Hotuba ya Rais ya Kikwete kwenye baraza la Idd-Mawazo yangu

Hotuba ile ya JK juzi kule Dom ni kati hotuba nzuri kabisa alizowahi kutoa kama Rais wa NCHI, wa WATANZANIA wote. Imesimamia KATIBA ya JMT kwa masuala ya DINI na KUABUDU. Hastahili kupongezwa sana kwa hili kwani ni wajibu wake kama Rais kuilinda na kuitetea KATIBA hii. Ameapa kuifanya kazi hii.
 
Naungana na mleta mada kuwa kuna media zinapotosha ukweli. Mimi nimeisikiliza hotuba ya Kikwete na nikaisoma yote humui JF. Sijaona ni wapi JMK alipokosea. Kaongea vizuri sana, na kwa mtazamo wangu JMK kawalaumu Waislaam kwa kuwa wamechelewa kupeleka maombi yao.
 
Kama nimekupata vizuri unaposema "patriotic journalism" una maana ya media kuficha baadhi ya mambo, hata kama ni ya kweli, ili kuepusha migongano au kutokuelewana baina ya watu, jumuia au taasisi za dini. Mimi siku zote huwa ninajiuliza hivi wanasiasa na viongozi wetu wa kiserikali huwa wanafuata nini kwenye shughuli za kidini? Si katiba ya nchi hii inaongelea suala la serikali kutokuwa na dini - yaani serikali kuwa Kafiri? Je rais anapoenda kwenye mkutano wa kidini anaongea pale kama nani? je anawakilisha taasisi ya kafiri ya urais au anaenda kama muumini wa kawaida?

Je ni sawa rais kuhudhuria kwenye kikao cha kidini akiwakilisha taasisi kafiri ya uraisi (yaani ambayo haina dini)? Je ni sawa rais kwenda kwenye shughuli za kidini kama muumini wa kawaida kisha akaongelea masuala ya kiserikali yanayohusiana na mamlaka yake kama rais wakati wa kutoa hotuba?

Nadhani tatizo la msingi hapa siyo vyombo vya habari bali ni la wanasiasa kutumia majukwaa ya kidini kuelezea sera zao kwa minajili ya kupata uungwaji mkono wa waumini wa dini husika. Rais ni kiongozi wa jamii (public figure) na chochote anachoongea ni lazima kitaandikwa na pia kutafsiriwa kulingana na uelewa wa mwandishi. Nadhani haitakuwa sahihi kuwaacha wanasiasa waongee wanachotaka kisha kuwatarajia waandishi watumie busara ya kuchambua lipi kkatika yale aliyoongea rais lina maslahi ya umma ili kuliripoti. Busara hii inatakiwa ianzie kwa viongozi kwani ndio waliopewa dhamana ya kuongoza wananchi.

Kimsingi sipingi rais kwenda kwenye hafla ya dini yoyote ile. Ila inapotokea akaalikwa kwenda kwenye majukwaa ya kidini ni vyema kwa kutumia busara ya kawaida tu akajikita zaidi kwenye masuala ya kiroho pale anapopewa fursa kuongea. Ninachopinga ni raisi kutumia jukwaa la kidini kuongelea masuala ya kisiasa, kiserikali au ya kitaifa utadhani yuko kwenye mkutano wa kampeni ya kisiasa.


hapo kwenye bold......je kama hao viongozi wa dini ndiyo walianza kutumia jukwaa la dini kuongelea mambo ya kiserikali yaliyohitaji majibu palepale wewe unataka JK angefanyaje?
 
Hapo tatizo sio media bali ni uelewa wa wahusika wenyewe kwani kama ni hotuba ya rais waliisikia wenyewe kwa masikio yao kwani ilisikika live hivyo maamuzi yoyote yatakayotolewa na waislamu yatakuwa ni maamuzi yanayotakana na utashi wao na si kupotoshwa na media.Acha waandamane kwani ni haki yao kikatiba na pia ni njia nzuri ya kufikisha ujumbe wao kwa rais.
 
Hapo tatizo sio media bali ni uelewa wa wahusika wenyewe kwani kama ni hotuba ya rais waliisikia wenyewe kwa masikio yao kwani ilisikika live hivyo maamuzi yoyote yatakayotolewa na waislamu yatakuwa ni maamuzi yanayotakana na utashi wao na si kupotoshwa na media.Acha waandamane kwani ni haki yao kikatiba na pia ni njia nzuri ya kufikisha ujumbe wao kwa rais.
lakini si ndiyo hawahawa ndugu zetu + ccm waliokuwa wanawapinga sana CHADEMA na maandamano yao?
kweli wahenga hawakukosea waliposema ..."ukimwona mwenzako ananyolewa , wewe tia maji kichwani kwako"
 







MEDIA MNATAKA KUTUPELEKA RWANDA?

