Hotuba ya Rais Kikwete - Sept 2013: Akubaliana na wapinzani muswada urejeshwe Bungeni

Unashangaa JK kujadili watu haushangai kina Obama, Bush, kumjadili Mugabe, kwenye hotuba zao.

Eti unataka, wewe nani mpaka utake kumpangia rais cha kuongea.

Hotuba ya rais Kikwete ni hotuba bora kabisa.
Ritz

Punguza kiherehere na kudandia mambo yasiyokuhusu mwisho utaelekea kizani.
Nilikuwa namjibu ndugu yako ZeMarcopolo kwahiyo yeye ndio anajua tumetoka wapi hadi nikamjibu hivi. Sasa wewe unadandia treni kwa mbele na kiherehere chako.
 
Last edited by a moderator:
Hivi kuna unafiki zaidi ya ule wa kumuita mtu mnafki alafu ukafata mawazo yake?

Hotuba nzuri my white foot!
 
Bado sijaona lolote la kupongezwa kwenye hii.hotuba.nimeisoma yote na sijaona dhamira ya kubadili chochote zaidi sana nimeona mpango wa kuwa single out chadema waonekane ndo wabaya.kuna mpango wa kuvunja ule.umoja wa wapinzani.tukumbuke umoja ule umeshikiliwa na hoja ya zenji kutohusishwa na jk kashupalia hapo na patarekebishwa ila hoja zingine zote zitabakia....je hizo hoja zingine cuf ama tume ya katiba ama nccr wana interest nazo? .divide and rule is wht he can do the best
 
Naona mimi tusubiri mazungumzo na wapinzani yafanyike. Kuanza kubashiri matokeo si sahihi sana.

Angalau Rais kaonyesha busara yakuleta amani ndani ya nyumba.
 
Ni ajabu kwa mtu msomi na anayejua sheria kuwa mwongo na mnafiki. tena kasomeshwa na kodi zetu.

Mamndenyi, huwa nazikubalisana comments zako. Lakini naomba kutofautiana nawe kwa hii comment yako inayokubali kuwa Lisu ni mwongo na Mzandiki kama mkuu wetu wa kaya alivyosema! Nadhani hapa umepotoka tu.
 
Hivi hii lugha "niyasemee" ina maana gani? Ni kana kwamba msemaji anafanya hivyo kwa niaba ya mtu au watu au jambo fulani. Kwamba si jukumu lake kusema anachokisema na anatoa tu msaada kwa kufanya hivyo. Kwamba kuna watu au mambo ambayo yalitakiwa kusema lakini kwa kuwa hayajafanya hivyo, huyu Mheshimiwa ameamua kuyasemea. This does not get across as coming from someone who think he has a role to play in all this.

Lugha hii (pamoja na maneno kama "nimeambiwa", "nimeshauriwa") pia inaashiria kuwa msemaji ni "passive" as opposed to "active". "Nimeshauriwa na nimekubali angalau niyasemee baadhi ya mambo huenda itasaidia". Hapa msemaji anaonesha kuwa si mtendaji na kwamba anasema tu ili kujaribu kubadili maoni na mtizamo katika jamii. He is not action oriented. Haoneshi kuwa ana mamlaka (authority). Na anaonesha kuwa kuna watu wanamtumia kusema pengine kwa maslahi yao. Lakini yeye mwenyewe yuko disconnected with reality on the ground.

Mheshimiwa pia anaonesha kuna mambo ya muhimu lakini "hatayasemea" sasa, let alone taking actions. "Niwieni radhi nisipoyasemea baadhi ya mambo siyo kwa kuyapuuza, bali kwa kuepuka hotuba kuwa ndefu mno". Anaogopa hotuba kuwa ndefu. Hii inaashiria kuwa hayo mambo si ya muhimu and there is no sense of urgency whatsoever. Kama jambo ni la muhimu, hotuba kuwa ndefu inaweza kuwa sababu ya kutolijadili na kulipatia ufumbuzi? Eti mpaka mwisho wa mwezi ufike?

