Hotuba ya Msemaji wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni Wizara ya Nishati na Madini

Aisee hotuba imetulia na imekwenda shule ngoja tuwasikie magamba wakianza kutoa mapovu
 
Hotuba hii imefanyia kazi, imesheheni tafiti stahili na imekaa kistaarabu bila kumumunya maneno. Kama kweli Bunge ni Msimamizi wa serikali, basi hotuba hii ni dira ya Bunge, ijipime ijipambanue kutoka lilipo liende mbele likemea serikali bila kujali itikadi na uchama!
 
Nimeipenda hii

Mheshimiwa Spika, katika hali inayozua maswali kuhusu umakini wa Bunge katika kusimamia maazimio yake mwaka 2011, Mbunge wa Monduli Mheshimiwa Edward Lowassa; aliyekuwa Waziri Mkuu na kujiuzulu kufuatia kashfa hiyo ya Richmond alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama iliyopewa dhamana na Bunge kufuatilia utekelezaji wa maazimio kuhusu mkataba kati ya TANESCO na Richmond. Katika hali hiyo, haishangazi kwamba kwa miaka miwili toka wakati huo, mpaka mabadiliko ya Kamati za Bunge yalipofanyika; Kamati hiyo katika Taarifa zake zote bungeni haijawahi kuisimamia Serikali kuhakikisha maazimio husika ya Bunge yanatekelezwa. Huu ndio uwajibikaji, ndani ya Serikali na uongozi wa Bunge; vyote vikiongozwa na CCM.
 
Nimegundua kumbe dawa ya Makinda na maccm ni kutumia nukuu za mwalimu Nyerere,maana
maneno hayohayo aliyonukuu JJ.Mnyika angeyasema yeye angeambiwa akayaondoe kwa sababu
yanaleta maudhi kwa wengine,lakini kwa sababu amenukuu toka kwa bosi wao wamenywea kimya'
 
Ehee,Chezea Jamiiforums wewe, kila kitu hadharani, hivi taarifa ya habari ya saa 2 usiku hapa ya nini tena, hotuba ndio hii hapa, vurugu za Mtwara tayari tunazo full e.t.c. Nikifika home tu, naenda kujiangalilizia CD tu za Marehem Kanumba, cause kila kitu nimeisha kipata hapa.

hahahahahaaaaa mkuu umenichekesha sana
 
Nimegundua kumbe dawa ya Makinda na maccm ni kutumia nukuu za mwalimu Nyerere,maana
maneno hayohayo aliyonukuu JJ.Mnyika angeyasema yeye angeambiwa akayaondoe kwa sababu
yanaleta maudhi kwa wengine,lakini kwa sababu amenukuu toka kwa bosi wao wamenywea kimya'
Hivi walivyo vilaza hata ukinukuu vya uongo watajua maana nina wasiwasi kama huwa wanajisomea somea..
 
Back
Top Bottom