Hotuba ya Mkapa ambayo niliikubali, lakini sasa!? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hotuba ya Mkapa ambayo niliikubali, lakini sasa!?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, May 15, 2009.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  May 15, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,361
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Rais Mkapa aliwahutubia wananchi katika mwaka mpya 2005, Januari 31. Hotuba ile ningeipa jina la "Uaminifu na maadili ya Taifa" ilinivutia wakati ule na niliipenda. Ukweli wake bado ni kweli hata leo hii. Kama ingetolewa na mtu mwingine basi bila ya shaka ingekuwa ni mojawapo ya hotuba zenye kugusa fikra na hisia za watu kwa mantiki yake, hoja zake na mahitimisho yake... Jisomee mwenyewe:(msisitizo ni wangu)

  HOTUBA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO
  WA TANZANIA, MHESHIMIWA BENJAMIN WILLIAM
  MKAPA, KWA WANANCHI, 31 JANUARI 2005

  Ndugu Wananchi,
  Katika salamu zangu za mwaka huu mpya kwenu, pamoja na mambo mengine, nilijenga hoja kuwa wakati umefika Watanzania tuweke mkazo mpya, na umuhimu unaostahili, kwenye maadili ya kitaifa. Maadili ya kitaifa, yanayotutambulisha kama Watanzania, yanayotupa sifa ya U-Tanzania, ni ya aina nyingi. Mwezi uliopita nilizungumzia zaidi maadili ya kisiasa na kiutawala, nikawalaumu zaidi viongozi wa kisiasa na kiutawala kwa dalili za mmomonyoko wa maadili yetu ya asili. Nilikuombeni, Ndugu Wananchi, mniunge mkono kuwakatalia viongozi wa kisiasa, kidini na kiutawala ambao, kwa kauli zao au vitendo vyao, wanachangia kumomonyoa sifa za U-Tanzania, ikiwemo maadili ya uhuru, umoja, amani, utulivu, upendo, kuvumiliana na mshikamano. Nilikuombeni tusaidiane kuwaambia HAPANA viongozi wanaotuletea mambo ya udini, ukabila, umajimbo, ubaguzi, visasi, chuki na fujo, maana mambo hayo kwa hakika ni kinyume kabisa cha U-Tanzania wetu.

  Leo nitaelekeza maneno yangu kwa wale wananchi wenzetu wachache ambao, kwa tabia na mienendo yao, nao wanahatarisha sifa za kijamii za Watanzania, ambazo nazo ni sehemu muhimu ya U-Tanzania wetu sote. Na leo nitazungumzia sifa moja tu ya maadili ya UAMINIFU. Maana, huko tulikotoka, Watanzania kwa ujumla tulisifika kwa uaminifu, hasa tukilinganishwa na mataifa mengine barani Afrika. Ingetazamiwa wengine wajifunze uaminifu kutoka kwetu. Lakini naona wapo baadhi ya Watanzania ambao sasa wanataka kutufikisha mahali ambapo na sisi tutaonekana hatuna tofauti na hao wengine.

  Ukweli ni kuwa sifa ya U-Tanzania si sifa itokanayo na maadili ya kisiasa na kiutawala peke yake; ni sifa itokanayo pia na tabia za raia, na maadili mengine ya kijamii, ikiwemo uaminifu. Kamusi ya Kiswahili Sanifu inaeleza kuwa Uaminifu ni “tabia ya mtu kuweza kuaminika, kama vile mtu kupewa amana za watu aziweke mpaka watakapokuja kuzitaka.”

  Ndugu Wananchi,
  Katika miaka ya 1970 na 1980, nchi yetu iliwekeza sana mikopo, misaada, rasilimali, amana na akiba za taifa letu katika mashirika ya umma. Zipo sababu nyingi zilizofanya mashirika hayo yadhoofu kiutendaji, na hatimaye mengi kufa kabisa. Lakini mojawapo ya sababu hizo ni kukosa uaminifu kwa baadhi ya wenzetu tuliowakabidhi kazi ya kusimamia na kuendesha mashirika hayo, yaani wenzetu tuliowakabidhi amana za taifa letu. Kweli, wengine walikuwa na elimu au ujuzi usiotosha, na pengine mazingira ya kibiashara na kiutawala wakati huo hayakuwa mazuri sana. Lakini, kwa baadhi yao, ukosefu wa uaminifu nao ulikuwa mojawapo ya sababu ya kudhoofika na hatimaye kufa kwa mashirika ya umma.

  Hayo yalikuwa mashirika ya umma, na yalipokufa waliopata hasara kwa kweli ni ninyi wananchi. Leo uchumi wetu, siku hadi siku, unazidi kuwa wa soko, na hivyo unakuwa uchumi wa ushindani. Ni uchumi utokanao na uwekezaji wa sekta binafsi, wa amana za watu binafsi. Serikali haiwekezi tena kwenye viwanda, huduma za kibiashara, makampuni, mabenki na asasi za fedha. Wanaow
   
 2. Komamanga

  Komamanga JF-Expert Member

  #2
  May 15, 2009
  Joined: May 2, 2009
  Messages: 221
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  heheee..MKJJ najua unapoelekea ila hii hotuba imelenga kabisa hali ya sasa na nafikiri jamaa alijua nini kitaendelea ndio maana akaamua kuchukua desa kwa Mwalim JK Nyerere.
   
 3. j

  jibabaz Member

  #3
  May 15, 2009
  Joined: Jun 23, 2008
  Messages: 55
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nikuulize MKJJ..how much ofthe speech imepigwa desa? Kama ni more that 10% basi ni straight "paljarism" na pia kama hakuweka reference (sijui kama speech zina reference) basi nayo ni wizi/matumizi ya kazi ya mtu mwingine bila kumpa reference.
  But then ndio maana inakuja kwamba pia ni muhimu kama hotuba za viongozi wetu hapo tanznaia zikiweka open kwa watuna inakua rahisi kukamata vitu kama hivi. Na actually ukichunguza sana sitashangaa kukuta hotuba za kina Obama enzi za kuanza kutafuta u seneta wakiwa wamezidesa..lol
   
 4. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #4
  May 15, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Well, who knows naye Nyerere alitoa wapi hilo wazo/ au hayo mawazo maana inasemekana naye alikuwa akinukuu na ku paraphrase beti za nyimbo za bendi za Uingereza wakati wa vita vikuu vya pili vya dunia bila kutoa attribution...
   
 5. M

  Mkandara Verified User

  #5
  May 15, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mzee Mwanakijiji,
  Mkuu wangu inasikitisha tu kwamba umefikiria hotuba hii kwa kuifananisha na.. lakini umeipenda sana..
  Damn, mkuu wangu mimi hotuba hii niliiona zuga toka siku ya kwanza kwa sababu nilijua Mkapa kafanya madudu gani na anatangaza vitu gani..Ati alifikiria Bongoland maana ina maana watu wanatumia Bongo ktk ubunifu wa uwekezaji na Ujasiriamali! .. yeye alifanya kipi kama sio Ujanja ujanja huo huo kufungua Ofisi akiwa Ikulu!..Katuibia ngapi jamanai hivi kweli mtu huyu alikuwa hana hata Aibu na Wabongo mkampigia makofi!...

  Mkapa alijua vizuri kwamba Bongoland ina maana watu wanaishi kiujanja ujanja na ndicho alichofanya yeye na wenzake wote..iweje huyu mtu ajue mambo ya Utajiju au Utalijua Jiji kisha aseme ati alidhania maana ya Bongoland ni kutumia Bongo ktk ubunifu... kwani wizi alofanya yeye sio ubunifu maanake haijatokea rais wa nchi kufungua kampuni yake akiwa Ikulu..

