Hotuba ya Rais ya Kikwete kwenye baraza la Idd-Mawazo yangu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hotuba ya Rais ya Kikwete kwenye baraza la Idd-Mawazo yangu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mkodoleaji, Sep 1, 2011.

 1. M

  Mkodoleaji JF-Expert Member

  #1
  Sep 1, 2011
  Joined: Apr 27, 2008
  Messages: 454
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimesoma kwenye magazeti na kusikiliza kwenye vyombo vya habari. Kwa kweli wengi wamemsifia kwamba ametoa hotuba nzuri. Lakini mimi kwa kweli nimekuwa na mtazamo tofauti. Naomba niseme wazi kwamba Raisi Kikwete amekuwa mean with the truth kwenye hii hotuba yake. Kwanza kwenye suala la Mahakama ya Kadhi, ni yeye na CCM yake ambao waliwaahidi waislamu mwaka 2005 kuwa watalipatia ufumbuzi.

  Sasa kwa waislamu wengi ufumbuzi ilikuwa serikali itaanzisha hiyo Mahakama. Lakini cha ajabu nadhani mwaka 2008, Kikwete huyo huyo mbele ya Maaskofu wa KKKT alikanusha kuhusika na suala la mahakama ya kadhi. Akasema lilianzishwa na Mrema na Sheikh Ramia. Kwa maana nyingine yeye asiulizwe.

  Leo anasema kuwa ni suala la waislamu wenyewe lakini hapo hapo anakiri kuwa Waziri Mkuu anaratibu. Waziri Mkuu ataratibu vipi suala la ibada. Kwangu mimi nadhani Kikwete angekiri walipoteleza na kueleza kuwa walifanya makosa kuingiza suala la dini kwenye siasa.

  Suala la pili ni kuhusu suala la MOU ambapo waislamu wamelalamika kuwa wakristo wanapewa fursa zaidi. Kikwete amesema kwa sababu wao hawaombi. Hapa kwa kweli panatia shaka. Kikwete kama mara mbili akiwa kwenye mikutano na viongozi wakristo alinukuliwa akitoa takwimu kuonyesha pesa ambazo taasisi za kikristo wamepata kutoka serikalini.

  Hivi alishindwa nini kutoa takwimu kuonyesha ni kiasi gani taasisi za kiislamu zinapokea kutoa serikalini? Kwa nini hakutoa hata mfano kuwa Muslim University kilitolewa na serikali? Je pia alishindwa kuonyesha kuwa hizo shule za makanisa kama zinazuia kusoma watu wa dini nyingine? Na pia kwa sababu alikuwa Waziri wakati Mzee Mwinyi atakuwa anajua kwanini MOU ilisainiwa, je alishindwa nini kutoa hiyo institutional memory ili kuondoa upotoshaji unaoendelea.

  Alichozalisha hapa ni kuonyesha kuwa wakristu wamekuwa wakipendelewa kwa sababu wanaomba na waislamu wamenyimwa kwa sababu hawaombi kitu ambacho nadhani si sahihi. Kama kwenye wamenyimwa serikali haitakiwi kusubiri hadi kuombwa, kwani Nyerere aliombwa na nani kutaifisha shule?

  Kwa kweli kwangu nadhani ni hotuba inayopalilia udini badala ya kuumaliza.

  NAWASILISHA
   
 2. p

  politiki JF-Expert Member

  #2
  Sep 2, 2011
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  Uliyoyasema ni kweli i wish watu wengi wangekuwa wanajiuliza maswali mengi kama wewe, ukijiuliza maswali majibu yako utakayoyapata mwishoni ni kuwa JK ni kiongozi mmoja mnafiki sana kwa mfano anachokifanya hivi sasa baada ya kugombana na baadhi ya madheebu ya kikristo sasa anajaribu ku balance ili kuwaonyesha viongozi wa kikristo kuwa hana upendeleo kwa maana ya kuegemea uislamu.

  Mamabo yote ambayo ameyazungumza angeweza kuzungumza mwaka 2008 au 2009 lakini alikuwa anavizia uchaguzi upite apate kura zao halafu awamwage waislamu walishaelezwa kabla ya uchaguzi kwamba kigugumizi cha jk kuzungumzia swala la kadhi kilikuwa na mshindo ndani yake lakini wengi hawakusikia.

  Kuhusu kauli yake ya kuwaambia viongozi walikuwa wapi siku zote mbona wamechelewa huo ni unafiki mwingine kwani yeye amekuwa akikutana na viongozi wa bakwata mara kwa mara kwanini asiwaulize kuhusu swala hilo miaka yote hiyo mpaka leo eti anatuambia kuwa anashangaa kwanini tumechelewa hivyo. kwanini ukuuliza swala hilo ulipokuwa ukikutana nao ikulu miaka yote hii. JK anajaribu kubalance mapenzi pande zote mbili lakini kwa kuwa hatumii principal bali unafiki mambo haya yatamtokea puani.
   
