Hotuba ya Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika, Dr. Rugemeleza A.K. Nshala katika Maadhimisho ya Siku ya Sheria

Oct 15, 2018
17
153
#WikiYaSheria2020

TAREHE 6, FEBRUARI, 2020

UKUMBI WA KIMATAIFA WA MAKONGAMANO WA MWL. JULIUS NYERERE DAR ES SALAAM

Ndugu Mh. Mgeni Rasmi, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr. John Pombe Joseph Magufuli
Mh. Jaji Mkuu, Prof. Ibrahimu Juma,
Mh. Waziri wa Katiba na Sheria, Balozi Augustino Mahiga, pamoja na mawaziri wengine mliopo,
Mh. Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ndg. Job Ndugai,
Waheshimiwa Majaji wa Mahakama ya Rufani na Mahakama kuu,
Mh. Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Prof. Adelardus Kilangi,
Mh. Mkurugenzi wa Mashitaka ya Jinai;
Mh. Wakili Mkuu wa Serikali,
Waheshimiwa Viongozi wa Serikali,
Mawakili wenzangu, Mabibi na Mabwana.


Tumekusanyika hapa kuadhimisha kilele cha maadhimisho ya Wiki ya Sheria ambayo ilianza tarehe 1 Februari 2020 na kuadhimishwa nchini kote. Ni adhimisho muhimu ambalo linatukumbusha juu ya msingi mkubwa wa utawala wa nchi yetu. Tunakumbushwa na kusisitiza kuwa nchi yetu ni ya jamhuri na ni ya kidemokrasia ambayo inaongozwa katiba na sheria zilizotungwa na Bunge. Kwamba watu wote katika nchi yetu wako chini ya sheria na wana mamlaka yao kwa mujibu wa sheria na wanatakiwa kuheshimu katiba na sheria za nchi yetu. Hakuna hata mmoja wao ambaye amepewa kinga ya kutofuata katiba na sheria na pale anapoikiuka basi anatakiwa kuwajibishwa. Aidha, ni siku ambayo tunakumbushwa majukumu muhimu sana ya muhimili wa mahakama. Huu ndiyo muhimili wenye jukumu azizi la kutoa haki katika nchi yetu na kutoa tafsiri sahihi ya katiba na sheria za nchi yetu. Kwa lugha ya kisheria ndiyo mlinzi asiyeyumba wa katiba na utawala wa sheria. Kwamba pale mahakama inapotoa maamuzi yake wahusika wote katika mgogoro huo n ahata wale walioko nje yake wanatakiwa kuheshimu na kutekeleza maamuzi hayo hata kama hawayapendi pasipo kuathiri haki yao ya kukata rufani au kuomba marejeo na mapitio. Uheshimuji wa katiba na sheria za nchi na maamuzi ya mahakama kunawapa hakikisho watu wote kuwa kikubwa na cha kufuatwa si mabavu au umbo la mtu bali ni sheria kwani watu wamekubali kuongozwa na sheria na si nguvu. Tunapozungumzia utawala wa sheria hatumaanishi utiifu wa sheria kandamizi. Watu wanatakiwa kukosoa utungwaji wa sheria ambazo zinapoka haki zao za kimsingi ambazo zinalindwa na katiba ya nchi yetu na hata kupinga ukatiba wa sheria hizo mahakamani.

Ndugu Mgeni Rasmi,

Mbiu ya maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini ni ‘Uwekezaji na Biashara: Wajibu wa Mahakama na Wadau Kuweka Mazingira Wezeshi ya Uwekezaji.’ Ni mbiu ambayo inataka tutafakari kwa kina maana yake. Nchi yetu ipo katika jitihada kubwa za kuvutia wawekezaji wa ndani na nje kuja kuwekeza. Tafiti nyingi duniani zinaonyesha kuwa kile ambacho huwapa Imani na imani kubwa wawekezaji si kiwango kidogo cha kodi au misamaha ya kodi bali utawala wa sheria na kuheshimika kwa mfumo mzima wa haki. Sababu nyingine ni miundomsingi, uthabiti wa kiwango cha kubadilisha fedha, kiwango cha kodi, ukubwa wa soko, eneo nchi ilipo na ubora wa wafanyakazi, na faida. Ni wazi kuwa utengamano wa nchi na utawala wa sheria ndicho kitu kikubwa kinachoweza kuwavutia wawekezaji kuwekeza katika nchi yetu na kukuza uchumi wetu. Na Imani hiyo inakua na kuongezeka pale maamuzi ya mahakama juu ya migogoro yote iwe ya kibiashara, kikodi, kijinai na madai yanapoheshimiwa.
Ibara ya 107(1)A ya Katiba ya Nchi yetu inasema:

Mamlaka ya utoaji haki katika Jamhuri ya Muungano itakuwa mikononi mwa Idara ya Mahakama na Idara ya Mahakama ya Zanzibar, na kwa hiyo hakuna chombo cha Serikali wala cha Bunge au Baraza la Wawakilishi la Zanzibar kitakachokuwa na kauli ya mwisho katika utoaji haki.

Katiba yetu ipo wazi juu ya mamlaka ya mahakama na hivyo basi pindi kunapokuwa na kesi au mashauri yote ikiwemo ya uwekezaji na biashara ni vema yapelekwe na kutatuliwa mahakamani. Licha ya kuwepo hakikisho hili mikataba mingi ambayo nchi yetu inasaini na mataifa mengine inapoka madaraka ya mahakama zetu na kuyapa mashirika ya usuluhishi au uamuzi wa migogoro ya uwekezaji madaraka hayo. Kitu hiki si kizuri kwani kinakiuka ibara ya 107(1)(A) ya Katiba ya nchi yetu na Kanuni ya Umiliki wa Milele wa Rasilimali (Azimio Namba 1803 la Mwaka 1962 Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa)na Azimio Namba 3281 la Mwaka 1974. Pale ambapo mahakama zetu zinaheshimiwa na kupewa fursa ya kuamua migogoro yote ile kwa haki na bila shinikizo imani ya wafanyabiashara na wawekezaji kwake itaongezeka na hivyo kuondoa matakwa ya mataifa yaliyoendelea na makampuni yanayotoka kwao kuwa migogoro hiyo iamuliwe na mabaraza ya uamuzi ambayo kwa kweli wao ndio wanayamiliki.

Mahakama zetu zitaweza kuheshimika kuwa ni waamuzi wa haki wa migogoro kama zitakuwa na rasilimali fedha na watu wa kutosha pamoja na vifaa vya kuandika na kurekodi hoja za wadaawa. Hivi sasa mahakimu na majaji wanaandika hoja na ushahidi wa wadaawa kwa mikono na hii inarefusha muda wa kusikilizwa kwa kesi. Katika nchi za wenzetu hali si hivyo kwani majaji na mahakimu wao husikiliza na pengine kuandika hoja chache sana kwani yote yanayosemwa na wadaawa huandikwa na wachapaji wa mahakama (stenographers) au hurekodiwa na vifaa vya kurekodi. Kulikuwa na jitihada za kuweka vifaa vya kurekodi katika Mahakama Kuu Kitengo cha Biashara lakini huu haujawa utamaduni dumivu. Ni rai ya TLS kuwa jitihada za makusudi zifaanyike ili kesi zote ziwe zinarekodiwa na kuandikwa na kuhakikisha kuwa kile kilichosemwa na wadaawa na mawakili wao kinaandikwa kwa ukamilifu na hivyo kuwezesha kusikilizwa kwa kesi nyingi.