Tulichukua Jukumu sote hapa kuifuatilia Hotuba hiyo na Tukitahadharisha wiki moja kabla ya Hotuba hiyo kuwa utakuwa Uwanja wa kuvurumisha turufu nzito za kisiasa na Hoja Tete. Kama tulivyotabiri hicho ndicho kilichotokea.

Toka Hotuba hiyo Media zinaendelea kuwachanganya Watanzania kwa kutoa taarifa zenye mlengo wa kuchafua Hotuba hiyo nzuri ya Rais kwa kuwatia hasira Waislam kwa habari ambazo hazina haja ya kuandikwa kwa sasa kutokana na suala hili lilivyoshughulikiwa kwa umakini na uwazi wa kipekee.

Shura ya Maimam leo inatangaza maandamano Nchi Nzima hii ni Hatari na Media inaandika habari hii. Mnaziuua habari ngapi huko kwenye MEDIA Zenu hii kwa nini mnaandika?

Jana tumejadili hapa japo kwa uchache saana miiko ya Taaluma hii, hivi patriotic journalism haiwezekani...MEDIA Mnatishia amani kaaeni chini mtafakari hili

ADIOS

Iwapo wataruhusiwa Waache waandamane, ni haki yao kikatiba, Ingawa ni lazima serikali ikumbuke kuwa hii ita- set a kind of precedent kwa dini nyingine ambapo zaweza kuandamana ku express displeasure yao kwa serikali iwapo zitajisikia.

Kuhusu suala la vita kila mwili wa Binadamu umeumbwa kwa damu na nyama kwa hiyo lisitumike na dini moja kutishia watu wengine/ dini nyingine maana vita ikianza majibu sahihi kuhusu mshindi yatajulikana uwanja wa vita.

Ukipenda waulize warundi na wanyarwanda maana ya vita, hata hivyo tunamwamini Mungu vita haitatokea Tanzania, twaweza kupishana kimawazo lakini mwisho wa siku waislamu, wakristo na dini nyingine tutaendelea kuishi kwa amani.

Amen.
 
Mimi nashangaa sana waislamu wanapodai sheria wasizozipenda. kama kweli muslims wanataka kutumia sheria zao za kidini hasa kwenye masuala ya mirathi me nafikiri itakuwa ni rahisi hata sasa wakiamua kuitumia pasipokuwa na mahakama ya kadhi coz wana viongozi wa dini wanaozifahamu sheria hizo na kama kweli wanazipenda sheria hizo ni vyema wakazitekeleza pasipo na haja ya kulazimishana kwa kutumia mahakama.
 
hapo hamna lolote mashehe ubwabwa wanatapatapa tu.wakipewa pilau na ndizi watatulia tu hao njaa zinawasumbua na umbumbumbu
 
Waislamu kama walivyo Wakiristo na madhehebu na dini nyingine ni lazima watofautiane. Muhimu ni namna ya kuzidhibiti, kuziongoza na kuzimudu tofauti hizi. Rais wetu kama kawaida yake amechelewa mno kulitolea ufafanuzi suala hili la kadhi, shule za dini mbalimbali zilizotaifishwa enzi za Mwalimu na baadhi zikarudishwa, akaacha watu wayazungumze wanavyotaka.

Kwa wenye uwezo mdogo wa kufikiri inakuwa vigumu kumwelewa kwa sasa. Wakiambiwa waandamane wataandamana kweli hata kama maandamano yenyewe hayatabadili kitu.
 
Hotuba ile ya JK juzi kule Dom ni kati hotuba nzuri kabisa alizowahi kutoa kama Rais wa NCHI, wa WATANZANIA wote. Imesimamia KATIBA ya JMT kwa masuala ya DINI na KUABUDU. Hastahili kupongezwa sana kwa hili kwani ni wajibu wake kama Rais kuilinda na kuitetea KATIBA hii. Ameapa kuifanya kazi hii.

Msitudanganye na kumsifia rais kuwa katoa hotuba nzuri,mlishazoea kudanganya kwenye hotuba zake na kuongelea mambo juu juu sasa rais kasema ukweli mtupu na kwa kujiamini ndipo mnasema nzuri.

Kutoka na ukweli aliousema utaona mlipuko wa mambo wameanza waislamu,hiki ndicho raisi asichotaka kuwagawa wananchi wake kwa kuwaambia ukwelh.ndo mana huwa hautubii.
 
Tatizo ni kwamba, wasilamu walitegemea sana JK awanyenyekee kwa sababu na yeye ni Muislamu, si ndio walisema tunamchangua muislam mwenzetu. Nani asiyejua hilo na baadhi ya wenye akili walipinga kuwa haya ni mambo ya siasa na yataishia kisiasa tu....Sasa juzi kawapa ukweli....

Nimeipenda hotuba yake kuhusu mahakama ya kadhi na ujumbe wangu kwa ndugu zangu waislam, wasijipendekeze kwa mtu kwa sababu ni muisalmu mwenzao huku the rest tukiitwa makafiri;

pili; kama kweli wanahitaji hio mahakama si waanzishe kwa gharama zao? Mbona madrasa hazijengwi na serikali? Au ndio ule utegemezi wa kiislamu? Yaani hawafanyi kazi, wao wanasubiri ijumaa wande kwene misikiti halafu wale wenye pesa wakitoka kuswali wawape wale maskini vishilingi....

No, tunahitaji kuona waislamu wenzetu na ndugu zetu wabadilishe mtazamo toka kwenye kulalamika na uetegemezi usio wa lazima na kuanza mambo yao wenyewe.
 
GR, wamesema wanaandamana kwa sababu zipi?

Hawakubaliani na Msimamo wa JK Mkuu...Ukisoma Al Noor ya leo ya septemba 2 - 8 inasomeka hivi JK AHALALISHA DHULUMA, UBAGUZI: Apuuza ya Waislam aegemea ya maoni ya Maaskofu
 
Mkodoleaji: Nimeisoma ile hotuba sikuona chochote kinachonishawishi kuwa JMK amebadili hulka. Nimesema siku zote ni kiongozi anayetaka kupendwa na kila mtu, hiyo si sifa ya kiongozi mzuri.
Suala la mhakama linadhihirisha jinsi gani Rais wetu anacheza na akili za watu kiujanja ujanja. Ni mfano mzuri wa undumila kuwili au kigeu geu chake. Hoja hiyo yeye aliitolea ahadi na kuiweka katika Ilani ya CCM ya 2005. Alipobanwa akasema ilikuwepo sera wakati wa BWM. Alipobanwa zaidi akasema hiyo ni sera ya chama na chama kinaifanyia kazi. Yaani sera aliyoiuza kwa waislam bila kuwa na majibu yatokanayo.

Ndivyo ilivyotokea kwa JMK aliposema Dowans watalipwa ndani ya CC, akaenda ubungo plaza na kusema suala hilo linamkera/
Ndiye yule yule aliyesema mafisadi wanamkera sana, akenda rombo na kusema Mramba ni shoka la zamani lenye makali.
Akasema Jairo hana makosa, wabunge walipohoji akatoa likizo kwa mtu asiye na makosa. Orodha inaendelea.
Huyu ndiye JMK halisi na kama yupo anayechukulia kauli zake kwa umakini ajaue ameingizwa chaka. Sikuona jipya katika ile hotuba inayosifiwa!!! Kamundu kuna mambo mawili yanayojitokeza katika hoja zako na nina hakika sehemu kubwa ya jamii inaelewa kama unavyoelewa.
Pili, kuna tatizo la Waislam kutoieleza vema dhana ya mahakama ya kadhi na kwahivyo kutafsiriwa kama alivyofanya kamundu.
Tatu, inawezekana watu wanaelewa lakini wanataka kufanya upotoshaji ambao mimi sikubaliani nao.

Mahakama za kadhi zilikuwepo hapa Tanzania na sheria za nchi zilikuwepo tena wakati wa ukoloni na sio kama ilivyo sasa.
Nchi za jirani zina mahakama za kadhi n.k kwahiyo sio jambo linaloweza kufanya watu waamini tofauti na ilivyo isipokuwa wasiojishughilisha kutaka kufahamu.

Sheria ya ndoa ya mwaka 1973? inatambua ndoa za aina tatu, za kimila, kidini na serikali. Sheria hizo zimetokana na katiba ya nchi, kwahiyo suala la kuabudu linaposemwa lipo nje ya katiba lizungumzwe kwa tahadhari kwasababu serikali haina dini lakini inatambua uwepo wa dini kikatiba.