 3. EasyFit

  EasyFit JF-Expert Member

  #3
  Sep 2, 2011
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 1,244
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  MAKANISA nchini yamesema hotuba ya Rais Jakaya Kikwete aliyotoa juzi katika Baraza la Idd ni nzito na kwamba, kama angekuwa anatoa hotuba kama hizo, matatizo mengi ya nchi yangekuwa yamepata ufumbuzi.Katika baraza hilo pamoja na mambo mengine, Rais Kikwete akijibu risala ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania, (Bakwata) alizungumzia mambo muhimu kuhusu taifa ikiwa ni pamoja na Mahakama ya Kadhi, viongozi wa dini na biashara ya dawa za kulevya na udini katika siasa.

  Jana, kwa nyakati tofauti wakizungumzia hotuba hiyo baadhi ya maaskofu akiwemo Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC), Yuda Thedeus Ruwai’chi, alimpongeza mkuu huyo wa nchi kwa hotuba hiyo nzito.

  Ruwai'chi
  Ruwai'chi ambaye pia ni Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Mwanza alisema: “Kauli kama za jana (juzi) zingekuwa zinatolewa mara kwa mara, masuala mengi ya nchi yangeshapata ufumbuzi, nimesoma hotuba hiyo kwenye magazeti, lakini nitafurahi sana nitakapopata hotuba yenyewe niisome kwa mtiririko wake”.

  Mahakama ya Kadhi
  Kuhusu suala la Mahakama ya Kadhi, Askofu Ruwai’chi aliunga mkono kauli ya Rais Kikwete kuhusu waumini hao kuanzisha mahakama hiyo wenyewe na kusisitiza kuwa Waislamu ni watu wazima wasiotaka kubebwa na mtu yeyote ili kufanikisha mambo yao.

  Askofu Ruwai'ch alifafanua: “Wakianzisha wenyewe Mahakama ya Kadhi hakuna anayewazuia..., kwa sababu ni dini isiyohitaji kubebwa, waanzishe chombo chao kisicho cha Serikali, wakiendeshe kwa fedha zao wenyewe”.
  Hata hivyo, alisema, bado Serikali inaonekana kuwa na kigugumizi juu ya suala la mahakama hiyo, ndiyo maana kuna kauli zinazogongana.

  Rais huyo wa Tec badala yake alisema, “Mara anasema suala lipo kwa Waziri Mkuu, mara waanzishe wenyewe..., wasijing’ate, wawaambie tu kuwa waanzishe mahakama yao kwa fedha zao na waiendeshe wenyewe”.

  Utaifishaji wa shule
  Akizungumzia madai ya kurejeshwa kwa shule zilizokuwa zikimilikiwa na taasisi za dini na baadaye kutaifishwa wakati wa Serikali ya awamu ya kwanza chini ya uongozi wa Baba wa Taifa, Julius Nyerere, Ruwai’chi alisema ingekuwa ni kulalamika, kanisa lingekuwa la kwanza kwa sababu mamia ya shule zake zilitaifishwa.
  “Lakini kanisa tumetulia na tumejenga shule zetu nyingine ambazo zinatoa huduma kwa Watanzania bila ubaguzi wowote..., tujipange tuanzishe shule na tuziendeshe,” alisema Askofu Ruwai’chi.

  Dawa za kulevya
  Ruwai’chi alisema Serikali ichukue hatua za kuwakamata watu wanaojihusisha na biashara hiyo bila kujali kama ni viongozi wa dini wala siasa.

  “Serikali itumie vyombo vyake kuhakikisha wote wanaojishughulisha na biashara hii wanakamatwa, siyo kuibua hoja ambayo itajificha nyuma yake na kuacha kushughulikia mambo muhimu yanayowakabili wananchi,” alisema Ruwai’chi.
  Kuhusu udini katika siasa, Ruwai’chi alisema kwamba, suala hilo lilienezwa na baadhi ya wanasiasa katika uchaguzi uliopita na sasa limedakwa na baadhi ya viongozi wa dini na baadhi ya vituo vya redio.

  Ruwai'ch alionya akisema: “Huku ni kucheza na moto, ni vyema Serikali ikahakikisha kuwa yeyote anayejaribu kuleta udini wa namna yoyote, anashughulikiwa mara moja, hili siyo suala la kucheza nalo hata kidogo”.

  CCT nayo yakunwa
  Kwa upande wa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), Askofu Peter Kitula, alisema hotuba ya Rais Kikwete ni nzuri na imeweza kutoa ufafanuzi wa mambo mengi yaliyokuwa yakiikabili nchi.

  Askofu Kitula ambaye pia ni Askofu wa Kanisa la African Inland (AICT),Dayosisi ya Mara na Ukerewe alifafanua: “Hotuba ni nzuri, haikuegemea popote..., imetoa ufafanuzi kwa mambo mengi ya nchi na msimamo wa Serikali tumeuona”.
  Kuhusu suala la Mahakama ya Kadhi, naye alisisitiza kwamba, inatakiwa ianzishwe na Waislamu wenyewe na uendeshwaji wake pia ufanywe na dini husika na isiwe na kufanya ujanja wa kuianzisha na baadaye Serikali ikajiingiza katika kuiendesha.