  Hizi ni hadithi za Mkulima kusingizia jembe baada ya mavuno kukosekana..Ni watu kama Mkapa ambao siku zote hawakosi sababu, kila mapungufu yao ni lazima kuna mkono wa mtu..Ni viongozi ambao walikuja omba kura za wananchi kwa kupiga magoti lakini mara tu walipopewa madaraka wakaota Uungu na kuwageuza wananchi kuwa somekind of an object!..sawa na mkulima na jembe lake au Horseman na farasi..

  Bila hata kumfikiria Nyerere, Hotuba kama hii kifupi inanipa kichefuchefu.. I said before 2005 na nitarudia tena kusema it sucks!..
   
 6. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #6
  May 15, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,361
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  unajua wakati mwingine sisi wengine tunapenda maneno sana.. sometimes we miss the point. Kama hotuba hiyo ingekuwa haijasemwa na Mkapa ni moja ya hotuba nzuri sana. Tatizo linakuja tunapojua nani kasema kwa sababu kwa kila kipimo hotuba hiyo inaonesha kilele cha UNAFIKI.

  Hivi alikuwa anamzungumzia nani?
   
 7. M

  Mkandara Verified User

  #7
  May 15, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Kumbe umeshtukia!... Nakwambia hivi Hata kama asingekuwa yeye sidhani kama rais mzuri angetoa hotuba kama hii hata kidogo kwa sababu hotuba nzima inazungumzia - WATU, tena kwa mafumbo.
  Trust me, hakuna kizuri ktk hotuba ile zaidi ya kukumbushana kugawana umaskini. Mashirika ya Umma yalikufa miaka 20 iliyopita na waliyaua wao sii wananchi hata kidogo kwa sababu leo hii waajiriwa ktk mashirka mengi yaliyouzwa na wale wale wa wakati ule. Kilichobadilika ni Mfumo, mbinu za biashara (Policies) na Uongozi, which means kama mashirka yalikufa wakiwa wao viongozi inabidi wao wenyewe wajitazame ktk kioo..Na siwezi kulaumu sana Mfumo kwa sababu toka tumebadilisha mfumo mbona mashirka mengine yaliyobakia chini ya serikali yanazidi kuporomoka wakati tupo ktk mfumo bora zaidi na wajuzi wenyewe wanaotumia bongo za ubunifu ndio wao!..
  Again, Mkuu wangu sidhani kama Nyerere angeweza kuhutubia kama Mkapa hata kidogo..Hata siku moja Nyerere hakuwahi kuwalaumu wananchi hata baada ya Ujamaa kufa..kwa sababu wananchi wanafuata policies na sheria ulizoziweka kulinda maslahi ya Taifa. Alichofanya Mkapa ni scare tactics.. katumia maneno ya chuki, wivu, Udini, Umajimbo na Ukabila..kuwatisha Wadanganyika.. ni misemo ambayo hadi leo inatumika sana na viongozi wote!

  Mimi leo hapa nilipo siwezi kuishi kiujanja Ujanja kwa sababu system nzima imejengwa kulinda upuuzi kama huo kutokea, lakini nikirudi Bongo ni lazima nibadilike kuwa kama wao ili niweze ku fit ktk system. Siwezi kuwa fisadi wala kula nao sahani moja isipokuwa mkuu wangu itanilazimu kuwatoa watu...itabidi nitoe rushwa ili nipate kutoa mzigo wangu bandarini kwa sababu TISS wanasema Container langu halipatikani.. Revenue wanataka nilipie millini 20 kwa container la feet 20 bila kujali kilichokuwa ndani..Immigration wanasema Uraia wangu una matatizo, niwakatie laa sivyo nitafikishwa Kituo cha kati..
  Hii ndio Bongo ujanja ujanja unaanzia serikalini..Kiutawala mwananchi ni farasi anayekimbia kufuata mzunguko wa mbio za Kentacky Durby!...
   
 8. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #8
  May 15, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,361
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Ndiyo maana nimeuliza tatizo la hotuba hiyo ni nini.. kwanini aliwazungumzia wa tanzania na uaminifu.. ? kwangu mimi inaonekana alikuwa anawazungumzia watanzania wawe waaminifu ili wawekezaji wawapende!!
   
