Hotuba ya Rais Magufuli kwa EALA: Kulikuwa na ulazima gani kuitambulisha CCM?

Mzalendo2015

JF-Expert Member
Aug 14, 2012
6,697
9,048
Wana JF,
Nauliza nani huandaa hotuba za RaIS Magufuli kwenye Mikutano ya Kitaifa na Kimataifa?
Nauliza hivi kwasababu Rais Magufuli hujikuta akiongea mambo fulani mbele ya hadhira ambayo aghalabu hayana uhusiano kabisa na hadhira anayoihutubia...!Hii ni aibu.

Nimeangalia hotuba ya JPM kwa Bunge la EALA akikitambulisha chama cha Mapinduzi kuwa ndiyo chama TAWALA TANZANIA...!!Nimesikitishwa sana Rais kuongelea mambo ya uchama kwenye jumuia ya Kimataifa ya East Afrika ina jumuisha nchi 6 na zenye Vyama na Makabila tofauti tofauti. Yawezekana ndiyo maana hata katika utambulisho wa Kiongozi wa KUB-Mhe. Mbowe camera za TV ya Bunge hazikumwonyesha kabisa Mhe. Mbowe.....kwa vile yeye si CCM.....!!

Kuzungumzia mambo ya CCM kwenye mkusanyiko kama huu ni kutaka kuchochea migawanyiko,utengano, uchama, utaifa na hatimaye ukabila na kubaguana. Hii si mara ya kwanza kwa JPM kuzungumzia mambo ya uchama kwenye hadhira inayohusisha zaidi ya nchi moja. Nakumbuka wakti wa uzinduzi wa Bomba la Mafuta Hoima-Uganda mpaka Chongoleani-Tanga JPM aligusia mambo ya CCM mbele ya mgeni wake M-7 lakini mgeni aliposimama hakusema chochote kuhusu NMR ya Uganda au chama chochote kinachotawala huko...!

JPM asaidiwe katika kuandaa hutuba zake....vinginevyo analigawa Taifa na hatimaye East Afrika yote!EAC ilikufa mwaka 1977 kwa ubinafsi wa Viongozi kama huu anaofanya Rais wa Tanzania..!
 
Mbona taifa alishaligawa tayari? Huu ni muendelezo wake tu wa kuligawa taifa. Mtu ambaye CCM kwake ni adui.
 
Anahitaji elimu!
Mnahabari kwamba hili jiwe linaidhalilisha tanzania kitaifa na kimataifa,
Ndio maana hathubutu kutoka nje ya afrika maana anaweza kwenda kwenye vikao huko washinton au huko ubelgiji ukashangaa anawaambia wazungu CCM HOYEEE!

Tumepata aibu ya karne eti
 
Kwa hiyo umeuuumiaaaa utanidhani Rais kaitambulisha ACT wazalendo. Kesho kwenye uzinduzi wa barabara atatambukisha CHADEMA endelea kusikiliza redio ufurahi.
 
Shida yako ni Magufuli kuitaja ccm, au Mbowe kutooneshwa.
Mtajigawa wenyewe.

Oil,
Kama wewe ni Oil basi ni OIL CHAFU...!!
Tatizo hapa ni UBAGUZI WA KIVYAMA, UKANDA NA UKABILA...!!!
Hivi wewe uko ndani ya Chama cha Majambazi hujui kuna mambo kama hayo anayoyafanya Mwenyekiti wako??
 
Back
Top Bottom