  Akizungumzia kurejeshwa shule zilizotaifishwa, alisema jambo la kufanya ni Serikali kusaidia katika uendeshaji wa shule zote binafsi na siyo kuzirudisha ambazo zilitaifishwa.Kuhusu dawa za kulevya, alisema ni vyema Serikali ikachukua hatua kwa mujibu wa sheria ama kutaja majina ya wahusika hadharani badala ya kutoa maelezo ya jumla.

  Mbatia
  Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia, amekitaka CCM kuwaomba radhi Watanzania kutokana na kile alichokiita kufanya ulaghai wa kisiasa kwa kuweka ahadi hewa katika uchaguzi wa mwaka 2005/2010.
  Mbatia alifafanua kwamba, hatua ya CCM kuwageuka Waislamu kuhusu kuanzishwa Mahakama ya Kadhi ni fundisho kwa Watanzania kupima ahadi za vyama katika uchaguzi kama zinatekelezeka.

  Alisema CCM katika baadhi ya ahadi zake za uchaguzi ilifanya ulaghai kwa Watanzania kwani hazitekelezeki.
  Kwa mujibu wa Mbatia, umefika wakati sasa mambo ya kitaalamu yakaachwa kuingizwa siasa akitoa mfano wa mahakama hiyo ya Waislamu kwamba ni jambo la wataalamu wa sheria na si wanasiasa.

  Source: Mwananchi
   
 4. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #4
  Sep 2, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Hapaswi kuweka reasonability kubwa sana kiasi hicho kwa wanasiasa wa Kitanzania ambao wao siasa ni mchezo mchafu na sehemu ya kuwahadaa wananchni.
   
 5. Shinto

  Shinto JF-Expert Member

  #5
  Sep 2, 2011
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 1,781
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Niliwahi kuandika humu hapo nyuma lakini watu wakajitia uziwi kama kawaida! CCM haijawahi kuwa pamoja na maslahi ya Waislamu tangu ianzishwe na hilo halitegemei kubadilika karibuni. Makanisakwa support CHADEMA kwenye uchaguzi 2010, they were only making a statement!

  Losers kwenye hili ni makundi haya mawili: WAISLAMU sasa hawana pa kukimbilia kwa maana wametumiwa na JK kwa malengo ya kisiasa na sasa hawahitaji tena!

  CHADEMA nao ni losers wengine katika hili., ni wazi Waislamu wataanza tena kuichukia CCM na jamii ya kikristo itarudi kuisupport CCM kimaslahi kama zamani! Ile support CDM ilikuwa ina pata toka jamii ya kiktisto ndio mwisho wake huo! 2015 political landscape itakuwa imebadilika sana, just wait and see!
   
 6. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #6
  Sep 2, 2011
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,109
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Hata kama hatukubaliani na Kikwete kuna ukweli mwingi kuhusu aliyosema.

  1. Kadhi ni swala la waislamu pekee na watu wa dini nyingine haliwahusu. Kama waislamu wanaamua kufanya mahakama yao basi ni lazima wakubali wenyewe na isiwe sheria za nchi kwani nchi yetu ina dini mbalimbali. Vilevile Tanzania kuna uhuru wa kidini lakini tunafata katiba kwa mahakama hivyo kama sheria za kidini zibakie kwenye misikiti.

  Vilevile hakuna Mtanzania anatakiwa kulazimishwa kufuata hizo sheria hata kama ni mwislamu ni lazima akubali kutumia hizo mahakama za dini. Mfano mimi ni mkatoliki lakini hatuwezi kuanzisha mahakama yakufuata sheria ya kikatoliki halafu ikawa ya nchi nzima kwani Tanzania ni nchi yenye dini tofauti.

  Kitu ambacho kila mtu anaweza kufuata ni mahakama za sasa za chini ya katiba lakini dini ziwe za dini. Wakatoliki wa wakistro kwa mfano wanaenda kujadili na mapadre na wachungaji matatitizo ya ndoa lakini ni kwa hiani yao na serikali haihusiki kwa hilo. Vilevile kama mtu anaona hatendewi haki anaweza kwenda kwenye mahakama ya kawaida.

  Ndoa vilevile ni mfano mwingine zinafungwa makanisani na misikitini lakini vilevile unaweza kufuta sheria na kufunga ndoa kiserikali na kufuata taratibu za kisheria na katiba.

  2. Kuhusu elimu sijui kama Waislaamu wananyimwa na vilevile ni lazima tuwe wakweli ili uweze kupata hii misaada ya vyuo na shule ni lazima ufikie kiwango fulani cha standard. Mimi siamini kama Agha Khan university itanyimwa pesa kama wakianzisha chuo! kwani ni chombo cha dini ya kiislam lakini wana fiki kiwango cha juu kabisa kwenye shule na hata chuo watakachofungua.

  Lakini ukweli ni kwamba kuna shule nyingi sana za kiislaamu ambazo zinafelisha watoto kila siku! na bado ziko wazi wakati huohuo Agha Khan watu wanagombea kuingia bila kujali dini kwasababu wana kiwango cha juu.