Ndugu Mgeni Rasmi,

Kwa kifupi napenda nichukue fursa hii kukumbushia historia ya Chama Cha Mawakili Tanganyika mpaka sasa. Mwezi wa Januari, 2020, Chama cha Wanasheria wa Tanganyika kimetimiza miaka 65 tokea kuanzishwa kwake. Kwa uhakika miaka 65 ni umri wa mtu mzima kustaafu utumishi isipokuwa tu kwa wale wenye majukumu maalumu na wale ambao huongezewa muda kupitia mikataba. Mapaka sasa orodha ya mawakili waliopo kwenye kitabu cha orodha ya mawakili (Roll of Advocates) imefikia 9372. Katika orodha hiyo waliotangulia mbele ya haki ni mawakili 234 na wanaofanya kazi ya uwakilishi mahakamani ni 8,667. Idadi hii ya 8,667 inabadilika badilika kwasababu kuna mawakili wa utumishi wa umma ambao sheria imewalazimu waache uwakilishi wa kujitegemea na hivyo wako kwenye hatua za kukamilisha mchakato. Wale walioahirisha kazi za uwakili wa kujitegemea wanafikia 412 na wale wanaofanya kazi ya kuapisha tu au kugonga mihuri (notorisation) ni 14. Katika idadi hii vijana wanakadiriwa kuwa ni asilimia 75% ya mawakili walio hai. Hivyo, tunajukumu kubwa la kuwajengea uwezo wa kimaadili na uzoefu wa kazi ya uwakilishi. Chama kimeweka na kinaendelea kuweka mifumo mbalimbali ya kuwajengea uwezo ikiwa ni pamoja na uadilifu, elimu endelevu ya kisheria, na uzoefu wa kazi ya kisheria. Kwa hali hii katika kuhakikisha kuwa kila mwanachama anapata huduma, chama kinatoa huduma yake ya ushauri kitaaluma, na kila mwanachama anapata nafasi ya kuihudumia jamii, chama kinaendelea kuanzisha matawi kwa katika mikoa ya Tanzania na haswa pale palipo na Mahakama kuu. Mpaka sasa tuna matawi 14 na tayari kuna maombi ya kuanzisha matawi mengine matatu katika mikoa ya Kigoma, Mara, Rukwa.

Hata hivyo napenda kusema kuwa mabadiliko ya sheria ya Chama chetu yatatuongezea mzigo mkubwa sana wa uendeshaji kwani kufanya mkutano mkuu kwa uwakilishi utasababisha chama chetu kitumie si chini ya shilingi milioni 300 kwa mwaka. Fedha hizo hatuna. Utaratibu wetu wa sasa ni kuwa kila mwanachama ana jukumu la kujigharimia ili ahudhurie Mkutano Mkuu na hakuna malalamiko yoyote kutoka kwa wanachama wetu juu ya hilo kwani wao wanaona kuwa Aidha, uanzishwaji wa Ofisi za Kanda ni mzigo mkubwa sana kwa chama chetu na una hatari ya kuleta tatizo la ukanda na hivyo kumomonyoa utaifa ambayo ni nguzo kubwa ya chama chetu.

Ndg. Mgeni Rasmi,
Ningependa kwa upekee niongelee suala la mabadiliko ya sheria katika mfumo jinai na haswa haswa katika mambo makubwa mawaili au matatu yanayohusu mihimili yetu. Jambo la kwanza ni lile linalohusu mfumo wetu wa jinai kubaki na misingi au madhumuni ya kikoloni ambayo malengo yake makuu yalilikuwa kushikilia mtuhumiwa au mharifu kwa kipindi kirefu ndani ya mahabusu au magereza kwa lengo la kuweka hofu kwa wanannchi ili watii amri za kikoloni bila kuhoji. Mara kadhaa tumekunukuu wewe na watangulizi wako mkihoji suala la kutokamilika kwa upelelezi ilihali mtu amekamatwa na ushahidi. Mfumo wa kikoloni ndivyo ulivyokuwa kwa sababu haukuwa na lengo la kumhukumu mtuhumiwa papo kwa papo. Ulikuwa na lengo la kutishia. Hivyo hata sasa waendesha mashitaka hulazimika kutumia mfumo huo huo kwa sababu wamejifunza na kufanyia kazi mfumo huo.
Inabidi ikumbukwe kuwa muda wa mwanadamu hapa duniani una ukomo wake na hakuna mwenye uwezo wa kuongeza ila Mwenyezi Mungu. Kila siku ambayo mtu anapokwa uhuru wake kwa kuwekwa ndani siku hiyo haitarudi. Na nchi yetu haina mfumo wa kumfidia mtu ambaye alipokwa uhuru wake na baadae kesi yake kufutwa au kukutwa hana hatia.
Ibara ya 14 ya Katiba ya Nchi yetu inatoa haki ya kuishi na “kupata kutoka kwa jamii hifadhi ya maisha yake kwa mujibu wa sheria”. Aidha, Ibara ya 15 (1) inasema “Kila mtu anayo haki ya kuwa huru na kuishi kama mtu huru.” Ibara ya 15(2) inataka mtu asishikwe na kuwekwa ndani au kuhamishwa kwa nguvu na kupoteza uhuru wake isipokuwa mujibu wa sheria na pindi mtu anapokuwa ametiwa hatiani. Hili kukidhi matakwa haya inabidi polisi na waendesha mashitaka kujiridhisha kuwa pale wanatoa tu amri ya kushikwa na kuwekwa ndani pale upelelezi unakuwa umekamilia. Aidha, haki ya kupata dhamana iheshimike. Ni vema pia uamuzi wa Mahakama ya Rufani katika kesi ya Attorney General v. Jeremiah Mtobesya Civil Appeal No 65 of 2016 ambapo ilisema kuwa kipengele kinachompa madaraka Mwendesha Mashitaka Mkuu wa Serikali kuweka cheti cha kuzuia dhamana hata kwa makosa yanayodhaminika ni kinyume cha katiba ya nchi yetu. Tulitegemea kuwa kutokana na uamuzi huo sheria zote zinazotoa mamlaka hayo zingebadilishwa lakini sivyo ilivyo. Hadi hivi sasa watuhumiwa wengi wenye kukabiliwa na kesi za jinai wapo ndani licha ya kuwa makosa yao yanadhaminika lakini wamewekewa hati hiyo.
Ni rai yetu kuwa mabadiliko ya suala hili linahitaji utashi wa kisiasa ili kubadilisha suala hili na pengine kuondokana kabisa na hali hii na kuepusha gharama kubwa za uendeshaji wa mashauri na kushikilia watuhumiwa kwa kipindi kirefu. Ni vyema tujikite kutafakari kwa makini ili tuweze kuweka mfumo mzuri wa kushikilia mahabusu na wafungwa kwa muda mfupi zaidi ili nchi yetu isikae na watuhumiwa wengi mahabusu hata magerezani kwa muda mrefu.
Vivyo hivyo, ni vyema tukafanya mabadiliko ya kuwa na namna bora ya kuwatumia wafungwa ikiwa ni pamoja na kifungo cha nje kilichopo kisheria hivi sasa ili walete tija katika uzalishaji wa kitaifa na kuchangia uchumi wa nchi kwa muda mfupi badala ya kuendelea kulipatia taifa gharama kwa muda mrefu wakati tayari kwa kupatkana hatia wameshatuingiza gharama kubwa. Kwa kufanya hivi nchi itafaidika na mambo mengi sana ikiwamo kupunguza msongamano kwenye magereza, kuonekana wazi tunaheshimu haki za binadamu na utawala wa sheria na wakati huo huo tukikuza uchumi wa taifa kupitia watuhumiwa na wafungwa.

