Lazaro Nyalandu ajiunga CHADEMA rasmi, Mabomu ya Machozi yapigwa

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,890

Aliyekuwa Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu amejiunga rasmi na CHADEMA leo katika mkutano wa hadhara wa kumnadi mgombea Udiwani wa Kata ya Mhandu Mkoani Mwanza.
6754a200b0e79d2e3b6422bce0747753.jpg

Former Singida North MP, Lazaro Nyalandu ultimately joins Chadema. Given membership card in Mwanza, Sunday.


MABOMU YAPIGWA

01c6b6ab360737a02da885a76c3d1d26.jpg


Mabomu ya machozi yapigwa kuwatanya wafuasi wa Chadema waliokuwa wakisindikiza msafara wa Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe akiambatana na Wanachadema akiwemo Nyalandu wakati wakitoka katika mkutano wa kumnadi mgombea udiwani wa kata ya Mhandu jijini Mwanza, Godfrey Mahame.

HOTUBA YA NYALANDU


Lazaro Nyalandu Mwanza, Tanzania

Mh. Freeman Mbowe, Mb.
Mwenyekiti wa Chadema-Taifa
Mh. Dr. Vicent Mashinji,
Katibu Mkuu wa Chadema-Taifa
Mh. Ezekiel Wenje, Mwenyekiti wa Kanda ya Mwanza
Mh. Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema: Mh. Godbless Lema,
Wah. Viongozi wa Kanda,
Mh. Mgombea Udiwani Kata hii
Ndugu Wana Chadema,
Ndugu Wananchi Wote mliohudhuria,
Ndugu Wanahabari,
Mabibi na Mabwana:

AMANI IWE NANYI:
PEOPLES! POWER!

NASIMAMA mbele yenu na mbele ya Watanzania wote nikiwa nimeisubiri kwa shauku kubwa siku hii ya leo ili nipate fursa ya KUJIUNGA na harakati za kupiganiq mageuzi ya kisiasa, kijamii, na kiuchumi nchini Tanzania, kwa kujiunga Rasmi na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, Chadema. Asanteni sana kwa upendo wenu na mapokezi makubwa!

Nilijiondoa CCM Oktoba 30 mwaka huu na kujiuzulu nafasi yangu ya Ubunge wa Singida Kaskazini kwa tiketi ya CCM, ikiwa ni pamoja na kujivua nafasi zote za Uongozi ndani ya CCM, ikiwepo Ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi, kwa kuwa katika miaka miwili ya Uongozi wa Awamu ya Tano, nimeamini na kujiridhisha kuwa CCM imepoteza mwelekeo, na kwamba niliporejea “Ahadi za Mwanachama wa CCM”, nikakumbushwa maneno haya:

Nitasema KWELI daima, na UONGO kwangu mwiko. Katika Majira na nyakati tunazozipitia kama Taifa,
Na mimi “Naogopa kusema UONGO”. Mabadiliko ya kisiasa ni lazima nchini Tanzania, na Wakati ni huu.

Wakati wa kuondoka CCM, nililijulisha Taifa azma yangu ya kutaka kujiunga na Chadema, endapo Wana Chadema wataona VEMA, kuniruhusu niingie malangoni mwenu. Niwe mmoja wenu, tushikamane pamoja!

Wakati naondoka CCM, nililijulisha TAIFA kuwa, daima nitakuwa mwaminifu kwa nchi yangu Tanzania, na kwamba naungana na Upinzani kupigania HAKI, kwa kuwa imeandikwa HAKI huinua TAIFA, na kwa pamoja tutaitafuta na kuilinda tunu hii muhimu kwa TAIFA letu.

Wakati naondoka CCM, nililijulisha TAIFA kuwa naamini kwamba, Tanzania inahitaji kupata Katiba Mpya, na kwamba tufanye rejea ya RASIMU ya mapendekezo ya Katiba ya Tume ya Warioba ili pamoja na Mambo mengine, kuwepo mgawanyo kamili wa madaraka katika mihilimi ya utawala wa Chini (Bunge, Serikali, na Mahakama), na kuondoa muingiliano na kuweka ukomo wa madaraka wa wazi kwa kila muhimili.
 
Kila la kheir Mh. Nyalandu!

CCM ni zaid ya Mtu ni Mfumo na haujawahi kutikiswa na Mtu!

Mwaka 1984 ilizuia Jaribio la kuvunja Muungano kwa kumtimua Rais wa Zanzibar

1987 ilimfukuza Uanachama aliekuwa Waziri Kiongozi wa Zanzibar kwa kutaka kuleta chokochoko Visiwani

1992 uliachana na Mfumo wa kishamba wa Kijamaa japo Nyerere alipinga lakin hakuweza Mabadiliko hayo




2007 CCM ilifanikiwa kumtenganisha Rais wa Nchi na genge la Wahuni waliomuingiza madarakani

2015 ilizuia Genge la Mafisadi kuchukua Nchi

Nyalandu ni tone la Maji kwny Bahari ya Atlantik uwepo au kutokuwepo kwake hakubadili chochote kwa CCM

Yeye anajua CCM ishahamwa na kufukuza Watu Wazito kweli kweli lakin ikabaki Imara
 
Back
Top Bottom