  Vyuo vyote vya dini ni lazima vipewe pesa au grants kutokana na kufia kiwango kilichowekwa kwani bila kufanya hivyo Tanzania itakuwa inarudisha nyuma watoto wetu. Hakuna sababu yeyote ya mtoto yeyote Tanzania kupewa elimu duni! bila kujali dini

  Ndugu zetu Waislaamu mimi ningeshauri waache kulaumu kila jambo na kusimama pamoja kuimarisha elimu. Kuna shule nyingi tu za kiislaamu za sekondari zinazofanya vibaya sana lakini sijawahi kusikia malalamiko wakati shule zinatoa Div 4 na 0 kila siku!

  Bado tunaruhusu watoto waende kwenye shule ambazo zinafelisha kila mwaka nenda rudi!.Agha Khan ni mfano mzuri wa shule iliyoanzishwa kwa dini lakini tunaona watu wanavyokimbilia kuanzia shule, hospitali na hata ukumbi wa diamond!.
   
 7. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #7
  Sep 2, 2011
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,109
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Nyerere alitaifisha shule kwa sababu Watanzania wengi hasa waislaamu walikuwa hawatendewi haki. Miaka ya 1950 na 1960 ulikuwa ukienda shule kutoka Primary kwenda secondary unapangiwa kutokana na mathehebu mfano wakina SUmay na Lowasa walienda Ilboru kwa sababu ilikuwa ya walutheri na kuna walioenda shule ya Umbwe kama Sokoine, Lemomo n.k waliokuwa wakatoliki.

  Je waislaamu walienda wapi? walikuwa na shule chache sana za kwenda na ndiyo maana nyerere alitaifisha baadhi ya shule kama Kawawa, Ilboru, Umbwe n.k na zikaanza kuchukuwa watu wa dini zote bila kujali dini. Vilevile kupunguza udini akaanzisha utaratibu wa kutumia namba kwenye mitihani.
   
 8. M

  Mkandara Verified User

  #8
  Sep 2, 2011
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Kamundu, mkuu wangu kama huelewi kitu ni bora ukae kimya itakusaidia sana kusilikiza...

  1. Huwezi kuchukua ya Uislaam ukayaweka sawa na wakristo, haiwezekani na ndio maaana tunaamini dini hizi tofauti. Kwanza kubali kuna tofauti baina ya dini hizi hivyo huwezi kulazimisha haramu ya upande mmoja kuwa halali pande zote au kinyume chake..Wewe huna sababu ya kua na mahakama ya kadhi kwa sababu kesi nyingi za madai zinaamuliwa kutokana na sheria tangulizi za kikristu (canon law) na zimefanyiwa marekebisho ya hapa na pale lakini bado utaona mahakimu wetu wakivaa wig na majoho ya sawa na yale ya waasisi wao.

  2. Huko Marekani kuna shule za watu weusi zinatoa matokeo mabaya sana ukilinganisha na zile zilizopo sehemu ya wazungu na sababu inajulikana wazi..watu weusi ni kama second citizen na wazungu wengi hawaelewi kabisa weusi wanalalamika nini wakati huo huo wakiwaita with a - N word!..

  Unachozungumza hapa huna tofauti kabisa na kaburu wa Zimbabwe au South Afrika na nasikitika sana kuona mtu kama wewe umeingia ktk kuamini ukweli unaotanguliwa na tatizo kubwa la matabaka ambalo limejengwa na hawa viongozi wetu mara tu baada ya Nyerere kujiuzulu.. Kama unaamini Tanzania ni nchi yetu sote inakuwaje wewe unasema Waislaam wako hivi ama vile kama sii kujiona wewe ni mbora na tofauti na hao Waislaam?..

  Maadam tumeona kuna tatizo katika baadhi ya shule zetu ni muhimu zitafutiwe ufumbuzi wa kitaifa kama tunavyoona shule za kata huwezi kusema hizo ni shule za maskini walalahoi - so it's their problem!
   
 9. N

  Ngereja JF-Expert Member

  #9
  Sep 2, 2011
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 796
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Nadhana JK kusema kwamba waziri mkuu anaratibu suala la mahakama ya kadhi haina maana kwamba ni serikali ndiyo inaanzisha, bali kuangalia na kuhakikisha kuwa ni mambo yale tu yahusuyo ndoa, mirathi na wakfu ndio yanashughulikiwa. Pamoja na kwamba waislam wenyewe ndio wanatakiwa kuianzisha na kiuendesha, lakini serikali ni lazima ijiridhishe kwamba hakutakuwa na masuala ya jinai yatakayoshughulikiwa na mahakama hiyo, maana masuala ya jinai yanashughulikiwa na mahakama za kitaifa kwa kufuata sheria za nchi zilizopo.

