Hotuba ya Rais apingana na hoja kupuliza dawa, kuweka karantini, wajifukize, hakuna lockdown. Kwanini hajakutana na sekta ya afya na kwanini Jeshi?

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
Kwa nilivyomsikiliza rais wa Tanzania nimegundua vitu vifuatavyo

1. Hakuna haja ya lockdown katika nchi kwa sababu nchi haitaenda hakuna vyanzo vya mapato na dar ndio center msahau kulockdown.

2. Kupuliza dawa ni upumbavu kwa sababu haiuwi virus inawezekana inasambaza sio kuuwa virus.

3. Dawa za hospital sio msaada ni vyema tukajifukiza hiyo inauwa virus kwa sababu havikai katika joto kali la mvuke.

4. Karantine haina maana kwa sababu wengine wako mtaani hao nao watoke wakapambane na walio mtaani.

5. Tanzania ni maskini inatakiwa kusamehewa madeni kwa sababu ya ugonjwa watashindwa kulipa madeni kwa wakati.

6. Na sisi tunatendence ukiumwa ugonjwa kama corona utajitengenezea kinga ivyo utapona tu ngoja uje.


Rais John Magufuli amesema hakuna upuliziaji dawa mitaani au kwenye vyombo vya usafiri unaoweza kuua vidudu vya corona hivyo kile kilichofanywa Dar es Salaam na kwingineko hivi karibuni ni upuuzi.

Kwa mujibu wa Rais dawa Chlorine haiwezi kuua virusi vya corona.

Amesema virusi hivyo ni mafuta hivyo vinaweza kumalizwa kwa kutumia sabuni, joto kali au maji ya moto.

Ameagiza ufanywe uchunguzi kufahamu ni nani alitoa agizo la upuliziaji dawa jijini Dar es Salaam."""""

Nilitegemea leo rais angekuja na mambo ya msingi kama haya

1. Uchumi wa nchi na namna ya kuokoa ajira na sekta binafsi zinazokufa (stumulus packages)

2. Vifaa tiba kupambana ugonjwa huu

3. Kufanya kikao na sekta ya afya badala ya walinzi wasioweza kupambana na corona ambayo iko kitabibu zaidi kuliko kijeshi

4. Nk
 
Tehe tehe
Bavicha huwa wanaugua kama Rais akiwa kimya
Tayari mtu katohoa hotuba kashusha dondoo zake
 
Huyu mtu anaboa balaa,
Yaani pale nilijiuliza anaongea Rais wa nchi au monitor wa darasa la kwanza A ?Jamani hapana. Kaongea mambo ya ajabu kabisa. Hivi jamani hao wa kwenye wanaandika mitandaoni si wa kuwapuuzia tu. Wizara hawapo transparent na ndo maana watu wanajiandikia. Wizara wangekuwa wazi hakuna watu wangeropoka ropoka mitandaoni.
Rais anasema eti tujifukizie mivuke above 100?Itauua Coronavirus. Huyu ni wanasayansi jamani.
Ooooh my God najisikia kutapika.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom