Hotuba Ya Mheshimiwa Zitto Zuberi Kabwe Kuhusu Miundombinu Bungeni

Mpaka Kieleweke

JF-Expert Member
Feb 27, 2007
4,132
1,571
HOTUBA YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI MHE. KABWE ZUBERI ZITTO (MB) KUHUSU MPANGO NA MAKADIRIO YA MATUMIZI YA BAJETI WIZARA YA MIUNDOMBINU , KWA MWAKA WA FEDHA 2008/2009
___________________

UTANGULIZI:

1. Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Kambi ya Upinzani naomba nitoe maoni ya Kambi ya Upinzani kuhusu hotuba ya bajeti ya Wizara ya Miundombinu kwa mwaka wa fedha 2008/2009 kwa mujibu wa Kanuni za Bunge Kanuni ya 99(7) toleo la Mwaka 2007.

2. Mheshimiwa Spika, Itakumbukwa kuwa kwa takribani miaka miwili iliyopita nilikuwa Waziri Kivuli wa Mipango na Uchumi. Kufuatia mabadiliko ya Baraza la Mawaziri yaliyofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kujiuzulu kwa Waziri Mkuu, Kiongozi wa Upinzani Bungeni naye ilimbidi kupanga upya timu yake na akaniteua kuwa Waziri Kivuli wa Miundombinu.


Kwa kuwa hii ni mara yangu ya kwanza kusimama mbele ya Bunge lako tukufu kama Msemaji Mkuu wa Wizara ya Miundombinu naomba nitoe shukrani zangu za dhati kwa Kiongozi wa Upinzani Bungeni Mhe. Hamad Rashid Mohamed (Mb) na Naibu wake Dr. Willibrod Peter Slaa (Mb) kwa kuniteua kushika nafasi hii. Vile vile napenda kuwashukuru kwa kunipatia msaidizi mahiri na mwenye uzalendo wa dhati kwa nchi yetu, Mheshimiwa Bakari Shamis Faki (Mb) kama Naibu Waziri Kivuli wa Miundombinu. Hotuba hii imefika hapa kwa Msaada mkubwa sana wa Mhe. Bakari Shamis Faki. Nawashukuru pia Wabunge wote wa Kambi ya Upinzani walio katika Kamati ya Bunge ya Miundombinu Mhe. Bi. Khadija Al-Quassmy wa Viti Maalumu na Mhe. Said Amour Arfi wa Mpanda Kati kwa msaada mkubwa walionipa katika kuandaa hotuba hii.

Mimi sio mhandisi, ni mchumi tu tena mchumi wa Biashara, hivyo imani waliyonayo viongozi wangu na Wabunge wenzangu kwangu ni faraja sana hasa ukizingatia kuwa Wizara hii ni Wizara nyeti sana kwa ustawi wa uchumi wa nchi yetu na hasa katika nyakati za sasa ambapo Tanzania inapaswa kuchukua nafasi yake katika Eneo la Maziwa Makuu kama nchi kiongozi kiuchumi (Uchumi wa Jiografia).

Ninamhakikishia Mheshimiwa Kiongozi wa Upinzani Bungeni na Watanzania wote wazalendo kuwa nitafanya kazi hii, kwa kushirikiana na Naibu wangu mhe. Bakari Shamis Faki (Mb), kwa uwezo wangu wote kwa lengo la kusaidia maendeleo ya Taifa letu zuri la Tanzania.

3. Mheshimiwa Spika, napenda pia kuwashukuru wananchi wa jimbo langu la Kigoma Kaskazini kwa ushirikiano mkubwa wanaonipa katika kazi zangu. Najua kuna changamoto nyingi sana zinazotukabili lakini tumeanza kuona mwanga kwani tayari mkataba wa ujenzi wa Barabara yetu ya Mwandiga – Manyovu na ile ya Kigoma - Kidahwe umesainiwa na ujenzi unatarajiwa kuanza mwaka huu. Tumekuwa Jimbo la Kwanza katika Mkoa wa Kigoma kupata barabara ya lami toka nchi yetu ipate uhuru!. Kufuatia ujenzi wa barabara hii ndugu zetu wa Kasulu Magharibi nao watafaidika na mradi huu kwani barabara hii pia itafika kwao. Kwa niaba ya wananchi wa Kigoma Kaskazini napenda kuishukuru Serikali kwa kutimiza wajibu wake bila kujali itikadi za kisiasa. Ninawataka wananchi wa Kigoma Kaskazini kuhakikisha kuwa wanajiandaa na mabadiliko ya kiuchumi yatakayotokana na ujenzi wa barabara hii na hivyo kushika Ardhi ya kutosha na kuongeza uzalishaji mashambani kwani soko la bidhaa zetu sasa litapanuka. Vilevile wakulima wa Kahawa wa kata za Kalinzi, Mukigo na Bitale waongeze uzalishaji na ubora wa Kahawa yetu uongezeke zaidi kwani sasa gharama za usafiri wa kahawa itapungua kufuatia ujenzi wa barabara hii.




1 Masuala ya Jumla

4. Mheshimiwa Spika, Katika Taarifa ya Hali ya Umasikini ya mwaka 2007 (Poverty and Human Development Report 2007) imeonekana kuwa itakuwa ni vigumu sana kwa Tanzania kufikia malengo ya MKUKUTA kwani kasi ya ukuaji wa uchumi imekuwa chini ya viwango vinavyotakiwa. Moja ya suala ambalo limeainishwa katika Sura ya Tatu ya Taarifa hiyo ni kuwa kama Taifa tumekuwa na rasilimali chache sana za kuweza kufikia malengo ya ukuaji uchumi lakini zaidi ni kuwa rasilimali chache tulizonazo tunazitawanya kila mahala ili mradi ‘kila mtu apate’ bila mkakati maalumu. Tunaridhishana!

5 Mheshimiwa Spika, Taarifa hiyo, kwa mara ya kwanza, imesema ukweli na kuonya kuwa bila kuweka mkakati mpya wa kutumia rasilimali za nchi kwa malengo mahususi hatutapiga hatua katika maendeleo ya uchumi ( Given our limited resources there is need for a clear direction for resource mobilization and a concentration of efforts – Tanzania needs a well focused national growth strategy).

6. Mheshimiwa Spika, Taarifa ya Hali ya Umasikini imeshauri kuwa sasa ni lazima tuchague sekta ongozi (growth drivers) na sekta ambayo Taarifa hii imeipendekeza ni sekta ya Miundombinu (Transport services for landlocked neighbours Rwanda, Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Zambia, Malawi and Uganda. Sekta hii ina mahusiano mazuri na chanya (strong linkages) na shughuli nyingine za kiuchumi pia inagawa vizuri faida za ukuaji uchumi (strongly supportive of broad based enabling environment) na inaweza kutengeneza ajira nyingi sana.

7. Mheshimiwa Spika, Taarifa ya Hali ya Umasikini inatuonya kuwa iwapo hatutaenda haraka katika suala hili nchi nyingine zenye bahari zaweza kuchukua mkakati huo na kuutekeleza haraka na Tanzania ikapoteza fursa hii na kuendelea na lindi la umasikini. Katika mchango wangu hapa Bungeni nilisema pia mkakati huu unaanza kuchukuliwa na Msumbiji na Angola. Tuwe makini na tusome taarifa hizi muhimu sana na kuzifanyia kazi. Ninashauri kwa nguvu kubwa kuwa Taarifa ya Hali ya Umasikini (Poverty and Human Development Report) na brief zake ziwe ni nyaraka muhimu kwa kila mbunge kuanzia sasa (a must read reports).

8. Mheshimiwa Spika, katika mwaka huu wa fedha 2008/2009 kambi ya upinzani itajikita katika maeneo machache yenye umuhimu wa kipekee katika Wizara ya Miundombinu. Maeneo hayo ni Barabara, Viwanja vya ndege na usafiri wa anga, Bandari na usafiri wa Maji, Reli na usafiri wa Reli na Chuo cha Taifa cha Usafirishaji Dar es Salaam. Tutajikita kutoa mapendekezo maalumu katika maeneo hayo ili kuifanya Serikali iliyopo madarakani iangalie upya mipango yake na kwa kushirikiana tujenge nchi yetu nzuri ya Tanzania.

9. Mheshimiwa Spika, kambi ya upinzani inatambua kuwa sekta ya ujenzi imekua ikichangia kwa kiasi kikubwa katika ukuaji wa uchumi wa nchi yetu. Ukiangalia taarifa ya hali ya uchumi wa Taifa kwa mwaka 2007 utakutana na takwimu ambazo zinaonesha kuwa sekta ya ujenzi na maendeleo ya ardhi imekuwa zaidi ukilinganisha na kipindi kama hicho kwa mwaka 2006. Mwaka 2007,kiwango cha ukuaji wa shughuli za ujenzi kilikuwa asilimia 9.7 ikilinganishwa na asilimia 9.5 mwaka 2006. Ukuaji huu ulichangiwa na kuongezeka kwa ujenzi wa majengo ya kuishi na yasiyo ya kuishi. Aidha mchango wa shughuli za ujenzi katika pato la taifa ulikuwa asilimia 6.5 mwaka 2007 ikilinganishwa na asilimia 6.4 mwaka 2006. Ukuaji wa sekta ya ujenzi katika uchumi wa nchi ni ishara njema sana kutokana na sababu nilizoeleza hapo juu na hasa suala la ajira kwa wananchi na kuchochea ukuaji wa sekta nyingine.