  @Mkodoleaji, kuhusu shule za dini, mara baada ya utaifishaji wa shule hakuna shule inayobagua wanafunzi kwa misingi ya dini. Ninachofahamu mimi ni kuwa shule zote za sekondari za mashirika ya dini zinachukuwa wanafunzi wa imani zote, ila kila mwanafunzi ni lazima afuate kanuni au masharti ya shule husika. Ni seminary pekee ambazo hazichachanganyi wanafunzi wa imani tofauti na hii ni kwa sababu seminari zina makusudi maalumu. Lakini zile za kawaida hilo halipo.

  Tatizo ni mawazo hasi ya waislamu kutotaka kuwapeleka watoto wao kwenye shule za madhehebu ya kikristo kwa kuhofia kwamba watoto wao watabadilishwa kuwa waislam. Sasa hilo nalo tuilalamikie serikali.? Kwenye elimu dunia soma shule yoyote bila kujali inamilikiwa na nani ili mradi upate elimu unayokusudia. Hakuna anayelazimishwa kubadili dini.

  Makamba, Lipumba, Mwinyi n.k walisoma shule za dini za kikristo mbona wao hawajawa wakristo? Ndugu zetu mnapenda sana kulalamika hata kwa vitu vilivyowazi.
   
 10. M

  Mkandara Verified User

  #10
  Sep 2, 2011
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mkuu wangu, hizi ni kamba tu hakuna kitu ambacho Pinda wala JK wanaweza kufanya kwa sababu makanisa hawataki kabisa kusikia hili.. Na italeta matatizo makubwa nchini mbali kabisa na kwamba Mahakama ya kadhi haiwezi kuwa suluhisho la matatizo ya Waislaam nchini. Binafsi nishasema sana kwamba hii mahakama ya kadhi ni mtaji kwa Bakwata wanatafuta mahala pa kuvuta posho kama wabunge wetu na vikao vyao kupitisha hizo bajeti za wizara na kadhalika..

  Katika mfumo wa mahakama ya kadhi, huwezi kuhukumu watu wanaofunga ndoa bila kujali dini zao, bila kujali haramu zilizowekwa na dini ili mradi wanataka kumkejeli Mwenyezi Mungu. Kwa hiyo JK alitakiwa toka mwanzo kuwaambia waislaam hili swala haliwezekani kwa sababu 1,2,3. na kama mtakuja na majawabu kuhusiana na maswala haya na haya basi serikali itayatazama. Na ili mahakama ya kadhi ifanye kazi vizuri itabidi hata serikali ipigi marufuku kutambua ndoa ya Muislaam kuoa nje ya dini yake na pia Waislaam kuzaa nje ya ndoa zao ili kuiwezesha sheria toka ktk shina la matatizo yenyewe..This case is a no no! - Tanzania bado tunafuata jadi zetu ktk ndoa zaidi ya mafundisho ya dini na lazima tukubali ukweli huu maana mtu anatozwa mahari na mkaja juu ni lazima, kuna Kitchen Party, Reception..

  Wakristu pia wanazitoa talaka kama hawana akili ili hali Biblia inakataza kuachana isipokuwa kwa sababu ya uzinifu, halafu wapo wengine hawatoi hizo talaka lakini hawaishi na wake zao kama kwamba dini imekataza kutoa kipande cha karatasi lakini unaruhusiwa kutoishi na mkeo - Hizo ni vows gani ktk dini?..Hivyo basi sii wakristu wala waislaam tunafuata ibada zetu ktk maswala ya ndoa na mirathi. lakini something has to be done kwa sababu wanawake wajane na watoto wetu wanaonewa sana na hawa Wajomba, mashangazi na hata wanafamilia wakubwa.

  JK hakutakiwa kabisa kujihusisha na maswala ya mahakama ya kadhi kwa sababu sheria zake haziwezi kuwa applied Tanzania kwani hao waislaam wenyewe katika maswala ya unyago hawana Mungu, wameitupa Kuran pembeni...Na please tafadhali Makamba, Mwinyi na Lipumba kusoma shule za Wakristu enzi za mkoloni hujui adha walizopitia.. Na hata siku moja usifikirie ilikuwa fun kwa sababu nimesoma shule hizo na nililazimika kubalisha jina hadi Nyerere alipozitaifisha.. Mzee Moses Mnauye unafikiri hilo jina alipenda kujiita Moses?..Acheni kutoa hukumu ktk vitu ambavyo hamvitambui kwa sababu hizi shule sasa hivi ni shule za kidini na upo ubaguzi mkubwa sana tofauti na wakati wa mwalimu.

  Hizi chuki za waislaam zimetoka wapi jamani?.. mbona wakati wa Nyerere tulikuwa tukila na kusherehekea Idd pamoja tukila kusherehekea Christimas pamoja nakumbuka vizuri zile misa za St. Peters wakati wa Pasaka na Christmas vijana wote tunakutana huko kisha tunaanguka mangomani, waya mkali wa Ujamaa na Kujitegemea!
   
 11. GHOST RYDER

  GHOST RYDER JF-Expert Member

  #11
  Sep 2, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 1,025
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135  MEDIA MNATAKA KUTUPELEKA RWANDA?

  Tulichukua Jukumu sote hapa kuifuatilia Hotuba hiyo na Tukitahadharisha wiki moja kabla ya Hotuba hiyo kuwa utakuwa Uwanja wa kuvurumisha turufu nzito za kisiasa na Hoja Tete. Kama tulivyotabiri hicho ndicho kilichotokea.

  Toka Hotuba hiyo Media zinaendelea kuwachanganya Watanzania kwa kutoa taarifa zenye mlengo wa kuchafua Hotuba hiyo nzuri ya Rais kwa kuwatia hasira Waislam kwa habari ambazo hazina haja ya kuandikwa kwa sasa kutokana na suala hili lilivyoshughulikiwa kwa umakini na uwazi wa kipekee.

  Shura ya Maimam leo inatangaza maandamano Nchi Nzima hii ni Hatari na Media inaandika habari hii. Mnaziuua habari ngapi huko kwenye MEDIA Zenu hii kwa nini mnaandika?

  Jana tumejadili hapa japo kwa uchache saana miiko ya Taaluma hii, hivi patriotic journalism haiwezekani...MEDIA Mnatishia amani kaaeni chini mtafakari hili

  ADIOS
   
 12. M

  Marytina JF-Expert Member

  #12
  Sep 2, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,035
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  toka lini?viongozi wamakanisa hutoa facts daima na ccm wanakwazika hapa
  ingelikuwa wakristo waliisupport CDM kwa iman ya ukristo nadhani leo CDM inekuwa ikulu.
   
 13. Julius Kaisari

  Julius Kaisari JF-Expert Member

  #13
  Sep 2, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 1,174
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 145
  Haya mambo ya udini ni full complicating. Hata bila kuyachanganya na siasa, bado yenyewe ni matatizo tupu. Nakumbuka mzee Kingunge aliwahi sema dini kamwe haijawahi kuwa kiunganisho cha matabaka ktk jamii. Kwa mantiki, kikwete na CCCM walijichanganya na ahadi zao mwaka ule 2005, ili mradi awapate waislam.

  Pengine ndipo napohoji uwezo wa kufikiri na kiuongozi wa Kikwete. Ona sasa anavyowaona waislam mabwege, as if hawawezi kufikiri. Hapa salama ya Kikwete na CCM ni kuwapa hiyo mahakama. Kwa upande mwingine, dini yenyewe ya kiislam na itikadi zake ni ya kiubinafsi zaidi. Ingefaa hii tz ingekuwa waislam tupu. Amin nawaambia, hata wakipewa kadhi, watadai OIC pia. Na tatizo kuu ni doctrine yao ya asiyemuislam ni KAFIR. Na kumuua kafir ni thwawabu.. Damn!
   
 14. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #14
  Sep 2, 2011
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,223
  Likes Received: 7,343
  Trophy Points: 280
  Mkodoleaji: Nimeisoma ile hotuba sikuona chochote kinachonishawishi kuwa JMK amebadili hulka. Nimesema siku zote ni kiongozi anayetaka kupendwa na kila mtu, hiyo si sifa ya kiongozi mzuri.
  Suala la mhakama linadhihirisha jinsi gani Rais wetu anacheza na akili za watu kiujanja ujanja. Ni mfano mzuri wa undumila kuwili au kigeu geu chake. Hoja hiyo yeye aliitolea ahadi na kuiweka katika Ilani ya CCM ya 2005. Alipobanwa akasema ilikuwepo sera wakati wa BWM. Alipobanwa zaidi akasema hiyo ni sera ya chama na chama kinaifanyia kazi. Yaani sera aliyoiuza kwa waislam bila kuwa na majibu yatokanayo.

  Ndivyo ilivyotokea kwa JMK aliposema Dowans watalipwa ndani ya CC, akaenda ubungo plaza na kusema suala hilo linamkera/
  Ndiye yule yule aliyesema mafisadi wanamkera sana, akenda rombo na kusema Mramba ni shoka la zamani lenye makali.
  Akasema Jairo hana makosa, wabunge walipohoji akatoa likizo kwa mtu asiye na makosa. Orodha inaendelea.
  Huyu ndiye JMK halisi na kama yupo anayechukulia kauli zake kwa umakini ajaue ameingizwa chaka. Sikuona jipya katika ile hotuba inayosifiwa!!!
  Kamundu kuna mambo mawili yanayojitokeza katika hoja zako na nina hakika sehemu kubwa ya jamii inaelewa kama unavyoelewa.
  Pili, kuna tatizo la Waislam kutoieleza vema dhana ya mahakama ya kadhi na kwahivyo kutafsiriwa kama alivyofanya kamundu.
  Tatu, inawezekana watu wanaelewa lakini wanataka kufanya upotoshaji ambao mimi sikubaliani nao.

  Mahakama za kadhi zilikuwepo hapa Tanzania na sheria za nchi zilikuwepo tena wakati wa ukoloni na sio kama ilivyo sasa.
  Nchi za jirani zina mahakama za kadhi n.k kwahiyo sio jambo linaloweza kufanya watu waamini tofauti na ilivyo isipokuwa wasiojishughilisha kutaka kufahamu.

  Sheria ya ndoa ya mwaka 1973? inatambua ndoa za aina tatu, za kimila, kidini na serikali. Sheria hizo zimetokana na katiba ya nchi, kwahiyo suala la kuabudu linaposemwa lipo nje ya katiba lizungumzwe kwa tahadhari kwasababu serikali haina dini lakini inatambua uwepo wa dini kikatiba.

  Suala la kazi limeelezwa kuwa ni kwa mirathi, ndoa na wakfu. Sheria ya ndoa ya serikali inatambua uwepo wa ndoa za kidini na wala sheria hiyo haielekezi ndoa hizo ziweje na kwa utaratibu gani. Hilo ni jukumu la dini husika. Sheria ya ndoa ya serikali inasimamiwa na serikali lakini inakinzana na sheria za dini kama ya kiislam katika baadhi ya mambo. Mfano, sheria inasema ndoa itafungwa bomani na kiongozi hata kama si wa dini ya wanandoa. Sheria za dini kama za kikristo na Kiislam zinautaratibu wa watu wanaoweza kufungisha.

  Sheria ya ndoa ya serikali inasema likitokea la kutokea mirathi itagawanywa kwa formula ya serikali. Sheria kama za kiislamu zina percentage. Kwahiyo kuwa na sheria moja ni kukiuka vifungu vya dini, ndiyo maana serikali ikatoa fursa ya kutambua ndoa za dini.
  Hapa ndipo Waislam wanasema wangependa kuwa na sheria zinazolingana na maadili ya dini yao katika ndoa,mirathi na wakfu.

  Labda nitoe mfano wa kufikirika. Ikitokea kuwepo sheria ya serikali inayolazimisha watu kuoa au kuolewa ili kupunguza maambukizi ya ukimwi, waislam hawatakuwa na lalamiko kwasababu itakuwa inakwenda sambamba na dini yao.
  Wakristo watakuwa na la kusema kwasababu wapo mapadre na masista wasioruhusiwa kuoa au kuolewa kwa mujibu wa dini yao.Je ,wao wakiomba utaratibu ili kutobanwa na sheria ya serikali katika imani yao watakuwa wamefanya kosa gani?

  Sidhani kuwa waislam wameomba sheria za makosa ya jinai yaingizwe katika sheria za nchi, na kwa vile ipo nafasi ya wao kuwa na utaratibu wao kuhusu mirathi, ndoa na wakfu waliopewa na katiba (sheria ya ndoa kutambua ndoa za kidini) sioni kuna tatizo gani wao kuruhusiwa kuwa na utaratibu wao.

  Ikumbukwe kuwa sheria ya kadhi haimhusu mtu asiye mwislam na hata mwislam haimfungi kuifuata.
  Hivi leo kuna waislam wana ndoa za bomani. Hiyo ni hiari yao.
  Wanandoa waliofunga ndoa kiislam na wakakubaliana kutofuata sheria za kadhi bali za serikali hawafungwi na chochote kile, kama vile mwislam anayeona ni vema kuwa na ndoa ya bomani. Hiyo ni yeye na imani yake na si kadhi wala serikali inaweza kumlazimisha wapi aegemee ili mradi tu yawepo makubaliano ya awali na ridhaa kati ya wanandoa kuhusu mustakabali wa ndoa zao.

  Mwisho: Swali kubwa hapa ni je utaratibu wa kuendesha mahakama ya kadhi uweeje? Ugharamiwe na serikali au wao wenyewe? Hili ndilo swali la msingi na lenye utata tunaouona.

  Jamii yote inakubaliana kuhusu dhana ya mahakama ya kadhi. Kwa bahati mbaya au makusudi kumekuwa na upotoshaji wa dhana hiyo kwa kuweka mambo yasiyohusu kabisa kama vile inaposemwa kuridhia utaratibu huo kutawalazimisha watu wote waufuate. Si kweli, badala yake mahakama ya kadhi itasaidia kutolifanya suala hilo kitaifa bali kiimani.

  Kuna upotoshaji kuwa waislam watalazimishwa kwenda mahakama ya kadhi, sio kweli. Kuna upotoshaji kuwa watazuiliwa kufuata taratibu za nchi, sio kweli. Kuna upotoshaji kuwa ndoa,mirathi na wakfu ni makosa ya jinai, sio kweli.

  Ninawaomba wanaJF kujaribu kuielewa issue vizuri kabla ya kuitolea hukumu. Tatizo letu ni kuwa ukiwa mkristo au mwislam unadhani kuwa una haki zaidi kuliko pagani. Baya zaidi hatutaki kujifunza na kuelewa mambo ya upande mwingine. Tunadhani ukisoma utaratibu wa wapagani(kama upo) basi itakuwa dhambi. Tunadhani ukisoma biblia au korani au sheria na taratibu za dini nyingine utakuwa umekiuka misingi ya dini.

  Wenye ueledi huwa ni wasomi wazuri sana wa canon law au sharia law hata kama haziwahusu. Jamii yetu itakuwa na utangamo zaidi tukiacha kusikiliza hadithi au mahubiri au mawaidha ya watu bila kuyafanyia tafiti zetu eti kwa vile ni viongozi wa dini. Wapo wenye agenda zao na hao ndio hawakawii kulisha sumu jamii. Let us exercise the culture of learning and being inquisitive in all matters in this world.