Mh. Mgeni Rasmi, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Jambo la pili linaangukia katika muhimili wetu wa Bunge katika utungwaji wa sheria. Ni wazi kwamba falsafa ya utungwaji wa sheria inahitaji mabadiliko kwa kiasi kikubwa kwa watunga sheria, wananchi na wasimamizi wa sheria kiujumla. Wapeleka miswaada bungeni, wabunge na hata wananchi bado hawajafahamu vyema dhana ya adhabu wanazopendekeza na baadae kufanywa kuwa sheria. Kwa kiasi kikubwa dhana iliyojengeka ni kutoa adhabu kali badala ya kutoa mafunzo kwa mkosaji na wengine ili kuzuia zaidi. Sheria ikijikita katika falsafa ya kutoa adhabu kubwa au kali huwa haitoi fundisho, haifadishi nchi, na pengine hutekelezeka kwa upande mmoja ambao ni kumshikilia mtuhumiwa lakini haitekelezeki upande wa pili ambao ni faini kwa sababu faini zinazowekwa hazilipiki na hivyo kujikuta tunajaza watu magerezani kwa wakosaji kushindwa kulipa faini!!

Ndugu Mgeni Rasmi, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Inajulikana wazi kuwa faini na adhabu za kifedha ni chanzo kikubwa cha mapato ya nchi. Kama sikosei ni chanzo cha tatu au nne ukiondoa kodi, tozo za leseni na michango ya mashirika ya umma. Faini au adhabu zikiwekwa katika kiwango kinachowezekana kulipika kwa wakosaji kinachangia kwa kiasi kikubwa katika pato la nchi kwa sababu kinalipika kiurahisi na wakati huo huo kinabadilisha tabia ya wakosaji wa kujirudia rudia kiurahisi pia. Faini au adhabu kubwa hailipiki na hivyo kulazimika kuchukua mfumo wa kuwekwa ndani (incarceration) ambao huleta gharama ya kuwahifadhi na pengine rushwa kwa wakosaji kutoa hongo ili kuepuka kufungwa. Tuchukue mfano ya makosa kadha wa kadha ya barabarani.
Ndio shilingi elfu 30 za kitanzania ni ndogo na zinalipika kiurahisi kwa mkosaji lakini zimeweza kupunguza makosa ya barabarani kwa kiasi kikubwa na wakati huo huo yamechangia kwa kiasi kikubwa kwenye pato la taifa. Ukiendesha gari lako kwa faulo kutoka Dar es Salaam kuja Dodoma unaweza jikuta unamaliza pesa ya mafuta. Hivyo ukikamatwa mara mbili yaani elfu 30 mara mbili tayari unaanza kumaliza fedha yako ya matumizi na hivyo kuogopa kuendesha kwa kasi kwa kuogopa kukamatwa. Na pengine hata ukiona mtu kavaa kanzu nyeupe kwa mbali unapunguza mwendo kwa kudhani ni afisa usalama barabarani.
Kwa kuweka adhabu zinazotekeleka ni imani yetu mawakili kuwa hata watendaji wa kimahakama na watendaji wengine wa umma watapata urahisi kuyasimamia na kukusanya adhabu hizo ili zichangie katika pato nchi.

Ndugu Mgeni Rasmi, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Jambo la tatu linahusu mamlaka ya mahakama za chini ambazo hazina mamlaka ya kusikiliza makossa makubwa ya jinai kama vile mauaji, uhujumu uchumi na mengine yote yaliyoainishwa na sheria mbalimbali yanayolazimisha kusikilizwa na mahakama kuu tu. Ni vyema suala hili likaangaliwa kwa makini hasa hasa mamlaka ya mahakama hizi kwani kwa kusema hazina mamlaka ya kusilikiza shauri hata kwa mambo madogo madogo na pengine makubwa kunachangia kwa kiasi kikubwa sana ucheleweshaji wa mashauri, kunyimwa kwa haki ya kusikilizwa kwa wakati, kutotabirika kwa muda wa uendeshaji wa shauri lake, kuongeza gharama kwa magereza ambao hulazimika kuwatunza mpaka pale shauri lao litakaposikilizwa. Mtu wa kawaida hujiuliza au watu wanyonge hujiuliza swali dogo tu kuwa, kama mahakama haina mamlaka sasa kwanini shauri lake linapelekwa kwa hakimu asiyekuwa na mamlaka? Ni vema utaratibu wa kupeleka kesi katika mahakama isiyo na mamlaka ukomeshwe na kesi zipelekwe tu kwa mahakama zenye mamlaka.
Aidha zuio la mawakilili kufanya kazi katika Mahakama za Mwanzo liondolewe kwani hivi sasa Mahakama hizo zinaongozwa na Mahakimu Wakazi wenye shahada ya kwanza ya sheria. Na katazo hili linazuia wananchi wengi kupata huduma ya uwakilishi. Mahakama hizi za mwanzo ndizo ambazo zinasikiliza kesi nyingi nchini. Hivyo mawakili kufanya kazi katika mahakama hizo kutawawezesha wananchi kupata huduma za mawakili na kuwezesha haki kupatikana katika ngazi zote.

Mh. Mgeni Rasmi, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Kama nilivyotangulia kusema hapo awali, uwepo wa chama kila mahali na idadi kubwa ya vijana chama kina majumu makubwa ya kuwajengea uwezo wa kimaadili na uzoefu wa kazi ya uwakilishi. Chama kimeweka na kinaendelea kuweka mifumo mbalimbali ya kuwajengea uwezo ikiwa ni pamoja na uadilifu, elimu endelevu ya kisheria, uzoefu wa kazi ya kisheria, na kutoa huduma ya kisheria nchini ikiwa ni pamoja na ushauri wa kisheria au uwakilishi wa bure kwa wasiojiweza/wanyonge wakiwemo. Hali hii inaleta changamoto ya kifedha na miundombinu. Chama kinahitaji kuwa na majengo ili kiweze kutoa mafunzo maalumu na endelevu ya kisheria ili kuwe na ubobevu (specialization) wa kisheria kwenye mambo ya kisheria yanayoongezeka kila kukicha; na chama kinahitaji fedha za kujiendesha na kujenga majengo ya kufundishia na kutoa hudumu kwa faida ya watanzania ili waweze kutatua migogoro yao kitaaluma na kisha kuwahi kwenye uzalishaji. Hivyo basi, chama kinahitaji kuungwa mkono kwa kupewa ardhi ikiwezekana na fedha kiasi ya kujenga katika mikoa mbalimbali ya Tanzania ikiwamo hapa Dodoma ili kiweze kutoa huduma hii kiufasaha.