10. Mheshimiwa Spika, licha ya kuongezeka kwa ukuaji wa sekta ya ujenzi katika uchumi, Serikali imekiri kuwa kuna wasiwasi wa kutoweza kufikia malengo ya program ya Maendeleo ya Sekta ya Uchukuzi (TSIP). Program hii kama mnavyofahamu ni ya miaka kumi na huu ni mwaka wake wa kwanza wa utekelezaji (2007/2008). Hata hivyo miradi yote mipya iliyopangwa kutekelezwa katika mwaka huo wa kwanza haikutekelezwa na wala haitatekelezwa katika mwaka huu wa fedha ambao umeanza (2008/2009). Habari hii sio njema hata kidogo na ni ya kukatisha tamaa sana kwa mpenda maendeleo yeyote.

11. Mheshimiwa Spika, kufuatia hali niliyoeleza hapo juu ni dhahiri kuwa miradi mingi iliyopo katika ilani ya uchaguzi wa CCM ya mwaka 2005 ambayo ilikuwa imepangwa kutekelezwa haitatekelezeka kwani Taifa halina fedha za kutekeleza. Sasa mtu atajiuliza hivi wakati wa uchaguzi CCM iliandika ‘wish list’ ili kuomba kura tu? Imefikia wakati sasa ni vizuri vyama vya siasa viwe makini vinapoandika ilani zao kwani hii tabia ya kurundika miradi mingi kwenye ilani halafu utekelezaji wake unakwama ni doa katika mchakato wa siasa.

12. Mheshimiwa Spika, Kambi ya Upinzani Bungeni inawaomba wabunge tujikite katika mjadala wetu katika suala zima la Fedha za ujenzi wa Miundombinu (Financing Infrastructure). Ninapata woga sana ninaposoma ripoti mbali mbali za Serikali kuhusiana na maendeleo ya miundombinu yetu ya kuwezesha ukuaji wa uchumi. Inabidi sasa tuache kujadili kila mtu na kabarabara kake na badala yake tuwe na mjadala mpana sana kuhusu ni vipi tunapata fedha za ujenzi wa miundombinu ya nchi. Kupiga kelele tunapiga kila mwaka. Ni jukumu sasa la viongozi wote wa kisiasa kukaa na kuangalia kwa mapana tunafanya nini kuhusu suala hili la ufinyu wa fedha za miundo mbinu.




13. Mheshimiwa Spika, Bajeti ya maendeleo ya miundombinu kwa mwaka 2008/2009 zinazoombwa kudhinishwa hapa ni Tshs. 592.182 Bilioni, na kati ya fedha hizo Tshs. 355. 156Billioni ni fedha za ndani na Tshs. 237.026Billioni ni fedha za nje. Katika fedha hizi Tshs. 164 Bilioni ni kwa ajili ya kutekeleza miradi inayoendelea na Tshs. 190 Bilioni ni kwa ajili ya kulipia madeni ya makandarasi waliotekeleza miradi ya Barabara. Mahitaji halisi ya miradi inayoendelea (bila kuweka miradi mipya) ni Tshs. 357 Bilioni. Hii maana yake ni kuwa Bunge hili linajadili asilimia 46 tu ya mahitaji halisi ya ujenzi wa miundombinu hapa nchini kwa mwaka 2008/2009. Hakuna miradi mipya na hata ile ya zamani tunaweza kuigharimia kwa 46% peke yake. Hatutafika hata kidogo. Ninashauri na kupendekeza kwamba tujielekeze katika mjadala mpana wa fedha za miundombinu vinginevyo Taifa hili litadumaa. Lazima tutafute vyanzo vingine vya fedha ili kujenga miundombinu.

14. Mheshimiwa Spika, kambi ya upinzani inatambua kuwa kuna juhudi za Serikali kutokana na fedha za Serikali ya Marekani za MCC kutatua tatizo hili kwa kujenga barabara na kiwanja kimoja cha ndege. Bado fedha za MCC hazitamaliza tatizo letu. Ninashauri serikali ikae na kuleta hapa Bungeni mpango mbadala wa kupata fedha za kujenga miundombinu hapa nchini. Kabla ya Bunge la mwezi wa Novemba Serikali iwe imemaliza kazi hiyo na kuieleza kamati ya Bunge ya Miundombinu na Kamati ya Bunge ya Fedha juu ya mpango huo. Kwa mfano hatuwezi kukwepa kuweka sovereign Bond ya angalau Tshs. 800 Bilioni ambapo tupate fedha za miradi yote ya sasa na kutengeneza miradi mipya. Miradi hii mipya lazima itokane na mjadala wa kina kuzingatia ushauri wa Taarifa ya Hali ya Umasikini (Poverty and Human Development Report 2007) kuhusiana na mkakati mpya wa kukuza uchumi (A new Framework for a Tanzanian Growth Strategy).

2. Hali ya barabara zetu (State of Roads)

15. Mheshimiwa Spika, Matengenezo ya kawaida ya barabara kuu ya kilometa 4,677.7 yalikamilishwa mwaka 2007, ikilinganishwa na kilometa 5,080.3 mwaka 2006. Hapa panaonyesha upungufu wa kilometa zipatazo 402.6 ukilinganisha na mwaka 2006. Hoja inayotolewa na Serikali kwenye upungufu huu wa kupungua kwa ujenzi kwenye sekta ya Barabara eti ni kutokana na utekelezaji wa sheria mpya ya manunuzi ambapo mchakato wa kutafuta makandarasi unachukua muda mrefu. Ninaomba tupate maelezo ya kina zaidi kuhusiana na ucheleweshaji huu wa ujenzi wa barabara zetu.

16. Mheshimiwa Spika, mwaka 2007 Barabara za mikoa zenye urefu wa kilometa 5,062.4 zilifanyiwa matengenezo ikilinganishwa na kilometa 8611 mwaka 2006, kwenye eneo hili pia palitokea upungufu wa ujenzi wa zaidi ya kilomita 3548.6, hii inaonyesha wazi kuwa kwa kipindi cha mwaka 2007 sekta ya miundombinu haikuwekewa mkazo unaostahili kwani kasi ya ukuaji wake ilipungua japokuwa Bunge lako tukufu lilipitisha fedha nyingi zaidi ukilinganisha na bajeti ya mwaka 2006. Kambi ya Upinzani inamtaka Waziri wa Miundombinu atoe sababu za kujitosheleza ni kwa nini kasi ya ujenzi wa barabara ilipungua kwa kipindi cha mwaka 2007? Kuna mkakati gani wa kuhakikisha kuwa kasi ya ujenzi wa barabara kwa mwaka huu inakua kwa kasi inayostahili?

17. Mheshimiwa Spika, Kambi ya Upinzani inataka kupata maelezo ya kina kutoka Serikalini ni kwa nini Sekta ya Ujenzi kwa mwaka 2007/2008 imetumia Shillingi bilioni 596.3 ikilinganishwa na shilingi bilioni 777.2 zilizotengwa kwa sekta ya Miundombinu ya barabara peke yake sawa na asilimia 76.7, ya fedha zilizotengwa. mpaka mwaka wa fedha unaisha iliweza kufikia asilimia 100?

18. Mheshimiwa Spika, hapo awali nimeshauri kuwe na mkakati mpya wa ujenzi wa miundo mbinu ya nchi. Hapa ningependa kupendekeza kwa upande wa barabara ili kuhakikisha mkakati mpya unaoweza kurejesha gharama za ujenzi baada ya muda mfupi. Mkakati mpya uzingatie kuunganisha mikoa ifuatayo kama hatua ya haraka kwa barabara za lami.

1. Mkoa wa Mbeya na Mwanza kwa maana ya barabara ya Chunya Tabora – Mwanza
2. Mkoa wa Mbeya na Kigoma kwa maana ya barabara ya Tunduma – Sumbawanga – Mpanda – Kigoma
3. Mkoa wa Mtwara na Ruvuma kwa maana ya barabara ya Mtwara – Tunduru – Songea – Mbamba Bay
4. Mkoa wa Arusha na Iringa kwa Maana ya barabara ya Arusha – Babati – Kondoa – Dodoma – Iringa
5. Mkoa wa Kigoma na Dar es Salaam kwa maana ya barabara ya Dodoma – Manyoni – Itigi – Tabora – Urambo – Kigoma.

19. Mheshimiwa Spika, barabara hizo nilizozitaja ni za kimkakati kiuchumi. Mkopo wowote utakaochukuliwa kwa ajili ya barabara hizi unaweza kulipika kwa muda wa miaka 20 mpaka 30 na mkopo unaokubalika kwani utachochea ukuaji wa uchumi wa nchi kwa kuongeza shughuli za kiuchumi na hivyo kupelekea nchi kupiga hatua na kuchukua fursa ya uchumi wa Jiografia. Nawasihi wabunge tuelekeze mjadala katika suala hili la ‘financing infrastructure’ kwani kama hakuna fedha hata tupige kelele vipi pesa hazitakuja maana tutajenga barabara lakini lazima tuendelee kulipia elimu, afya, huduma za serikali, pensheni kwa wastaafu wetu ambazo tunataka ziongezeke mpaka ngazi ya kima cha chini nk.

20. Mheshimiwa Spika, naomba nisemee kidogo mradi mmoja wa barabara, nayo ni barabara ya Sam Nujoma. Ujenzi wa barabara ya Sam Nujoma ambao ni kutokea Mwenge hadi Ubungo umeshachukua muda mrefu sana na bado ujenzi wake haujakamilika, pamoja na Mheshimiwa Rais kuahidiwa kuwa ujenzi wake ungekamilika mwaka 2006 mwezi November ila mpaka leo hii ujenzi huo bado haujakamilika. Kambi ya Upinzani inaitaka Serikali kutoa majibu ya kina nini kimesababisha ujenzi wa barabara hiyo kuchelewa kwa kiasi hicho? Tatizo liko wapi?mkandarasi ama ni serikali?

3. Hali ya Bandari zetu na usafiri wa Majini (The state of our
ports and marine transport).

21. Mheshimiwa Spika, nchi yetu imejaaliwa na Mungu kwa kuzungukwa na Bahari ya Hindi na Maziwa makuu matatu ambayo ni Ziwa Nyasa, Ziwa Tanganyika na Ziwa Victoria. Mungu angeweza kutunyima rasilimali nyingine zote na akatuacha na rasilimali hizi tu na tungeweza kukua kama Taifa kutokana na utajiri unaoweza kuzalishwa na Rasilimali hizi. Hata hivyo Mungu ametujaalia mengine mengi sana kama Madini, Mito yenye kuzalisha Umeme na Watu wapenda amani na wakarimu. Hata hivyo bado hatujaweza kutumia rasilimali hizi kujiendeleza inavyopaswa.

22. Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Taarifa ya Hali ya Uchumi, katika mwaka wa 2007, bandari ya Dar es salaam ilihudumia shehena zenye jumla ya tani 5,703 milioni ikilinganishwa na tani 6,320 milioni mwaka wa 2006, sawa na upungufu wa asilimia 9.8. Vile vile, jumla ya meli 4,380 zilihudumiwa katika kipindi cha 2007, ikilinganishwa na meli 4,147 mwaka wa 2006, sawa na ongezeko la asilimia 5.6. Kambi ya upinzani imeshtushwa na hali hii ya kushuka kwa idadi ya makontena ambayo yamehudumiwa na Bandari yetu kuporomoka kwa takribani asilimia 10 katika kipindi cha mwaka mmoja. Kulikoni?

23. Mheshimiwa Spika, mwaka 2007 kitengo cha kontena kilihudumia tani 3,327 milioni kati ya shehena yote iliyohudumiwa katika bandari ya Dar es salaam. Aidha, mwaka 2007, kitengo hiki kilihudumia kontena 333,980 zenye urefu wa futi ishirini kila moja, ikilinganishwa na kontena 273,128 mwaka wa 2006, sawa na ongezeko la asilimia 22.3. Katika mwaka wa 2007, muda wa kukaa bandarini kwa kontena zilizoingia nchini uliongezeka toka wastani wa siku 14.5 mwaka wa 2006 hadi siku 23. aidha, ufanisi katika kitengo cha kontena ulipungua hadi kufikia mizunguko 18 kwa saa ikilinganishwa na mizunguko 21 kwa saa mwaka 2006. Taarifa hizi sio nzuri kwa Bandari ambayo ingeweza kuleta utajiri mkubwa kwa nchi yetu. Tunataka kupata maelezo ya kutatua matatizo haya ili kitengo cha makontena kiwe na ufanisi zaidi.

24. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa 2007, bandari za Tanga na Mtwara zilihudumia shehena zenye jumla ya tani 542 milioni na 112 milioni ikilinganishwa na tani 519 milioni na 153 miloni mwaka 2006 kwa mtiririko huo. Bandari hizi za Mtwara na Tanga ni lulu kwa nchi lakini hatutumii lulu hii.

25. Mheshimiwa Spika, ni lazima Pawepo na mkakati madhubuti wa kuziimarisha Bandari za Mtwara na Tanga , ili kuhakikisha kuwa Meli kubwa za mizigo zinaweza kutia nanga kwenye maeneo hayo .Hatua hii inalenga kwenye kuongeza mapato zaidi na hata kupanua wigo wa soko la malighafi zinazozalishwa hapa nchini , kwa mfano Kama bandari ya Tanga itaimarishwa itawezesha usafirishaji wa malighafi yatokanayo na mkonge kusafirishwa kwa urahisi zaidi kuliko hali ilivyo hivi sasa kwani ni lazima malighafi hizo zisafirishwe kwanza kwa njia ya Barabara hadi Dar es salaam ndipo zinapakiwa kwenye Meli. Lakini pia Mkakati wa Bandari ya Tanga ni lazima ufungamanishwe na mkakati wa sekta ya madini.

26. Mheshimiwa Spika, Mwaka 2012 Tanzania itakuwa ni nchi yenye kuzalisha madini ya Nikeli kuliko nchi nyingine zote duniani kama mipango ya uchimbaji wa Nikeli kule Kabanga wilayani Ngara itakamilika. Ni muhimu sasa kuweka mikakati ili Bandari ya Tanga iwe ‘Port of Choice’ kwa kusafirisha Nikeli na madini mengine yanayochimbwa nchini.

