HOTUBA ya Msigwa Bungeni; Makamu wa Rais Mazingira; CCM inageuza nchi jangwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

HOTUBA ya Msigwa Bungeni; Makamu wa Rais Mazingira; CCM inageuza nchi jangwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Tumaini Makene, Jul 4, 2012.

 1. Tumaini Makene

  Tumaini Makene Verified User

  #1
  Jul 4, 2012
  Joined: Jan 6, 2012
  Messages: 2,617
  Likes Received: 291
  Trophy Points: 180
  [FONT=&amp]HOTUBA YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI WIZARA YA MALIASILI UTALII NA MAZINGIRA MHESHIMIWA MCH. PETER MSIGWA KUHUSU MPANGO WA OFISI YA MAKAMU WA RAIS MAZINGIRA WA MAPATO NA MATUMIZI KWA MWAKA WA FEDHA 2012/2013[/FONT] [FONT=&amp]1: UTANGULIZI[/FONT] [FONT=&amp]

  Mheshimiwa Spika,[/FONT]
  [FONT=&amp] kwa niaba ya Kambi Rasmi ya Upinzani,nakushukuru kwa kunipa nafasi hii ya kuwasilisha Maoni na Mapendekezo ya Kambi yetu kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maliasili na Utalii kwa mwaka wa fedha 2011/2012, kwa mujibu wa Kanuni za Bunge Kifungu cha 99(3) na (7) toleo la 2007.[/FONT]
  [FONT=&amp]
  Mheshimiwa Spika,[/FONT]
  [FONT=&amp] nachukua fursa hii kumsifu, kumtukuza na kumshukuru Mwenyezi Mungu, mwenye nguvu na hekima tele kwa kunipa afya njema na kuendelea kunipigania siku kwa siku. Nichukue nafasi hii pia kuwashukuru watumishi wa Mungu popote pale walipo ndani na nje ya nchi, kwa maombi yenu yanayonifanya niendelee kuchapa kazi ya kulijenga taifa, naomba msichoke kuniombea mtumishi mwenzenu na Taifa letu kwa ujumla.[/FONT]
  [FONT=&amp]
  Mheshimiwa Spika, [/FONT]
  [FONT=&amp]kwa nafasi ya kipekee kabisa napenda kuishukuru familia yangu, na hasa mke wangu mpenzi Victoria, kwa upendo na sala zao kwangu. Na huko waliko naomba niwakumbushe tena kuwa, thamani ya utu wetu hapa duniani haitatokana na kile tunachokichuma katika jamii, bali itatokana na kile tunachokitoa kwa jamii. Naisihi familia yangu iendelee kuniunga mkono wakati wote ninapokuwa mbali, nikishughulikia kero na matatizo ya wananchi wa Iringa Mjini na taifa kwa ujumla. [/FONT]
  [FONT=&amp]
  [/FONT]
  [FONT=&amp]Mheshimiwa Spika[/FONT][FONT=&amp], kwa moyo wa dhati na kwa unyenyekevu mkubwa, nawashukuru wananchi wangu wa Jimbo la Iringa Mjini kwa kunielewa, kushirikiana nami na kuendelea kuniamini na hatimaye kuendelea kulijenga jimbo letu na taifa kwa ujumla. Niwashukuru sana kwa kunitia moyo,na hasa ninapokuwa nafanya ziara hapo jimboni. Niwaombe Wana Iringa kamwe tusiruhusu akili ndogo kutawala akili kubwa katika jimbo letu. Mungu awabariki, sita wangusha.[/FONT]
  [FONT=&amp]
  Mheshimiwa Spika, [/FONT]
  [FONT=&amp]shukrani na pongezi zangu za dhati pia nazielekeza kwa viongozi wakuu wa CHADEMA, kwa kukiongoza vema chama chetu na kuwa tumaini pekee na la uhakika la Watanzania wengi. [/FONT]
  [FONT=&amp]
  Mheshimiwa Spika[/FONT]
  [FONT=&amp], kabla ya kuanza kueleza yale yote ambayo Kambi ya Upinzani inaona ni muhimu kuyatoa, nitoe dira ya Taifa ya sekta nzima ya mazingira inayosema kuwa “Tanzania yenye mazingira salama, yenye afya na endelevu”[/FONT][FONT=&amp]. [/FONT]Jambo muhimu la kujiuliza ni; je, Serikali inaendana kivitendo na dira hii ya Taifa?
  [FONT=&amp]
  2.0. Mabadiliko ya Tabia Nchi[/FONT]

  [FONT=&amp]
  Mheshimiwa Spika, [/FONT]
  [FONT=&amp]uharibifu na uchafuzi wa mazingira umesababisha mabadiliko ya tabia nchi ambayo kwa jumla huathiri mfumo mzima wa hali ya hewa. Matokeo ya kuathirika kwa mfumo wa hali ya hewa ni kuongezeka kwa joto duniani, viwango vya mvua kutokuwa na mpangilio jambo ambalo husababisha ukame na mafuriko na hivyo kuathiri maisha ya wananchi.[/FONT]
  [FONT=&amp]
  Mheshimiwa Spika[/FONT]
  [FONT=&amp], kutokana na kuongezeka kwa idadi ya watu duniani na kwa maana hiyo kuongezeka kwa shughuli za binadamu na hivyo kusababisha uharibifu wa mazingira kwa kiasi kikubwa. Mabadiliko ya tabia nchi duniani, ambayo kwa ujumla yamesababisha ongezeko la joto, kupungua kwa viwango vya mvua, yameathiri sana ubora wa ardhi , upatikanaji wa maji safi na salama, upatikanaji wa chakula kwa wanyama na binadamu na hivyo kusababisha vifo kwa viumbe hai ulimwenguni. [/FONT]
  [FONT=&amp]
  Mhwashimiwa Spika,[/FONT]
  [FONT=&amp] mabadiliko hayo ya tabianchi yamesababisha kina cha bahari kupanda kwa sentimeta 17 juu ya usawa wa bahari kwa kipindi cha miaka 100 iliyopita, joto la dunia kuongezeka kwa nyuzi joto 0.74 centigrade kwa kipindi cha miaka 50 iliyopita ,pia gesi ya joto aina ya karbon dioxide limeongezeka sana .[/FONT]
  [FONT=&amp]
  Mheshimiwa Spika, [/FONT]
  [FONT=&amp]mwaka 2011 katika kukabiliana na tabianchi Serikali iliandaa mkakati wa taifa wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na miradi miwili iliyotekelezwa ni mradi wa kuhimili mabadiliko ya tabianchi katika sekta za kilimo, maji, afya, wanyamapori, misitu, mifugo , ardhi na mpango wa kupunguza uzalishaji wa ukaa itokanayo na ukataji wa miti na uharibifu wa misitu.[/FONT]
  [FONT=&amp]
  Mheshimiwa Spika[/FONT]
  [FONT=&amp], Kambi ya Upinzani tunataka kupata taarifa za kina kuhusiana na utekelezaji wa miradi hii na hatua ambazo zimeweza kufikiwa mpaka sasa katika kukabiliana na hali hii nchini mwetu.[/FONT]
  [FONT=&amp]
  Mheshimiwa Spika[/FONT]
  [FONT=&amp], ni dhahiri kwamba bila mazingira rafiki, maisha ya binadamu hayana nafasi hapa duniani. Mazingira ndio msingi wa shughuli zote anazofanya binadamu katika kutegemeza maisha yake. Hali kadhalika, mazingira ni nyenzo ya msingi kabisa katika kujenga uchumi wa taifa. Hivyo, ili binadamu aweze kuishi duniani na kujishughulisha na kazi mbalimbali za kutegemeza maisha yake na kujenga uchumi wa Taifa lake, ni lazima mazingira yalindwe ili yaweze kukidhi mahitaji ya binadamu.[/FONT]
  [FONT=&amp]
  2.1 Mkutano wa RIO +20 .[/FONT]

  [FONT=&amp]
  Mheshimiwa Spika, [/FONT]
  [FONT=&amp]ni hivi majuzi tu ulimwengu mzima ulikuwa kwenye mkutano ulioandaliwa na Umoja wa Mataifa uliokuwa ukijadili masuala mbalimbali kuhusiana na mabadiliko ya tabia nchi ambao ulifanyika nchini Brazili na kupewa jina la RIO +20. Mkutano huu ulikuwa na maazimio mbalimbali juu ya mbinu na mkikakati ya kukabiliana na hali hii na serikali yetu iliweza kuwakilishwa na Mheshimiwa Makamu wa rais , Mawaziri wa Mazingira Muungano na kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar .[/FONT]
  [FONT=&amp]
  Mheshimiwa Spika,[/FONT]
  [FONT=&amp] Mkutano wa mwaka huu ulijadili kuhusu maazimio ya mwaka 1992 na namna yalivyotekelezwa na nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa wapatao 182. Sambamba na hilo mkutano huu ulipitisha maamuzi mapya kuhusu kuiweka dunia na mazingira yake katika hali ya usalama ili yaweze kusaidia vizazi vya sasa bila kuathiri haki ya vizazi vijavyo. [/FONT]
  [FONT=&amp]
  Mheshimiwa Spika[/FONT]
  [FONT=&amp], lengo la mkutano huu lilikuwa ni pamoja na [/FONT][FONT=&amp]ufanisi wa nishati na mchango maradufu wa nishati mbadala kwa wote – ifikapo mwaka 2030. Zaidi ya mashirika 50 ya serikali kutoka Afrika, Asia, Amerika Kusini na mataifa ya visiwa vidogo yalikubaliana kutilia mkazo jambo hilo.[/FONT]
  [FONT=&amp]
  Mheshimiwa Spika[/FONT]
  [FONT=&amp], moja ya azimio kuu la mkutano huo lilikuwa ni [/FONT][FONT=&amp]kuanzishwa kwa mfuko utakaowezesha kuharakisha upatikanaji wa nishati, usalama wa chakula, maji na usafiri endelevu kwa nchi mbalimbali hususan zile maskini. Na katika mkutano huo zilitolewa taarifa kuwa kiasi cha Dola bilioni 5 na ahadi ya dola zaidi ya 700 bilioni zilitolewa kwa ajili ya kuufadhili mfuko huu.[/FONT]
  [FONT=&amp]
  Kambi ya upinzani,[/FONT]
  [FONT=&amp] inataka kupata majibu kuhusiana na mambo yafuatayo ili kuondokana na tabia ya nchi yetu ya muda mrefu ya kuhudhuria mikutano na makongamano mbalimbali lakini hakuna utekelezaji wa maazimio husika ;[/FONT]
  [FONT=&amp]
  i. [/FONT]
  [FONT=&amp]Je, tumejiandaa vipi kama taifa ili kuweza kunufaika na fedha za mfuko huu? Tumeweka mpangomkakati gani?[/FONT]
  [FONT=&amp]
  ii. [/FONT]
  [FONT=&amp]Je, tunajiandaa vipi kuweza kulitekeleza kwa vitendo azimio la kupata na kutumia nishati mbadala, upatikanaji na usalama wa chakula, maji na usafiri endelevu nchini mwetu? [/FONT]
  [FONT=&amp]
  iii. [/FONT]
  [FONT=&amp]Je, bajeti yetu ya mwaka huu wa 2012/2013 imezingatia azimio hilo?[/FONT]
  [FONT=&amp]
  3.0 UHARIBIFU NA UCHAFUZI WA MAZINGIRA NCHINI[/FONT]

