Hotuba ya Muammar Gaddaffi ndiyo iliyonitoa machozi

Kwa taarifa yaki Gaddafi alikuwa rafiki mkubwa sana wa Nyerere. Achana na vita ya Uganda walimalizana siju nyingi sana. Kabla ta kufariki Nyerere alimuomba amjengee msikiti Butiama kajenga msikiti wa hela nyingi sana
 
16 REAL REASONS WHY COL. GADDAFI WAS KILLED:
1. There is no electricity bill in Libya, electricity is free for all its citizens.
2. There is no interest on loans, banks in Libya are state-owned and loans given to all its citizens at 0% interest by law.
3. Home considered a human right in Libya – Gaddafi vowed that his parents would not get a house until everyone in Libya had a
home. Gaddafi’s father has died while him, his wife and his mother are still living in a tent.
4. All newlyweds in Libya receive $60,000 Dinar (US$ 50,000 ) by the government to buy their first apartment so to help start up
the family.
5. Education and medical treatments are free in Libya. Before Gaddafi only 25% of Libyans are literate. Today the figure is 83%.
6. If Libyans want to take up farming career, they would receive farm land, a
farming house, equipment, seeds and livestock to kick- start their farms – all for free.
7. If Libyans cannot find the education or medical facilities they need in Libya, the government funds them to go abroad for it – not only free but they get US $2, 300/mth
accommodation and car allowance.
8. In Libyan, if a Libyan buys a car, the government subsidized 50% of the price.
9. The price of petrol in Libya is $0. 14 per liter.
10. Libya has no external debt and its reserves amount to $150 billion – now frozen globally.
11. If a Libyan is unable to get employment after graduation the state would pay the
average salary of the profession as if he or she is employed until
employment is found.
12. A portion of Libyan oil sale is, credited directly to the bank accounts of all Libyan citizens.
13. A mother who gave birth to a child receive US $5 ,000
14. 40 loaves of bread in Libya costs $ 0.15
15. 25% of Libyans have a university degree
16. Gaddafi carried out the world’s largest irrigation project, known as the Great Man- Made River project, to make water readily available throughout the desert country.
 
They will forever miss him
No, they won't. Wakati mwingine kama nchi inabidi kupita katika moto na misukosuko ili hatimaye muweze kuaminiana na kuheshimiana. Wamarekani wamefika hapo walipo baada ya ile civil war. Walibya watavuka na watajenga taifa imara zaidi kwani wameshaunguzwa na moto. Gaddafi hakuwa mungu na angeweza kufa wakati wo wote hata kama asingeuwawa. Hebu msimpe sifa za uungu mtu dikteta na gaidi huyu aliyempa madege na pesa Idd Amin atupige kule Kagera wakati huo huo akihubiri umoja wa Afrika. Sipendi mabeberu wa Magharibi walivyomuua kama mnyama lakini pia naye alishindwa kusoma alama za nyakati na ku-adjust accordingly na mipango ya kumwandaa mwanawe aje atawale baada yake ilivurugwa. Kuna kipindi kilirushwa na NPR na hakikuwa biased bali kiliongelea mema yake mengi na mabaya yake mengi. Historia itamhukumu lakini siyo sahihi kumvisha umalaika kwani her was no angel japo kwa nje alitaka sana watu (na hasa Waafrika) wamwone kama mkombozi. He got what he deserved na hii iwe reminder kwetu binadamu no matter who you are, you can die or be eliminated anytime na maisha yataendelea. Hata misukosuko itokee lakini historia inatufundisha kwamba mambo yatatulia na hatua mpya zitapigwa. Libya will be OK!
 
Mada za huyu gaidi zimejaa humu. Kabla hujapost jaribu kuchunguza

Gaddafi alikua gaidi kama wengine wote

wwe ↑↑↑↑↑ ni moja ya waafrica wengi ambao wamekuwa brain washed na sera za magharibi .ila jua tu hao waliomuuua gaddafi leo hii wanajuta ma kutamani kumrudisha duniani
 
Nilimdharau sana alipompa madege Idd Amin na pesa wakati wa vita vya Kagera. Anahubiri umoja wa Afrika wakati huo huo anamuunga mkono huyu na kumuacha huyu.

Ali-underestimate presha za mabeberu na watu wake akidhani kuwa ni business as usual mpaka akashindwa kusoma alama za nyakati. Na walinzi wake wale makomandoo wa kike wakasepa akaishia kuuawa kama jambazi. Historia itamhukumu!
Nipe sababu za kupinduliwa iddi amini? Hakuna zaidi ya uislam, kama MAPINDUZI ya Zanzibar chini ya Nyerere
 
Nipe sababu za kupinduliwa iddi amini? Hakuna zaidi ya uislam, kama MAPINDUZI ya Zanzibar chini ya Nyerere
Huwa sipotezi muda kujadili mambo ya dini hasa hizi za kuletewa na watawala wetu. Kama unataka tujadili mambo ya dini basi tujadili dini za mababu zetu kabla hatujavamiwa na makafiri kutoka nje.
 
tuna Mengi ya kujifunza. USA hawana jema kwa Africa

Mimi ni mkristo. Nimefuatilia kwa kina utawala wa Qaddafi na jinsi alivyoongoza. Kwa roho moja kabisa nasema Afrika haijapata kiongozi kama Qaddafi. Kama mwanadamu alikuwa na madhaifu yake, lakini alijitahidi sana kutenda kwa haki Mungu amrehemu.

Halafu licha ya yote, bado tunaendelea kujikomba kwa mataifa ya magharibi!? Kifo cha Qaddafi kilitokana na juhudi zake kujaribu kututoa kwenye kongwa la utumwa.
 
Ukisoma harakaharaka bila kutafakari kwa makini unaweza kuona Gadafi alikuwa mtu mwema sana na hakuwa na hatia. Yaliyoandikwa kwenye hotuba yake baadhi yana ukweli,baadhi ni uongo mtupu!Baadhi ya mapungufu ya kiongozi huyu yalikuwa kama ifuatavyo:

*Huyu jamaa alikuwa anafuja rasilimali za nchi ya libya,yeye pamoja na familia yake, mfano mzuri ni mali alizokuwa anamiliki yeye pamoja na watoto wake. Aidha,Mutassim Gadafi pamoja na Seif al Islam Gadafi walikuwa wanamiliki majumba na magari ya kifahari.

*Huyu jamaa alileta utengano katika bara la Afrika,angalia katika vita ya Uganda na Tanzania mwaka 1978 alikuwa upande wa Uganda,badala kuhakikisha amani inapatikana kwa njia ya mazungumzo.

*Alikuwa anamwandaa mwanae Seif Al Islam ili aweze kurisi kiti cha urais,hii ni kinyume na misingi ya demokrasia.

*Libya ilikuwa haina katiba inayowaruhusu wananchi kuamua hatma ya nchi yao.

Mkuu, usicheze ngoma ya mabepari. Walichofanya ni kumpa Qaddafi jina baya ili wamuue.

Kwamba alifuja raslimali, nionyeshe kiongozi mmoja tu Afrika aliyetenda sawa sawa naye, aliyejali nchi na watu wake. Hata ulaya hakuna!

Kwamba alileta utengano, ni mambo ya kale sawa sawa na mwalimu Nyerere alivyosapoti Biafra. Lakini Qaddafi siku zote amekuwa akipigania umoja wa waafrika. Na hii ni mojawapo ya sababu iliyopelekea kuuawa kwake.

Kwamba Libya haikuwa na katiba. Qaddafi aliipinga mfumo wa demokrasia ya kimagharibi akisema inawapa ustawi wachache tu. Hata bunge hakulitaka kwani alisema ni genge linalo conspire kuwaibia wananchi. Aliona ni bora wananchi wajiwakilishe wenyewe. Aliandika "The green book " ambamo mojawapo ya masuala makubwa ni kufanya makazi kama hitaji la msingi la binadamu.

Kwamba alikuwa akimwandaa mwanae, inategemea unamsikiliza nani. Kama unalishwa habari na CNN na BBC, basi uko sahihi. Lakini kama unafahamu kuwa hizo media ni by in no vya propaganda, utajiongeza!
 
Kwa hiyo unataka kutuambia Libya ya sasa ina demokrasia? MBNA unaongeo utumbo mkuu
 
Sitaandika tena nilishajibu hapo nimeweka link na unaweza kusearch zaidi kuhusu matukio ya kigaidi aliyoyasponsor

Gaddafi alikua gaidi na kupinduliwa kwake hadi kupelekea mauti yake ilikua inevitable. Tatizo mnasoma hizi habari zinazompamba tu ila Yale maovu yake hamyasemi wala kufuatilia kwa kina

Ni Gaddafi huyu aliyeisaidia Uganda pindi inapigana na iddi Amin yet mitanganyika bado inamsifia

Gaddafi kasponsor matukio ya kigaidi mengi tu kwa pesa za serikali ya Libya alizokuwa anachukulia kama zake binafsi.

Unakumbuka disco bombing in German 1986, hijacking of PAN AM, bombing of uta flight 1989; state sponsored assassination attempts against the leaders of Tunisia, DRC, Chad et cetera et cetera.. Mengi ya hayo matukio he pleaded guilty na kulipa fidia kwa wahanga. Kifupi jamaa alikua gaidi na kupinduliwa kwake kulikua inevitable. Remember hakuuwawa na wamarekani bali na watu wa nchi yake kama angekua mwema hivyo kama mnavyodai wasingemuua kikatili vile

Kama yai linapanda ingia hapa: Muammar Qaddafi and Libya's Legacy of Terrorism
Tatzo hujui ulisemalo
 
HOTUBA YA MWISHO YA GADDAFI

QADAFFI ANAANZA HIVI: "Kwa jina la Mwenyezi Mungu (Allah), Mungu mpaji, na mwenye rehema.

Kwa miaka takribani 40 ama ilikuwa zaidi sikumbuki. Nachokumbuka ni kuwa nilifanya kila nilichoweza kuwapa watu wangu nyumba, hospitali na shule. Na kila walipohisi njaa niliwapa chakula. Niliifanya Benghazi kutoka jangwa kuwa ardhi nzuri ya kilimo.

Nilisimama imara dhidi ya Ronald Regan (Rais wa zamani wa Marekani), alipomuua binti yangu niliyemuasili. Alikua anajaribu kuniua mimi lakini akamuua yule binti yatima masikini. Niliwasaidia kaka na dada zangu waafrika fedha kupitia AU.

Nilifanya kila nililoweza kuwafanya watu wangu waelewe maana halisi ya demokrasia; ambapo watu wa tabaka la chini niliwapa madaraka.

Lakini hawakuridhika. Hata aliyekuwa na nyumba ya vyumba kumi, nguo mpya, na fanicha nzuri, hakuridhika. Alihitaji zaidi.

Kwa jinsi walivyokuwa wabinafsi walihitaji zaidi. Hivyo wakawaambia Marekani kuwa wanataka "demokrasia" na "uhuru". Hawakujua kuwa "demokrasia" waliyoitaka ilikua ni mfumo wa unyonyaji ambapo mbwa mwenye nguvu zaidi huwala mbwa wadogo.

Walikua hawasikii wala hawaoni. Walitaka "demokrasia". Wakasahau kuwa hata Marekani hakukuwa na huduma za afya za bure, dawa bure, elimu bure na chakula cha bure. (Huduma hizi za bure zilipatikana Libya tu).

Nchini Marekani mtu masikini/fukara hana cha bure. Labda awe ombaomba au avuje jasho kuhemea.

Haikujalisha nilifanya kwa kiasi gani bado hawakuridhika. Lakini wapo waliojua mimi ni mtoto wa Gamal Abdel Nasser, mwarabu pekee halisi na kiongozi wa kiislamu tuliyewahi kuwa nae tangu enzi za Salah-al-Deen.

Wakati Nasser anapigania mfereji wa Suez kwa watu wake nami nilikua naipigania Libya kwa watu wangu. Nilikua najaribu kufuata nyayo zake ili kuwaweka watu wangu huru kutoka kwenye makucha ya wakoloni wanaotuibia.

Lakini kwa sasa niko mateka katikati ya majeshi makubwa ya dunia katika historia. Mwanangu mpendwa mwenye asili ya Afrika, Obama anataka kuniua.

Ili achukue uhuru wetu, achukue haki yetu ya huduma za bure za afya, huduma za bure za elimu, na chakula chetu; na kutuletea mfumo mpya wa kimarekani wa kuiba uitwao "Ubepari"

Lakini wote katika dunia ya tatu tunajua maana yake. Maana yake ni kuwa "washirika" wanatawala mataifa, wanatawala dunia, na watu wanaishia kuteseka.

Kwa hiyo hakuna mbadala kwangu. Lazima niwe na msimamo. Na kama Mungu atapenda nitakufa kwa mapenzi yake.

Mapenzi yake yaliyofanya nchi yetu kuwa na ardhi yenye rutuba, chakula bora, na huduma bora za afya. Mapenzi ya Allah yaliyowezesha tukawasaidia kaka na dada zetu waafrika na waarabu waliokuwa na shida.

Sipendi kufa; lakini kama nitakufa ili kuiokoa ardhi hii, kuokoa watu wangu, na wengine ambao ni kama wanangu; acha nife.!

Acha sauti hii iwe agano langu kwa dunia kuwa nilisimama kupinga uvamizi wa NATO. Nilisimama kishujaa kupinga usaliti wa nchi za magharibi na nia mbaya za kikoloni. Na hapa nimesimama na ndugu zangu waafrika, kaka na dada zangu waislamu kama ngao yangu ya matumaini.

Wakati wengine walipokuwa wanajenga majumba ya kifahari, mimi niliishi kwenye nyumba ya kawaida na kwenye mahema. Siwezi kusahau maisha yangu ya utoto kule Sirte.

Sikutapanya rasilimali za nchi yangu kipumbavu. Na kama alivyokua Salah-al-Deen, kiongozi wetu katika uislamu, nilichukua kidogo sana kwa ajili yangu, na sehemu kubwa niliwapa wananchi.

Watu wa magharibi wameniita "kichaa", "mwendawazimu" lakini wanajua ukweli kuwa mimi si kichaa wala mwendawazimu; ila waache waendelee kudanganya. Wanajua hii ardhi ni huru na haipo kwenye himaya ya kikoloni. Huu ndio msimamo wangu na dira yangu na imekuwa wazi kwa watu wangu.

Nitapambana hadi pumzi yangu ya mwisho ili watu wangu wawe huru. Mwenyezi Mungu atusaidie tubaki waaminifu na tuwe huru.

-- Mu'uammar Qaddafi.

You will forever remain MY TRUE AFRICAN HERO. Rest in Jannah Colonel Muammar Ghadafi
 
Mkuu, usicheze ngoma ya mabepari. Walichofanya ni kumpa Qaddafi jina baya ili wamuue.

Kwamba alifuja raslimali, nionyeshe kiongozi mmoja tu Afrika aliyetenda sawa sawa naye, aliyejali nchi na watu wake. Hata ulaya hakuna!

Kwamba alileta utengano, ni mambo ya kale sawa sawa na mwalimu Nyerere alivyosapoti Biafra. Lakini Qaddafi siku zote amekuwa akipigania umoja wa waafrika. Na hii ni mojawapo ya sababu iliyopelekea kuuawa kwake.

Kwamba Libya haikuwa na katiba. Qaddafi aliipinga mfumo wa demokrasia ya kimagharibi akisema inawapa ustawi wachache tu. Hata bunge hakulitaka kwani alisema ni genge linalo conspire kuwaibia wananchi. Aliona ni bora wananchi wajiwakilishe wenyewe. Aliandika "The green book " ambamo mojawapo ya masuala makubwa ni kufanya makazi kama hitaji la msingi la binadamu.

Kwamba alikuwa akimwandaa mwanae, inategemea unamsikiliza nani. Kama unalishwa habari na CNN na BBC, basi uko sahihi. Lakini kama unafahamu kuwa hizo media ni by in no vya propaganda, utajiongeza!
*Hata kama hakuna kiongozi wa Africa aliyetenda mazuri kama yeye lakini ukweli unabaki palepale, ni kweli aliwatendea watu wake mazuri, lakini pia alifuja rasilimali za nchi.
*Nyerere kwa aliyoyafanya kuhusiana na Biafra na alichokifanya Gadafi kwenye vita ya Tanzania na Uganda, hawa wote wawili hawawezi kuchukuliwa kama watawala waliopigania umoja wa Afrika labda tuwe tumeamua kujivua ufahamu.
*Mkuu katiba ni sheria mama, kwa vyoyote vile kutokuwepo kwa katiba katika nchi yoyote duniani ni tatizo, hata iwe kwa nia njema ipi,umuhimu wa katiba unabaki palepale.
*Iwe wametangaza al jazira,CNN au BBC ukweli unabaki palepale, kuna ushahidi wa kutosha unaoonyesha Gadafi alikuwa anamwandaa Saif Al Islam Gadafi kurithi kiti chake.
 
Hauko sahihi hata kidogo.. Tatizo la Libya au Africa kwa ujumula siyo katiba au uwezo wa kufanya chaguzi kila baada ya muda fulani, tatizo ni kuwa mali zetu zinamfaidisha nani. Wazungu, ambao nahisi wewe ni kibaraka wao, wakiwa wanatambua hatma ya kuwepo kwao bila raslimali kutoka Africa, watafanya kila njia ili wasikose. Watawavuruga watu ili kuwaaminisha ujinga, wataleta propaganda ili kuwagawa watu au wataleta makombora ili kuwaua nyote msiotaka waibe mali zenu. Kilichotokea kwa Ghadafi (RIP) ndicho huwatokea viongozi shupavu (Lumumba, Sankara, Machel, Abdel Nasser, nk). Tukirudi kwetu hapa, usidanganyike kudhani kwamba wazungu na vibaraka wao wanafurahia anachokifanya JPM... la hasha. Wapo wanapanga figisu fugisu ilimradi waendelee kutuibia. Kuna hili lazima tulitambue, makampuni toka Uingereza yanayofanya biashara hapa tz hayalipi kodi na hili serikali inalitambua na awam zilizopita zimekuwa zikifumbia macho si kwa utashi wao bali ushawishi toka Uingereza kwa vidingizio mbali mbali. Moja wapo ya kisingizio ni misaada inayotolewa na Uingereza kwa Tz. Hiyo misaada ni ya kishetani na ya kidhalilishaji na hailingani na kiasi cha kodi ambacho kingelipwa. Challenge kwa Magufuli ni kukataa misaada ili terms zibaki "msaada wako chukuwa, kodi yangu nipe yote". Mpaka hilo litokee, wazungu watapiga kelele, wataita majina ya ajabu ajabu, mara dikteta, gaidi, tyrant, nk..

Ni vema yaliyotokea Libya yakatupa lesson sisi kama Waafrika na si propaganda nyepesi kama democrasia na upuuzi mwingine.. Tuko vitani dhidi ya wizi wa mchana, dhidi ya uongo na propaganda kwa manufaa yetu sisi na vizazi vijavyo baada yetu.. Tusijitoe ufaham kumlaani Ghadafi huku tukiwapongeza wazungu la sivyo kumukumbu zetu zitakuwa fupi kama chu/pi. Nawasilisha

Ila wakati wa JK walikuwa wanafurahia kwa kuwa alishirikiana nao kutuibia kupitia mikataba ya siri...na ninyi mlikuwa mnachekelea na kuwabeza waliokuwa wanahoji...

Dunia imejaa unafiki. Wacha kila mtu aishi miaka yake aondoke!
 
*Hata kama hakuna kiongozi wa Africa aliyetenda mazuri kama yeye lakini ukweli unabaki palepale, ni kweli aliwatendea watu wake mazuri, lakini pia alifuja rasilimali za nchi.
*Nyerere kwa aliyoyafanya kuhusiana na Biafra na alichokifanya Gadafi kwenye vita ya Tanzania na Uganda, hawa wote wawili hawawezi kuchukuliwa kama watawala waliopigania umoja wa Afrika labda tuwe tumeamua kujivua ufahamu.
*Mkuu katiba ni sheria mama, kwa vyoyote vile kutokuwepo kwa katiba katika nchi yoyote duniani ni tatizo, hata iwe kwa nia njema ipi,umuhimu wa katiba unabaki palepale.
*Iwe wametangaza al jazira,CNN au BBC ukweli unabaki palepale, kuna ushahidi wa kutosha unaoonyesha Gadafi alikuwa anamwandaa Saif Al Islam Gadafi kurithi kiti chake.
Alifuja nini? Una ushahidi wowote? Tuonyeshe rais amvaye ni malaika. Watu wengi wanaendeshwa na western propaganda. Wamagharibi wanatumia msemo wa "ukitaka kumuua mbwa mpe jina baya
 
Global Politics are too complicated. Kwa utawala bora ni kufuata matakwa yao ya kiunyonyaji. RIP bro, kwani sasa hivi wanachi wako wa Libya uliowaacha wanakukumbuka kutokana na uliyowafanyia na wanaendelea kukukumbuka pia kutokakana na wanayofanyiwa na vibaraka wa mwamarekani. RIP our hero.
 
Back
Top Bottom