Nsaji Mpoki
JF-Expert Member
- Nov 5, 2007
- 396
- 65
Tuna imani kuwa jana mlisikiliza hotuba ya Rais wa Tanzania kuhusu mustakabali wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki. Rais ameweka msimamo wazi kuwa Tanzania haina nia ya kujitoa kwenye Jumuiya hiyo pamoja na kuwa marais wa Kenya, Uganda na Rwanda wamekuwa wakiingilia masuala yaliyoridhiwa na nchi wanachama. Amekwenda mbali zaidi kusema marais hao wamekuwa wakifanya mikutano inayoashiria kuitenga Tanzania. Wakenya, Waganda na Wanyarwanda mnasemaje? Mnaona ni sahihi wakati huu hasa baada ya kuwekeza kwa siku nyingi katika umoja huu kufarakana?