Hotuba ya Prof. Ibrahim Haruna Lipumba, mbobezi wa uchumi duniani

Trump2

JF-Expert Member
May 28, 2017
1,553
2,608
Bila shaka yoyote hakuna mtu hata Mmoja aliyewahi kutia shaka uwezo wa Kielimu na Uzalendo wa Prof Ibrahim Haruna Lipumba kwa Nchi yake ya Tanzania.

Kama kuna wanasisa utawataja kwa kushiriki kusimamisha Demokraisa hata hii iliyopo kwa kupingana na Serikali ya CCM mpaka kupelekea Kuvunjwa mkono na kuporwa SAA ni Mwamba huyu kutoka ILOLANGURU TABORA Prof Ibrahim Lipumba.

HOTUBA YA PROF IBRAHIM LIPUMBA IKULU D'SALAAM.TAREHE 23/10/2017

NANUKUU.

''Kwanza namshukuru Rais kwa kutukaribisha katika hafla hii, kwa niaba ya viongozi wa vyama vya siasa akiwemo mwenyewe Rais ni kiongozi wa chama cha siasa Mwenyekiti wa CCM,

Naomba kumpongeza Rais Nampongeza Rais kwa juhudi alizozifanya kwa swala hili la Madini, Sisi viongozi wa vyama vya siasa hususani vyama vya upinzani kwa muda mrefu kwa miaka mingi hasa tokea mwaka 2000 tumekuwa tukipiga kelele sana kuhusu maliasili kuibiwa.

Itakuwa ajabu sana sisi tuliokuwa kukipiga kelele kwamba mali ya asili ya nchi inaibiwa ndio tupinge juhudi hizi zinazofanywa na Mhe Rais Magufuli.

Tunashukuru sana kamati za Prof Mruma na Prof Usorro kwa kazi kubwa sana walizofanya na kufikia hapa. Lakini bila kusahamu juhudi na kazi iliyofanywa na mtani wangu Prof Kabudi.

Kama alivyoeleza Prof Kabudi kuhusu mafanikio haya lakini sio yeye tu hata Mwewnyekiti wa Barrick amesema kwamba sasa tunahitaji kuunda kampuni ya karne ya 21 yenye uwazi na usawa.

Kwa hili lazima tupongeza kwa dhati timu yako ikiongozwa na Prof Kabudi kama nilivyosema hata mwenyekiti wa Barrick anasema Tanzania sasa itakuwa mfano wa Kampuni bora Duniani.

Haya ni mafanikio mbakubwa sana kwa faida kugawanywa Nusu kwa Nusu hivyo changamoto iliyopo ni wale watakaoingia katika BODI au KAMPUNI wawe ni wazalendo kweli kweli.

Unaweza kukubaliana kugawana faida Nusu kwa Nusu lkn kama walioingia katika bodi sio wazalendo wanaweza kushirikiana na wawekezaji kusema hawajapata faida au faida ni Sifuri hivyo sifuri kugawanya kwa mbili ni Sifuri hiyo hiyo

Hivyo tunapaswa wale wote watakaoingia kwenye Bodi ya Kampuni wawe ni wazalendo kweli kweli.

Mhe Rais sisi kwa hili tutakuunga mkono tupingane kwenye mambo kama kiongozi anakiuka maslahi ya Nchi

Lazima tuwe na mtazamo wa Tanzania kwanza vyama baadae tukosoane kama mtu au kiongozi halindi maslahi ya nchi na tupongezane kama mtu anatetea maslahi ya Nchi.

Sijachukua muda mrefu maana siku hizi mikutano ya hadhara haipo watu pwaaa pwaa pwaaa pwaa

MWISHO wa kunukuu.

Wasalaam

Mwamba kamaliza UKUKU chaaaaaliiiii
 
Anachokitetea kinajilikana

Ubobezi wake wa uchumi huku njaa inamuua kwa kujidgalilisha..

Bora std 7 anaejihudumia kuliko PHD za kulamba miguu
 
Siku hizi mna msemo mkiona MTU anaipinga chadema nikilaza.wakati washabiki wenu wengi walikuwa wapiga debe na vijana wa mtaani wasiojitambua. Hivyo hilo neno limekuwa likiwavunja moyo na kuona ndio wao mnaowambia mojawapo mm mwenyewe!
 
hii kugawana faida nusu kwa nusu wengine wanasema ni baada ya kodi wengine kabla ya kodi yaani ni vurugu mechi
Prof. Palamagamba Kabudi alishalifafanua hili kwamba baada ya kulipa kodi zote ndio faida inagawanywa.
 
Siku hizi mnasemo mkiona MTU anaipinga chadema nikilaza.wakati washabiki wenu wengi walikuwa wapiga debe na vijana wa mtaani wasiojitambua. Hivyo hilo neno limekuwa likiwavunja moyo na kuona ndio wao mnaowambia mojawapo mm mwenyewe!
Kumbe wewe ni Kilaza? Pole yako.
 
Prof. Palamagamba Kabudi alishalifafanua hili kwamba baada ya kulipa kodi zote ndio faida inagawanywa.
Hivi hata kama hukwenda shule ni wapi dunia hii mwenye 16% na mwenye hisa 84% wanagawana faida 50 kwa 50?

Ukiamini uongo kama huu hata huyo anayekupiga fix atakudharau.
 
Ndiyo maana lwa ufinyu wa akili zetu tuliamua kumuondoa mlalimani ili tuongee tutakayo bila wao kujua tuongeacho. Sasa sijui bado hawajapata tafsiri ya tulicho kiongea au vipi.
 
Bila shaka yoyote hakuna mtu hata Mmoja aliyewahi kutia shaka uwezo wa Kielimu na Uzalendo wa Prof Ibrahim Haruna Lipumba kwa Nchi yake ya Tanzania.

Kama kuna wanasisa utawataja kwa kushiriki kusimamisha Demokraisa hata hii iliyopo kwa kupingana na Serikali ya CCM mpaka kupelekea Kuvunjwa mkono na kuporwa SAA ni Mwamba huyu kutoka ILOLANGURU TABORA Prof Ibrahim Lipumba.

HOTUBA YA PROF IBRAHIM LIPUMBA IKULU D'SALAAM.TAREHE 23/10/2017

NANUKUU.

''Kwanza namshukuru Rais kwa kutukaribisha katika hafla hii, kwa niaba ya viongozi wa vyama vya siasa akiwemo mwenyewe Rais ni kiongozi wa chama cha siasa Mwenyekiti wa CCM,

Naomba kumpongeza Rais Nampongeza Rais kwa juhudi alizozifanya kwa swala hili la Madini, Sisi viongozi wa vyama vya siasa hususani vyama vya upinzani kwa muda mrefu kwa miaka mingi hasa tokea mwaka 2000 tumekuwa tukipiga kelele sana kuhusu maliasili kuibiwa.

Itakuwa ajabu sana sisi tuliokuwa kukipiga kelele kwamba mali ya asili ya nchi inaibiwa ndio tupinge juhudi hizi zinazofanywa na Mhe Rais Magufuli.

Tunashukuru sana kamati za Prof Mruma na Prof Usorro kwa kazi kubwa sana walizofanya na kufikia hapa. Lakini bila kusahamu juhudi na kazi iliyofanywa na mtani wangu Prof Kabudi.

Kama alivyoeleza Prof Kabudi kuhusu mafanikio haya lakini sio yeye tu hata Mwewnyekiti wa Barrick amesema kwamba sasa tunahitaji kuunda kampuni ya karne ya 21 yenye uwazi na usawa.

Kwa hili lazima tupongeza kwa dhati timu yako ikiongozwa na Prof Kabudi kama nilivyosema hata mwenyekiti wa Barrick anasema Tanzania sasa itakuwa mfano wa Kampuni bora Duniani.

Haya ni mafanikio mbakubwa sana kwa faida kugawanywa Nusu kwa Nusu hivyo changamoto iliyopo ni wale watakaoingia katika BODI au KAMPUNI wawe ni wazalendo kweli kweli.

Unaweza kukubaliana kugawana faida Nusu kwa Nusu lkn kama walioingia katika bodi sio wazalendo wanaweza kushirikiana na wawekezaji kusema hawajapata faida au faida ni Sifuri hivyo sifuri kugawanya kwa mbili ni Sifuri hiyo hiyo

Hivyo tunapaswa wale wote watakaoingia kwenye Bodi ya Kampuni wawe ni wazalendo kweli kweli.

Mhe Rais sisi kwa hili tutakuunga mkono tupingane kwenye mambo kama kiongozi anakiuka maslahi ya Nchi

Lazima tuwe na mtazamo wa Tanzania kwanza vyama baadae tukosoane kama mtu au kiongozi halindi maslahi ya nchi na tupongezane kama mtu anatetea maslahi ya Nchi.

Sijachukua muda mrefu maana siku hizi mikutano ya hadhara haipo watu pwaaa pwaa pwaaa pwaa

MWISHO wa kunukuu.

Wasalaam

Mwamba kamaliza UKUKU chaaaaaliiiii
Mkilipwa 50 na hao wezi wenu na sisi mtatulipa 50% za Muungano ,tunasubiri WAZANZIBAR
 
Back
Top Bottom