Hotuba ya Mwenyekiti mpya wa SADC, Rais Magufuli ni ya matumaini makubwa kwa SADC

Elius W Ndabila

JF-Expert Member
Jul 17, 2019
322
645
Muda mfupi uliopita Mh Rais wa Tanzania Dkt John Joseph Pombe Magufuli amehotubia mkutano wa nchi za kusini mwa Afrika yaani SADC.

Mh Rais pamoja na kuishukuru Jumuiya ya kusini mwa Afrika kwa kumuamini na kumkabidhi uenyekiti wa juimiya hiyo kwa kipindi cha mwaka mmoja yaani 2018/2019 ametoa hotuba ambayo imekuwa nzuri sana.

Mh Rais amezungumza mambo mbalimbali yakiwepo mambo ya kiuchumi. Mh Rais amesistiza kuwa nchi za SADC bado hazijatumia vizuri rasilimali zilizopo ili kukuza uchumi wa nchi hizo. Amesema kuwa pamoja na nchi hizi kuwa na kila kitu lakini bado uchumi wake umekuwa wa kusua sua. Matharani amesema kwa miaka kumi uchumi wa nchi hizi umekuwa unashuka badara ya kukua. Mh Rais ambaye ndiye Mwenyekiti mpya wa SADC kuonyesha uzalendo wake na kusimamia kile anachokiamini amewanyoshea vidole secretarieti ya SADC kuwa ndio tatizo. Amesema kuwa Secratarieti ndio wanafanya kazi za SADC za kila siku, lakini wameshindwa kuja na majawabu ya nini kifanyike kukuza GDP badara ya hivi ilivyo.

Amewataja marehemu Baba wa Taifa Mwl Nyerere, Agostino Neto, Mandela, Mzee Mgabe na wanzilishi wengine wa SADC kuwa walikuwa na malengo makubwa, lakini bado ndoto za wazee hawa hazijafanikiwa vizuri.

Mh Rais kwa suala la biashara amesema kuwa hakuna sababu nchi wanachama kuagiza bidhaa nje kama bidhaa hizo zinapatikana SADC. Amesema kunatakiwa kufungua milango ili wananchi wa nchi hizi kujua furusa zilizopo ktk nchi mwanachama. Amesema katka ziara yake ya mwezi may alishangaa nchi kuagiza nafaka nje wakati Tanzania kuna ziada ya kutosha.

Rais amesistiza wakati SADCC inabadirika na kuwa SADC ilitegemea kumaliza changamoto zote zilizokuwepo mwanzo, lakini uhalisia bado changamoto zipo. Ameshauri ni lazima sasa milango ya biashara ifunguliwe na kuondoa vikwazo vinavyoweza kuturudisha nyuma.

Amesema swala la siasa katika nchi hizi iko vizuri pamoja na changamoto ndogo ndogo. Amesema kwenye kipindi chake ataendelea kufanya yale yote kwa ajili ya Afrika.

Baada ya hotuba hii ya Mh Rais ambayo imejaa mambo mengi, binafsi imenionyesha dira mpya ya SADC. Ninamuona Brudozza kwenda kubadiri kabisa jumuia na kuwa na ufanisi mkubwa. Sura na maneno ya JPM yanaonyesha dira na matumaini makubwa kwa viongozi wote waliohudhuria mkutano huu.

Kila la heri JPM.

=====

MWENYEKITI mpya wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), ambaye pia ni Rais wa Tanzania, Dk. John Magufuli amesema nchi za kiafrika si maasikini hivyo ziache kujitangaza kuwa ni duni mbele ya mataifa mengine.
H1.jpg

“Tusikubali kusafirisha tu malighafi nje ya Afrika, hii inaatufanya tuwe tunasafirisha ajira. Nchi zetu si masikini, narudia tena nchi zetu si masikini tunao utajiri wa kutosha kwenye madini, mafuta na ardhi yenye rutuba. Vitu vyote vinavyotufanya tuwe matajiri tunavyo, kwanini tushindwe kupiga hatua,” alisema Rais Magufuli.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa uenyekiti wa jumuiya hiyo katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam leo, Rais Magufuli amesema mbali ya kuwa na rasilimali nyingi lakini bado Afrika inalalamika hali duni ya kiuchumi.

Rais Magufuli amesema Tunaagiza sukari, magari na mafuta katika nchi za mbali huku tukijua baadhi ya mataifa ya SADC yanaweza kuuza bidhaa hizo kwa bei nafuu. Ndio maana katika mwaka wangu wa uongozi nimeamua kuongozwa na kaulimbiu ya mazingira bora ya viwanda, ufanyaji biashara na kutengeneza ajira.

Vievile, fursa nyingi za kibiashara zinapelekwa katika mataifa ya mbali huku baadhi ya nchi zinazozalisha bidhaa nzuri ikiwemo magari na bidhaa nyingine za viwanda zikiachwa mbali ya kuwa na bidhaa bora na zilizo karibu.

Aidha, Rais Magufuli aliigeukia Sekretarieti ya SADC na kuitaka ieleze kwanini uchumi katika nchi wanachama wa jumuiya hiyo unashindwa kufikia viwango vya kukua. Kwanini kwa miaka 10 lengo la kuondokana na tatizo la kiuchumi halijafikiwa.

Awali Rais Magufuli akielezea changamoto zinazoikabili jumuiya hiyo na kushindwa kufikia baadhi ya makubaliano, Rais Magufuli alisema changamoto ya kwanza ni vurugu za kisiasa, kutokamilika ahadi za kubadili uchumi na ukosefu wa taarifa za fursa katika nchi wanachama.

“Bado hatujafanikiwa katika ukuaji wa uchumi, niseme kweli bado tunasuasua. Na tusipibadilika hatutaweza kufanikiwa katu. Bado tupo nyuma katika lengo letu la kiuchumi, uhaba wa taarifa unasababisha tunashindwa kujua wapi pa kuuza bidhaa zetu,” alisema Rais Magufuli.

Naye Mwenyekiti aliyemaliza muda wake ambaye pia ni Rais wa Namibia, Dk. Hage Geingob alisema katika vitu alivyovutiwa katika mkutano huu wa kawaida wa 39 ni namna viongozi wastaafu walivyohudhuria wote na kuonyesha mshikamano.

“Mmeonyesha mfano mzuri kwa nchi za kiafrika, hii ndiyo Afrika tunayoitaka kuona viongozi wanaachia madaraka kwa mujibu wa katiba na wote wanakuwa na maelewano. Ninamuona rais wa awau ya pili, ya tatu na ya nne. Huu ni utekelezaji mzuri maneno ya Mwalimu Julius Nyerere,” alisema Dk. Geingob.

Katika hotuba yake ya kukabidhi uongozi alisema, Jiji la Dar es Salaam litabaki kuwa eneo la kihistoria kutokana na kuwa kitovu cha vuguvugu la harakati za ukombozi kwa nchi za kusini mwa Afrika.

Alisema, anayo furaha kuachiaa madaraka wakati nchi tano zilizo ndani ya SADC zilifanya uchaguzi huru na wa haki ukiofuata vigezo vyote vya jumuiya hiyo ndani ya kipindi chake.

“Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), kwa mara ya kwanza imefanya uchaguzi huru na wa haki tangu ipate uhuru miaka ya 1960, katika kipindi cha uongozi wangu nimeshuhudia mabadiliko ya kiuongozi katika nchi hiyo.

“Tukisema tunataka kufanikiwa kiuchumi lazima tuhakikishe tunaondokana na vurugu za kisiasa, ulinzi na amani ndiyo kitu cha kwanza katika kupata maendeleo,” alisema na kubainisha bado kunahitajika huduma muhimu katika jumuiya hiyo ikiwemo maji safi na salama.

Alisisitiza, vijaana wanahitaji kupewa kipaumbele katika maendeleo kwa kuwa wao ndio nguvu kazi. Pia aligusia suala la mabadiliko ya tabianchi yaliyosababisha uhaba wa chakula na vimbunga vilivyoharibu miundombinu kutokana na mvua kubwa zilizonyesha kwenye baadhi ya nchi wanachama.

“Kujumuisha vijana katika utungwaji wa sera na kuhuisha ufanyaji biashara baina ya nchi wanachama ni baadi ya changamoto zinazohitaji ufumbuzi wa haraka. Usafirishaji bidhaa katika mipaka ya nchi wanachama pia ni tatizo linalohitaji ufumbuzi wa haraka,” alisema Dk. Geingob.

Katibu Mtendaji wa SADC, Dk. Stergomena Tax alisema kwa muda wa mwaka mmoja uliopita Tanzania ndiyo iliyoonyesha mfano mzuri katika ukuaji uchumi na kufikia malengo ya kuanzishwa kwa jumuiya hiyo.

Alisema, ukuaji wa uchumi kwa asilimia 7 umeonyesha mfano mzuri wakati baadhi ya nchi wanachama ukuaji wake uchumi ulikuwa chini ya asiimia tatu. Alisema, wameonyesha mfano mzuri kwa kutoa misaada ya kiutu wakati baadhi ya nchi wanachama ziipokumbwa na majanga ya kimbunga ikiwemo Zimbabwe na Msumbiji.

Ameongeza kuwa “Tunavutiwa na kasi ya ajabu ya ujenzi wa miundombinu hasa miundmbinu ya nishati, kwa mfano hivi karibuni Tanzania imeonyesha mfano kwa kuanza mradai wa kufua umeme wa Nyerere HP katika Mto Rufiji. Mradi huu ukikamilika utazalisha Megawati 2,115 za umeme ambapo ni miongoni mwa mikakati ya SADC kuhuisha ukuaji wa uchumi kwa kuweka uhakika wa upatikanaji umeme kwa nchi wanachama,” alisema Dk. Tax.
 
Mwaka jana mkutano kama huu ulifanyika nchi gani?na mwenyekiti wa huko hotuba yake,ilikuwa haitoi matumaini?je utekelezaji wake hadi mamemaliza muda wake umefikia wapi?hicho ni kikao kama vile viongozi huwa wanageuza nchi kwenda kutalii,leo ni miaka 39,lakini ukisikiliza hotuba utafikili SADC ndiyo imeanzishwa leo.
 