Ndugu Mgeni Rasmi, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Nimalizie sasa kwa kusema machache kuhusu muhimili wa Mahakama ambao unatija za kimsingi nchini kwetu katika hali zote za kiuchumi, kisiasa, kiutamaduni na hata mila na desturi zetu. Ningependa kutoa rai kwa mahakama ambayo ina dhamana ya kulinda haki kwa watu na vyombo vyote vilivyomo kwenda mbele zaidi ili iweze kushiriki kikamilifu katika kufanya maboresho ya sheria kwa njia ya hukumu. Naiomba mahakama isiogope kufanya maamuzi magumu ya kutengua vipengele vya sheria ambavyo vinaonekana vinaleta ukakasi kwenye katika utekeleza wa haki. Tafsiri sahihi za kiutendaji zinafanywa na mahakama. Hivyo mahakama isaidie jamii kufanya hivyo. Najua mawakili wanaleta mashauri yanayoiomba mahakama kufanya mabadiliko ya sheria kwa kutengua baadhi ya vifungu. Kama maombi hayaambatani ni utafiti unaojitosheleza, ni vyema mahakama iwaamuru mawakili wakafanye utafiti wa kina ili iweze kutoa maamuzi yanayojitosheleza katika kufanya maboresho ya sheria kwa faida yetu sote.
Baada ya kusema hayo machache ninapenda kushukuru sana kwa mwaliko huu na kutoa wito wa kudumishwa kwa utawala wa sheria katika nchi yetu na uhuru wa mahakama.

Asanteni sana kwa kunisikiliza
1581056374147.png
1581056399387.png
1581056414625.png
1581056439045.png

Pia soma: Maadhimisho ya Siku ya Sheria: Rais Magufuli adai hata yeye mshahara haumtoshi, awaasa wapelelezi kuharakisha upelelezi
 

Attachments

  • 1581056343241.png
    1581056343241.png
    48.9 KB · Views: 2
Alichoongea raisi wa TLS kwenye hotuba yake ni mambo ya msingi sana:

1.Kuhimiza zaidi mfumo wa faini ili kupunguza gharama za kuhudumia wafungwa

2.Kutoa adhabu mbadala za kuhudumia jamii pia kunapunguza gharama kwa serkali

3.Vifungo vya nje husaidia kumfanya mhusika aendelee kuzalisha hivyo kuchangia katika uchumi wa familia na nchi

4.Kesi zipelekwe kwenye mahakama ambazo zinauwezo wa kusikiliza ila kupunguza muda wa kusikiliza watuhumiwa na usumbufu(Yale mambo ya mshatakiwa hakutakiwa kujibu chochote kwa kuwa mahakama haina uwezo wa kusikiliza shauri hili yataisha)

5.Iangaliwe upya sheria ya kushikilia watu bila kuwapa dhamana kwa kuwa sheria hii imekaa kikoloni zaidi na lengo ni kutisha au kukomoa

6.MTU akamatwe upelelezi unapokuwa umekamilika.

Nakadhalika nakadhalika,kwakua sikufualitia tukio zima sijui Mheshimiwa raisi alijibu nini ila haya mambo ni ya muhimu kama kama kweli tunataka taifa linalotenda haki na utawala wa sheria.

Nukuu muhimu kutoka kwenye hotuba

"Inabidi ikumbukwe kuwa muda wa mwanadamu hapa duniani una ukomo wake na hakuna mwenye uwezo wa kuongeza ila Mwenyezi Mungu. Kila siku ambayo mtu anapokwa uhuru wake kwa kuwekwa ndani siku hiyo haitarudi. Na nchi yetu haina mfumo wa kumfidia mtu ambaye alipokwa uhuru wake na baadae kesi yake kufutwa au kukutwa hana hatia."

Hongera raisi wa TLS.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
February 6, 2020
Dar es Salaam, Tanzania

DAKIKA 10 NONDO ZA RAIS WA TLS MBELE YA RAIS MAGUFULI

Mfumo wa sheria za jinai ulioko sasa nchini, hauna tofauti na sheria za kikoloni, zilizotumika kutia hofu wananchi ili watii amri za kikoloni bila kuhoji. Kauli hiyo imetolewa na Dk. Rugemeleza Nshala, Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS), leo tarehe 6 Februari 2020, jijini Dar es Salaam katika maadhimisho ya siku ya sheria nchini. Dk. Nshala ameishuri serikali ya Rais John Magufuli kufanya mabadiliko ya sheria katika mfumo huo, ili kuondoa sheria kandamizi zinazonyima watuhumiwa dhamana.

Rais wa chama cha sheria Dk. Nshala Rugemeleza katika hotuba yake ya mwaka kuadhimisha siku ya sheria ametoa hotuba iliyogusia mambo mengi yenye umuhimu kwa ujenzi wa Taifa imara linaloongoza kwa haki na kufuata sheria. source: MwanaHALISI TV

Ukumbini kulikuwapo Mh. Rais John Pombe Joseph Magufuli, mh. Jaji Mkuu Ibrahim Juma, Spika wa Bunge Job Ndugai , Mwanasheria Mkuu wa Serikali Profesa Adelardus Kilangi majaji wakuu wastaafu kina Mohamed Chande, Majaji wa Mahakama za Rufani na Mahakama Kuu pamoja na kadamnasi ya mawakili wanasheria.

Bila kupepesa macho Rais wa TLS anena mbele ya Rais Magufuli: Hili ni kinyume na Katiba watu wanatishwa



Source: ABC Habari
 
Hotuba nzima ya Dk. Rugemeleza Nshala

TAREHE 6, FEBRUARI, 2020

UKUMBI WA KIMATAIFA WA MAKONGAMANO WA MWL. JULIUS NYERERE DAR ES SALAAM


Ndugu Mh. Mgeni Rasmi, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr. John Pombe Joseph Magufuli

Mh. Jaji Mkuu, Prof. Ibrahimu Juma,
Mh. Waziri wa Katiba na Sheria, Balozi Augustino Mahiga, pamoja na mawaziri wengine mliopo,
Mh. Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ndg. Job Ndugai,
Waheshimiwa Majaji wa Mahakama ya Rufani na Mahakama kuu,
Mh. Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Prof. Adelardus Kilangi,
Mh. Mkurugenzi wa Mashitaka ya Jinai;
Mh. Wakili Mkuu wa Serikali,
Waheshimiwa Viongozi wa Serikali,
Mawakili wenzangu, Mabibi na Mabwana.


Tumekusanyika hapa kuadhimisha kilele cha maadhimisho ya Wiki ya Sheria ambayo ilianza tarehe 1 Februari 2020 na kuadhimishwa nchini kote.

Ni adhimisho muhimu ambalo linatukumbusha juu ya msingi mkubwa wa utawala wa nchi yetu. Tunakumbushwa na kusisitiza kuwa nchi yetu ni ya jamhuri na ni ya kidemokrasia ambayo inaongozwa katiba na sheria zilizotungwa na Bunge.

Kwamba watu wote katika nchi yetu wako chini ya sheria na wana mamlaka yao kwa mujibu wa sheria na wanatakiwa kuheshimu katiba na sheria za nchi yetu. Hakuna hata mmoja wao ambaye amepewa kinga ya kutofuata katiba na sheria na pale anapoikiuka basi anatakiwa kuwajibishwa.

Aidha, ni siku ambayo tunakumbushwa majukumu muhimu sana ya muhimili wa mahakama. Huu ndiyo muhimili wenye jukumu azizi la kutoa haki katika nchi yetu na kutoa tafsiri sahihi ya katiba na sheria za nchi yetu.

