka 1968!

BAKWATA hii iliyoundwa na Nyerere na ambayo juzi JK kaongea nao iliundwa kwa KATIBA ya TANU na kilichoondolewa kwenye ile katiba ni neno TANU na kuingizwa BAKWATA! na viongozi wa waislam waliopinga kuundwa na Bakwata walitiwa ndani na Nyerere na kuundwa kwake ilikuwa ni kuwa onyesha waislam kuwa anajaribu kutatua matatizo yao wakati huo huo mwaka 1969 Nyerere huyo huyo aliyekuwa anapinga zoezi la kubinafsisha shule za kanisa akawa bize kuzitaifisha kama vile kupinguza ile hasira za waislam kwa kuwaonyesha kuwa hana udini na anataifisha shule za Kanisa!

MOU:

JK anasema waislam wakitaka waende na MOU yao lakini huko nyuma kasahau kuwa jumuia za kanisa zilizosign MoU ndizo zilikuwa vinara wa kupinga na kufanikiwa waislam kupata misaada toka OIC kwa kudai kuwa OIC ni jumuia ya kidini! (Tazama tamko la baraza la kanisa la Pentecostal tar 9 September 2000)

Ukweli ni kuwa baada ya kusign MoU kanisa wamekuwa wakipata misaada direct toka serikali za nje na bila kusahau personnel na hakuna aliyedai kuwa kuna udini ndani yake ambao juzi JK aliamua kuwashushua waislam.

Cha kujiuliza ni why should the churches set conditions kwenye mambo ya waislam na serikali? Je kuna kipengele gani kwenye katiba kinachowapatia wao haki zaidi ya waislam na wasio wakristo?

Je JK anavyosema waislam waende na MoU yao serikali je atatuhakikishia vipi kuwa hayatowakuta yaliyowakuta ile asisi ya MIDECE kule Mtwara?

umetumwa?
 
Haa haa haa! Hapana Makristo ni wale wanapenda sana kutukana, kushabikia Udini na sii wale wanaotaka kuelimishana..Siku zote nawasifia kanisa na mpango wake ktk jamii lakini kwangu mimi Muislaam hilo sii jukumu na kazi ya kiimani kwa sababu Yesu kasema ya Kaizali tumwachie Kaizali.. !..
QUOTE]

Sasa mtaishije kama uwekezaji katika miradi hata ya kijamii halipewi kipaumbele? Shida nyingine ninayoona ni kwamba hivi vitabu vya dini (biblia or koran) havifanyiwi update obviously kwa sababu kila kilichoondikwa kinaaminika ni holly and will remain so. Sasa challenges za nyakati zinapoingia kunakuwa na limitation kwenye response strategy. Wakatoliki walipata shida sana na talaka maana biblia ina kasheshe zake when it comes to marriage! hata hivyo wakubwa wamesoma kwa kutumia mawani mazito na sasa talaka ipo ila process yake is no small matter!. Kama ni sababu za hivi hivi sijui pua imeelekea kushoto au mara kanenepa sana utajikuta unamrudia mke na pua hiyo hiyo kutokana na process ilivyo complex. msalaba wako watakuambia!

Anyway, goodluck na crusade and I hope mgao ujao mpo! but watch out the menu ...coming out soon! Na kama hutupata wala usijali, karibu Bungando Hospital. hatubagui sisi:)
Duh! Bugando mkuu wangu mbona mbali sisi wengine tunaishi Nyamanoro kutoka huko hadi Bugando sii mgonjwa atakuwa kesha ganda tayari!..Kitu kimoja tu kama serikali yetu ingekuwa na ujasiri wangefanya kama huku. Hospital karibu zote ni za kidini lakini wanakuwa subsidized na government na wananchi wote wanatibiwa kwa gharamiwa za serikali. Mwananchi halipi hata senti tano labda tukienda kununua dawa Pharmacy. Inawezekana sana tu ikiwa ukusanyaji wa kodi utaboreshwa kuliko hivi sasa.. hii misamaha, ubabaishaji na mirija ikizibwa fedha ipo nyingi sana kwa matumizi muhimu kama Elimu na Afya.

Sasa niende Bugando ambako serikali inamwaga mahela kisha bill ikija nadaiwa millioni nzima kwa operation ya Appendix kweli kuna kuponyesha hapo!..Kitanda kwa siku ni ghali kuliko Mwanza Hotel - Hapana mkuu wangu tunamalizwa kushoto na kulia maanake hata sisi tunaishi Ulaya imekuwa hatuwezi kujiendeleza bali kutuma fedha nyumbani kuuguza wazee wetu...