  [FONT=&amp]
  Mheshimiwa Spika[/FONT]
  [FONT=&amp], kwa kuwa mabadiliko haya ya tabia nchi yanasababishwa na uchafuzi mkubwa wa mazingira unaosababishwa na uzalishaji mkubwa wa gesi ukaa kutoka katika viwanda vikubwa katika nchi zilizoendelea kiviwanda, na uharibifu na uchafuzi mkubwa wa mazingira unaofanywa katika nchi zinazoendelea kwa kukata miti hovyo, uchimbaji wa madini usiojali mazingira, utupaji wa taka hovyo hasa katika miji nk. na kwa kuwa athari za uharibifu na uchafuzi huu wa mazingira unaifanya dunia isewe mahali pazuri pa kuishi, ni dhahiri kwamba kunahitajika jitihada za kitaifa na kimataifa kukabiliana na tatizo hili. [/FONT]
  [FONT=&amp]
  Mheshimiwa Spika[/FONT]
  [FONT=&amp], Pamoja na nchi yetu kutambua umuhimu wa Mazingira na hivyo kuunda Wizara mahsusi ya mazingira chini ya ofisi ya Rais, na kutunga Sera ya Mazingira ya Mwaka 1998 na kuridhia mikataba mbalimbali ya kimataifa kuhusu utunzanji wa Mazingira mfano Agenda 21, bado nchi yetu ina tatizo kubwa la uchafuzi wa mazingira.[/FONT]
  [FONT=&amp]
  Mheshimiwa Spika[/FONT]
  [FONT=&amp], nchi yetu inaelekea kuwa jangwa kutokana na ukataji miti hovyo bila kupanda mingine, miji yetu imezidi kuwa michafu jambo ambalo ni hatarishi kwa afya za wananchi wetu. Kambi ya Upinzani inaitaka Serikali ieleze ni kwa nini tuipatie fedha Wizara hii ya Mazingira wakati mazingira yanaendelea kuharibiwa na kuchafuliwa kila kukicha?[/FONT]
  [FONT=&amp]
  3.1 Kuteketea kwa misitu na miti Nchini[/FONT]

  [FONT=&amp]
  Mheshimiwa Spika[/FONT]
  [FONT=&amp], ukataji miti na uchomaji wa misitu Tanzania umeendelea kwa kiwango kikubwa sana. Maeneo yaliyoathirika kwa kiwango kikubwa ni yaliyoko katika Mikoa ya Dodoma, Singida, Shinyanga, Pwani, Mwanza, Mara na Tabora. Sababu kubwa za uchomaji huu wa misitu ni kwa ajili ya shughuli za kilimo, kutafuta nishati hasa mkaa na kuni kwa matumizi ya kupikia na upasuaji wa mbao.[/FONT]
  [FONT=&amp]
  [/FONT][FONT=&amp]3.2 Usimamizi wa Misitu Nchini[/FONT]
  [FONT=&amp]
  Mheshimiwa Spika, taarifa ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali kuhusu ukaguzi uliofanyika kuhusiana na utendaji wa kifedha na matumizi ya fedha za Usimamizi wa Misitu (PFM) kwa mwaka wa fedha wa 2010/2011 umebaini kuwa kulikuwa na fedha za mradi kiasi cha Sh. 178,826,876 katika Halmashauri kumi na moja (11) ambazo hazikutumika hadi mwisho wa mwaka ulioishia tarehe 30Juni, 2011. Kambi ya Upinzani inaitaka Serikali kueleza kama fedha za usimamizi hazikutumika, ni kwa vipi wilaya tajwa zilifanya kazi ya usimamizi wa misitu wakati fedha hazikutumika?[/FONT]
  [FONT=&amp]
  [/FONT][FONT=&amp]Mheshimiwa Spika[/FONT][FONT=&amp], kukosekana au kutokutolewa kwa fedha za usimamizi ndio sababu kubwa ya kuongezeka kwa ukataji wa misitu na uchomaji mkaa. Aidha, umekuwa ni muda mrefu sana kwa uharibifu wa mazingira katika msitu wa Shengena uliopo Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro ambapo yupo mwekezaji ambaye ameingia kwenye makubaliano na Halmashauri ya Kijiji cha Marieni, Kata ya Chome kuhusu uchimbaji wa udongo wa Bauxite ambao umekuwa ukisafirishwa kwenda nchi ya jirani ya Kenya. Suala hili bado lipo na linaendelea na limesababisha uharibifu mkubwa wa mazingira na kusababisha ukame katika vijiji vya jirani vya Bwambo, Tae, Malindi, Gonjanza na Kata ya Chome kwa ujumla.[/FONT]
  [FONT=&amp]
  Mheshimiwa Spika,[/FONT]
  [FONT=&amp] kuna dalili zote za nchi hii kugeuka kuwa jangwa hasa baada ya Serikali hii ya CCM kupandisha ushuru wa mafuta ya taa ili kukabiliana na tatizo la uchakachuaji wa mafuta ya dizeli. Hii ina maana ya kwamba wananchi watashindwa kumudu bei ya mafuta ya taa kama nishati mbadala na hivyo watageukia miti na misitu kujipatia nishati hiyo. Hii ina maana Serikali ya CCM inavyoendelea kutatawala ndio jinsi ambavyo nchi yetu inaendelea kuwa jangwa. Kambi ya upinzani inapinga utawala wa namna hii na tunatoa wito kwa wananchi pia kukataa kuongozwa na Serikali inayowaelekeza jangwani.[/FONT]
  [FONT=&amp]
  [/FONT][FONT=&amp]3.3 Uchimbaji wa Madini na Hatima ya Mazingira Tanzania.[/FONT]
  [FONT=&amp]
  [/FONT]
  [FONT=&amp]Mheshimiwa Spika,[/FONT][FONT=&amp] ni ukweli uliowazi kuwa kutokana na shughuli za utafutaji na uchimbaji wa madini ya aina mbalimbali hapa nchini mwetu zinachangia kwa kiasi kikubwa katika kuharibu mazingira yetu ,na hili linathibitishwa na ripoti mbalimbali za kiutafiti zilizotolewa kuhusiana na mahusiano yaliyopo baina ya uchimbaji wa madini na uharibifu wa mazingira.[/FONT]
  [FONT=&amp]
  Mheshimiwa Spika,[/FONT]
  [FONT=&amp] kwa kiasi kikubwa sana madhara makubwa zaidi husababishwa na shughuli za uchimbaji unaofanywa na makampuni makubwa na yenye zana za kisasa, ikilinganishwa na kiwango kinachofanywa na wachimbaji wadogo wadogo.[/FONT]
  [FONT=&amp]
  [/FONT][FONT=&amp]Mheshimiwa Spika,[/FONT][FONT=&amp] ripoti mbalimbali zimeonyesha kuwa wananchi pamoja na viumbe mbalimbali waishio karibu na migodi mikubwa ya uchimbaji wa madini nchini mwetu zimeonyesha kuwa wananchi na viumbe wamekuwa wakiathirika sana , mathalani mgodi wa Barrick North Mara,Geita Gold Mine na migodi mingine mikubwa nchini mwetu.[/FONT]
  [FONT=&amp]
  Mheshimiwa Spika[/FONT]
  [FONT=&amp], tathmini ya athari ya mazingira katika migodi mikubwa imekuwa ikifanywa baada ya miradi kuidhinishwa badala ya miradi kufanywa kabla. Hivyo thamini hizi hazisaidii kudhibiti athari za mazingira kwa kuwa tathmini haziathiri usanifu miradi. Miradi kama Geita Mine na North Mara imegeuka kuwa majanga ya kimazingira kwa sababu hii.[/FONT]
  [FONT=&amp]
  [/FONT][FONT=&amp]Mheshimiwa Spika, [/FONT][FONT=&amp]Kambi ya Upinzani inasikitishwa na uchafuzi mkubwa wa mazingira uliofanyika katika Migodi ya Dhahabu ya Geita na North-Mara ambao umeleta athari kubwa sana za kiafya kwa wananchi wa maeneo hayo.[/FONT]
  [FONT=&amp]
  Mheshimiwa Spika[/FONT]
  [FONT=&amp], kwa mujibu wa utafiti wa Manfred Felician Bitala (2008) na tafiti zilizofanywa chini ya ufadhili wa Norwegian University of Life Scieces na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(2009) na Utafiti uliofanywa na Idara ya Biolojia, Chuo Kikuu cha Oslo(2011) kuhusu Uchafuzi wa Mazingira Geita na North-Mara ni kwamba kuna kiasi kikubwa sana cha kemikali-sumu (kwa mfano “cyanide”) madini ya zebaki (Mercury) na madini chuma yenye sumu (heavy metals) katika maji na udongo katika maeneo ya makazi ya wananchi wa maeneo yaliyozungukwa na migodi hiyo.
  [/FONT]
  [FONT=&amp]Mheshimiwa Spika,[/FONT][FONT=&amp] kwa mujibu wa matokeo ya tafiti hizi ni kwamba wananchi wa maeneo hayo wameathirika vibaya na kemikali hizi zenye sumu kwa viwango vya juu sana kuliko athari za wastani za waathirika katika nchi nyingine zenye tatizo kama hilo. Aidha hata mifugo ya wananchi hawa imeathirika kwa kiasi kikubwa sana.[/FONT]
  [FONT=&amp]
  [/FONT]
  [FONT=&amp]Mheshimiwa Spika,[/FONT][FONT=&amp] Kambi ya Upinzani inaitaka Serikali iingilie kati na kunusuru maisha ya wananchi wa maeneo hayo ya migodi. Aidha Kambi ya Upinzani inataka kujua kama Serikali ina taarifa ya tafiti hizi na imechukua hatua gani hadi sasa kudhibiti uchimbaji wa madini ambao si rafiki kwa mazingira. Kadhalika, Kambi ya Upinzani inataka kuelewa fidia kwa watu wote walioathirika na uchafuzi huo wa vyanzo vya maji wanayotumia utafanyika lini?[/FONT]
  [FONT=&amp]
  Mheshimiwa Spika,[/FONT]
  [FONT=&amp] ni kutokana na hali hii ndio maana tunakubaliana na tamko la kamati ya viongozi wa dini na asasi za kiraia lijulikanalo kama tamko la Ngurdoto la tarehe 20 Octoba 2011 na tunaitaka serikali kuwa tayari kufanya haya yafuatayo;[/FONT]

