Hotuba ya rais Kikwete ililenga kujibu tuhuma za Godbless Lema? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hotuba ya rais Kikwete ililenga kujibu tuhuma za Godbless Lema?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mohamedi Mtoi, Jun 3, 2012.

 1. Mohamedi Mtoi

  Mohamedi Mtoi R I P

  #1
  Jun 3, 2012
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 3,326
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 0
  Wakuu salaam alykum.

  "Afadhali vita inayosaka haki na heshima kuliko amani inayopumbaza akili na kudhalilisha utu wa mwanadamu"
  haya ni maneno yanayo penda kutamkwa na aliyekuwa Mheshimiwa mbunge wa Arusha mjini kila alipopata fursa ya kuongea na wananchi, mara ya mwisho nimemsikia akitamka maneno hayo kwenye uzinduzi wa M4C tarehe 26 Mei 2012.

  Mtakumbuka kuwa alinyang'anywa ubunge kwa hukumu ya mahakama. Hukumu ambayo ilizaa minong'ono na kupigiwa kelele kwenye kila kona ya wapenda haki. Na hata alipo kuwa anahutubia umati wa wanachama wa Chadema pale NMC mwenyeki wa Chadema mheshimiwa Mbowe alisema "Hatuwezi kunyamaza kwa kukubali hukumu yenye maamuzi ya kihuni na ukandamizaji wa haki" ukumbuke pia kuwa kauli ya Mbowe ilisha tanguliwa na kauli ya Godbless Lema mara tu baada ya hukumu iliyo mpoka ubunge wake, alisema "Nilishapata taarifa mapema juu ya hitimisho ya kesi hii, nimenyang'anywa ubunge kwa maelekezo ya mkubwa wa ikulu".

  Kama mtakumbuka siku hiyohiyo kurugenzi ya mawasiliano Ikulu ikatoa tamko (taarifa kwa vyombo vya habari) kukanusha kauli za Lema. Kwenye taarifa hiyo kwa vyombo vya habari yalitumika maneno na kauli zilizo zaa mijadala mipya mitaani kwa walala hoi hai. Moja ya wapo ya kauli ilisema kwenye taarifa ile ilisema "Mheshimiwa lema aache kutapatapa na asimtafute mchawi... Apuuzwe maana kauli zake ni upuuzi mtupu" lakini pia taarifa ile ilisema "Rais hakufanya mawasiliano ya aina yoyote iwe ya simu, au barua kuingilia uhuru wa mahakama"

  Jana kwenye hotuba yake ya mwisho wa Mwezi wakati rais anahutubia alisema

  Kwenye hiyo kauli hapo juu kuna kifuniko cha siri ambacho ni mkuu tu peke yake ndio anajua kinafunguliwaje.

  Miaka miwili iliyopita Arusha haikuwa na amani?! Nani aliitowesha amani iliyokuwa Arusha?! Wenye dhamana ya kusimamia na kuidumisha amani nao walikuwa hawataki Arusha iwe Geniva ya Afrika?! Kwani hiyo miaka miwili iliyopita, yaani baada ya uchaguzi wa 2010 hadi mwaka huu 2012 nani alikuwa muwakilishi wa wananchi aliye shindwa kuihubiri amani na kuiacha itoweke?! Yeye ndio alitowesha amani na kuharibu sifa ya Geniva kwa kuwauwa raia 3 mmoja akiwa wa nchi jirani?! Kwa nini yaliyopita yaitwe ndwele ili tusi yagange hasa kwa Arusha? Na tusigange yapi, ya kutokuwa na amani Arusha au zile lawama za kipuuzi za kuingilia uhuru wa mahakama? Au tusiyagange kwa wananchi wa Geneva kutokuwa na muwakilishi wanayempenda hata kama anatafsirika kuwa anapenda kwenda jela pale anapotishiwa kuuwawa?

  Mimi sio mbobezi wa somo la Mantiki (logic) bado ni mwanafunzi ninae jitahidi kulifaulu somo hilo. Tunao magwiji wabobezi wanaojua tundu la sindano linaingia uzi wenye ukubwa gani. Wanaweza kung'amua maneno aliyo shona mkuu kwenye hotuba yake ikiwa ni pamoja na kuunganisha nukta za kauli za mara kwa mara za yule mkuu wa mkoa wa Arusha.

  Labda nitamuuliza lakini sijui kwa nini Lema hupenda kusema "Afadhari vita inayosaka haki na heshima kuliko amani inayo pumbaza akili na kudhalilisha utu wa mwanadamu"

  Nimeamka angalau niandike baada ya kukumbuka maneno ya Martin Luther King aliyekuwa kuwa mpigania haki za weusi kule Marekani. Alisema "Our lives begin to end the day we become silent about things that matter", halafu aliwahi kusema tena "It has come a time when silence become a betrayal"
   
 2. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #2
  Jun 3, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  It was a matter of time only before realizing it. Lema was right
   
 3. Havizya

  Havizya JF-Expert Member

  #3
  Jun 3, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 1,573
  Likes Received: 169
  Trophy Points: 160
  Siku za kutawala Kikwete na ccm yake zinahesabika. Utamu wa kuwa wapinzani na chama cha upinzani wataanza kuupata muda si mrefu sana kuanzia sasa. Kikwete asituaminishe watz kuwa Lema ni mleta vurugu, sisi tunaamini Lema ni mtetezi na mpigania haki kwa Watz wote. Lema usikatishwe tamaa na muuza sura huyo!
   
 4. C

  Chokler Member

  #4
  Jun 3, 2012
  Joined: Feb 16, 2012
  Messages: 69
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kila nafsi itasaka haki popote na kwa vyovyote itakapobidi. Hata wakati wa mkoloni kulikuwa na baadha ya watu walipenda kuendelea kutumikishwa na kukosa haki ila kuna waliochukia ndio maana zama hizo zilitoweka na kudidimizwa kabisa. Sasa niwakati wa mapambano ya kumtokomeza adui ujinga kwa Watanzania tudhubutu kujaribu mabadiliko....
   
 5. Kasimba G

  Kasimba G JF-Expert Member

  #5
  Jun 3, 2012
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,571
  Likes Received: 571
  Trophy Points: 280
  Nina wasiwasi mkubwa na IQ za viongozi wetu, hata kama kulikuwa na mkono wake! sasa anatutangazia waziwazi kuwa hukumu ni yeye kaandika, mahakama zitasimamia wapi na aibu hiyo kubwa? Jamani viongozi wetu ji janga la Taifa! Hivi hata kama kahusika si afadhali angekaa kimya? au ilikuwa laazima atangaze kuwa kahusika na hukumu? Mmmh! Kwa kweli nchi yetu imekosa viongozi wenye Muono, i mean walioko madarakani!

  Sasa amamdhalilisha jaji, kajidhalilisha mwenyewe, hivi kweli huyu bwana ana washauri? Au ndio haambiliki? Hotuba ya jana kajidhalilisha saana na system nzima!
   
 6. bg_dg_dy

  bg_dg_dy JF-Expert Member

  #6
  Jun 3, 2012
  Joined: Feb 27, 2009
  Messages: 452
  Likes Received: 163
  Trophy Points: 60
  hahahaha kikwete bana, ndo mana uchaguzi haujaitishwa mapema walikuwa wanasubiria kikao hicho hapo Arusha. Ila all in all uchaguzi ukifanyika Chadema watachukua jimbo pale Arusha CCM hawana chao
   
 7. mamaWILLE

  mamaWILLE Senior Member

  #7
  Jun 3, 2012
  Joined: Jul 27, 2011
  Messages: 152
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Nimeamini alichokisema Lema pale uwanjani Arusha. Kuvuliwa Lema ubunge hakika ikulu ina mkono wake kama mawazo yangu ni sahìhi. Kwani ni kweli Lema baada ya kutoa tamko dhidi ya ikulu ghafla ikulu ilijibu na si utaratibu wa ikulu kujibu kwa ghafla kama ilivyofanya dhidi ya Lema.

  Kuna uwezekano mkubwa Lema alisema kweli dhidi ya ikulu kumuondolea ubunge. Mungu tusaidie
   
 8. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #8
  Jun 3, 2012
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,856
  Likes Received: 2,432
  Trophy Points: 280
  Wananchi wa Arusha wana akili timamu.....muda wote wameteswa kwa kuchagua mpinzani....,serikali kwa makusudi umeacha kuleta mikutano...,barabara kwa makusudi hata zile ambazo pesa zipo ..ujenzi ujenzi uakasimamishwa ....siasa uchwara...
   
 9. Comi

  Comi JF-Expert Member

  #9
  Jun 3, 2012
  Joined: Oct 2, 2011
  Messages: 3,347
  Likes Received: 478
  Trophy Points: 180
  Du sikujua kuwa kugombania haki yako ni uvunjufu wa amani.

  Kwa mkazi wa Arusha ndiye anajua kuwa Lema ni kiongozi wa aina gani, walishakula hela za barabara lema kawashikia chini mda huu barabara zinatengenezwa, machinga walikuwa wananyanyaswa lema kuja wanafanya biashara zao, wanafurahi wamama wanavyochukuliwa mboga zao na manispaa yao ya CCM? Mgambo walikuwa wanafunga watu mashati je baada ya lema kuchaguliwa kuna kitu kama hicho? La hasha, kiwanja cha pale kilombero CCM wameuza kinyemela na wakataka kujenga kama lema asingekuwa mzalendo asingezuia ujenzi.

  TUTAPAMBANA NAO MPAKA KIELEWEKE
   
 10. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #10
  Jun 3, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  batilda vs jiwe....,,jiwe linaibuka mshindi.huu ndio ukweli mchungu.
   
 11. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #11
  Jun 3, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Yana mwisho na mwisho wenyewe ndio huu kwani CCM imekufa!
   
 12. nashy

  nashy JF-Expert Member

  #12
  Jun 3, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 679
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  ipo siku itafahamika tu kama si leo ni kesho, na hayu mbayuwayu atang'oka tena kwa aibu kubwa, tumechoka na unafiki wake
   
 13. S

  Sheshejr JF-Expert Member

  #13
  Jun 3, 2012
  Joined: Jan 14, 2012
  Messages: 435
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  "Ukweli cku zote hauwez kushndana na uongo na hata ikitokea uongo ukashnda, ushnd huu wa uongo utadum muda mfupi sana kabla ya ukweli kujdhihirisha." - G . Lema, na kweli kikwete u made it come true.
   
 14. mwenyenguvu

  mwenyenguvu Senior Member

  #14
  Jun 3, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 166
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  sasa mwenyewe kikwete amethibitisha yote aliyosema kamanda lema kuwa ikulu ilitia mkono,hapo ndio movie inaanza upya kabisa yaan vasco da gama mwenyewe amekiri kuwa mahakama ilipewa kimemo cha hukumu toka ikulu,hakika ccm na serkali yake mmefika mwisho wash*** *zi nyinyi
   
 15. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #15
  Jun 3, 2012
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,962
  Likes Received: 1,284
  Trophy Points: 280
  mkuu wa kaya siku zote ni kilaza
   
 16. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #16
  Jun 3, 2012
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,548
  Likes Received: 2,276
  Trophy Points: 280
  Yani mimi nashawishika kusema CCM hawtaki kusikia jimbo la Arusha linachukuliwa mikononi mwao hivyo wakotayari kuhatarisha amani na kumwaga damu pale ili mradi kiti hicho kinakaa kwao lakini mwisho wasiku wananchi wa Arusha ndio wenye uamzi wa mwisho.
   
 17. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #17
  Jun 3, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Kwa ishu ya Arusha hotuba ya Jk ya jana ilijaa usanii na siasa za maneno. Kama ni kutoweka kwa amani ya Arusha mtuhumiwa namba moja ni Kikwete, anafuatia Mwema, Andengenye na Mwombeji.
  Jk asifikiri watanzania ni wajinga kama anavyofikiri, na kutoa hotuba ambayo yeye mwenyewe alijionea haya wakati anaongea. Uso wake ulionekana umejaa hofu. Ni dhahiri hata anayemtengenezea hotuba hana nia njema na Jk.

  NI HERI YA VITA INAYOTAFUTA HAKI NA USAWA, KULIKO AMANI INAYOPUMBAZA NA KUDHALILISHA UTU WA MWANADAMU - G. Lema
   
 18. Ibra Mo

  Ibra Mo JF-Expert Member

  #18
  Jun 3, 2012
  Joined: Oct 27, 2010
  Messages: 795
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Uchambuzi mzuri sana Mohamed hongera kwa sana...Hii kauli ya Mheshimiwa Raisi wetu kwakweli inasikitisha nakudhiirisha kabisa ubakaji wa Demokrasia ambapo wananchi wamenyimwa fursa yakuwakilishwa na kiongozi wao waliemchagua,Pili inajidhiirisha kabisa kuingiliwa kwa chombo muhimu kama Mahakama katika kutenda Haki na hapo ndo inakuja point ya msingi juu ya mamlaka ya Raisi kuteua Majaji ambao wanawajibika kwake(Mteuzi)na sio kusimamia haki kama inavyowapasa.Hii ni kauli nzito ambayo Chadema wanatakiwa kuitumia kama nukuu katita Rufaa yao dhidi ya Lema.
   
 19. mashami

  mashami Senior Member

  #19
  Jun 3, 2012
  Joined: May 8, 2012
  Messages: 183
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  "Afadhali vita inayosaka haki na heshima kuliko amani inayopumbaza akili na kudhalilisha utu wa mwanadamu"haya maneno DAIMA HAYATATOKA MIIOYONI MWETU WANA ARUSHA
  "msiogope niko tayari kufa kwa ajili ya kusaka haki ya wanyonge"
  2015 siyo mbali
   
 20. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #20
  Jun 3, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  watu watano akiwemo mwenyekiti wa chadema USA river wameuawa kikatili huko huko arusha hiyo unayosema ni ipi?au amani ya kuendeleza tenda za kifisadi.
   
Loading...