 9. M

  Mkandara Verified User

  #9
  May 15, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mzee Mwanakijiji.
  Mkuu hata siku moja Mwekezaji hahitaji uaminifu wa mwananchi isipokuwa serikali iliyopo madarakani...Hawa sii Tourist wanakuja kutembea wakaogopa Vibaka au utekaji nyara..Wao huitazama nchi nzima ktk Policies zake kibiashara, soko, kodi, Usalama (National security) na sheria inawalinda kiasi gani.. wewe na mimi ni mtumwa tu unaetakiwa kufuata sheria za serikali au za kampuni...
  Sasa wakati Mkapa anatupaka mafuta sisi kwa lawama za uaminifu ambao sisi wenyewe hatufahamu kutokuwa nao yeye anaburuza mabillioni..At the same time anawakomesha Maaskofu na Masheikh ambao walianza kuzungumzia Ufisadi wa Mkapa kabla hata wanasiasa hawajaona ndani..
  Mkuu hotuba nzima ilikuwa kujisafisha yeye, kuweka lawama kwa watu wengine na kupotosha (brain wash) fikra za wananchi. kwani hakuna zuga baabu kubwa kama mtu atakulaumu kwa kitu usichokifahamu...Utabakia eeeh!
   
 10. Recta

  Recta JF-Expert Member

  #10
  May 15, 2009
  Joined: Dec 8, 2006
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mkuu Mwanakijiji, nimejaribu kutafuta mazuri unayoyazungumzia kutoka kwenye hotuba hiyo (hapo juu) bila kuyaona kwa uhakika. Simaanishi kuwa hotuba hiyo si nzuri, ila haina manufaa ya kina kama inavyotakiwa iwe. Sababu za kusema hayo ni kutokana na timing, contents na hata uwezekano wa kuleta matamanio yanayoelezewa kwenye hotuba yenyewe.

  Mkuu, timing ya hotuba hii (Jan 31, 2008) ni mbovu. Ni mbovu kwa kuwa kauli kama hizi zilitakiwa zitolewe nae at least Nov 1995 aliposhika kiti cha urais kwa mara ya kwanza. Ni kauli ambayo kwa wakati ule ingeweza kuleta chachu mpya, mwelekeo mpya na matumaini mapya kwa serikali yake na jamii nzima.

  Pili, content ya hotuba au maelezo yoyote yanatakiwa walau yawe complete. Hotuba hii inaelezea kilio cha upotevu wa maadili, uaminifu na mengine yote yanayoweza kusomeka kutoka kwayo. Ila haielezei walengwa wanaoliliwa kupotosha, kupindisha au kuharibu uaminifu huo, uadifu, na hata mafanikio yanayotajwa ni akina nani. Ingekuwa na manufaa zaidi kama ingeweza kubainisha kwa ukamilifu kabisa inakusudiwa kwa watu gani, wako wapi, wanafanya nini na nini kinachotakiwa/kusudiwa kufanywa dhidi yao. Mapungufu tuliyonayo hivi sasa nchini yanatokana na kufumbiana macho kama huku. Yanatokana na kuoneana soni au kutotanabaisha mapungufu kwa kina kwa kutajana, na kukosoana kikamilifu.

  Mkuu, kutokana na yote niliyoyataja hapo juu, ni dhahiri kuwa hakuna mabadiliko ya maana yanayosababishwa na hotuba hii.
   
 11. J

  Jibaba Bonge JF-Expert Member

  #11
  May 15, 2009
  Joined: May 6, 2008
  Messages: 1,224
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160

  Shirika kubwa kabisa 'TANZANIA' liliongozwa na wewe mwenyewe Mkapa ! Mkapa tupe amana zetu tumekuja tunazitaka sasa. Naorodhesha chache hapa
  - madini
  - NBC - kumbuka ulivyomuondoa Mwakyembe kwenye bodi ya wakurugenzi alipokuwa anaonyesha uaminifu wake kupinga wewe kuuza NBC yetu
  -NMB - kumbuka ulivyomfanya Ibrahimu Kaduma
  -Kiwira Coal Mine
  -EPA
  .........
   
