Hotuba ya Rais Magufuli ni fumbo la fursa kwa vijana

mzalendo iq1

JF-Expert Member
Mar 10, 2020
1,261
2,000
Habari wadau,

Leo kama ulikuwa unafuatilia hotuba ya Rais John Pombe Magufuli Kama una akili utakuwa umemuelewa Rais wetu ni kiasi Gan Yuko Makin katika kutengeneza fursa kwa vijana. So vijana hamtakiwi kulala inabidi mchukue hatua.

Nadhani wote tunajua kabisa katika maneno mia ya Rais Magufuli 99 huwa yana maana nzito sana kama utakuwa mfuatiliaji wa hotuba zake utagundua hilo.

Pia, amekuwa mtabiri mzuri mwenye kujua kitu ambacho kitakachotokea mbele wazungu wanasema (future) wengi wameweza kumuamini baada ya Corona kuja na kutoa kauli ambazo zimekuwa matokea ya dunia mzima.

Turudi kwenye hotuba.

Rais Magufuli amesema watanzania tulime kwa bidii na tuweke nguvu kubwa katika kilimo pia Bei tutakayouza mazao yetu iwe nzuri na yenye faida kwetu.Tusikubali kulaliwa na walanguzi.

Kwanini Magufuli amesema tulime?

Mh Rais Magufuli kasema tulime kwa nguvu zetu zote kwa sababu anajua kabisa situation walionayo ndugu zetu wa nchi jirani. Now wameanza kuishiwa chakula hivyo baada ya muda watahitaji sana chakula na ndio itakuja kuwa bidhaa muhimu hivyo vijana ambao mnalia hali ngumu mnatakiwa mkamate fursa hiyo.

Nawashauri mkitaka kulima angalieni mazao muhimu katika nchi ambazo ni majirani zetu. Mwenzenu nina mpango wa kulima vitunguu.

Watanzania amkeni atakayelima sasa hivi baada ya miezi sita atauza mazao yake kwa bei nzuri na atapata faida, tuache kukaa vijiweni tukafanye kazi.

Chukueni fursa wadau muda ndiyo huu wakati wenzetu wamejifungia sisi tufanye kazi kwa juhud zetu zote ili wakija kuamka tuwe mbele yao kwa hatua nyingi pia tuwe tegemeo kwao.

Kumbuka wakati Uingereza anapigana Vita Marekani alikuwa bize anajijenga.

Wenye akili watakuwa wameelewa, wajinga watabaki na ujinga wao.
 

Mpatuka

JF-Expert Member
Nov 15, 2015
646
1,000
Mazao ya msimu, hayafanyiki muda wowote utegemea majira ya mwaka. Horticultural crops most depend on irrigation, Hivyo kwa mazingira hayo bado huyu kijana ana wakati mgumu kuchangamkia fursa hii.

Ni sawa na kumpeleka mwanajeshi vitan halafu umwache eneo la vita bila silaha yoyote Ile, Japo wapo watakaoweza kupambana kutokana na misingi imara kiuchumi walionayo, Hii kauli ya Raisi inamfaa sana Sumry yule mfanya biashara wa mabasi alieamua kuuza yote na kuwekeza kwenye kilimo.
 

evonik

JF-Expert Member
Jun 12, 2015
2,879
2,000
Huna mtaji unaenda kulima nini, wanaolima wote wana mitaji, anakwambia analima huku mshahara upo, sasa we kalime afu una hela hiyoyo
 

Mwaikibaki

JF-Expert Member
Mar 19, 2015
2,045
2,000
Wacha tu watu waendelee kujitoa akili na kujiaminisha kila lisemwalo, mwanzo mlisema huyu ndiye tuliyekua tukimngoja, mara maisha yamekua magumua, mara fursa etc... endeleeeni tu! Mtaelewa...
 

mzalendo iq1

JF-Expert Member
Mar 10, 2020
1,261
2,000
Kwaio unataka upewe mtaji ndio ukalime? Aisee hiv wewe ni jisnia Gan Mana nisije kuku dharau kumbe ni wakike na kuomba mtaji ni haki yako Ila Kama ni mwanaume pole

Kwaio wanao Lima wote wamepewa mitaji
Huna mtaji unaenda kulima nini, wanaolima wote wana mitaji, anakwambia analima huku mshahara upo, sasa we kalime afu una hela hiyoyo
 

mzalendo iq1

JF-Expert Member
Mar 10, 2020
1,261
2,000
Maisha yamekua magum kwa wavivu na wategemea porojo ili wale
Wacha tu watu waendelee kujitoa akili na kujiaminisha kila lisemwalo, mwanzo mlisema huyu ndiye tuliyekua tukimngoja, mara maisha yamekua magumua, mara fursa etc... endeleeeni tu! Mtaelewa...
 

mzalendo iq1

JF-Expert Member
Mar 10, 2020
1,261
2,000
Wale ni mabingwa wa muulize maaaa wao kazi wanayo taka ni kushinda na cm kutukana serekal wakimaliza wanaenda kwa Dj kugawana hela za ruzuku maisha yanaenda.

Ila watanzania wapambanaji naiman uko vijijn wako wanalima kwa speed ya 5g
Wakaa vijiweni na kucheza pool table hawataelewa na watakuja na povu
 
May 18, 2020
52
125
Nenda uone wenye vitunguu wanavyokula loss hapo kuingia kenya.hatukukatazi kumpongeza mtu ila unaandika mada na unaongea kinyume cha hali halisi
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom