Hotuba ya Mwalimu Nyerere kuhusu Moyo wa Kujitolea

TandaleOne

JF-Expert Member
Sep 4, 2010
1,644
709
Mwaka 1988, Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere akiwa bado ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi alialikwa kama mgeni rasmi wa maadhimisho ya miaka 11 ya CCM ambayo yalifanyika Kitaifa Mkoani Tabora.

Katika Hotuba yake, Mwalimu Nyerere aliwakumbusha wazee wa Tabora na kuwashukuru kwa MOYO WAO WA KUJITOLEA, Mwalimu alisema isingelikuwa kwa ujasiri wao, tusingelikuwa na Tanzania huru.

Mwalimu anautaja mji wa Tabora kama kitovu kikuu cha harakati zake, anasema kuwa aliishi Tabora miaka 9, akiwa mwanafunzi Tabora School kwa miaka 6 na baadae Mwalimu wa Saint Mary's kwa miaka 3. Anasema ameishi Tabora wakati wa Vita na wakati wa Amani, anasema alijifunza kucheza bao katika viunga vya mji wa Tabora akiwa bado ni mwanafunzi bali akitoka kanisani alikuwa akienda kwenye vijiwe vya wazee na kucheza nao bao, Mwalimu anasema alijifunza hekima, busara nyingi na namna ya kuishi na watu kutoka kwao.

Katika hotuba ile Mwalimu anataja siku alizoziita SIKU ZA HATARI, anasema kuanzia walipounda TANU mwaka 1954,55 mpaka 1958 ilikuwa ni siku za hatari, na wengi katika watu na wanaharakati walipotea na kuteswa sana katika siku hizo, zilikuwa ni siku za hofu kuu na Mwalimu anasema TANU ilipata wanachama wachache sana katika miaka hiyo na kila mmoja aliogopa kuwa mwanachama ama kujihusisha na siasa za kudai uhuru. Mwalimu anasema hapa ndipo alipoishuhudia MIOYO ILIYOJITOLEA ambayo ilikuwa tayari kuondoka katika dunia hii kuliko kutawaliwa, walioweka rehani maisha yao, mali zao, familia zao, utu na heshima zao kwa maslahi ya WENGI.

Mambo makubwa yote duniani yanafanywa kwa kujitolea, hayafanywi kwa malipo na atakuwa amepotoka yule ambaye anadhani kuwa kufanya kwake jambo kubwa kwa maslahi ya nchi hii anapaswa malipo. Hatuwezi kujenga nchi kubwa yenye sifa bila kuwepo MTU ama KUNDI la watu wenye kujitolea. KUNDI KUBWA ZURI.

Mwalimu katika kumalizia anasimulia kuhusu mazungumzo yake na Padri mmoja aliyekuwa Headmaster pale tabora, Padri aliyemsaidia kwenda ulaya kusoma. Mwalimu alimuambia kuwa atafanikiwa kuiletea nchi uhuru akiwa na watu wanane (8) tu, kwani kipindi iko majimbo yalikuwa manane, Padri akamwambia, Mwalimu, jitahidi. Unaweza ukawapata, lakini hao peke yao hawatoshi lazima utafute wengine waaminifu.

Labda sijaandika kwa muda mrefu kwenye ukurasa huu, lakini leo naandika kumsifu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Joseph Magufuli kwa MOYO WAKE WA KUJITOLEA, lakini nisema tena, katika zama na masiku ya hatari anahitaji zaidi ya WATU WANANE (8) kuipatia Tanzania UKOMBOZI wa pili.

wp7d30a8eb.png
 
Hapa kwetu ni wachache tu wanaojitolea na katika hao wachache; wengi hujitolea kwenye mambo ya kipuuzi.

Ni heri kiongozi wetu ajitoleaye kwenye mambo makubwa ya kitaifa ijapokuwa bado changamoto ni nyingi.
 
Back
Top Bottom