Suala la kazi limeelezwa kuwa ni kwa mirathi, ndoa na wakfu. Sheria ya ndoa ya serikali inatambua uwepo wa ndoa za kidini na wala sheria hiyo haielekezi ndoa hizo ziweje na kwa utaratibu gani. Hilo ni jukumu la dini husika. Sheria ya ndoa ya serikali inasimamiwa na serikali lakini inakinzana na sheria za dini kama ya kiislam katika baadhi ya mambo. Mfano, sheria inasema ndoa itafungwa bomani na kiongozi hata kama si wa dini ya wanandoa. Sheria za dini kama za kikristo na Kiislam zinautaratibu wa watu wanaoweza kufungisha.

Sheria ya ndoa ya serikali inasema likitokea la kutokea mirathi itagawanywa kwa formula ya serikali. Sheria kama za kiislamu zina percentage. Kwahiyo kuwa na sheria moja ni kukiuka vifungu vya dini, ndiyo maana serikali ikatoa fursa ya kutambua ndoa za dini.
Hapa ndipo Waislam wanasema wangependa kuwa na sheria zinazolingana na maadili ya dini yao katika ndoa,mirathi na wakfu.

Labda nitoe mfano wa kufikirika. Ikitokea kuwepo sheria ya serikali inayolazimisha watu kuoa au kuolewa ili kupunguza maambukizi ya ukimwi, waislam hawatakuwa na lalamiko kwasababu itakuwa inakwenda sambamba na dini yao.
Wakristo watakuwa na la kusema kwasababu wapo mapadre na masista wasioruhusiwa kuoa au kuolewa kwa mujibu wa dini yao.Je ,wao wakiomba utaratibu ili kutobanwa na sheria ya serikali katika imani yao watakuwa wamefanya kosa gani?

Sidhani kuwa waislam wameomba sheria za makosa ya jinai yaingizwe katika sheria za nchi, na kwa vile ipo nafasi ya wao kuwa na utaratibu wao kuhusu mirathi, ndoa na wakfu waliopewa na katiba (sheria ya ndoa kutambua ndoa za kidini) sioni kuna tatizo gani wao kuruhusiwa kuwa na utaratibu wao.

Ikumbukwe kuwa sheria ya kadhi haimhusu mtu asiye mwislam na hata mwislam haimfungi kuifuata.
Hivi leo kuna waislam wana ndoa za bomani. Hiyo ni hiari yao.
Wanandoa waliofunga ndoa kiislam na wakakubaliana kutofuata sheria za kadhi bali za serikali hawafungwi na chochote kile, kama vile mwislam anayeona ni vema kuwa na ndoa ya bomani. Hiyo ni yeye na imani yake na si kadhi wala serikali inaweza kumlazimisha wapi aegemee ili mradi tu yawepo makubaliano ya awali na ridhaa kati ya wanandoa kuhusu mustakabali wa ndoa zao.

Mwisho: Swali kubwa hapa ni je utaratibu wa kuendesha mahakama ya kadhi uweeje? Ugharamiwe na serikali au wao wenyewe? Hili ndilo swali la msingi na lenye utata tunaouona.

Jamii yote inakubaliana kuhusu dhana ya mahakama ya kadhi. Kwa bahati mbaya au makusudi kumekuwa na upotoshaji wa dhana hiyo kwa kuweka mambo yasiyohusu kabisa kama vile inaposemwa kuridhia utaratibu huo kutawalazimisha watu wote waufuate. Si kweli, badala yake mahakama ya kadhi itasaidia kutolifanya suala hilo kitaifa bali kiimani.

Kuna upotoshaji kuwa waislam watalazimishwa kwenda mahakama ya kadhi, sio kweli. Kuna upotoshaji kuwa watazuiliwa kufuata taratibu za nchi, sio kweli. Kuna upotoshaji kuwa ndoa,mirathi na wakfu ni makosa ya jinai, sio kweli.

Ninawaomba wanaJF kujaribu kuielewa issue vizuri kabla ya kuitolea hukumu. Tatizo letu ni kuwa ukiwa mkristo au mwislam unadhani kuwa una haki zaidi kuliko pagani. Baya zaidi hatutaki kujifunza na kuelewa mambo ya upande mwingine. Tunadhani ukisoma utaratibu wa wapagani(kama upo) basi itakuwa dhambi. Tunadhani ukisoma biblia au korani au sheria na taratibu za dini nyingine utakuwa umekiuka misingi ya dini.