27. Mheshimiwa Spika, hapa ndipo suala linaloitwa fungaminisho linapopata maelezo rahisi. Tutakapoimarisha Reli ya Kati ili iwe ‘Railway of Choice’ kwa usafiri wa Shaba na Kobalti kutoka Mashariki ya Kongo, maana yake ni kuwa mizigo kwa ajili ya Bandari ya Tanga kama ‘Port of Choice’ kwa usafirishaji wa Madini itaongezeka. Shughuli za kiuchumi zitapanuka, ajira zitakuwa bwelele na vijana hawataimba tena ‘Tanga Kunani’. Serikali itapata mapato na kuhudumia sekta za kijamii. Hii ndio inaitwa ‘strategic Thinking’ ambayo kambi ya upinzani inaimba kila mwaka. Tubadili mindset! kwa kupanga mipango yetu kwa kuangalia mbele kuna fursa zipi kwa upande wetu.

28. Mheshimiwa Spika, Bandari ya Mtwara maelezo yake hayatofautiani na ya Tanga. Licha ya kusarisha Korosho na mazao ya misitu, Bandari ya mtwara ni muhimu sana kufungamanishwa na Miradi ya Mchuchuma na Liganga. Vile vile Bandari hii yaweza kuwa ni Bandari ya nanga kwa uvuvi wa bahari kuu.

29. Mheshimiwa Spika, usafiri na haswa kwa njia ya maji Ziwa Victoria umekuwa hauridhishi kwani meli ambazo zinatumika kuwasafirisha abiria zimekuwa zikilalamikiwa kila mara kutokana na meli hizo kuwa ama ni chakavu sana kutokana na kukaa muda mrefu bila kufanyiwa matengenezo au kutokana na kuwa ni za zamani sana. Meli hizi zinahatarisha maisha ya wananchi wetu kila wanaposafiri , hivyo Kambi ya Upinzani inaitaka serikali kutoa maelezo ya kina juu ya hali hii ya kuhatarisha maisha ya wananchi wetu na kuna mkakati gani wa kuhakikisha kuwa wananchi wetu wanakuwa salama kila wakati.

30. Mheshimiwa Spika, Kambi ya Upinzani inaamini kuwa sasa huu ni wakati muafaka wa kuwa na Bandari za nchi kavu (Dry Ports) ili kuweza kupunguza msongamano wa makontena katika bandari ya Dar es salaam na pia kukuza uchumi maeneo mengine ya nchi kwa kukuza nafasi za ajira .
Serikali inapaswa kuweka mkakati wa kina kuwa Bandari ya Dar es salaam iwe ni kwa ajili ya kupitisha mizigo yote ambayo inaenda nje ya nchi kama ifuatavyo;

31. Mheshimiwa Spika, Mizigo yote ambayo inaenda nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na Burundi ijengewe bandari ya nchi kavu Kigoma, na hapo ni kuwa mizigo yote ambayo inaingia bandarini kwa ajili ya kupelekwa kwenye nchi hizo basi isafirishwe moja kwa moja hadi Kigoma na ndipo iweze kuchukuliwa pale. Jambo hili litasaidia kuinua uchumi wa Kigoma na pia litawezesha kuimarisha shirika letu la reli kwani litatumika kusafirisha mizigo hiyo kutoka Dar es salaam hadi Kigoma ,wananchi wataweza kupata ajira kwenye mkoa huo na pia litawezesha kuharakisha ukarabati wa miundombinu kwenye mkoa huo, Biashara itaimarika na pia litapunguza wingi wa mizigo ama makontena kwenye bandari ya Dar es salaam.

32. Mheshimiwa Spika, Mizigo yote ambayo inaenda nchi za Uganda na Rwanda, pajengwe bandari ya nchi kavu Isaka Shinyanga na hili litaharakikisha kukua kwa uchumi katika mikoa ya kanda ya ziwa kwani ajira nyingi zitaweza kupatikana na hatimaye kuimarika kwa uchumi kwenye maeneo husika.

33. Mheshimiwa Spika, Mizigo yote inayoenda nchi za Zambia na Malawi ,pajengwe bandari ya nchi kavu mkoani Mbeya ili kuhakikisha kuwa mizigo hiyo inachukuliwa kwenye eneo husika. Hii itasadia kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi kwenye mikoa ya nyanda za juu kusini kama vile Iringa ,Mbeya na Ruvuma . Pia kwenye maeneo haya makampuni yote yanayohusika na clearing and forwarding yawe yanafanyia shughuli zake kwenye maeneo hayo ambayo yana bandari hizo za nchi kavu. Dar es salaam iachwe na kuwa ni kwa ajili ya mizigo ya ndani ambayo haiendi kwenye mikoa husika ,na pia liwe ni eneo la kupokelea mizigo husika na kuisafirisha kwenye maeneo husika (Transit port).

34. Mheshimiwa Spika, nitakuwa mbunge wa ajabu kama sitazungumzia matatizo ya wafanyakazi ya iliyokuwa AMI katika Bandari ya Kigoma. Baada ya AMI kutopata zabuni ya kuendesha Bandari ya Kigoma, wafanyakazi wake hawajalipwa mafao yao na wanahangaika mpaka leo. Niliwasiliana na Katibu Mkuu wa Wizara juu ya suala hili bila kupata majibu yeyote. Ninaomba serikali inipe maelezo hapa Bungeni juu ya sakata la wafanyakazi hawa. Watazania hawa wanateseka sana kufuatilia haki zao. Tafadhali naomba majibu ya kina kabisa yatakayopelekea wananchi hawa kupata haki yao ya mafao.

34. Hali ya Reli na Usafiri wa Reli ( The State of our Railways
and Rail Transport)

35. Mheshimiwa Spika, Usafiri wa Reli ni usafiri muhimu sana kwa nchi na hasa kuhusiana na usafiri wa mizigo yenye uzito mkubwa. Hatuwezi kuendelea kamwe kwa kutegemea usafiri wa barabara kusafirisha mizigo yenye uzito mkubwa kama Madini na bidha nyingine. Tanzania tuna reli mbili yaani ya TAZARA na ile ya Kati. Wabunge wamezugumza humu Bungeni kuhusiana na adha ya usafiri wa Reli. Waziri Mkuu ametoa majibu kuhusiana na suala hili na ameeleza kwamba kwa kiasi kikubwa sisi ni chanzo cha matatizo haya na siyo mwekezaji ambae amekodisha Reli hii kwa ubia katika ya Serikali ya Tanzania na kampuni ya Rites ya India.

36. Mheshimiwa Spika, nilipokuwa Nguruka mkoani Kigoma watu wa Nguruka waliniambia kwamba ukitaka kusafiri kwa Reli inabidi uweke sahihi hukumu ya kifo. Kuna taarifa za vifo vilivyotokea maeneno ya Uvinza kufuatia mwanamke mmoja kukosa hewa alipokuwa akisafiri na treni ya Abiria kwenda Kigoma. Serikali ifuatilie kujua usahihi wa taarifa hizi. Vilevile kumekuwa na ugumu mkubwa wa kupata tiketi za kusafiria katika stesheni karibu zote za Reli na kuwa usumbufu mkubwa sana kwa wananchi wetu. Hali ya Reli inasikitisha mno kwa wananchi wa mikoa ya Kigoma na Tabora.

37. Mheshimiwa Spika, katika Bunge la 11, Mheshimiwa Said Amour Arfi alitoa hoja binafsi hapa Bungeni kuhusu hali ya Shirika la Reli na Serikali iliahidi kutoa majibu. Ni vizuri basi Serikali itoe majibu kama nyongeza ya majibu aliyoyatoa Mheshimiwa Waziri Mkuu alipokuwa akijibu hoja za Wabunge kuhusiana na tatizo la usafiri wa Reli ya Kati.


38. Mheshimiwa Spika, Katika mwaka wa 2007, Shirika la Reli Tanzania lilisafirisha mizigo tani 714,000, ikilinganishwa na tani 775,281 mwaka 2006, sawa na upungufu wa asilimia 7.9. kati ya hizo, tani 173,516 ilikuwa ya nchi jirani za Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo, Rwanda, Burundi na Uganda. Hivi sasa kuna kitu kinaitwa ‘mineral boom’ kule Kongo ya Mashariki. Inakuwaje tena usafiri wa mizigo unashuka kiasi hiki? Kwa kuwa Shirika hili bado Serikali ina hisa za kutosha, ni vema serikali kupitia wakurugenzi wake ambao wengine ni wabunge wenzetu iwe na mkakati wa kutangaza huduma ya Reli kwa nchi hizi. Hata hivyo ni lazima tuboreshe kwanza huduma hizi na kupanua Reli hii ili kupata biashara zaidi.

39. Mheshimiwa Spika, Shirika la Reli lilipata mapato ya sh.33.6 bilioni mwaka 2007, ikilinganishwa na sh.42.6 mwaka wa 2006, sawa na upungufu wa asilimia 21.1. Huku ni kuporomoka kwa kasi kwa mapato ya shirika ambapo ni lazima serikali itolee maelezo. Kambi ya Upinzani pia inapenda kufahamu kama Shirika lina Corporate Plan na kama inafuatwa katika kuboresha huduma za Reli.

40. Mheshimiwa Spika, kama ilivyo viwanja vya ndege kwa usafiri wa anga, Stesheni za Reli zina umuhimu mkubwa sana kwa usafiri wa Reli. Kwa muda mrefu sana Stesheni za Reli zimekuwa ndio maofisi ya Shirika la Reli na pia zimekuwa zinamilikiwa kwa pamoja na Reli. Stesheni za Reli, hasa zile stesheni kubwa kama vile Tabora, Kigoma, Urambo, Mpanda, Kilosa, Dodoma, Morogoro, Tanga, Mwanza na Dar es Salaam zimekuwa hazitumiki kwa asilimia 100 na kwa kweli stesheni nyingine zimekuwa chafu na hazihudumiwi ipasavyo. Sijui kama katika mkataba wa kukodisha Reli na pia makubaliano ya wanahisa wamesema nini kuhusu Stesheni hizi na hasa umilliki wake.

