Hotuba ya Rais Magufuli kwenye mkutano wa CCM iwe silaha kwenu vijana

Elius W Ndabila

JF-Expert Member
Jul 17, 2019
322
645
Kwenye hotuba yake Mwenyekiti wa CCM amezungumza mambo mengi. Lakini ninataka ninukuu mambo mawili.

Jambo la kwanza amesema yeye na viongozi wengine hawana mgombea mfukoni. Jambo la pili amewaagiza viongozi kutenda haki kwenye vikao vya uteuzi na kutokuwakatisha tamaa wengine.

Funzo kubwa kwenye nukuu hizi ni kuwa kijana yeyote mwenye nia ya Udiwani akajaribu bahati yake. Vijana waache kutumia muda mwingi kuwanadi watu, badala yake vijana watumie muda kujitengeneza wao na si kutengeneza watu.

Si hivyo tu, pia vijana waache kuaminishwa na watu wanaopita majimboni kuwa wametumwa na watu wakubwa, hizo ni propaganda za kutafuta huruma za kupendwa.

Kama wewe huna mpango wa kugombea na kazi yako ni kuwanadi watu, basi tumia vizuri hiyo fursa bila kuwaathiri wengine.

My take: Hadi Sasa mwenye uhakika wa kuteuliwa kugombea ni Konde boy tu, wengine huko majimboni wasiwasumbue kuwa wametumwa. Wamejituma!
 
Kwani kuna Uchaguzi mwaka huu? Mie nilidhani wale wenye viti wa vijiji wawe madiwani na wenye viti wa mitaa wawe Wabunge tuwapandishe vyeo hakuna haja ya kupoteza pesa
 
Kama kijana nimejipanga vilivyo. jimbo la Njombe mjini. m/kiti wetu yuko vema. Anaesema ametumwa wakati si kweli, ni ishara tosha kuwa hajiamini. Na kutijiamini nikushindwa
 
Kebwe umesikia eee?
Ushindwe Morogoro ukuu wa mkoa,halafu unakwenda kuwadanganya watu eti umetumwa na mh?
Tafuta kiki nyingine sasa.
Acha kumsumbua Katibu wa CCM Serengeti amekuchoka Acha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vijana wa Tanzania ebu tujaribu kuwa wabunifu ili kijenga tija katika uzalishaji si kila mtu kukimbilia kwenye siasa za udiwani na ubunge!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom