Hotuba ya Rais Karume kwenye Sherehe za Mapinduzi Zanzibar:The Best Ever! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hotuba ya Rais Karume kwenye Sherehe za Mapinduzi Zanzibar:The Best Ever!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pascal Mayalla, Jan 12, 2010.

 1. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #1
  Jan 12, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,560
  Likes Received: 18,289
  Trophy Points: 280
  Rais Karume ndio kwanza amemaza kuhutubu sherehe za Mapinduzi Zanzibar kutokea kisiwani Pemba.

  Kwa maoni yangu, its the best ever tangu nimekuwa nikimsikiliza Mheshimiwa huyu huko nyuma.  Dondoo Muhimu:
  1. Amesema hatogombea tena kwa mujibu wa katiba.
  2. Ameupongeza muafaka wake na Maalim Seif na kusifu motokea mema yake ya awali.
  3. Ametumia lugha ya kistaaranu iliyojaa hekima na busara, huko nyuma zilikuwa ni mafumbo na vijembe.
  4. Amezungumzia issue zote muhimu kwa mustakabali wa Zanzibar
  5. Amezungumzia Muungano ni Dhima.
  6. Ametoa hakikisho la Uchaguri huru na wa haki.
  7. Wenye sifa wote, wataandikishwa. ZEK itapitisha tena uandikishaji upya.
  8. Wote wenye sifa za kupata ZID, watapatiwa na wote wenye ZID walionywima kwenda kuzichukua, wakazichukue.
  9. Kwa ujasiri mkubwa na lugha ya kistaarabu sana, ameyaomba gesi na mafuta yao, yawe yao, kama ilivyo bara na dhahabu yetu.
  10. Amemsifu sana Rais Kikwete, na kumalizia kwa ile ile kauli Adhimu "Mapinduzi Daima".
   
 2. O

  Omumura JF-Expert Member

  #2
  Jan 12, 2010
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Tungoje vitendo mkuu,baada ya hotuba ameulizwa Alli Ameir kuhusu karume kasema hatagombea, jamaa akajibu, amesema kwa mujibu wa katiba lakini sio kwamba hatagombea!! Mambo ya zenj hayo!
   
 3. FairPlayer

  FairPlayer JF-Expert Member

  #3
  Jan 12, 2010
  Joined: Feb 27, 2006
  Messages: 4,166
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Karume hatogombea tena hilo nina uhakika nalo.
   
 4. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #4
  Jan 12, 2010
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Tangu lini dhahabu, almasi n.k. vimekuwa vya watu wa bara peke yao? Mapato yake yote si yanakwenda kwenye wizara ya fedha ambayo ni ya muungano? Jeshi,mabalozi, vyuo vikuu si vyote vinahudumiwa kutokana na mapato hayo? Vyote hivi si vinatoa huduma kwa Zanzibar pia? Mahospitali nayo si yanahudumiwa kutokana na mapato hayo? Wazanzibari si wanapata huduma katika hizi hospitali kama mtanzania mwengine yeyote? Mimi ningeelewa kuwa hayo madhahabu, matanzanite, gesi, pamba, kahawa ni vya watu wa bara peke yao kama wangekuwa na wizara yao ya fedha na bajeti yao peke yao. Katika hali iliyopo sasa, si sahihi kusema kuwa hivyo ni vya bara. Wakitaka iwe hivyo basi tuwe na wizara ya fedha yetu kama ilivyo Zanzibar. Hapo nasi tutafaidika na hayo madini kama vile wenzetu wanavyofaidika na karafuu yao!

  Amandla......
   
 5. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #5
  Jan 12, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,560
  Likes Received: 18,289
  Trophy Points: 280
  Mode, naomba nieditie, ondoa hiyo prefix ya very important, pia isomeke Hotuba na pale pasomeke Mapinduzi ya Zanzibar sio pemba.
   
 6. BinMgen

  BinMgen JF-Expert Member

  #6
  Jan 12, 2010
  Joined: Jun 18, 2008
  Messages: 1,816
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  zanzibar wameelewana tanganyika mlie tu!
   
 7. Nono

  Nono JF-Expert Member

  #7
  Jan 12, 2010
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,305
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Mkifanikiwa katika hili, pia bara nao watakuwa na cha kujifunza. Unajua, 1995 walipokwenda kumzui Maalim kushinda urais wa Zanzibar nini madhara yake kwa Tanzania nzima? Siku CUF/Safina n.k watakapofanikiwa kutawala, huenda upepo wa siasa hata bara ukabadilika na watu kuamini kuwa kumbe inawezekana na ndivyo inavyokuwa. Binafsi kwa hili nawasifu wazenj kuwa mko mbali, ni haya mabavu tu, huenda zenj ingekuwa nyingine kabisa.
   
 8. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #8
  Jan 12, 2010
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  On the contrary. We will be laughing all the way to the bank!

  Amani ikiwepo Zanzibar nasi tuna farijika maana mkivurugana ni sisi ambao itabidi tuokote vipande na kuviunganisha pamoja.

  Amandla..........
   
 9. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #9
  Jan 12, 2010
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Naona hata wanachama na wapenzi wa CUF wameunga mkono muafaka huo, kama inavyoonekana kwenye picha hii, ambapo wanacuf wakipita mbele ya Rais Karume...

  [​IMG]

  Picha kwa hisani ya Father Kidevu
   
 10. Facts1

  Facts1 JF-Expert Member

  #10
  Jan 12, 2010
  Joined: Dec 23, 2009
  Messages: 308
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Mimi kwa kawaida yangu ni kama tomaso huwa siwaamini sana wanasiasa
  tatizo si kusema tatizo ni kutenda inapofika kwenye utekelezaji wako tayari hata kupinga walichosema jana yake,

  Kwanza kauli yake 'hatogombea kwa mjibu wa katiba ' ni sawa, lakini ina maana ingekuwa si katiba alikuwa bado anataka kuendelea, je katiba ingasema vipindi kumi ina maana asingepisha wengine angekuwa raisi maisha? nina wasi wasi na kauli hiyo nasubiri vitendo.

  Vile vile si mara ya kwanza kutoa hakikisho la uchaguzi huru na wa haki Zanzibar kila mara viongozi wamekuwa wakiimba hilo hata Komandoo Salimin ndio ulikuwa wimbo wake wa kila siku hatujasahau eti kila uchaguzi unapokuja wenyewe ni mashaidi wa vurugu za Zanzibar zikiongozwa na jenjewedi na polisi, sipingi kama kweli ana nia nzuri lakini nasubiri utekelezaji wake.

  Rais Karume amesema mara ngapi kwamba kila Mzanzibar mwenye sifa ya kupiga kura ataandikishwa kila mwenye ZaID ataandikishwa matokeo yake nini masheha ndio wamekuwa waamuzi wa nani aandikishwe wakiongozwa na ma-DC yote yamekuwa yakifanyika kupingana na kauli za rais sijui ni kitu gani special alichofanya leo kinifanye niamini, ndo maana nimesema mimi ni kama tomaso.

  Kuhusu suala la mafuta na gesi kuwa ni ya Zanzibar tu au la, hili sina uhakika nalo zaidi kwa sababu hata hayo mafuta ndo bado yanatafutwa hadi yatakapopatikana. Siwezi kwa sababu sijui yatapatikana wapi Unguja, Pemba, Mafia au Lindi sasa yakipatikana Mafia sijui wazanzibar watasema yao au yakipatikana baharini sijui mipaka ya Rep. of Tanzania inaishia wapi. Whatever the case kama dhahabu huwa inaenda hazina basi chochote kitakachopatikana kwenye mafuta na gesi kiende hazina, nafikiri hazina wana fomula ya mgawanyo wa kila kitu.
   
 11. K

  Kizito Member

  #11
  Jan 12, 2010
  Joined: Feb 23, 2008
  Messages: 70
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sijapata Muda wa kuisikiliza hotuba hii inayoonekana tamu sana, je amezungumza lolote kuhusu Serikali ya Mseto?Au serikali ya umoja wa kitaifa!
   
 12. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #12
  Jan 12, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,560
  Likes Received: 18,289
  Trophy Points: 280
  .
  No hakuzungumza lolote kuhusu hilo, hayo ni mambo yake na Seif, sio ya kumwaga kwenye kuku wengi ila alivyomshukuru Seif na kurecognize presence yake, this time Karume seems he is genuine.
   
 13. P

  Pakacha JF-Expert Member

  #13
  Jan 12, 2010
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 816
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  How genuine? percentage wise -40,50,90? Nan tuyaone mwaka huu!!!!!!!
   
 14. Abunwasi

  Abunwasi JF-Expert Member

  #14
  Jan 12, 2010
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 3,166
  Likes Received: 1,061
  Trophy Points: 280
  Hilo ndiyo tatiza la wanzanzibari hata sijui hizo pesa za muungano wanafikiri zinatoka wapi sijui.
  Waache wanunue mbeleko kabla ya uzazi kwa maana ninaamini TZ-Bara yatapatikana mafuta mengi na vilevile madini kedede hasa nyanda ya juu kusini. Sijui ikiwa hivyo watataka kugawana.
  UKIWA MROHO USIWE MCHOYO
   
 15. P

  Pakacha JF-Expert Member

  #15
  Jan 12, 2010
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 816
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Tangu lini SMT ikawasaidia wananchi wa Zanzibar katika mambo yao ya ustawi wa jamii- Elimu kwa watoto wao, afya kwao na watoto wao kilimo chao japo ni cha mpunga na viazi tona, Umeme ( si ndio mna ona hilo sakata sasa nani anahangaika SMT au Mansour). Fundi kuwa Fundi bwana . Mimi nategemea kuwa wewe unayaangalia haya mambo kwa utuo. Futa kama lipo ni lao la Zenj,. Na dhahabu hawafaidiki. Ikienda hazina wanapata majeshi na Mapolisi upo hapo?
   
 16. P

  Pakacha JF-Expert Member

  #16
  Jan 12, 2010
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 816
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Inshalla. Hakuna anayetaka kugawana. Hivyo lini umewasikia wale kule (Zenj) kupigia kelele -hata huo mchele wenu wa Kyela. Si wanakuja na kuununua (kwa mujibu wa taratibu za biashara) Sasa Futa ni lao na nyinyi pateni madini na kila mtachojaaliwa ni chenu- watakuja kununua. Mkiwapa -kama sadaka- basi huo ndio Muungano na undugu.
   
 17. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #17
  Jan 12, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Kitakachowaliza Wabara ni kipi? Yaani Wazenj wakielewana ndio kiwe kilio kwa bara? Mbona unaleta lugha za uchochezi na uchonganishi? Kama huna cha kuchangia si ukae pembeni badala ya kumwaga pumba?
   
 18. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #18
  Jan 12, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Hivi kumbe polisi na wanajeshi wengine wanapatikana hazina? Rudi standard one ndugu yangu ukaanze upya!
   
 19. Recta

  Recta JF-Expert Member

  #19
  Jan 12, 2010
  Joined: Dec 8, 2006
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35

  Zanzibar wanae Waziri wao wa fedha, kama walivyo na Waziri wa Afya, Mawasiliano na kadhalika. Mawaziri hao, si wa muungano. Mawaziri wa Muungano ni pamoja na, Waziri wa Mambo ya Nje, Waziri wa Mambo ya Ndani, Waziri wa Ulinzi. Lakini hilo si hoja.

  Mimi nawaelewa waZanzibar wanapotaka rasilimali zao zibaki kwa maendeleo ya Zanzibar kwasababu zifuatazo:

  1. Maliasili/utajiri wa bara kwa kiasi kikubwa hubaki Bara
  2. Zanzibar haina rasilimali nyingi, na ili iweze kuendelea kwa kasi, ni lazima iweze kujikimu
  3. Fedha za mikopo na misaada ambayo Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hupata, kiasi kikubwa haipelekwi Zanzibar

  Nadhani kama kuna nia ya dhati ya kudumisha Muungano, ni vyema wakarudi kwenye makubaliano ya Muungano na kuuacha kama ulivyokuwa awali au kuufanya uwe bora kwa pande zote mbili.

  Makubaliano yale kwa uchache yalikuwa kwamba, Rais akiwa wa Bara, Makamu wa Rais atakuwa kutoka Zanzibar. Nia ilikuwa ni kulinda maslahi ya pande zote. Ilivyo sasa, ni rahisi kusema Muungano umevunjwa kama ilivyo kwa siasa ya Ujamaa na Kujitegemea (bila kelele).
   
 20. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #20
  Jan 12, 2010
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160

  Nimefarijika kuwa akina Tomaso tuko wengi. Hata siku moja siwezi kumuamini mwanasiasa. Siasa ni kusema kile watu wanataka kusikia wakati huo hata kama kitu hicho unajua ni ndoto za alinacha. Kwangu mimi sikiliza hotuba za wanasiasa wakati mwingine ni sawa na kuangalia watoto wanaocheza kidari po! Nothing is real and genuine! Tusubiri hadi Oct tuone.
   
Loading...