Recap: "Kuyasemea", "Nimeambiwa", "Nimeshauriwa".
 
Safari Hii anawaandalia Juice ya aina gani huko IKULU??AU TOGWA KAMA ANAVOSEMA Nguruvi3??


CCM ina laana hii,si bure...
 
Last edited by a moderator:
Kuna watu walimsihi Mhe. Rais asizingatie hoja za Wapinzani na watu wenye nia njema kuhusu sheria hii na atie saini mswada kuwa sheria. Watu hao ni pamoja na Mhe. Chikawe, Ritz, Zemarcopolo, Nape,Kinana na wengineo. Rais anachanganya akili za kupewa na za kwake anaona kuna hoja. Kimsingi, anakataa kutia saini muswada ule na anaurudisha bungeni. Mhe. Chikawe analipi la kusema zaidi ya kujiuzulu?

Mhe. Chikawe na wenzake walidanganya kuwa Wazanzibari walishirikishwa. Leo Rais anakubaliana na hoja kuwa Wazanzibari hawakushirikishwa. Mhe. Chikawe na wenzake ni waongo na watu ambao ni hatari kwa taifa. Mhe. Chikawe na wenzake wanatoa wapi uhalali wa kuendelea kushika nafasi walizonazo? Mimi nadhani wajipime na wafanye maamuzi yenye busara. Hawa watu watatoa wapi uthubutu wa kumshauri Mhe. Rais siku zijazo? Kwa maneno mengine, Mhe. Rais ni kama ameliambia taifa kuwa hawa watu ni reject.

umemsahau balozi seif na yeye alishupalia kusema asichokijua kulinda maslahi yake
 
Rais akumbuke mfano aliowapa wafanyakazi walipogoma pale alipowahutubia wazee wa dar kwenye ukumbi wa diamond jublee kwa kutoa mfano wa Kongota kutoboa viota huku Mbayuwayu wakinyeshewa na mvua,ukiambiwa changanya na akili zako sio kufanyia kazi tu cha kuambiwa.

Kwa nn yeye amafanyia kazi akilio za kuambiwa badala ya kuchanganya na zake?
Hapa Rais umejifunza nn?huna washauri makini.
 
Tayari Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ndugu Jakaya Mrisho Kikwete 'amewashambulia' waziwazi watanzania wawili katika hotuba zake kwa Wazee wa Dar es Salaam na ya Mwezi Septemba. Hotuba,bila kupepesa macho wala kumung'unya maneno imewataja wananchi wawili wa Tanzania ambao 'walimgusa' Rais.

Wa kwanza alikuwa Nicholaus Mgaya wa TUCTA (wakati huo alikuwa akikaimu Ukatibu Mkuu). Mgaya alitajwa na kusemwa na Rais katika hotuba yake mbele ya Wazee wa Dar es Salaam. Wa pili ni Tundu A.M.Lissu. Ni katika hotuba ya Septemba mwaka huu huu. Juzi tu hapa.

Wakati Mgaya alitajwa kama mtu ambaye asingekuwa msaada kwa wafanyakazi ambao wangegoma kwakuwa 'asingekuwepo', Lissu yeye ameitwa mzandiki na mzushi.

Kimsingi, hotuba za Rais wa nchi ni hotuba zenye mamlaka zaidi nchini. Ni kuu zaidi ya zote. Ukitajwa kwa mema katika hotuba hizo, utavimba kichwa. Kwa mabaya, panakuwa hapatoshi. Kutajwa vibaya katika hotuba ni vitisho tosha. Ni kuonywa na kupewa muda wa kujirekebisha. Lakini, kwa kosa lipi hasa? Kosa litokanalo na kutimiza wajibu wao? Kwanini kabla ya vitisho hivyo watajwa hawajapewa nafasi ya kujieleza na wakaeleweka vyema?

Siuoni utaratibu huu kama ni wa kufaa sana. Ukiepukwa ni bora zaidi.Sasa nani atafuata?

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
 
Usishangae sana watu wa pwani ndo wako hivyo?? Lissu piga kazi baba tuko nyuma yako..!!!
 
Back
Top Bottom