 12. Kite Munganga

  Kite Munganga JF-Expert Member

  #12
  May 15, 2009
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,298
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Nilisikia majuzi Rais wa Sudan Al Bashir akijiteea kuwa yaliyotokea Darfur si mauaji ya kudhamiria, bali wale walikuwa ni waasi ambao serikali yoyote ingekabiliana nao waasi ili kuwasambaratisha, sasa iwapo ilikuwa hivyo na bado Al Bashir anatakiwa na ICTR, Inakuwaje Mkapa asiwajibike na wale wapemba alioowamaliza
   
 13. I

  Interested Observer JF-Expert Member

  #13
  May 15, 2009
  Joined: Mar 27, 2006
  Messages: 1,400
  Likes Received: 432
  Trophy Points: 180
  The best!
   
 14. I

  Interested Observer JF-Expert Member

  #14
  May 15, 2009
  Joined: Mar 27, 2006
  Messages: 1,400
  Likes Received: 432
  Trophy Points: 180
  Bob,
  Naiona hasira yako kwa the traitor and the wise hooligan, Mr. Benjamin William Mkapa, an educated elite, who can make such a speech; of the best! He preached what he didn't do. The pundits will tell you he "wokeup" the economy. He inherited an economy which was in tatars; making sound macroecomics work for the country which was heading to the death pit! He became emotional and big headed (that is what I think) and satrted stealing from the same sound economy he made. From my rough arthmetic he made above a USA Dollar billion and up. The Kiwira, the other assets in Real Estate etc. He is among the richest retired presidents. He deserves more than a jail sentence.

  But I remind you that, and frankly, I was even furious about this traitor, the way he protected his head traitor, another blood sucker, Mr. Ali Hassan Mwinyi who escaped impeachment in office. These are two thieves who are going to be forgotten very soon and the country will still go on.

  But the stories are emerging, the above two traitors have taken a minute of a portion which the modern traitors, by the help of a sitting president are going to part with after their terms. The 2005 to 2015 term will see Tanzanians loosing hope, and wealth, and the decision makers of all policies will be centred to the haves; the havenots will be few and dictated. Have you heard of a president who have shares in all sound projects in a country? I heard about Mobutu Seseko Wa Zabanga; but let me tell you that we have in our incubation chamber the most corrupt famailies and which are going to lead Tanzania in the 15 to 20 years from now.
   
 15. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #15
  May 15, 2009
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,313
  Likes Received: 5,604
  Trophy Points: 280
  Hata mimi bwm namkubali sana kwa hotuba zake nzuri sana na uwezo wake kwa ujumla......ila washikaji wamempoteza mwelekeo alopewa na baba yake jkn....hapo tu ndio ame bugi step.....nae amekuwa fisadi kiwembe...hafai kabsaa tunajuta hata kumjua....na kumchagua.
   
 16. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #16
  May 15, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Hapa ndipo utaelewa rationale yangu ya kumkataa mtu anayekuja na appeal za uzalendo na utaifa, hata mafisadi wanajua ghiliba hii.
   
 17. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #17
  May 15, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Utamkubali atakayekuja na appeal ipi?
   
 18. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #18
  May 15, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Vitendo, a tested dynamic track record, multidimensional solid reason, intellectually engaging input, facts, figures, time framed working plan, useful ammunition and energy, genuine self inquiry,non condescending tone, hipocrisy and denialism free diction, ombudsmanship lacking debate, clear thoughts, organized chaos and factors symmetrically analogical to these.
   
 19. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #19
  May 15, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,361
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  mimi nadhani tukimsomea yeye mwenyewe hotuba yake hii anaweza kuinamisha kichwa kwa aibu
   
 20. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #20
  May 15, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Huyo itabidi umuumbe mwenyewe....
   
Loading...