  Tutumie technology kujifunza mambo na sio kusikia na kuamini tu. Tusome vitabu, majarida tufuatilie mijadala ili kuongeza upeo wetu wa kuielewa dunia bila kujifunga katika kasehemu kamoja tu, tukisubiri fulani asome halafu aje kutuambia, hiyo ndiyo chanzo cha misconception.

  Utawezaje ku criticise freemason kama huna idea ya Uislam, ukristo, atheist na upagan na vinavyoendelea within japo kidogo!!!
   
 15. Hassani

  Hassani JF-Expert Member

  #15
  Sep 2, 2011
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 267
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 45
  Sioni kama ni busara sana kwa maaskofu au wanasiasa kureact mapema kwenye hotuba hii ukichukulia kwamba imeamsha hasira kwa waislam dhidi ya serikali.
   
 16. s

  sweke34 JF-Expert Member

  #16
  Sep 2, 2011
  Joined: Sep 28, 2010
  Messages: 2,533
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  kwanini umeiacha hiyo segment hapo juu kwenye habari yako? au ni kwa sababu inahusu dini fulani sana?
   
 17. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #17
  Sep 2, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,091
  Likes Received: 6,558
  Trophy Points: 280
  Enyi walinzi wa kondoo za Bwana, siasa kwenu iwe mwiko, angalieni sasa mnaingia humo mwisho mnajiingiza kwenye migogoro ya madawa ya kulevya; siasa waachineni wenye siasa.
   
 18. s

  sweke34 JF-Expert Member

  #18
  Sep 2, 2011
  Joined: Sep 28, 2010
  Messages: 2,533
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  hata kama imeamsha hasira kwa waislam , ulitaka wasubiri siku/miezi mingapi ndiyo wa react?
   
 19. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #19
  Sep 2, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Haya ndio matatizo yetu watanzania pamoja na viongozi wetu kila kitu mpaka upande mwingine ufanyareact.
  Rais akiongea jambo litakalowapendeza Wakristu Mashekh wanatoa tamko na kipiga vijembe, Rais akiongea jambo litalowapendeza Waislam Maaskofu nao wanatoa tamko la kupiga vijembe.
  Hii tabia naona inazidi kushika kasi na sijui nani kaileta
   
 20. T

  Tata JF-Expert Member

  #20
  Sep 2, 2011
  Joined: Dec 3, 2009
  Messages: 4,732
  Likes Received: 651
  Trophy Points: 280
  Kama nimekupata vizuri unaposema "patriotic journalism" una maana ya media kuficha baadhi ya mambo, hata kama ni ya kweli, ili kuepusha migongano au kutokuelewana baina ya watu, jumuia au taasisi za dini. Mimi siku zote huwa ninajiuliza hivi wanasiasa na viongozi wetu wa kiserikali huwa wanafuata nini kwenye shughuli za kidini? Si katiba ya nchi hii inaongelea suala la serikali kutokuwa na dini - yaani serikali kuwa Kafiri? Je rais anapoenda kwenye mkutano wa kidini anaongea pale kama nani? je anawakilisha taasisi ya kafiri ya urais au anaenda kama muumini wa kawaida?

  Je ni sawa rais kuhudhuria kwenye kikao cha kidini akiwakilisha taasisi kafiri ya uraisi (yaani ambayo haina dini)? Je ni sawa rais kwenda kwenye shughuli za kidini kama muumini wa kawaida kisha akaongelea masuala ya kiserikali yanayohusiana na mamlaka yake kama rais wakati wa kutoa hotuba?

  Nadhani tatizo la msingi hapa siyo vyombo vya habari bali ni la wanasiasa kutumia majukwaa ya kidini kuelezea sera zao kwa minajili ya kupata uungwaji mkono wa waumini wa dini husika. Rais ni kiongozi wa jamii (public figure) na chochote anachoongea ni lazima kitaandikwa na pia kutafsiriwa kulingana na uelewa wa mwandishi. Nadhani haitakuwa sahihi kuwaacha wanasiasa waongee wanachotaka kisha kuwatarajia waandishi watumie busara ya kuchambua lipi kkatika yale aliyoongea rais lina maslahi ya umma ili kuliripoti. Busara hii inatakiwa ianzie kwa viongozi kwani ndio waliopewa dhamana ya kuongoza wananchi.

  Kimsingi sipingi rais kwenda kwenye hafla ya dini yoyote ile. Ila inapotokea akaalikwa kwenda kwenye majukwaa ya kidini ni vyema kwa kutumia busara ya kawaida tu akajikita zaidi kwenye masuala ya kiroho pale anapopewa fursa kuongea. Ninachopinga ni raisi kutumia jukwaa la kidini kuongelea masuala ya kisiasa, kiserikali au ya kitaifa utadhani yuko kwenye mkutano wa kampeni ya kisiasa.


   
Loading...