Hayo ya ndoa mkuu wangu watu wameitafsiri biblia wapendavyo na wengine hata kubadilisha maana ili mradi kukidhi matakwa yao. nakumbuka mwaka jana nikiwa Sinza nilikutana na mchungaji akinambia nipige maji tu imekubaliwa ktk biblia halafu yeye mwenyewe nikampa offer eeeh bwana wee anaondoka na beer huyo kuliko maelezo alipotoka hapo chakaliii!
 
toka lini?viongozi wamakanisa hutoa facts daima na ccm wanakwazika hapa
ingelikuwa wakristo waliisupport CDM kwa iman ya ukristo nadhani leo CDM inekuwa ikulu.

Naona kama unaota? Kwa sensus gani unayo reffer hapa? Au unaleta hadithi za kwenye vigango Jumapili?

Kama hujui tazama hapa: Tanzania

Religions:​
mainland - Christian 30%, Muslim 35%, indigenous beliefs 35%; Zanzibar - more than 99% Muslim
SOURCE: CIA WORLD FACT BOOK- TANZANIA 2011
 
Kuwapo na sheria hakuna maana kulazimishana. Kumbuka kuwa si wote wanaozijuwa hizo sheria na pande mbili zinapo hitilafiana lazima kuwe na msuluhishi ambae anakubalika kisheria na lazima awe na support ya dola husika.<br />
<br />
Hata mkicheza mpira uwanjani kuna refa, kwani wanaocheza wote hawajui sheria za mpira? ya nini wawe na refa anaekubalika kisheria?<br />
<br />
Mahakama zinakuwepo pale ambapo hakuna maelewano na kila mmoja anajiona yeye ndiye mwenye haki zaidi, hapo inatakiwa chombo &quot;neutral&quot; kinachokubalika na pande zote kuwasuluhisha. Kwa Waislaam chombo chao cha kusuluhishwa ni kadhi. Kadhi inabidi nchi ambazo hazifati sheria za kiislaam zikubali uwepo wake na kipi anachoweza kuamuwa. Kwa Tanzania, kama ulivyomsikia Kikwete, Kadhi ataruhusiwa kuamuwa kesi za mirathi, ndoa, wakfu na zinazohusiana na hizo. Zaidi ya hapo hakuna. <br />
<br />
Mimi naona &quot;something is better than nothing&quot;. Nyerere aliondoa kabisaa. Sijui kwanini? lakini my guess ni ukurusedi wake na hayo ndio kati ya mambo yanayotaka kumpatia utakatifu. Au kuna zaidi ya haya ya kuuwa Uislaam kwa makusudi kabisa yanayofikia kumpatia utakatifu? kwani kama ni nchi basi ilimshinda kuongoza na akang'atuka huku kaiacha nchi taabani hata senti za kigeni haina.<br />
<br />
Mpaka sasa ni nchi nyingi sana zinakubali makadhi kisheria kabisa. Namsifu sana Kikwete kuwafunguwa macho Waislaam na sijui kwa nini hawaoni kuwa, Serikali kuridhia wao wenyewe waendeshe mahakama yao ya kadhi ni faraja kubwa kuliko ingekuwa chini ya Serikali. Mradi Serikali imetowa Ruksa inatosha kabisa.<br />
<br />
Sidhani kama ni jambo baya kuwa &quot;independent&quot;. Kwa mtazamo wangu ni jambo jema sana kuliko kung'ang'ania kuwa chini ya Serikali. Kuwa chini ya Serikali kwa mahakama ya kadhi kutapelekea iwe kama Bakwata, chombo cha serikali na si cha Waislaam wenyewe.
<br />
<br />
 
mbona hamuulizi MIDECE walifanyiwa nini kule Mtwara?

Its easy kusimama majukwaani na kuwaambia waislama wandae MoU zao huku tunajua fika kuwa yaliowakuta MIDECE walipotaka kufanya hivyo kule Mtwara

Mkuu unaweza kufafanua zaidi hao MIDECE walifanywa nini huko Mtwara?
 
lakini si ndiyo hawahawa ndugu zetu + ccm waliokuwa wanawapinga sana CHADEMA na maandamano yao?
kweli wahenga hawakukosea waliposema ..."ukimwona mwenzako ananyolewa , wewe tia maji kichwani kwako"

Waliopinga maandamano ya CHADEMA ni BAKWATA na si SHURA YA MAIMAMU.
 
Back
Top Bottom