Wenye ueledi huwa ni wasomi wazuri sana wa canon law au sharia law hata kama haziwahusu. Jamii yetu itakuwa na utangamo zaidi tukiacha kusikiliza hadithi au mahubiri au mawaidha ya watu bila kuyafanyia tafiti zetu eti kwa vile ni viongozi wa dini. Wapo wenye agenda zao na hao ndio hawakawii kulisha sumu jamii. Let us exercise the culture of learning and being inquisitive in all matters in this world.

Tutumie technology kujifunza mambo na sio kusikia na kuamini tu. Tusome vitabu, majarida tufuatilie mijadala ili kuongeza upeo wetu wa kuielewa dunia bila kujifunga katika kasehemu kamoja tu, tukisubiri fulani asome halafu aje kutuambia, hiyo ndiyo chanzo cha misconception.

Utawezaje ku criticise freemason kama huna idea ya Uislam, ukristo, atheist na upagan na vinavyoendelea within japo kidogo!!!


haya sasa tujadili, ni sawa kodi za watanzania zitumike kulipa mishahara ya mahakimu wa mahakama ya kadhi?
 
Kama nimekupata vizuri unaposema "patriotic journalism" una maana ya media kuficha baadhi ya mambo, hata kama ni ya kweli, ili kuepusha migongano au kutokuelewana baina ya watu, jumuia au taasisi za dini. Mimi siku zote huwa ninajiuliza hivi wanasiasa na viongozi wetu wa kiserikali huwa wanafuata nini kwenye shughuli za kidini? Si katiba ya nchi hii inaongelea suala la serikali kutokuwa na dini - yaani serikali kuwa Kafiri? Je rais anapoenda kwenye mkutano wa kidini anaongea pale kama nani? je anawakilisha taasisi ya kafiri ya urais au anaenda kama muumini wa kawaida?

Je ni sawa rais kuhudhuria kwenye kikao cha kidini akiwakilisha taasisi kafiri ya uraisi (yaani ambayo haina dini)? Je ni sawa rais kwenda kwenye shughuli za kidini kama muumini wa kawaida kisha akaongelea masuala ya kiserikali yanayohusiana na mamlaka yake kama rais wakati wa kutoa hotuba?

Nadhani tatizo la msingi hapa siyo vyombo vya habari bali ni la wanasiasa kutumia majukwaa ya kidini kuelezea sera zao kwa minajili ya kupata uungwaji mkono wa waumini wa dini husika. Rais ni kiongozi wa jamii (public figure) na chochote anachoongea ni lazima kitaandikwa na pia kutafsiriwa kulingana na uelewa wa mwandishi. Nadhani haitakuwa sahihi kuwaacha wanasiasa waongee wanachotaka kisha kuwatarajia waandishi watumie busara ya kuchambua lipi kkatika yale aliyoongea rais lina maslahi ya umma ili kuliripoti. Busara hii inatakiwa ianzie kwa viongozi kwani ndio waliopewa dhamana ya kuongoza wananchi.

Kimsingi sipingi rais kwenda kwenye hafla ya dini yoyote ile. Ila inapotokea akaalikwa kwenda kwenye majukwaa ya kidini ni vyema kwa kutumia busara ya kawaida tu akajikita zaidi kwenye masuala ya kiroho pale anapopewa fursa kuongea. Ninachopinga ni raisi kutumia jukwaa la kidini kuongelea masuala ya kisiasa, kiserikali au ya kitaifa utadhani yuko kwenye mkutano wa kampeni ya kisiasa.


Hili linamgarimu JK kwa sababu alitoa ahadi ambayo ilikua ni moja ya sera aliyoitoa msikitini kwamba atafanikisha mahakama ya kadhi alipokua anaomba kura kipindi cha uchaguzi, Nilazima JK aongelee siasa kwenye jukwaa la msikiti kwa sababu alijaribu ku-buy trust kwa waislam ili wampe kura. Jk kama mgeni rasmi hapo msikitini alikua anajibu risala iliyotolewa na viongozi wa kiislam ambao waliulizia ahadi yao ya KADHI waliyopewa na J.K ili wampe kura. Kila siku TZ tunapiga kelele kupinga UDINI ila baada ya hotuba hii ya J.K mimi binafsi kwa akili yangu bila kusukumwa na hisia yoyote ya kichama au dini nimen'gamua kuwa aliyeanzisha na kupalilia Udini hapa TZ ni J.K kwa kutoa ahadi ya kidini kama sera ya CCM ili kupata KURA za watu wa dini husika.
Hali ni tete, sera ya CCM iliyotolewa kwa waislam leo hii inachochea udini katika Tanzania ya leo.Je hii ndo Tanzania tunayoitaka???
 
Back
Top Bottom