Hotuba ya msemaji mkuu wa kambi ya upinzani bungeni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hotuba ya msemaji mkuu wa kambi ya upinzani bungeni

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kakke, Jun 15, 2012.

 1. Kakke

  Kakke JF-Expert Member

  #1
  Jun 15, 2012
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 1,797
  Likes Received: 389
  Trophy Points: 180
  [h=1][/h]
  HOTUBA YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI BUNGENI, MHE. RIZIKI OMAR JUMA (MB), KUHUSU MAKADIRIO NA MATUMIZI YA OFISI YA MAKAMU WA RAIS MAMBO YA MUUNGANO KWA MWAKA WA FEDHA 2009/2010
  ….
  ….
  Mheshimiwa Spika,
  Wakati tunaheshimu sana na tunaamini njia ya mazungumzo kama suluhisho la pekee kufikia utatuzi wa matatizo yanayolikabili taifa, hatuamini kuwa mazungumzo kwa maana ya mazungumzo tu yanaweza kutufikisha popote. Mazungumzo yenye uwezo huo wa kutoa suluhisho ni yale yanayozingatia nini kinazungumzwa, nani wanazungumza, vipi na kwa nini yanazungumzwa. Kila moja kati ya maswali haya lina maana kubwa kwa hitimisho na suluhisho litokanalo na mazungumzo yenyewe. Tunachelea kusema kwamba, haya yanayofanyika baina ya Ofisi za Waziri Mkuu na Waziri Kiongozi ni mazungumzo kwa manufaa ya mazungumzo na sio mazungumzo kwa manufaa ya suluhisho. Na kwayo, fedha za walipa kodi wa nchi hii zinateketea lakini tatizo la Muungano halitatuliwi, zaidi ya kulizidisha.
  Mheshimiwa Spika,
  Turuhusu tupige mfano mmoja wa karibuni, kati ya mingi iliyokwishatokezea, kuthibitisha khofu yetu kwamba mazungumzo haya hayatatui tatizo halisi la Muungano. Mfano huu unakhusu Ripoti ya Baraza la Mapinduzi la Zanzibar ya 2003.
  Mheshimiwa Spika,
  Tarehe 29 Mei 2003, Ikulu ya Zanzibar ilichapisha Ripoti ya Baraza la Mapinduzi juu ya Matatizo na Kero za Muungano na Taratibu za Kuziondoa, ambapo katika sura yake ya tatu, ripoti hiyo ilitoa orodha ya mambo yanayopaswa kuondolewa katika Muungano. Mambo hayo ni:
  Mafuta na Gesi Asilia
  Elimu ya Juu
  Posta
  Simu (Mawasiliano)
  Biashara ya Nje
  Kodi ya Mapato
  Ushuru wa Bidhaa
  Usafiri wa Anga
  Takwimu
  Utafiti
  Ushirikiano wa Kimataifa
  Leseni za Viwanda
  Polisi
  Usalama
  Mheshimiwa Spika,
  Katika kuhakikisha kuwa haya yanatekelezeka, SMZ ilitaka kuwepo kwa misingi mitano ya kuzingatiwa, ambayo ni:
  Masuala ya Muungano yalindwe kwa misingi ya Katiba na Sheria badala ya siasa na maelewano
  Muungano uwe na maeneo machache yanayoweza kusimamiwa na kutekelezwa kwa urahisi
  Muungano uanishe washirika wake wakuu, mipaka na haki zao
  Muungano utowe fursa sawa za kiuchumi kwa pande zote mbili za Muungano
  Lazima pawe na Muungano unaoweza kuhimili mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi
  Mheshimiwa Spika,
  Hivi ndivyo SMZ ilivyosema tangu mwaka 2003; na kwa hakika – angalau katika hili – serikali hii imesema vile ambavyo Wazanzibari wamekuwa wakisema tangu siku za mwanzo za Muungano huu. Ni wazi kuwa ripoti hii ya SMZ iko mezani kwa Ofisi zote mbili, ya Waziri Mkuu na Waziri Kiongozi. Lakini kinachotokezea kila baada ya kikao cha watendaji wakuu wa serikali mbili, ni taarifa ya kuhuzunisha panapohusika kile hasa kinachohitajika kutatuliwa.
  .
  .
  Mheshimiwa Spika,
  Kambi yetu inaitupia lawama za moja kwa moja serikali ya Muungano kwamba imejiundia siasa zake maalum kuelekea suala la Muungano huu. Siasa hizo zinasomeka katika nukta mbili: moja ni kupuuzia maoni yoyote yanayotolewa na watu kuhusiana na Muungano wenyewe na ya pili ni kuudharau uhalisia wa Muungano wenyewe.
  3.1 Kupuuzia Maoni Yanayohusu Muungano
  Mheshimiwa Spika,
  Nilitagulia kusema kwamba, panapohusika suala la Muungano, Watanzania tuna bahati mbaya ya kuwa na serikali yenye utamaduni wa kujifungia kwenye viambaza vyake vinne, ikajisemesha yenyewe, ikijisikiliza yenyewe na kisha ikatoka na mwangwi wa sauti yake yenyewe kwenda kuufanyia kazi. Bila ya shaka, haya hayakuanza leo, bali ni muakisiko na muendelezo wa utamaduni huo mkongwe; kwamba kila kinachosemwa na Watanzania wengine wowote ambao hawamo kwenye “Super Structure” ya Muungano, ni kelele za mlango ambazo hazimzuii mwenye nyumba kulala. Kitabu cha bajeti iliyopo mbele yetu sasa ni shahidi wa hayo.
  …
  …
  Riziki O. Juma (Mb)
  Msemaji wa Kambi ya Upinzani Bungeni (Muungano)
   
 2. t

  tpmazembe JF-Expert Member

  #2
  Jun 15, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 2,474
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  sasa kama huu muungano mpaka polisi na usalama (jeshi ),ushirikiano wa kimataifa na biashara za nnje mtavitoa kwenye muungano huo muungano utakaobaki utakuwa ni muungano au jina tu?bora tu tuwe wawazi mngesema tu moja kwa moja tu vunje muungano
   
 3. Borakufa

  Borakufa JF-Expert Member

  #3
  Jun 15, 2012
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 1,503
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Tuacheni wazenj jamani **** mwatung'ang'ania?
   
Loading...