Kwa lugha ya kisheria ndiyo mlinzi asiyeyumba wa katiba na utawala wa sheria. Kwamba pale mahakama inapotoa maamuzi yake wahusika wote katika mgogoro huo n ahata wale walioko nje yake wanatakiwa kuheshimu na kutekeleza maamuzi hayo hata kama hawayapendi pasipo kuathiri haki yao ya kukata rufani au kuomba marejeo na mapitio.

Uheshimuji wa katiba na sheria za nchi na maamuzi ya mahakama kunawapa hakikisho watu wote kuwa kikubwa na cha kufuatwa si mabavu au umbo la mtu bali ni sheria kwani watu wamekubali kuongozwa na sheria na si nguvu.

Tunapozungumzia utawala wa sheria hatumaanishi utiifu wa sheria kandamizi. Watu wanatakiwa kukosoa utungwaji wa sheria ambazo zinapoka haki zao za kimsingi ambazo zinalindwa na katiba ya nchi yetu na hata kupinga ukatiba wa sheria hizo mahakamani.

Ndugu Mgeni Rasmi,
Mbiu ya maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini ni ‘Uwekezaji na Biashara: Wajibu wa Mahakama na Wadau Kuweka Mazingira Wezeshi ya Uwekezaji.’ Ni mbiu ambayo inataka tutafakari kwa kina maana yake. Nchi yetu ipo katika jitihada kubwa za kuvutia wawekezaji wa ndani na nje kuja kuwekeza.

Tafiti nyingi duniani zinaonyesha kuwa kile ambacho huwapa Imani na imani kubwa wawekezaji si kiwango kidogo cha kodi au misamaha ya kodi bali utawala wa sheria na kuheshimika kwa mfumo mzima wa haki. Sababu nyingine ni miundomsingi, uthabiti wa kiwango cha kubadilisha fedha, kiwango cha kodi, ukubwa wa soko, eneo nchi ilipo na ubora wa wafanyakazi, na faida.

Ni wazi kuwa utengamano wa nchi na utawala wa sheria ndicho kitu kikubwa kinachoweza kuwavutia wawekezaji kuwekeza katika nchi yetu na kukuza uchumi wetu. Na Imani hiyo inakua na kuongezeka pale maamuzi ya mahakama juu ya migogoro yote iwe ya kibiashara, kikodi, kijinai na madai yanapoheshimiwa.

Ibara ya 107(1)A ya Katiba ya Nchi yetu inasema:
Mamlaka ya utoaji haki katika Jamhuri ya Muungano itakuwa mikononi mwa Idara ya Mahakama na Idara ya Mahakama ya Zanzibar, na kwa hiyo hakuna chombo cha Serikali wala cha Bunge au Baraza la Wawakilishi la Zanzibar kitakachokuwa na kauli ya mwisho katika utoaji haki.

Katiba yetu ipo wazi juu ya mamlaka ya mahakama na hivyo basi pindi kunapokuwa na kesi au mashauri yote ikiwemo ya uwekezaji na biashara ni vema yapelekwe na kutatuliwa mahakamani.

Licha ya kuwepo hakikisho hili mikataba mingi ambayo nchi yetu inasaini na mataifa mengine inapoka madaraka ya mahakama zetu na kuyapa mashirika ya usuluhishi au uamuzi wa migogoro ya uwekezaji madaraka hayo.

Kitu hiki si kizuri kwani kinakiuka ibara ya 107(1)(A) ya Katiba ya nchi yetu na Kanuni ya Umiliki wa Milele wa Rasilimali (Azimio Namba 1803 la Mwaka 1962 Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa)na Azimio Namba 3281 la Mwaka 1974.

Pale ambapo mahakama zetu zinaheshimiwa na kupewa fursa ya kuamua migogoro yote ile kwa haki na bila shinikizo imani ya wafanyabiashara na wawekezaji kwake itaongezeka na hivyo kuondoa matakwa ya mataifa yaliyoendelea na makampuni yanayotoka kwao kuwa migogoro hiyo iamuliwe na mabaraza ya uamuzi ambayo kwa kweli wao ndio wanayamiliki.

Mahakama zetu zitaweza kuheshimika kuwa ni waamuzi wa haki wa migogoro kama zitakuwa na rasilimali fedha na watu wa kutosha pamoja na vifaa vya kuandika na kurekodi hoja za wadaawa.

Hivi sasa mahakimu na majaji wanaandika hoja na ushahidi wa wadaawa kwa mikono na hii inarefusha muda wa kusikilizwa kwa kesi. Katika nchi za wenzetu hali si hivyo kwani majaji na mahakimu wao husikiliza na pengine kuandika hoja chache sana kwani yote yanayosemwa na wadaawa huandikwa na wachapaji wa mahakama (stenographers) au hurekodiwa na vifaa vya kurekodi.

Kulikuwa na jitihada za kuweka vifaa vya kurekodi katika Mahakama Kuu Kitengo cha Biashara lakini huu haujawa utamaduni dumivu. Ni rai ya TLS kuwa jitihada za makusudi zifaanyike ili kesi zote ziwe zinarekodiwa na kuandikwa na kuhakikisha kuwa kile kilichosemwa na wadaawa na mawakili wao kinaandikwa kwa ukamilifu na hivyo kuwezesha kusikilizwa kwa kesi nyingi.

Ndugu Mgeni Rasmi,
Kwa kifupi napenda nichukue fursa hii kukumbushia historia ya Chama Cha Mawakili Tanganyika mpaka sasa. Mwezi wa Januari, 2020, Chama cha Wanasheria wa Tanganyika kimetimiza miaka 65 tokea kuanzishwa kwake. Kwa uhakika miaka 65 ni umri wa mtu mzima kustaafu utumishi isipokuwa tu kwa wale wenye majukumu maalumu na wale ambao huongezewa muda kupitia mikataba.

Mpaka sasa orodha ya mawakili waliopo kwenye kitabu cha orodha ya mawakili (Roll of Advocates) imefikia 9372. Katika orodha hiyo waliotangulia mbele ya haki ni mawakili 234 na wanaofanya kazi ya uwakilishi mahakamani ni 8,667. Idadi hii ya 8,667 inabadilika badilika kwasababu kuna mawakili wa utumishi wa umma ambao sheria imewalazimu waache uwakilishi wa kujitegemea na hivyo wako kwenye hatua za kukamilisha mchakato.

Wale walioahirisha kazi za uwakili wa kujitegemea wanafikia 412 na wale wanaofanya kazi ya kuapisha tu au kugonga mihuri (notorisation) ni 14. Katika idadi hii vijana wanakadiriwa kuwa ni asilimia 75% ya mawakili walio hai.

Hivyo, tunajukumu kubwa la kuwajengea uwezo wa kimaadili na uzoefu wa kazi ya uwakilishi. Chama kimeweka na kinaendelea kuweka mifumo mbalimbali ya kuwajengea uwezo ikiwa ni pamoja na uadilifu, elimu endelevu ya kisheria, na uzoefu wa kazi ya kisheria.

Kwa hali hii katika kuhakikisha kuwa kila mwanachama anapata huduma, chama kinatoa huduma yake ya ushauri kitaaluma, na kila mwanachama anapata nafasi ya kuihudumia jamii, chama kinaendelea kuanzisha matawi kwa katika mikoa ya Tanzania na haswa pale palipo na Mahakama kuu. Mpaka sasa tuna matawi 14 na tayari kuna maombi ya kuanzisha matawi mengine matatu katika mikoa ya Kigoma, Mara, Rukwa.