Sioni Magufuli akiwa na matokeo yoyote chanya kwenye huo umoja. Magufuli anaweza kuonyesha tija yake pale tu anapopata nguvu ya dola kwani hana uwezo wa ushawishi. Ukiangalia kwenye huo umoja, ushawishi pekee ndio unaweza fanikisha jambo. Ikumbukwe katika hiyo jumuiya hana popote anapoweza kupeleka vyombo vya dola, na wala yeye sio msemaji wa mwisho. Katika mazingira hayo yeye ni kama bunduki isiyo na risasi ndani.
 
Nilikuwa nashangaa JF hata uzi wa kuponda hiyo hotuba haikuruhusia, hata kama ni kweli bwana yule kanunua jukwaa? Mara paap, kauzi kakapenya. Ngoja tuone itabarizi muda gani kabla hakajashtukiwa na kufutiliwa mbali.
 
Kiuhalisia rais Magufuli anaonyesha dhamira kwenye hotuba zake. Kwa kauli hizi tu anaonyesha ni kiongozi mwenye dira..

-Afrika ni tajiri. Tanzania sio maskini sisi ni tajiri.
-Tunasafirisha malighafi unauza tani za pamba unanunulia tractor ambayo ungezalishia bidhaa hapa nyumbani ungetengeneza ajira na faida ingeweza kununua tractors nyingi.

-Nchi zetu hazina taarifa...nchi za kusini zinaagiza bidhaa kutoka nje wakati hizo bidhaa zipo nchi jirani.... Ni moja ya viongozi wazuri tuliwahi kuwapata.
 
Muda mfupi uliopita Mh Rais wa Tanzania Dkt John Joseph Pombe Magufuli amehotubia mkutano wa nchi za kusini mwa Afrika yaani SADC.

Mh Rais pamoja na kuishukuru Jumuiya ya kusini mwa Afrika kwa kumuamini na kumkabidhi uenyekiti wa juimiya hiyo kwa kipindi cha mwaka mmoja yaani 2018/2019 ametoa hotuba ambayo imekuwa nzuri sana.

Mh Rais amezungumza mambo mbalimbali yakiwepo mambo ya kiuchumi. Mh Rais amesistiza kuwa nchi za SADC bado hazijatumia vizuri rasilimali zilizopo ili kukuza uchumi wa nchi hizo. Amesema kuwa pamoja na nchi hizi kuwa na kila kitu lakini bado uchumi wake umekuwa wa kusua sua. Matharani amesema kwa miaka kumi uchumi wa nchi hizi umekuwa unashuka badara ya kukua. Mh Rais ambaye ndiye Mwenyekiti mpya wa SADC kuonyesha uzalendo wake na kusimamia kile anachokiamini amewanyoshea vidole secretarieti ya SADC kuwa ndio tatizo. Amesema kuwa Secratarieti ndio wanafanya kazi za SADC za kila siku, lakini wameshindwa kuja na majawabu ya nini kifanyike kukuza GDP badara ya hivi ilivyo.

Amewataja marehemu Baba wa Taifa Mwl Nyerere, Agostino Neto, Mandela, Mzee Mgabe na wanzilishi wengine wa SADC kuwa walikuwa na malengo makubwa, lakini bado ndoto za wazee hawa hazijafanikiwa vizuri.

Mh Rais kwa suala la biashara amesema kuwa hakuna sababu nchi wanachama kuagiza bidhaa nje kama bidhaa hizo zinapatikana SADC. Amesema kunatakiwa kufungua milango ili wananchi wa nchi hizi kujua furusa zilizopo ktk nchi mwanachama. Amesema katka ziara yake ya mwezi may alishangaa nchi kuagiza nafaka nje wakati Tanzania kuna ziada ya kutosha.

Rais amesistiza wakati SADCC inabadirika na kuwa SADC ilitegemea kumaliza changamoto zote zilizokuwepo mwanzo, lakini uhalisia bado changamoto zipo. Ameshauri ni lazima sasa milango ya biashara ifunguliwe na kuondoa vikwazo vinavyoweza kuturudisha nyuma.

Amesema swala la siasa katika nchi hizi iko vizuri pamoja na changamoto ndogo ndogo. Amesema kwenye kipindi chake ataendelea kufanya yale yote kwa ajili ya Afrika.

Baada ya hotuba hii ya Mh Rais ambayo imejaa mambo mengi, binafsi imenionyesha dira mpya ya SADC. Ninamuona Brudozza kwenda kubadiri kabisa jumuia na kuwa na ufanisi mkubwa. Sura na maneno ya JPM yanaonyesha dira na matumaini makubwa kwa viongozi wote waliohudhuria mkutano huu.

Kila la heri JPM.
Asante kwa taarifa mkuu,lakini duh,hii lafudhi ni ya wapi,matharani,tubadiri,
inabadirika.Nadhani ni mathalani,kubadili na inabadilika.Mtiririkowako ni mzuri mkuu,lakini
maneno hayo yanatia dosari sana bandiko lako.
 
Back
Top Bottom