Hotuba ya Nape yaliza watu mkutanoni, Mbunge wa CUF na wafuasi wake wamshangilia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hotuba ya Nape yaliza watu mkutanoni, Mbunge wa CUF na wafuasi wake wamshangilia

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Nipe tano, Jun 26, 2011.

 1. N

  Nipe tano Senior Member

  #1
  Jun 26, 2011
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 101
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  HOTUBA NA NAPE YALIZA WATU MKUTANONI,
  MBUNGE WA CUF NA WAFUASI WAKE WAMSHANGILIA


  NA BASHIR NKOROMO, KILWA

  HOTUBA aliyotoa Katibu wa NEC Itikati na Uenezi CCM Nape Nnauye, juzi
  katika mji mdogo wa Kilwa Masoko, imeacha historia baada ya kuwaliza
  baadhi ya wananchi waliohudhuria mkutano huo.

  Wakati baadhi wakilizwa wengine wakiwemo wafuasi wa chama cha CUF
  chini ya mbunge wa Kilwa Kusini kwa tiketi ya chama hicho, Selemani
  Bungara maarufu kwa jina la *****, walilipuka kushangilia hotuba hiyo
  huku wakipiga kofi za furaha.

  Miongoni mwa walioangua kilio huku akitokwa machozi ni Asha
  Likalangala (45) ambaye aliangua kilio hicho hadi Katibu wa NEC,
  Oganaizesheni Asha Abdallah Juma aliyefuata na na Nape kulazimika
  kushuka meza kuu kwenda kumyamanzisha kwa kumkumbatia.

  Mkutano huo uliofayika katika viwanja vya Mkapa Garden, ulihudhuria na
  mamia ya watu, wengi wao wakiwa ni wanachama wa CCM, wananchi wa
  kawaida na baadhi ya wafuasi wa vyama vya upinzania ambao baadhi
  walikuwa na nguo zenye nembo za vyama hivyo.

  Nape ambaye alihutubia kwa zaidi ya saa moja huku akishangiliwa mara
  kwa mara kwenye mkutao huo, akifafanua lengo na hatima ya maamuzi
  yaliyofanywa na CCM mjini Dodoma Aprili mwaka huu alisema, kufuatia
  mabadiko hayo yaliyopewa falsafa ya kujivua gamba, sasa Chama kimekuwa
  na nguvu zaidi katika maeneo mengi.

  Akizungumzia baadhi faida za baada ya mabadiliko hayo, Nape alisema
  kama alivyo nyoka akijivua gamba, sasa Chama kimekuwa na sumu kali
  yenye kukipa uwezo zaidi wa kuisimamia serikali katika kutekeleza
  ilani ya uchaguzi na pia kimepata nguvu ya kuweza kurejesha haki pale
  inapopotea.

  "Tunajua kumekuwepo na baadhi ya watumishi wa serikali wasitekeleza
  wajibu wao kama kujigeuza miungu watu, Polisi ambao kesi zikiingia
  vituoni wanazigeuza 'dili', manesi na wauguzi ambao wananyanyasa
  wagonjwa badala ya kuwatibu na wale tunaowapa ilani kusimamia
  utekelezaji wa ilani ya Chama halafu wanatekeleza ilani za matumbo
  yao, tunasema hawa wote siku zao zinahesabika, tutawashughulikia la
  sivyo waabadilike haraka", alisema Nape na kushangiliwa.

  Aliwaonya baadhi ya madiwani waliopata nafasi hiyo kwa tiketi ya CCM
  ambao wanajihusisha na ulanguzi wa ufuta wilayani Kilwa, na kuwataka
  waache mara moja kwa kuwa kufanya hivyo ni kuwaibia wakulima na
  kutokitendea haki Chama Cha Mapinduzi.

  Nape alidai baadhi ya madiwani wa CCM wamekuwa wakishirikiana na
  mbunge wa Kilwa Kusini katika biashara hiyo, ambapo alisema licha ya
  nunua ufuta huo kwa bei ya chini, pia wanawaibia wakulima kwa kuwa
  kuna madai kwamba huichakachua mizani na kuonyesha imepina kiasi
  kidogo badala ya kile halisi.

  "Taarifa tulizo nazo ni kwamba walanguzi hawa mizani yao huichakachua
  kiasi kwamba wakati wa kupima kilo moja na nusu huonekanan ni kilo
  moja tu na hulipa kati ya sh.1,150 na sh. 1,200 wakati kwa kupitia
  utaratibu uliopo wa serikali wa stakabadhi ghalani.


  Nape alisema, walanguzi wanawibia wakulima kwa sababu katika utaratibu
  wa stakabadhi ghalani wa serikali mkulima anapewa kianzio cha sh.
  1,000 kwa kilo moja na baadaye huongezwa fedha kulingana na bei ya
  soko katika mnada.

  Aliseama hadi sasa bei ya mnada ya ufuta Kilwa imefikia sh. 1,700 kwa
  kilo ambapo kwa kiwango hicho baada ya makato ya gharama za uendeshaji
  mkulima atapata sh. 1,490 na kutokana na hali hiyo walanguzi
  wanawaibia wakulima sh. 290.