Hata hivyo napenda kusema kuwa mabadiliko ya sheria ya Chama chetu yatatuongezea mzigo mkubwa sana wa uendeshaji kwani kufanya mkutano mkuu kwa uwakilishi utasababisha chama chetu kitumie si chini ya shilingi milioni 300 kwa mwaka. Fedha hizo hatuna.

Utaratibu wetu wa sasa ni kuwa kila mwanachama ana jukumu la kujigharimia ili ahudhurie Mkutano Mkuu na hakuna malalamiko yoyote kutoka kwa wanachama wetu juu ya hilo kwani wao wanaona kuwa Aidha, uanzishwaji wa Ofisi za Kanda ni mzigo mkubwa sana kwa chama chetu na una hatari ya kuleta tatizo la ukanda na hivyo kumomonyoa utaifa ambayo ni nguzo kubwa ya chama chetu.

Ndg. Mgeni Rasmi,
Ningependa kwa upekee niongelee suala la mabadiliko ya sheria katika mfumo jinai na haswa haswa katika mambo makubwa mawaili au matatu yanayohusu mihimili yetu. Jambo la kwanza ni lile linalohusu mfumo wetu wa jinai kubaki na misingi au madhumuni ya kikoloni ambayo malengo yake makuu yalilikuwa kushikilia mtuhumiwa au mharifu kwa kipindi kirefu ndani ya mahabusu au magereza kwa lengo la kuweka hofu kwa wanannchi ili watii amri za kikoloni bila kuhoji.

Mara kadhaa tumekunukuu wewe na watangulizi wako mkihoji suala la kutokamilika kwa upelelezi ilihali mtu amekamatwa na ushahidi. Mfumo wa kikoloni ndivyo ulivyokuwa kwa sababu haukuwa na lengo la kumhukumu mtuhumiwa papo kwa papo. Ulikuwa na lengo la kutishia.

Hivyo hata sasa waendesha mashitaka hulazimika kutumia mfumo huo huo kwa sababu wamejifunza na kufanyia kazi mfumo huo.
Inabidi ikumbukwe kuwa muda wa mwanadamu hapa duniani una ukomo wake na hakuna mwenye uwezo wa kuongeza ila Mwenyezi Mungu. Kila siku ambayo mtu anapokwa uhuru wake kwa kuwekwa ndani siku hiyo haitarudi. Na nchi yetu haina mfumo wa kumfidia mtu ambaye alipokwa uhuru wake na baadae kesi yake kufutwa au kukutwa hana hatia.

Ibara ya 14 ya Katiba ya Nchi yetu inatoa haki ya kuishi na “kupata kutoka kwa jamii hifadhi ya maisha yake kwa mujibu wa sheria”. Aidha, Ibara ya 15 (1) inasema “Kila mtu anayo haki ya kuwa huru na kuishi kama mtu huru.” Ibara ya 15(2) inataka mtu asishikwe na kuwekwa ndani au kuhamishwa kwa nguvu na kupoteza uhuru wake isipokuwa mujibu wa sheria na pindi mtu anapokuwa ametiwa hatiani.

Hili kukidhi matakwa haya inabidi polisi na waendesha mashitaka kujiridhisha kuwa pale wanatoa tu amri ya kushikwa na kuwekwa ndani pale upelelezi unakuwa umekamilia. Aidha, haki ya kupata dhamana iheshimike.

Ni vema pia uamuzi wa Mahakama ya Rufani katika kesi ya Attorney General v. Jeremiah Mtobesya Civil Appeal No 65 of 2016 ambapo ilisema kuwa kipengele kinachompa madaraka Mwendesha Mashitaka Mkuu wa Serikali kuweka cheti cha kuzuia dhamana hata kwa makosa yanayodhaminika ni kinyume cha katiba ya nchi yetu.

Tulitegemea kuwa kutokana na uamuzi huo sheria zote zinazotoa mamlaka hayo zingebadilishwa lakini sivyo ilivyo. Hadi hivi sasa watuhumiwa wengi wenye kukabiliwa na kesi za jinai wapo ndani licha ya kuwa makosa yao yanadhaminika lakini wamewekewa hati hiyo.

Ni rai yetu kuwa mabadiliko ya suala hili linahitaji utashi wa kisiasa ili kubadilisha suala hili na pengine kuondokana kabisa na hali hii na kuepusha gharama kubwa za uendeshaji wa mashauri na kushikilia watuhumiwa kwa kipindi kirefu.

Ni vyema tujikite kutafakari kwa makini ili tuweze kuweka mfumo mzuri wa kushikilia mahabusu na wafungwa kwa muda mfupi zaidi ili nchi yetu isikae na watuhumiwa wengi mahabusu hata magerezani kwa muda mrefu.

Vivyo hivyo, ni vyema tukafanya mabadiliko ya kuwa na namna bora ya kuwatumia wafungwa ikiwa ni pamoja na kifungo cha nje kilichopo kisheria hivi sasa ili walete tija katika uzalishaji wa kitaifa na kuchangia uchumi wa nchi kwa muda mfupi badala ya kuendelea kulipatia taifa gharama kwa muda mrefu wakati tayari kwa kupatkana hatia wameshatuingiza gharama kubwa.

Kwa kufanya hivi nchi itafaidika na mambo mengi sana ikiwamo kupunguza msongamano kwenye magereza, kuonekana wazi tunaheshimu haki za binadamu na utawala wa sheria na wakati huo huo tukikuza uchumi wa taifa kupitia watuhumiwa na wafungwa.

Mh. Mgeni Rasmi, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Jambo la pili linaangukia katika muhimili wetu wa Bunge katika utungwaji wa sheria. Ni wazi kwamba falsafa ya utungwaji wa sheria inahitaji mabadiliko kwa kiasi kikubwa kwa watunga sheria, wananchi na wasimamizi wa sheria kiujumla.

Wapeleka miswaada bungeni, wabunge na hata wananchi bado hawajafahamu vyema dhana ya adhabu wanazopendekeza na baadae kufanywa kuwa sheria. Kwa kiasi kikubwa dhana iliyojengeka ni kutoa adhabu kali badala ya kutoa mafunzo kwa mkosaji na wengine ili kuzuia zaidi. Sheria ikijikita katika falsafa ya kutoa adhabu kubwa au kali huwa haitoi fundisho, haifadishi nchi, na pengine hutekelezeka kwa upande mmoja ambao ni kumshikilia mtuhumiwa lakini haitekelezeki upande wa pili ambao ni faini kwa sababu faini zinazowekwa hazilipiki na hivyo kujikuta tunajaza watu magerezani kwa wakosaji kushindwa kulipa faini!!

Ndugu Mgeni Rasmi, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Inajulikana wazi kuwa faini na adhabu za kifedha ni chanzo kikubwa cha mapato ya nchi. Kama sikosei ni chanzo cha tatu au nne ukiondoa kodi, tozo za leseni na michango ya mashirika ya umma.

Faini au adhabu zikiwekwa katika kiwango kinachowezekana kulipika kwa wakosaji kinachangia kwa kiasi kikubwa katika pato la nchi kwa sababu kinalipika kiurahisi na wakati huo huo kinabadilisha tabia ya wakosaji wa kujirudia rudia kiurahisi pia.

Faini au adhabu kubwa hailipiki na hivyo kulazimika kuchukua mfumo wa kuwekwa ndani (incarceration) ambao huleta gharama ya kuwahifadhi na pengine rushwa kwa wakosaji kutoa hongo ili kuepuka kufungwa. Tuchukue mfano ya makosa kadha wa kadha ya barabarani.

Ndio shilingi elfu 30 za kitanzania ni ndogo na zinalipika kiurahisi kwa mkosaji lakini zimeweza kupunguza makosa ya barabarani kwa kiasi kikubwa na wakati huo huo yamechangia kwa kiasi kikubwa kwenye pato la taifa.

Ukiendesha gari lako kwa faulo kutoka Dar es Salaam kuja Dodoma unaweza jikuta unamaliza pesa ya mafuta. Hivyo ukikamatwa mara mbili yaani elfu 30 mara mbili tayari unaanza kumaliza fedha yako ya matumizi na hivyo kuogopa kuendesha kwa kasi kwa kuogopa kukamatwa. Na pengine hata ukiona mtu kavaa kanzu nyeupe kwa mbali unapunguza mwendo kwa kudhani ni afisa usalama barabarani.

Kwa kuweka adhabu zinazotekeleka ni imani yetu mawakili kuwa hata watendaji wa kimahakama na watendaji wengine wa umma watapata urahisi kuyasimamia na kukusanya adhabu hizo ili zichangie katika pato nchi.

Ndugu Mgeni Rasmi, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Jambo la tatu linahusu mamlaka ya mahakama za chini ambazo hazina mamlaka ya kusikiliza makossa makubwa ya jinai kama vile mauaji, uhujumu uchumi na mengine yote yaliyoainishwa na sheria mbalimbali yanayolazimisha kusikilizwa na mahakama kuu tu.

Ni vyema suala hili likaangaliwa kwa makini hasa hasa mamlaka ya mahakama hizi kwani kwa kusema hazina mamlaka ya kusilikiza shauri hata kwa mambo madogo madogo na pengine makubwa kunachangia kwa kiasi kikubwa sana ucheleweshaji wa mashauri, kunyimwa kwa haki ya kusikilizwa kwa wakati, kutotabirika kwa muda wa uendeshaji wa shauri lake, kuongeza gharama kwa magereza ambao hulazimika kuwatunza mpaka pale shauri lao litakaposikilizwa.

Mtu wa kawaida hujiuliza au watu wanyonge hujiuliza swali dogo tu kuwa, kama mahakama haina mamlaka sasa kwanini shauri lake linapelekwa kwa hakimu asiyekuwa na mamlaka? Ni vema utaratibu wa kupeleka kesi katika mahakama isiyo na mamlaka ukomeshwe na kesi zipelekwe tu kwa mahakama zenye mamlaka.

Aidha zuio la mawakilili kufanya kazi katika Mahakama za Mwanzo liondolewe kwani hivi sasa Mahakama hizo zinaongozwa na Mahakimu Wakazi wenye shahada ya kwanza ya sheria. Na katazo hili linazuia wananchi wengi kupata huduma ya uwakilishi. Mahakama hizi za mwanzo ndizo ambazo zinasikiliza kesi nyingi nchini. Hivyo mawakili kufanya kazi katika mahakama hizo kutawawezesha wananchi kupata huduma za mawakili na kuwezesha haki kupatikana katika ngazi zote.

Mh. Mgeni Rasmi, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Kama nilivyotangulia kusema hapo awali, uwepo wa chama kila mahali na idadi kubwa ya vijana chama kina majumu makubwa ya kuwajengea uwezo wa kimaadili na uzoefu wa kazi ya uwakilishi. Chama kimeweka na kinaendelea kuweka mifumo mbalimbali ya kuwajengea uwezo ikiwa ni pamoja na uadilifu, elimu endelevu ya kisheria, uzoefu wa kazi ya kisheria, na kutoa huduma ya kisheria nchini ikiwa ni pamoja na ushauri wa kisheria au uwakilishi wa bure kwa wasiojiweza/wanyonge wakiwemo.

Hali hii inaleta changamoto ya kifedha na miundombinu. Chama kinahitaji kuwa na majengo ili kiweze kutoa mafunzo maalumu na endelevu ya kisheria ili kuwe na ubobevu (specialization) wa kisheria kwenye mambo ya kisheria yanayoongezeka kila kukicha; na chama kinahitaji fedha za kujiendesha na kujenga majengo ya kufundishia na kutoa hudumu kwa faida ya watanzania ili waweze kutatua migogoro yao kitaaluma na kisha kuwahi kwenye uzalishaji.

Hivyo basi, chama kinahitaji kuungwa mkono kwa kupewa ardhi ikiwezekana na fedha kiasi ya kujenga katika mikoa mbalimbali ya Tanzania ikiwamo hapa Dodoma ili kiweze kutoa huduma hii kiufasaha.

Ndugu Mgeni Rasmi, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Nimalizie sasa kwa kusema machache kuhusu muhimili wa Mahakama ambao unatija za kimsingi nchini kwetu katika hali zote za kiuchumi, kisiasa, kiutamaduni na hata mila na desturi zetu.

Ningependa kutoa rai kwa mahakama ambayo ina dhamana ya kulinda haki kwa watu na vyombo vyote vilivyomo kwenda mbele zaidi ili iweze kushiriki kikamilifu katika kufanya maboresho ya sheria kwa njia ya hukumu.

Naiomba mahakama isiogope kufanya maamuzi magumu ya kutengua vipengele vya sheria ambavyo vinaonekana vinaleta ukakasi kwenye katika utekeleza wa haki. Tafsiri sahihi za kiutendaji zinafanywa na mahakama. Hivyo mahakama isaidie jamii kufanya hivyo.

Najua mawakili wanaleta mashauri yanayoiomba mahakama kufanya mabadiliko ya sheria kwa kutengua baadhi ya vifungu. Kama maombi hayaambatani ni utafiti unaojitosheleza, ni vyema mahakama iwaamuru mawakili wakafanye utafiti wa kina ili iweze kutoa maamuzi yanayojitosheleza katika kufanya maboresho ya sheria kwa faida yetu sote.

Baada ya kusema hayo machache ninapenda kushukuru sana kwa mwaliko huu na kutoa wito wa kudumishwa kwa utawala wa sheria katika nchi yetu na uhuru wa mahakama.
Asanteni sana kwa kunisikiliza
DSC_0005-1024x683.jpg
DSC_0078-1024x683.jpg


Source: Kwa hisani kubwa ya TLS HOTUBA YA RAIS WA CHAMA CHA WANASHERIA WA TANGANYIKA, DR. RUGEMELEZA A.K. NSHALA KATIKA MAADHIMISHO YA SIKU YA SHERIA
 
6 Feb 2020

Mahojiano maalum :

RAIS WA TLS AFUNGUKA ASEMA NI VIGUMU KUWANYAMAZISHA WANASHERIA

MCL DIGITAL Imefanya mahojiano maalumu na Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) Daktari Rugemeleza Nshala ili kujua mambo kadha wa kadha kuhusu sheria na haki nchini



Februari 06, 2020 ni kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini Tanzania ambapo Rais Daktari John Pombe Magufuli atakuwa mgeni rasmi. Maudhui ya Maadhimisho haya yanaashiria kuanza rasmi kwa mwaka mpya wa shughuli za Mahakama na huwa yanaambatana na kauli mbiu yenye maudhui mahsusi ya kutoa elimu kwa umma juu ya shughuli za utoaji haki. Maudhui ya Mwaka 2020 ni: “Uwekezaji na Biashara: Wajibu wa Mahakama na Wadau kuweka Mazingira wezeshi ya Uwekezaji.’’ .