  [FONT=&amp]i. [/FONT][FONT=&amp]Ni muhimu utafiti na taarifa za madhara kwa mazingira na jamii kutokana na shughuli za uchimbaji wa madini ziwe zinaandaliwa na taasisi au wataalamu wanaoaminika na kuheshimika ambao wako huru kufanya kazi zao bila kuingiliwa na serikali na wawekezaji binafsi. Utafiti huo ufanywe mara kwa mara wakati shughuli za uchimbaji zinaendelea na baada ya shughuli hizo kusitishwa. [/FONT]
  [FONT=&amp]
  ii. [/FONT]
  [FONT=&amp]Ni dhahiri kuwa uharibifu wa mazingira kutokana na uchimbaji wa madini utaathiri pia vizazi vijavyo, na unaweza kuzisababishia jamii hizo kuishi maisha ya dhiki na mashaka. Kutokana na hilo, ni lazima kufanya utafiti kuhusu madhara yote ambayo yanaweza kutokea siku zijazo kutokana na shughuli za uchimbaji wa madini na kuhakikisha kunakuwa na njia za kuwafidia ipasavyo watu wote watakaoathirika;[/FONT]
  [FONT=&amp]
  iii. [/FONT]
  [FONT=&amp]Jamii zinazoishi karibu na migodi ya madini, pamoja na wale ambao wameondolewa kwenye maeneo yao ya asili kupisha uchimbaji madini, mara nyingi wamekuwa wakisahaulika na kuna haja ya kuhakikisha kuwa nao wanafaidika na shughuli hizi kwa kuwezeshwa katika kujenga maisha yao na haswa kutokana na uharibifu wa mazingira uliofanywa. [/FONT]
  [FONT=&amp]
  iv. [/FONT]
  [FONT=&amp]Uharibifu wa mazingira kutokana na shughuli za uchimbaji madini unaathiri sana jamii katika maeneo ya uchimbaji na nchi nzima kwa jumla, lakini jukumu la kurekebisha mazingira haya linaachwa kwa serikali na si kwa wachimbaji. Kampuni za uchimbaji madini zinapaswa kuwa na jukumu la kurekebisha na kutengeneza mazingira bora baada ya kukamilika kwa shughuli zao. [/FONT]
  [FONT=&amp]
  v. [/FONT]
  [FONT=&amp]Serikali itoe ufafanuzi wa kina na wa kueleweka katika suala la fidia, kwa kuainisha kiwango mahsusi cha fidia kwa watu na jamii ambazo zimeathirika na sumu zinazotokana na shughuli za uchimbaji wa madini na uharibifu wa mazingira yao;[/FONT]
  [FONT=&amp]
  vi. [/FONT]
  [FONT=&amp]Serikali ihakikishe kuwa ni lazima jamii zinapewa taarifa muhimu na kuwezeshwa kushiriki kwenye shughuli za uchimbaji wa madini na kuwa suala hilo liwekwe kwenye sheria na si hiari kutokana na matakwa ya makampuni au serikali.[/FONT]

  [FONT=&amp]3.4 Madini ya Urani (uranium).[/FONT]