  Nape pia alisisimua kwa jinsi alivyofafanua madhara ya wafuasi wa
  vyama kushabikia viongozi wanaochochea uvunjifu wa amani ambapo
  alisema, wanaoathirika si viongozi hao bali wananchi ambao hujipeleka
  mstari wa mbele.

  Alifafanua kwa kina kadhia hiyo, akitoa mfano machafuko yaliyotokea
  nchi moja Afrika Masharikimbako baada ya uchaguzi mkuu wa nchi hiyo,
  kulizuka kutoelewana baina ya viongozi wakahamasisha wananchi kuingia
  mitaani hatimaye wakakumbwa na madhara ya vifo na ulemavu huku wale
  waliokuwa wakigombana wakiwa sasa wanakunywa chai pamoja Ikulu.

  Katika ziara hiyo mkoani Lindi, Nape amefuatana na Katibu wa NEC,
  Oganaizesheni, Asha Abdallah Juma na Katibu Msaidizi Mkuu wa Idara ya
  Itikadi na Uenezi, Sixtus Mapunda.

  mwisho.
   
 2. l

  lumumba the son Senior Member

  #2
  Jun 26, 2011
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 194
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Aminia kamanda Nape na timu yenu ya sekretarieti. Hakika mnatupatia raha sana wana CCM, endeleeni kuwatetea wanyonge wa kusini na walanguzi wa ufuta na korosho.
   
 3. Daffi

  Daffi JF-Expert Member

  #3
  Jun 26, 2011
  Joined: Jun 25, 2011
  Messages: 3,803
  Likes Received: 178
  Trophy Points: 160
  Ninapita tu,ntarudi baadaye
   
 4. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #4
  Jun 26, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  kwani sisiem hawatuwafahamu kwa kupenda media coverage yaani hapo hao walio lia unakuta walikodiwa kenda kulia tu pale wameshachkua chao
   
 5. z

  zamwamwa Member

  #5
  Jun 26, 2011
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 46
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa wale ambao hawakuwepo kwenye mkutano wanaweza kusema huyo mama alichukuliwa. Lakini kwa sisi tuliokuwa pale tuliona wengi tu wakisisimkwa na hotuba ya CCM mpya na jinsi inavyorudi kwenye maadili yake ya asili. Viva CCM vivaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa! Aluta continuaaaa!
   
 6. s

  suley Member

  #6
  Jun 26, 2011
  Joined: Aug 24, 2010
  Messages: 53
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nape ana vituko kweli ndo kaibukia Lindi. Sasa mimi najiuliza siku zote hivi CCM haikuwa na makatibu wa enezi? yaani CCM tunaisikia kila siku hata katibu wao mkuu hazunguki kama yeye. Wapi mapuri, mwanri na chiligati kipindi mlipokuwa na nafasi hiyo? Au Nape ana agenda yake ya siri na si ya CCM? Maana waliotangulia hawakuwa na style hiyo?
   
 7. Pasco_jr_ngumi

  Pasco_jr_ngumi JF-Expert Member

  #7
  Jun 26, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 1,811
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Upupu 2ph
   
 8. lifeofmshaba

  lifeofmshaba JF-Expert Member

  #8
  Jun 26, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 868
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  sijaona kilichomliza kwenye hiyo habari hapo juu na hali mbunge anayetajwa alikishangilia
  hii kitu imechakachulia
   
 9. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #9
  Jun 26, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 12,000
  Likes Received: 2,655
  Trophy Points: 280
  Hatudanganyiki,je mliwauliza kwamba ni nini kinawaliza?
   
 10. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #10
  Jun 26, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,329
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Mtoa habari hajakamilisha hii habari. Hajatuambia ilichomliza huyo mama ni nini? Inaweza anasikitika kupoteza muda wake kusikiliza pumba! Labda alitegemea angewatangaza mapacha watatu kuondolewa rasmi kwenye uongozi wa chama lakini hajasikia. Na kama hotuma ya Nape ilikuwa inamfurahisha au inakidhi matarajio yake, kwanini alie? Acheni usanii! Hii sio Tz ya mwaka 77. Hatudanganyiki ng'o!
   
 11. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #11
  Jun 26, 2011
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,118
  Trophy Points: 280
  hao walikuwa watatengeneza move tu, kama hamuwafahamu ccm, basi muwajue hivyo.katika matatizo yote yanayo wakabili wananchi wa lindi hilo ndo kubwa kuliko yote? Mbona mimi naona yapo makubwa hata kuzidi hilo? Kwa nini na mengine wasilie waje kulia kwenye ishu ya ufuta? Mbona kule shinyanga wasukuma wanaibiwa na wanunuzi wa pamba lakini hawajawahi lia?

  Hiyo ni move ya nape, na hao wakina mama ndo wakulima wa ufuta peke yao? Mbona wanaume hawalii hapo? Hao wakina mama watakuwa waliandaliwa na wakaambiwa nikianza kuhutubia nyie ectin kama mnalia vile
   
 12. lifeofmshaba

  lifeofmshaba JF-Expert Member

  #12
  Jun 26, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 868
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  hiyo habari hiko HABARI LEO na hapo ndio imekamilika mengine mtoa hoja kaongezea
  • mbunge wa CUF kushangilia hali huyo mbunge ndiye mtuhumiwa
  • na watu kulia kwenye mkutano haya hayapo kwenye hiyo habari hapo juu yawezeka yeye ndiye source ya hizo nyongeza lakini kama mtuhumiwa anashangilia kuna walakini mkuu hapo, hiyo ni dharau kwa hiyo tamko na anajiamini kwamba hizo ni kelele tu za dogo
   
 13. Rugaijamu

  Rugaijamu JF-Expert Member

  #13
  Jun 26, 2011
  Joined: Jul 10, 2010
  Messages: 2,833
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Inawezekana kabisa anaitumia nafasi ya uenezi na fedha za magamba kutengeneza mtandao wake ili hatimaye afanikiwe kutimiza azma yake(na wenzake)kuunda chama kipya(rejea ushiriki wake kuanzisha CCJ).Sio bure!
   
 14. Rejao

  Rejao JF-Expert Member

  #14
  Jun 26, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 9,239
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Hongera sana kamanda Nape! Wanamagwanda mpo???
   
 15. Rugaijamu

  Rugaijamu JF-Expert Member

  #15
  Jun 26, 2011
  Joined: Jul 10, 2010
  Messages: 2,833
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  kwani mbunge anayetajwa kushangilia si ndo Nape amemwita mlanguzi na kumtaka arudi bungeni,ama nimechanganya madesa...lol
   
 16. D

  Domo Zege JF-Expert Member

  #16
  Jun 26, 2011
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 687
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  Umedhamiria kweli mwaka huu Nnape,hii ni ID yako ya ngapi?
   
 17. D

  Domo Zege JF-Expert Member

  #17
  Jun 26, 2011
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 687
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  Unajijibu mwenyewe,hivi vichekesho.Mnatujazia ma ID mengii yasiyo na tija hapa jamvini.
   
 18. N

  NewOrder JF-Expert Member

  #18
  Jun 26, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 489
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 45
  CCM bado mna hali ngumu sana lakini bado mna ujanja mwingi pia. Kilwa Masoko?? Hebu Nape fanya mikutano sehemu hizi (Mara, Mwanza, Shinyanga, Kigoma, Arusha, Kilimanjaro, Dar es Salaam) halafu ueleze hayo uone kama chozi za mtu hata mmoja zitadondoka!! Endelea kuzungukia sehemu za mashambani ndio watakusikiliza.

  Huyu mleta mada kweli ni mpotoshaji. Mama kalia lakini hatujui kalizwa na nini. Labda ni jinsi anavoibiwa ufuta na akina Nape wanajua na hawajachukua hatua ya au kumrejeshea alichoibiwa au kusimamisha wizi huo. Eti mbunge amshangilia Nape!! Kwa kutajwa kuwa ni mmoja wa walanguzi?? Nape anataka kuwazuia madiwani wasishirikiane na mbunge katika ulanguzi lakini wakati huo huo hafanyi chochote kumzuia mbunge au hata kumfikisha kwenye vyombo vya sheria huku akijua anachofanya ni kosa.

  Bado tuna hamu ya kujua RACHEL watafanywa nini!!
   
 19. Averos

  Averos JF-Expert Member

  #19
  Jun 26, 2011
  Joined: Aug 6, 2010
  Messages: 648
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 45
  Jana nilikuwa ndani ya gari kutoka Masasi kwenda Lindi, mjadala mkubwa ulikuwa jinsi serilkali inavyotumia wakuliwa kujinufaisha, wananchi walikuwa wakilalamika sana kuwa kila siku utasikia viongozi wakisema kuwa tunataka kuboresha hali za wakuliwa wakati ni unafiki mtupu, Mjadala ulikwenda mbali na wengine wakasema kuwa wapo tayari kukata mikorosho na kupanda Minazi!, Hali inaonekana kuwa mbaya huko tunakokwenda kama serikali haitafanya juhudi za kutosha itakula kwao!
   
 20. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #20
  Jun 26, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  nadhani nafasi yeyewe inajieleza,kuwa ni itikadi na uenezi,huwezi kukaa ofisini kama una nafasi ya uenezi ni lazima uzunguke nchi nzima kueneze sera na kukijenga chama,hivyo ndivyo ilivyo,lakini wale wazee hawakutaka kufanya kama nafasi inavyo wahitaji kufanya

  ok Nape endelea na kazi uliyotumwa kwani chama kikifa juwa kimekufa mikonopni mwako,hivyo huna budi kukikomboa kutoka ktk janga la kuzama

  lakini pia kuna yule jamaa aliyesababisha tukanunua rada kwa uro 41 badala ya uro 21 msipo mchukulia hatu kwa sisi tusio na vyama hatuta waelewa kabisa
   
Loading...