Ground Zero
JF-Expert Member
- Jan 13, 2011
- 342
- 95
TBC1 imetangaza kwenye taarifa ya saa 2 usiku kwamba rais Kikwete atahutubia taifa: Hii hapa Taarifa Hotuba yake. Pekua chini kwa hotuba yake kimaandishi.
Last edited by a moderator:
TBC-Televisheni ya Taifa inapotoa tangazo, halifanyiki na hawatoi ufafanuzi tuwaeleweje?Sisi kama watanzania tunaihitaji sana hiyo hotuba, tena hotuba inayotoa ufafanuzi wa matatizo ya wananchi na sio kuwatuhumu watu au vyama juu ya vitu fulani.
Hotuba nzuri sana, amejitahidi kuelezea juu ya uraia wa nchi mbili kitu ambacho kimekuwa kikisumbua sana wananchi. Nadhani baada ya hii hotuba watu watakuwa wameshapata majibu ya matatizo yao mbalimbali.
Pananitatiza pale kwenye red: Hajui au anajifanya hajui hali halisi. Orodha ya wapiga kura ni ileile ya mwaka jana hivyo kuna maelfu ya watu (vijana) waliotimiza miaka 18 katika kipindi cha takriban mwaka mmoja uliopita hawamo katika orodha, kwa sababu NEC haiikufanya utaratibu wa kuwaandikisha.
Pili kuna maelfu pia ambao wamepoteza kadi zao za uandikishaji ambao hawataweza kupiga kura kwa sababu NEC haikufanya utaratibu wa kuwapatia kadi nyingine.
Sasa hiyo haki ya Kikatiba iko wapi?