Mada za huyu gaidi zimejaa humu. Kabla hujapost jaribu kuchunguza
Gaddafi alikua gaidi kama wengine wote
Ukisoma harakaharaka bila kutafakari kwa makini unaweza kuona Gadafi alikuwa mtu mwema sana na hakuwa na hatia. Yaliyoandikwa kwenye hotuba yake baadhi yana ukweli,baadhi ni uongo mtupu!Baadhi ya mapungufu ya kiongozi huyu yalikuwa kama ifuatavyo:
*Huyu jamaa alikuwa anafuja rasilimali za nchi ya libya,yeye pamoja na familia yake, mfano mzuri ni mali alizokuwa anamiliki yeye pamoja na watoto wake. Aidha,Mutassim Gadafi pamoja na Seif al Islam Gadafi walikuwa wanamiliki majumba na magari ya kifahari.
*Huyu jamaa alileta utengano katika bara la Afrika,angalia katika vita ya Uganda na Tanzania mwaka 1978 alikuwa upande wa Uganda,badala kuhakikisha amani inapatikana kwa njia ya mazungumzo.
*Alikuwa anamwandaa mwanae Seif Al Islam ili aweze kurisi kiti cha urais,hii ni kinyume na misingi ya demokrasia.
*Libya ilikuwa haina katiba inayowaruhusu wananchi kuamua hatma ya nchi yao.
tuna Mengi ya kujifunza. USA hawana jema kwa Africa
Mkuu soma kwa makini nichoandika,wapi nimesema alikuwa Gaidi?ok fine huyo gadaff alikua gaidi vipi ukiangalia wananchi wake kipindi yupo hai na sasa ivi hua unafuatilia watu wa libya?kama ndio basi usingeandika ulichoandika
Mada za huyu gaidi zimejaa humu. Kabla hujapost jaribu kuchunguza
Gaddafi alikua gaidi kama wengine wote
Mnaompinga Qadafi na wengine mkimuita ghaidi nina imani mna elimu duni sana na pia ni wavivu wa kutafuta elimu ili muwe huru. Hayo mambo mnayosema eti Qadafi aliwaadaa wanaye ili kumrithi au kuwa alikuwa na utajiri mwingi ni habari mlizosikia katika vyombo vya habari vya kibeberu, cnn, bbc, skynews, etc.. vinginevyo hakuna mwenye ushaidi wa hayo madai, mnashabikia msivyovijua kama mazuzu tu.. hata siku moja mzungu hatakaa awaseme mazuri watu wa Africa, abadan! Tusiwe mapopoma.. tujiongeze kwa kila tunachoambiwa. Kuhusu vita ya tz na uganda na kuhusika kwa Qadafi, imekaa kipropaganda zaidi lakini usisahau Tanzania imeshajihusisha kivita katika nchi kadhaa japo hayo hamtaki kukumbuka.
Jaribu kuchunguza kila jambo kwa jicho la pili. Mara nyingi vyombo vya habari vna nguvu sana ya kufanya uongo wowote wa kpropaganda uonekane kama ukweli. Gadafi ni gaidi,kwa nini hakumkamata mara kadhaa alipotembelea nchi zao?
vipi ukiyaangalia maisha ya walibya sasa hivi?jf imekua na watoto wengi sana
Gaidi babu yako aliyekulea Bila kukufundisha Nidhamu.Usitudanganye wewe gadafi alikua gaidi au umesahau alimfadhili idd amini atupige?tafuta cha kuandika wewe
HOTUBA YA MWISHO YA GADDAFI
QADAFFI ANAANZA HIVI: "Kwa jina la Mwenyezi Mungu (Allah), Mungu mpaji, na mwenye rehema.
Kwa miaka takribani 40 ama ilikuwa zaidi sikumbuki. Nachokumbuka ni kuwa nilifanya kila nilichoweza kuwapa watu wangu nyumba, hospitali na shule. Na kila walipohisi njaa niliwapa chakula. Niliifanya Benghazi kutoka jangwa kuwa ardhi nzuri ya kilimo.
Nilisimama imara dhidi ya Ronald Regan (Rais wa zamani wa Marekani), alipomuua binti yangu niliyemuasili. Alikua anajaribu kuniua mimi lakini akamuua yule binti yatima masikini. Niliwasaidia kaka na dada zangu waafrika fedha kupitia AU.
Nilifanya kila nililoweza kuwafanya watu wangu waelewe maana halisi ya demokrasia; ambapo watu wa tabaka la chini niliwapa madaraka.
Lakini hawakuridhika. Hata aliyekuwa na nyumba ya vyumba kumi, nguo mpya, na fanicha nzuri, hakuridhika. Alihitaji zaidi.
Kwa jinsi walivyokuwa wabinafsi walihitaji zaidi. Hivyo wakawaambia Marekani kuwa wanataka "demokrasia" na "uhuru". Hawakujua kuwa "demokrasia" waliyoitaka ilikua ni mfumo wa unyonyaji ambapo mbwa mwenye nguvu zaidi huwala mbwa wadogo.
Walikua hawasikii wala hawaoni. Walitaka "demokrasia". Wakasahau kuwa hata Marekani hakukuwa na huduma za afya za bure, dawa bure, elimu bure na chakula cha bure. (Huduma hizi za bure zilipatikana Libya tu).
Nchini Marekani mtu masikini/fukara hana cha bure. Labda awe ombaomba au avuje jasho kuhemea.
Haikujalisha nilifanya kwa kiasi gani bado hawakuridhika. Lakini wapo waliojua mimi ni mtoto wa Gamal Abdel Nasser, mwarabu pekee halisi na kiongozi wa kiislamu tuliyewahi kuwa nae tangu enzi za Salah-al-Deen.
Wakati Nasser anapigania mfereji wa Suez kwa watu wake nami nilikua naipigania Libya kwa watu wangu. Nilikua najaribu kufuata nyayo zake ili kuwaweka watu wangu huru kutoka kwenye makucha ya wakoloni wanaotuibia.
Lakini kwa sasa niko mateka katikati ya majeshi makubwa ya dunia katika historia. Mwanangu mpendwa mwenye asili ya Afrika, Obama anataka kuniua.
Ili achukue uhuru wetu, achukue haki yetu ya huduma za bure za afya, huduma za bure za elimu, na chakula chetu; na kutuletea mfumo mpya wa kimarekani wa kuiba uitwao "Ubepari"
Lakini wote katika dunia ya tatu tunajua maana yake. Maana yake ni kuwa "washirika" wanatawala mataifa, wanatawala dunia, na watu wanaishia kuteseka.
Kwa hiyo hakuna mbadala kwangu. Lazima niwe na msimamo. Na kama Mungu atapenda nitakufa kwa mapenzi yake.
Mapenzi yake yaliyofanya nchi yetu kuwa na ardhi yenye rutuba, chakula bora, na huduma bora za afya. Mapenzi ya Allah yaliyowezesha tukawasaidia kaka na dada zetu waafrika na waarabu waliokuwa na shida.
Sipendi kufa; lakini kama nitakufa ili kuiokoa ardhi hii, kuokoa watu wangu, na wengine ambao ni kama wanangu; acha nife.!
Acha sauti hii iwe agano langu kwa dunia kuwa nilisimama kupinga uvamizi wa NATO. Nilisimama kishujaa kupinga usaliti wa nchi za magharibi na nia mbaya za kikoloni. Na hapa nimesimama na ndugu zangu waafrika, kaka na dada zangu waislamu kama ngao yangu ya matumaini.
Wakati wengine walipokuwa wanajenga majumba ya kifahari, mimi niliishi kwenye nyumba ya kawaida na kwenye mahema. Siwezi kusahau maisha yangu ya utoto kule Sirte.
Sikutapanya rasilimali za nchi yangu kipumbavu. Na kama alivyokua Salah-al-Deen, kiongozi wetu katika uislamu, nilichukua kidogo sana kwa ajili yangu, na sehemu kubwa niliwapa wananchi.
Watu wa magharibi wameniita "kichaa", "mwendawazimu" lakini wanajua ukweli kuwa mimi si kichaa wala mwendawazimu; ila waache waendelee kudanganya. Wanajua hii ardhi ni huru na haipo kwenye himaya ya kikoloni. Huu ndio msimamo wangu na dira yangu na imekuwa wazi kwa watu wangu.
Nitapambana hadi pumzi yangu ya mwisho ili watu wangu wawe huru. Mwenyezi Mungu atusaidie tubaki waaminifu na tuwe huru.
-- Mu'uammar Qaddafi.