Source: MCL Digital
 
Huyu jamaa, namuaminia sana, ni no nonsense man when it comes to kutetea haki.
P

Tundu Lissu alituasa wakimalizana na wapinzani watasakamwa wengine pia sasa tunaona sheria mpya iliyopitishwa bungeni chini serikali ya serikali ya CCM Mpya kujaribu kuidhibiti TLS imepitishwa na wabunge walio wengi wa CCM.

Je mwezi huu February 2020 sheria hiyo kandamizi imepitishwa kuna tegemeo lilolote kuwa uchaguzi wa 2020 pia hautadhibitiwa na sheria pia matamko gandamizi ? Maana kama wameweza kufanya shambulio la kuidhoifisha TLS watashindwa vipi kufanya hivyo kwa vyama vya upinzani na asasi zingine zinazoonekana tishio kwa utawala wa CCM Mpya maana masuala ya sheria na katiba mbovu ni masuala mtambuka yanagusa maisha na sekta zote za maisha ya wananchi-huru.
 
Doh, nakumbuka nilizamia hili tukio, Hotuba ya Rais Magufuli ilikua nzuri sana.

Rais Magufuli alisifia pia Hotuba ya Rais wa TLS.

Event ilikua nzuri sana.
 
8 Feb 2020

Mwanasheria Mkuu wa Serikali Professor Adelardus Kilangi. atoa ufafanuzi kuhusu Falsafa ya Sheria upande wa maadili :

Mwanasheria Mkuu wa Serikali Professor Adelardus Kilangi. atoa ufafanuzi kuhusu Falsafa ya Sheria upande wa maadili na kukazia hasa kuhusu ushoga! Hii imetokea katika Maadhimisho ya Siku ya Sheria TANZANIA yaliyofanyika Jijini Dar-es-Salaam TANZANIA na kuhudhuriwa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli, pamoja Spika wa Bunge Mhe Ndugai na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma.



Source: Shalom TV online
 
February 6, 2020
JAJI MKUU IBRAHIM JUMA MBELE YA RAIS MAGUFULI KUFUNGA MAADHIMISHO YA WIKI YA SHERIA

 
Doh, nakumbuka nilizamia hili tukio, Hotuba ya Rais Magufuli ilikua nzuri sana.

Rais Magufuli alisifia pia Hotuba ya Rais wa TLS.

Event ilikua nzuri sana.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ameipongeza Mahakama ya Tanzania kwa utendaji mzuri wa kazi ikiwemo matumizi bora ya fedha za Serikali.

Akizungumza katika sherehe za kilele cha Siku ya Sheria nchini, Februari 06, 2020 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Mwl. Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam, Mhe. Rais alionyeshwa kufurahishwa na utendaji wa Mahakama katika Maboresho yaliyofanyika ikiwemo kupunguza mlundikano na ucheleweshaji wa mashauri, matumizi ya Tehama, Huduma ya Mahakama inayotembea ‘mobile court services’, maboresho ya miundombinu ya majengo na kadhalika.

“Leo nina furaha kubwa sana, kwa kuwa Mahakama imepata mafanikio makubwa katika kipindi cha miaka minne (4) iliyopita, hivyo nakupongeza Mhe. Jaji Mkuu na Watumishi wote wa Mahakama kwa kazi nzuri ya utoaji haki nchini,” alisema Mhe. Rais.

Mbali na pongezi hizo, Mhe. Rais aliisifu pia Mahakama kwa matumizi mazuri ya fedha zinazotolewa na Serikali kwa ajili ya matumizi mbalimbali ikiwemo ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya Mhimili huo.

“Hakuna ufisadi Mahakama, fedha zinazotolewa zinatumika vizuri, hivyo nawapongeza sana,” alieleza Mhe. Dkt. Magufuli.

Aidha; Mhe. Rais aliongeza kuwa suala la ucheleweshwaji wa usikilizwaji wa Mashauri limepungua kwa asilimia 100, huku akitoa mfano kuwa katika mwaka 2016 mlundikano wa mashauri umepungua kutoka asilimia 12 hadi asilimia 5 kwa sasa.

Katika hatua nyingine, Rais Magufuli alizungumzia juu ya mafanikio ya uanzishwaji wa Mahakama Kuu-Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi maarufu kama ‘Mahakama ya Mafisadi’ kuwa Mahakama hiyo imepata mafanikio makubwa.

“Tangu Mahakama ya Mafisadi ianzishwe mwaka 2016 jumla ya mashauri ya uhujumu uchumi 119 yamesajiliwa na mashauri 89 yamemalizika ambapo faini ya sh. bil. 13.6 na fidia ya bil.30.6 zimetolewa,” alieleza.

Aliongeza kuwa uanzishwaji wa Mahakama ya Mafisadi umeondoa dhana iliyokuwa imejengeka miongoni mwa wananchi kuwa mapambano dhidi ya rushwa nchini yamekuwa yakiwalenga wananchi wa chini na kuwaacha vigogo.

Hali kadhalika Mhe. Rais amemuhakikishia Mhe. Jaji Mkuu kushughulikia changamoto zilizopo ndani ya Mahakama ikiwemo upungufu wa rasilimali watu, maslahi duni ya watumishi, pamoja na kuongeza fedha matumizi ‘OC’.

Awali akizungumza kabla ya kumkaribisha Mhe. Rais, Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma alisema Mfumo wa Kielekitroniki wa Kusajili na Kuratibu Mashauri (JSDS II) uliouzindua mwaka jana umeendelea kuwa msaada mkubwa katika kurahisisha shughuli za uendeshaji wa mashauri.

Mhe. Prof. Juma alisema kuwa mfumo huu ambao unatoa taarifa kwa wadau kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi na barua pepe, umeunganishwa pia na wa malipo ya serikali (Government Electronic Payment Gateway (GEPG)) na Mfumo wa Kusimamia Mawakili (TAMS).

“Kuunganishwa Mfumo wa JSDS2 na mfumo wa malipo ya Serikali umeiwezesha Mahakama kudhibiti ukusanyaji wa Tozo na Ada. Udhibiti huu umewezesha ongezeko la maduhuli toka shilingi bilioni 1.6 mwaka 2017 mpaka shilingi bilioni 2.5,” alieleza Mhe. Jaji Mkuu.

Aliongeza kuwa katika kipindi cha mwaka jana jumla ya mashauri 2,435 yalifunguliwa kwa kielektroniki. Lengo la Mahakama ni kuendelea kuboresha mfumo kwa kutumia wataalamu wa ndani.

Siku ya Sheria nchini, ilitanguliwa na Maonesho ya Wiki ya Utoaji Elimu ya Sheria ambayo kitaifa ilifanyika kuanzia Januari 31 hadi Februari 05 mwaka huu ambapo kwa mwaka huu Kaulimbiu ni “Uwekezaji na biashara; Wajibu wa Mahakama na wadau katika kukuza uwekezaji na biashara.” source: https://www.judiciary.go.tz/web/index.php?r=posts/webview&id=166
 
Back
Top Bottom