Hotuba ya Rais Magufuli yawa "Lulu" duniani kote, Wachina na Wahindi wataka itafsiriwe kwa lugha za mataifa yao

Internal

JF-Expert Member
Feb 23, 2017
3,535
2,000
Lengo la wao kutaka itafsiriwe kwenye lugha yao ni kwasababu wameikubali hio hotuba?

Na kama wameikubali kuwa ni nzuri inamaana wameielewa.

Huenda kuna kitu wanataka kusikiliza tu ambacho mimi na wewe hatujui n nini.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Savimbi Jr

JF-Expert Member
Sep 23, 2011
6,815
2,000
Haya ninayoyashuhudia kwenye mitandao ikiwa ni comments ya wana Afrika mashariki walioko sehemu tofauti tofauti duniani yanaiingiza Tanzania katika historia mpya.

Kwanza watu wengi wamefuatilia hotuba ya Rais Magufuli iliyorekodiwa na kuwekwa mitandaoni. Na wengi wameusifu utafiti uliofanywa na timu ya Dr Magufuli. Baadhi ya watu kutoka China na India wameomba hotuba hiyo itafsiriwe kwa lugha za mataifa yao ili ikawanufaishe watu wengi zaidi katika nchi zao.

Mjini Mombasa, Kenya hotuba hiyo ya Rais Magufuli imezuwa gumzo kubwa na wengi wamekubaliana na Rais Magufuli juu ya wasiwasi wa ubora wa vifaa. Mombasa wanaingia katika zoezi la mass testing lakini wananchi wanataka waelimishwe zaidi kabla ya kupimwa.

Maendeleo hayana vyama!
Nilichoona mimi kwamba ile hotuba imekuwa kichekesho maana vyombo vingi vimeikejeli....Hata wataalamu wabobezi wamesema kabisa kifaa ambacho kimekuwa calibated kupima covid19 kwa sample ya binadamu hakiwezi kutoa jibu sahihi kwa viumbe au non-living things vingine lazima litatoa jibu lisiloeleweka na ndio maana ukaona oil ina corona19.
 
Imeloa

JF-Expert Member
Jan 28, 2013
8,195
2,000
The end always justifies the means. Ukishaona mwandishi ni nani inatosha kabisa kukufanya uitupe post kwenye dustbin kwani ni takataka tu.
 
Zeedaya

Member
Jan 17, 2019
80
125
Amekuwa kituko duniani kote kweli ni aibu huku ughaibuni tunadharauliwa.

Umejuaje kama tunadharauliwa?! Na mbona unajali?! Na umejuaje kama Rais hayuko sahihi?! Huenda anawachallenge mabeberu ndo maana yanampaka matope na kumfanya aonekane kituo. Yanatumia wananchi wa nchi yake kumu attack Rais. Lait ungejua jinsi mabeberu yanavyotenda kazi na nia yao hata usingejali yanafikiria nini ila ungetumia akili yako kufikiria kila anachokitenda mkuu. Usitumie media au akili ya mwingine kujudge.
 
fazili

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
8,850

Nyie ndio wafia-magu. Poleni sana kwa kazi ngumu. Madagascar ndio wametangaza jana kwamba ile dawa ya corona wanaanza kuifanyia utafiti wa kitaalam manake ilikuwa inatumika kienyeji tu kama vile mwarobaini hako kwetu. Lakini kiongozi tuliyenaye tayari alishasema atatuma ndege kuchukua dawa! Unawanyweshaje watoto wako dawa isiyothibitishwa? Unawepanda kweli?

Ishu nyingine ya aibu kubwa ni kupeleka sample za maembe, mbuzi na mapapai kupima corona. Wanaojua sayansi ya maabara ni kwamba vipimo hivi ni very specific. Huwezi kupeleka sample ya oil chafu ya magari eti kucheki ubora wa vipimo, au hata sample ya mafenesi. Wangepaswa kuchukua sample ya binadamu kwani vipimo hivi havipimi kila sample kuna specificity. Tunachekwa sana duniani.
 
Mi nipo neutral. I don't judge. Sijui nani yupo sahihi kati ya Magu na wapinzani wake.
 
residentura

JF-Expert Member
Mar 1, 2017
4,345
2,000
Mi nipo neutral. I don't judge. Sijui nani yupo sahihi kati ya Magu na wapinzani wake.
Ufunuo 3:15-16
"Nayajua matendo yako yakuwa hu baridi wala hu moto ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto. Basi kwa sababu una uvuguvungu, wala hu baridi wala moto nitakutapika utoke katika kinywa changu."

Sent using Jamii Forums mobile app
 
sengobad

JF-Expert Member
Aug 13, 2017
4,573
2,000
Tanzania tunazidi kuonekana kichwa cha mwendawazimu, kufanyia test mapapai yakakutwa positive kuna athari kubwa mbele ya safari.

Wengi wataugulia majumbani wakiamini Corona ni ugonjwa wa kawaida, wataambukiza wengi zaidi, na watakufa wengi pia.

Nchi zote duniani zinakabiliana na hili janga scientifically, nchi zote zimepoteza watu wake, but sisi bado hatujawa tayari kukubaliana na huu ukweli, kila siku tunadanganyana kwa kutafuta sababu nyepesi kulazimisha Corona ionekane sio tatizo, ulimwengu wote lazima utushangae.

Sent using Jamii Forums mobile app
Unataka wafe mara ngapi?
 
Sijijui

JF-Expert Member
Jan 14, 2018
7,893
2,000
Mkuu

Kuhusu ubora wa vifaa ni mataifa mengi yamelalamika haswa vifaa kutoka China

Na Nakumbuka wakati Msaada wa Jack ma ulivokuja kuna mtu alisema pamoja na kushukuru kwa Msaada lkn ni lazima Tuwe makini na Hivyo vifaa Kwa kuvitest ukizingatia tayariii Spain alikuwa kashalalamika juu ya vifaa from China

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwani Magufuli alisema mapapai yake yamepimwa kwa vifaa alivyopewa msaada au alivyonunua kwa pesa za walipa Kodi wa Tanzania
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom