Hotuba ya Muammar Gaddaffi ndiyo iliyonitoa machozi

Walibya Wenyewe wanasema hivi sasa :

“It was better under Gaddafi,” says the young Libyan student, studying the froth bubbling over the top of his cappuccino in a cafe in Tunis as he contemplates the revolution that sweptMuammar Gaddafi-from power four years ago. “I never thought to say this before, I hated him, but things were better then. At least we had security.”

SOURCE : Libya's Arab spring: the revolution that ate its children | World news | The Guardian
 
Mada za huyu gaidi zimejaa humu. Kabla hujapost jaribu kuchunguza

Gaddafi alikua gaidi kama wengine wote
 
Nilimdharau sana alipompa madege Idd Amin na pesa wakati wa vita vya Kagera. Anahubiri umoja wa Afrika wakati huo huo anamuunga mkono huyu na kumuacha huyu.

Ali-underestimate presha za mabeberu na watu wake akidhani kuwa ni business as usual mpaka akashindwa kusoma alama za nyakati. Na walinzi wake wale makomandoo wa kike wakasepa akaishia kuuawa kama jambazi. Historia itamhukumu!
 
Usitudanganye wewe gadafi alikua gaidi au umesahau alimfadhili idd amini atupige?tafuta cha kuandika wewe
 
Aisee mkuu usirudie kupost mada za Ghaddaf humu, unatonesha mioyo ya Walibya. Walikengeuka wakawaamini wazungu na siasa zao kandamizi!
Mwafrika anaepinga mazuri aliyofanya Ghaddaf, huyo bado atakuwa mtumwa na hasa akiwa Mtanzania ndo namdharaau kabisa make harakati afanyazo Magufuli sahizi ndizo alianza nazo Ghaddaf. Ila harakati hizi zikikuwa na kutanuka zaidi kiasi cha kugusa makalio ya wazungu ndo hapo utawasikia wanataharuki na kuja juu kwakujifanya wanatetea ngozi nyeusi!!?... Jiulize tangu lini ngozi nyeusi ikatetewa na mzungu? hata historia inakataa!
Ukigusa au kujinemeesha zaidi kuliko masrahi ya mzungu.. watakupachika majina mengi na mwisho wa siku watakupiga na kukuibia... ndicho walichofanya Libya-Nchi iliyokuwa imefikia kiwango cha juu kabisa katika ustawi!!
RIP Ghaddaf
VIVA Mughabe
ALUTA CONTINUA Magufuli.
 
Ukisoma harakaharaka bila kutafakari kwa makini unaweza kuona Gadafi alikuwa mtu mwema sana na hakuwa na hatia. Yaliyoandikwa kwenye hotuba yake baadhi yana ukweli,baadhi ni uongo mtupu!Baadhi ya mapungufu ya kiongozi huyu yalikuwa kama ifuatavyo:

*Huyu jamaa alikuwa anafuja rasilimali za nchi ya libya,yeye pamoja na familia yake, mfano mzuri ni mali alizokuwa anamiliki yeye pamoja na watoto wake. Aidha,Mutassim Gadafi pamoja na Seif al Islam Gadafi walikuwa wanamiliki majumba na magari ya kifahari.

*Huyu jamaa alileta utengano katika bara la Afrika,angalia katika vita ya Uganda na Tanzania mwaka 1978 alikuwa upande wa Uganda,badala kuhakikisha amani inapatikana kwa njia ya mazungumzo.

*Alikuwa anamwandaa mwanae Seif Al Islam ili aweze kurisi kiti cha urais,hii ni kinyume na misingi ya demokrasia.

*Libya ilikuwa haina katiba inayowaruhusu wananchi kuamua hatma ya nchi yao.
 
Hauko sahihi hata kidogo.. Tatizo la Libya au Africa kwa ujumula siyo katiba au uwezo wa kufanya chaguzi kila baada ya muda fulani, tatizo ni kuwa mali zetu zinamfaidisha nani. Wazungu, ambao nahisi wewe ni kibaraka wao, wakiwa wanatambua hatma ya kuwepo kwao bila raslimali kutoka Africa, watafanya kila njia ili wasikose. Watawavuruga watu ili kuwaaminisha ujinga, wataleta propaganda ili kuwagawa watu au wataleta makombora ili kuwaua nyote msiotaka waibe mali zenu. Kilichotokea kwa Ghadafi (RIP) ndicho huwatokea viongozi shupavu (Lumumba, Sankara, Machel, Abdel Nasser, nk). Tukirudi kwetu hapa, usidanganyike kudhani kwamba wazungu na vibaraka wao wanafurahia anachokifanya JPM... la hasha. Wapo wanapanga figisu fugisu ilimradi waendelee kutuibia. Kuna hili lazima tulitambue, makampuni toka Uingereza yanayofanya biashara hapa tz hayalipi kodi na hili serikali inalitambua na awam zilizopita zimekuwa zikifumbia macho si kwa utashi wao bali ushawishi toka Uingereza kwa vidingizio mbali mbali. Moja wapo ya kisingizio ni misaada inayotolewa na Uingereza kwa Tz. Hiyo misaada ni ya kishetani na ya kidhalilishaji na hailingani na kiasi cha kodi ambacho kingelipwa. Challenge kwa Magufuli ni kukataa misaada ili terms zibaki "msaada wako chukuwa, kodi yangu nipe yote". Mpaka hilo litokee, wazungu watapiga kelele, wataita majina ya ajabu ajabu, mara dikteta, gaidi, tyrant, nk..

Ni vema yaliyotokea Libya yakatupa lesson sisi kama Waafrika na si propaganda nyepesi kama democrasia na upuuzi mwingine.. Tuko vitani dhidi ya wizi wa mchana, dhidi ya uongo na propaganda kwa manufaa yetu sisi na vizazi vijavyo baada yetu.. Tusijitoe ufaham kumlaani Ghadafi huku tukiwapongeza wazungu la sivyo kumukumbu zetu zitakuwa fupi kama chu/pi. Nawasilisha

Tunaomba uthibitisho, maana kuongea tu huna ushahidi ni maigizo tu

Gaddafi alikua gaidi na kupinduliwa kwake hadi kupelekea mauti yake ilikua inevitable. Tatizo mnasoma hizi habari zinazompamba tu ila Yale maovu yake hamyasemi wala kufuatilia kwa kina

Ni Gaddafi huyu aliyeisaidia Uganda pindi inapigana na iddi Amin yet mitanganyika bado inamsifia

Gaddafi kasponsor matukio ya kigaidi mengi tu kwa pesa za serikali ya Libya alizokuwa anachukulia kama zake binafsi.

Unakumbuka disco bombing in German 1986, hijacking of PAN AM, bombing of uta flight 1989; state sponsored assassination attempts against the leaders of Tunisia, DRC, Chad et cetera et cetera.. Mengi ya hayo matukio he pleaded guilty na kulipa fidia kwa wahanga. Kifupi jamaa alikua gaidi na kupinduliwa kwake kulikua inevitable. Remember hakuuwawa na wamarekani bali na watu wa nchi yake kama angekua mwema hivyo kama mnavyodai wasingemuua kikatili vile

Kama yai linapanda ingia hapa: http://www.pbs.org/wgbh/frontline/article/muammar-qaddafi-and-libyas-legacy-of-terrorism/
 
Hauko sahihi hata kidogo.. Tatizo la Libya au Africa kwa ujumula siyo katiba au uwezo wa kufanya chaguzi kila baada ya muda fulani, tatizo ni kuwa mali zetu zinamfaidisha nani. Wazungu, ambao nahisi wewe ni kibaraka wao, wakiwa wanatambua hatma ya kuwepo kwao bila raslimali kutoka Africa, watafanya kila njia ili wasikose. Watawavuruga watu ili kuwaaminisha ujinga, wataleta propaganda ili kuwagawa watu au wataleta makombora ili kuwaua nyote msiotaka waibe mali zenu. Kilichotokea kwa Ghadafi (RIP) ndicho huwatokea viongozi shupavu (Lumumba, Sankara, Machel, Abdel Nasser, nk). Tukirudi kwetu hapa, usidanganyike kudhani kwamba wazungu na vibaraka wao wanafurahia anachokifanya JPM... la hasha. Wapo wanapanga figisu fugisu ilimradi waendelee kutuibia. Kuna hili lazima tulitambue, makampuni toka Uingereza yanayofanya biashara hapa tz hayalipi kodi na hili serikali inalitambua na awam zilizopita zimekuwa zikifumbia macho si kwa utashi wao bali ushawishi toka Uingereza kwa vidingizio mbali mbali. Moja wapo ya kisingizio ni misaada inayotolewa na Uingereza kwa Tz. Hiyo misaada ni ya kishetani na ya kidhalilishaji na hailingani na kiasi cha kodi ambacho kingelipwa. Challenge kwa Magufuli ni kukataa misaada ili terms zibaki "msaada wako chukuwa, kodi yangu nipe yote". Mpaka hilo litokee, wazungu watapiga kelele, wataita majina ya ajabu ajabu, mara dikteta, gaidi, tyrant, nk..

Ni vema yaliyotokea Libya yakatupa lesson sisi kama Waafrika na si propaganda nyepesi kama democrasia na upuuzi mwingine.. Tuko vitani dhidi ya wizi wa mchana, dhidi ya uongo na propaganda kwa manufaa yetu sisi na vizazi vijavyo baada yetu.. Tusijitoe ufaham kumlaani Ghadafi huku tukiwapongeza wazungu la sivyo kumukumbu zetu zitakuwa fupi kama chu/pi. Nawasilisha

Mkuu! mimi nimepangilia hoja zangu vizuri,nimemkosoa gadafi katika maeneo manne,kipi kati ya hivyo nilivyovielezea hakiko sahihi?

*Libya ilikuwa na katiba iliyoruhusu demokrasia?

*Gadafi na familia yake hawakujilimbikizia mali?

*Gadafi hakuwa upande wa Uganda wakati wa vita vya Tanzania na Uganda? kwanini hasingesimama upande wa kutafuta amani badala ya kushabikia vita?

*Je hakuna ushahidi unaoonyesha gadafi alikuwa anamwandaa mwanae Seif Al Islam kuwa kiongozi wa Libya?

*Seif al Arab Gadafi,Mutassim Gadafi,Seif Al Islam Gadafi walikuwa na nyazifa gani katika utawala wa gadafi?

Jifunze kusimamia ukweli!
 
RIP Son of Africa MUAMAR as an icon you will always be in our hearts, and remembered for the good deeds. We are quite certan that, right now your seat is adjacent with Mwalimu, Tata Madiba, Ernesto Che, Kwame, Gamal,Sankara and Patrice. HAMBA KALE!!!!
 
Ni ubaguzi wa kidini tu kati ya dini yake wasiokuwa wadini yake ndo aliokuwa anauneza; na haya ni madhara mabaya kabisa ktk yeyote ya kibinadamu dunia: na kwasababu ya ubaguzi mkubwa udini aliokuwa gadafi, basi yaliyompata yalimsitahili kwasababu hiwezi kuwa mtawala ktk jamii kisha uanze kueneza chuki za kidini la sivyo unatafuta kuwaangamiza wote walio na dini tofautivna yako othwerwise (R.I.P Gaddafi).
 
Back
Top Bottom