  [FONT=&amp]Mheshimiwa Spika,[/FONT][FONT=&amp] taarifa za kugunduliwa kwa madini ya urani katika nchi yetu ni habari njema kwa kuwa madini haya yatakuwa na mchango mkubwa katika uchumi wetu. Kwa kuwa madini haya yanahitaji uangalifu mkubwa, kwa sababu ya kuwa na asili ya sumu, Serikali imejiandaa vipi kisera, kisheria na kiutaratibu kuhakikisha kuwa uchimbaji wa madini hayo hauathiri mazingira na afya za wananchi na wanyama katika maeneo hayo?[/FONT]
  [FONT=&amp]
  Kambi ya Upinzani
  inaitaka Serikali kujiandaa vema katika suala hili la madini ya urani na gesi mapema kabla ya kuingia mikataba na wachimbaji ili kuepuka migogoro isiyo ya lazima hasa pale wananchi na mazingira kwa ujumla watakapoathirika na uchimbaji huo. [/FONT] [FONT=&amp]

  4.0 UTEKELEZAJI WA MPANGO WA MAENDELEO NA MAZINGIRA[/FONT]


  [FONT=&amp]Mheshimiwa Spika[/FONT][FONT=&amp], Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano, pamoja na mikakati mingine, una mkakati mahsusi wa kuboresha muindombinu ya usafi katika maeneo ya mijini na vijijini. Kwa mujibu wa Mpango wa Maendeleo mwaka huu wa fedha zilipaswa kutengwa kiasi cha shilingi billioni 7.620 kwa ajili ya kampeni ya Taifa ya Mazingira safi na kusafisha shule. La kushangaza ni kuwa ukisoma taarifa ya waziri kuhusiana na idara ya mazingira malengo ya mwaka 2012/13 (uk.41) hakuna kipengele hata kimoja ambacho kimelenga kutekeleza malengo haya ya mpango wa maendeleo wa miaka mitano kwa kuwa hakuna fedha iliyoombwa kutekeleza Mpango wa Maendeleo. [/FONT]

  [FONT=&amp]Mheshimiwa Spika[/FONT][FONT=&amp], huu ni ushahidi wa wazi kuwa Serikali haina nia ya dhati ya kutekeleza Mpango wa Maendeleo. Kama Serikali inajiwekea Mpango wake wa Maendeleo, halafu Serikali hiyohiyo inashindwa kutekeleza Mpango wake yenyewe, Kambi ya Upinzani na wananchi wenye kupenda maendeleo tunapata wasiwasi na uwezo wa Serikali hii ya CCM kuendelea kuongoza nchi yetu kwani hata mipango inayojiwekea yenyewe inashindikana kutekelezeka.[/FONT]

  [FONT=&amp]Mheshimiwa Spika[/FONT][FONT=&amp], fedha kwa ajili ya matumizi ya maendeleo zilizotengwa kwa mwaka huu wa fedha ni shilingi bilioni 7.07 na kati ya hizo fedha za ndani ni kiasi cha shilingi bilioni 1.3 tu (randama uk .46) na nyingine tunategemea kuzipata kutoka nje, na miradi ambayo inaenda kutekelezwa ni miradi namba 5306, 6569, 6571, 5301, 5302, 5305 na 6504. Kati ya miradi yote hii hakuna hata mmoja unaohusiana na kuboresha miundombinu ya usafi mijini na vijijini.[/FONT]
  [FONT=&amp]
  Mheshimiwa Spika, [/FONT]
  [FONT=&amp]Kambi ya Upinzani inaiasa Serikali kutofanya mzaha na Mpango wa Maendeleo ambao una maslahi kwa wananchi. Kitendo cha kutotenga fedha kuboresha miundombinu ya usafi mijini na vijijini kama Mpango ulivyoelekeza na kutozingatia vipaumbele vya Mpango wa Taifa wa Maendeleo ni dharau na dhihaka kwa wananchi. Kwani suala la mazingira ni suala la afya. Mtu anayekaa katika mazingira machafu anawezaje kuwa na afya bora na kufanya kazi ili alipe kodi kwa Serikali? Serikali sasa iwekeze katika usafi wa Mazingira ili ikusanye kodi katika mazingira safi vilevile. Serikali isilenge tu kukusanya isiko wekeza.[/FONT]

  [FONT=&amp]5.0 UTEKELEZAJI WA MAAGIZO YA BUNGE[/FONT]
  [FONT=&amp]Mheshimiwa Spika,[/FONT][FONT=&amp] katika bunge la bajeti lililopita kamati ya bunge ya maliasili na mazingira ilitoa maagizo mbalimbali na kati ya maagizo hayo yapo ambayo hayajatekelezwa na serikali mpaka wakati huu. Mojawapo ya maagizo hayo ni Agizo namba 4 – ambalo linasema “serikali itenge fedha za kutosha ofisi ya makamu wa rais mazingira katika bajeti ya 2012/13 ili kuwezesha kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na utunzaji wa mazingira”. Ila uhalisia ni kuwa fedha zilizotengwa ni kidogo sana na hii inaonyesha kuwa pamoja na serikali kutokuthamini mazingira pia haitekelezi maagizo na maazimio mbalimbali ya bunge. (Randama ya Ofisi ya Makamu wa Rais uk.26)[/FONT]
  [FONT=&amp]
  Mheshimiwa Spika[/FONT]
  [FONT=&amp], agizo lingine ni Agizo namba 5ambalo lilisema “serikali ihakikishe kwamba fidia zote stahiki kwa wananchi wanaozunguka mgodi wa dhahabu wa North Mara zinalipwa na ahadi zilizotolewa na mwekezaji wa mgodi kwa jamii ya eneo husika zinatekelezwa”. Taarifa ya serikali ya Januari - Mei 2012 inasema kuwa jumla ya wananchi 474 wamelipwa jumla ya shilingi 22,387,234,156/= ikiwa ni fidia zao kwa maeneo yaliyopo ndani ya mita 200 kutoka kwenye mgodi. Hii ni kwa mujibu wa taarifa ya serikali kuhusu utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2011/2012 (Randama uk 26).[/FONT]
  [FONT=&amp]
  Mheshimiwa Spika,[/FONT]
  [FONT=&amp] taarifa hizi za serikali sio sahihi kwani kwa wastani ni kuwa kila mwananchi amelipwa kiasi cha shilingi 47,230,451. Kambi ya Upinzani inaitaka serikali kueleza kwa kina ni lini fedha hizi zililipwa na zililipwa kwa kutumia utaratibu gani? Ni vigezo gani vilitumika katika kuwateua wananchi waliopaswa kulipwa fidia hii ? [/FONT]
  [FONT=&amp]
  Mheshimiwa Spika,[/FONT]
  [FONT=&amp] katika bunge la mwezi februari 2012 siku ya tarehe 03/02/2012 wakati Naibu waziri wa Nishati na madini Adam Malima akijibu swali namba 48 la Mheshimiwa Ester Matiko kuhusiana na fidia kwa wananchi hawa alisema, naomba kunukuu hansard [/FONT][FONT=&amp]“[/FONT][FONT=&amp]Mheshimiwa Naibu Spika,…... Pamoja na kufanyika tathmini kwa kaya zinazozunguka mgodi, kumejitokeza matatizo mbalimbali; mfano, kaya tano hazijaridhia kufanyika kwa tathmini hiyo ya fidia. Majadiliano yanaendelea kwa kushirikisha Kijiji cha Nyangoto. Familia 40 ziliamua kurudi katika maeneo waliyokwishalipwa na kwa sasa wanadai fidia upya.

  ……..Mheshimiwa Naibu Spika, zoezi la kulipa fidia kwa Wananchi wanaotakiwa kupisha shughuli za Mgodi wa North Mara linasimamiwa na Serikali katika ngazi ya Halmashauri ya Wilaya ya Tarime”. [/FONT]

  [FONT=&amp]
  Kambi ya Upinzani,[/FONT]
  [FONT=&amp] tunataka maelezo ya kina juu ya taarifa hizi, na kukinzana kwa taarifa za Serikali na zile za wananchi kuhusiana na ulipaji wa fidia kwa wananchi. Tuchukue jibu lipi ? Lililopo kwenye hansard, la wananchi au la waziri mwenye dhamana ya mazingira?[/FONT]
  [FONT=&amp]
  Fidia hizi zililipwa kwa ajili ya fidia ya uchafuzi wa mazingira uliofanywa na mgodi wa North Mara kwa wananchi hawa au ni fidia ya aina gani hii?[/FONT]
  [FONT=&amp]
  Mheshimiwa Spika,[/FONT]
  [FONT=&amp] taarifa hiyohiyo ya serikali inasema kuwa visima vya maji 16 vimechimbwa katika vijiji vya Kewanja, Nyamwaga, Nyakunguru, Genkuru, Kerende, Matongo na Nyangoto na kuwa kati ya visima hivyo ni visima 14 ndio vinatoa maji.[/FONT]
  [FONT=&amp]
  Mheshimiwa Spika[/FONT]
  [FONT=&amp], taarifa ni kuwa mwekezaji kwenye mgodi wa North Mara ameweka utaratibu wa kusambaza maji kwa wananchi kwa kutumia magari. Kambi ya Upinzani inajiuliza kama visima vimechimbwa na kuwa vinatoa maji ni kwa nini magari yatumike kusambaza maji tena kwa ratiba maalum?[/FONT]
  [FONT=&amp]
  5.1 Mbinu za kuhifadhi mazingira yetu.[/FONT]


  [FONT=&amp]Mheshimiwa Spika[/FONT][FONT=&amp], kuhusu kutunza na kulinda mazingira yetu, Kambi ya Upinzani inaona kuwa Serikali haijaweka suala la kutunza na kulinda mazingira katika vipaumbele vyake, jambo ambalo ni hatari kwa mifumo ya ikologia na maisha ya binadamu na viumbe hai vingine kwa ujumla. Hili ni janga kubwa na Serikali inapaswa kuzinduka sasa na kuchukua hatua za kukabiliana na janga hili. Kama kawaida Kambi ya Upinzani tunawapa Serikali bila choyo mbinu za kufanya kukabiliana na tatizo kama ifuatavyo:

  [/FONT] [FONT=&amp] i. [/FONT][FONT=&amp]Serikali ihimize na ijenge mazingira wezeshi ya kutumia nishati mbadala na hasa kwa kutumia vyanzo vya upepo, jua na umeme vijijini na hii itasaidia kuokoa miti mingi ambayo hutumika kwa ajili ya nishati na Serikali igharimie uwepo na upatikanaji wa nishati hizo. Hii inatokana na ukweli kuwa ni asilimia 14 tu ya Watanzania ndio wameunganishwa kwenye umeme wa gridi ya Taifa;[/FONT]

  [FONT=&amp] ii. [/FONT][FONT=&amp]Gharama za vifaa vya ujenzi ipunguzwe, na hii ni kwa vifaa kama sementi ili wananchi waweze kujenga nyumba kwa kutumia tofali badala ya kutumia miti na hii itaokoa asilimia kubwa ya miti ambayo hutumika kwa ajili ya ujenzi;[/FONT]
  [FONT=&amp]
  iii. [/FONT][FONT=&amp]Itolewe elimu ya kina katika kupanda miti na kutunza miti pamoja na misitu iliyopo kwani hali hii isipochukuliwa hatua madhubuti sehemu kubwa ya taifa itageuka jangwa. Ukame uliokithiri maeneo mbalimbali ya nchi ni kiashiria cha unyemelezi wa jangwa.[/FONT]

  [FONT=&amp] iv. [/FONT][FONT=&amp]Mitaala ya Shule za Msingi na Sekondari ibadilishwe na iweke msisitizo katika umuhimu wa kupanda miti na kutunza miti. Hili litasaidia katika kizazi kinachokuja kujua umuhimu huu wa miti katika maisha yao na maisha ya vizazi vijavyo;[/FONT]

  [FONT=&amp] v. [/FONT][FONT=&amp]Watendaji wa Vijiji, Mitaa na Kata kote nchini, moja ya majukumu yao liwe ni kuhakikisha kuwa kila mwananchi anapanda miti na hiki kiwe ni kipimo kimojawapo katika kupima utendaji kazi wa viongozi hawa; na[/FONT]

  [FONT=&amp] vi. [/FONT][FONT=&amp]KilaHalmashauri nchini itenge fedha kwa ajili ya kununua miche ya miti na kuigawa bure kwa wananchi kila kipindi cha masika kwenye maeneo husika na Watendaji wa Vijiji, Mitaa na Kata wagawe miche hiyo kwa kila kaya na kila mwananchi apande miche hiyo.[/FONT]
  [FONT=&amp]
  vii. [/FONT][FONT=&amp]Usafi mijini uwe ndio kipimo cha utendaji wa Mameya wa miji na majiji.[/FONT]
  [FONT=&amp]
  Mheshimiwa Spika,[/FONT]
  [FONT=&amp] mwisho kabisa na kwa umuhimu napenda kuchukua nafasi hii kumshukuru Mwenyekiti wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira Mhe. James Lembeli (Mb) pamoja na wajumbe wa kamati hii kwa ushirikiano katika kutetea maslahi ya taifa.[/FONT]
  [FONT=&amp]
  Mheshimiwa Spika[/FONT]
  [FONT=&amp], baada ya kusema hayo kwa niaba ya Kambi ya Upinzani, nawashukuru waheshimiwa wote kwa kunisikiliza,[/FONT]
  [FONT=&amp]
  Mheshimiwa Spika[/FONT]
  [FONT=&amp], naomba kuwasilisha.[/FONT]

  [FONT=&amp]……………………………………[/FONT]


  [FONT=&amp]Mch. Peter Msigwa (Mb)[/FONT]


  [FONT=&amp]Msemaji Mkuu Kambi ya Upinzani- Wizara ya Maliasili, Utalii na Mazingira[/FONT]


  [FONT=&amp]04.07.2012[/FONT]

   
 2. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #2
  Jul 4, 2012
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0
  ahsante waziri kivuli,umefanya kazi kubwa kuliko waziri mwenyewe BIG UP
   
 3. 1

  19don JF-Expert Member

  #3
  Jul 4, 2012
  Joined: May 13, 2011
  Messages: 572
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  big up kamanda wamesikia ulichoongea , subili tuone mipasho jioni watakapo anza kuchangia
   
 4. luhala

  luhala JF-Expert Member

  #4
  Jul 4, 2012
  Joined: Feb 25, 2012
  Messages: 412
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Sasa namkubali Mch. Msigwa kuwa kichwa kuliko hawa wachumia tumbo waungaji mkono hoja zote toka CCM kwa asilimia "mia kwa mia" huku wakilalamikia mapungufu kibao hadi povu kuwatoka midomoni. Hongereni wana Iringa mjini.
   
 5. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #5
  Jul 4, 2012
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  khaaa kumbe huyu baba ana akili hivi?.... mweeee...akili ndogo kutawala akili kubwa ....hahaaa
   
 6. Christine1

  Christine1 JF-Expert Member

  #6
  Jul 4, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 12,278
  Likes Received: 1,206
  Trophy Points: 280
  ckupoteza kura yangu
   
Loading...