41. Mheshimiwa Spika, Kambi ya upinzani inashauri tuwe na mwono tofauti na kugeuza Stesheni hizi kuwa vituo vya Biashara katika miji yetu. Stesheni nyingine kama ile ya Kigoma, Tabora, Dodoma na Dar es Salaam zaweza pia ‘tourist Attraction’ hasa kwa watalii kutoka Ujerumani kutokana na ukweli kuwa Stesheni hizi ni moja ya usanifu wa Kijerumani. Stesheni hizi zina zaidi ya miaka 100 na baadhi ya vyumba vyake vyaweza kugeuzwa kuwa hoteli na migahawa na maduka ya vitu mbali mbali na hivyo kuzifanya hizi stesheni kuwa ‘live’ usiku na mchana. Ninaiomba Wizara ya Miundombinu itafakari hili na kualika Makampuni ya Kitanzania ‘private sector’ kuangalia uwezekano wa kuzibadili Stesheni hizi kwa maana ya majengo kuwa maeneo ya Biashara. Inawezekana, hebu tujaribu.

42. Mheshimiwa Spika, kama ilivyokuwa kwa ATC Serikali iliunda RAHCO kwa ajili ya kuuza mali za iliyokuwa TRC. Moja ya mali zilizouzwa ni pamoja na Gerezani Railway Social Club ambayo kimsingi ilikuwa ni mali ya Wafanyakazi. Ninapenda kupata maelezo ya serikali kuhusiana na uuzwaji wa mali hizi. Vile vile tunapenda kujua hatua zilizochukuliwa kutokana na Mataruma ya Reli yaliyokatwa na kukutwa katika kiwanda cha Nondo.

5. Daraja la Kigamboni

43. Mheshimiwa Spika, Daraja la Kigamboni ni suala linalosemwa kila mwaka na wala hatuoni aibu kuendelea kulisemea. Naomba Waziri wa Miundombinu alieleza Bunge hili ni lini tutaacha kusema na kutenda kuhusiana na suala hili. Suala hili sasa liishe maana tumekuwa Taifa la maneno matupu mpaka inakuwa ni aibu sasa.

6. Hali ya viwanja vya ndege na Usafiri wa Anga (The state
of our Airports and Air Transport)

44. Mheshimiwa Spika, nafasi ya Tanzania kijiografia inatoa fursa kubwa kwa usafiri wa anga kuwa na manufaa kwa Taifa. Hivi sasa Taifa letu lina viwanja vya ndege viwili vya kimataifa yaani Julius Nyerere International Airport na Kilimanjaro International Airport. Kiwanja cha Songwe kinamaliziwa kujengwa. Viwanja vya ndege vya Mwanza, Kigoma, Tanga, Mtwara na Mafia ni viwanja muhimu sana kwa ukuaji wa sekta na uchumi kwa ujumla.

45. Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Taarifa ya Hali ya Uchumi wa nchi, huduma za usafiri wa anga nchini ziliendelea kutolewa na mashirika kadhaa ya ndege na idadi kubwa ni makampuni binafsi. Makampuni hayo ni pamoja na Air Tanzania Company Limited, Precision Air, Coastal Travel, Regional Air Services, Eagle Air, Air Excel, Flight Link, Zan Air na kampuni kadhaa nyinginezo. Abiria wa ndani waliosafiri kwa ndege hizo ni jumla ya watu 1,074,424 mwaka 2007 ikilinganisha na abiria 1,011,265 mwaka 2006. Kampuni ya Precision ilisafirisha takriban abiria 470,000 kati ya abiria wote walisafiri ndani ya nchi kwa ndege, hii ni sawa na asilimia 43 ya wasafiri wote. Tanzania hatuna tabia ya kutambua mchango wa Watanzania wenzetu wanaofanya vizuri katika nyanja mbalimbali. Tunapenda kuchukua fursa hii kuwapongeza wamiliki na wafanyakazi wa Kampuni ya Precision kwa Huduma wanayotoa kwa Watanzania. Licha ya mapungufu kadhaa yaliyopo lakini hivi tukijiuliza kama hawa Precision wasingekuwapo hali ya usafiri wa anga Tanzania ingekuwaje?

46. Mheshimiwa Spika, Kampuni yetu ya Umma ya Air Tanzania ambayo ilianzishwa baada ya kuvunjwa kwa mkataba na Kampuni ya South Africa Airways iliendelea kusuasua katika mwaka uliopita. ATCL ilisafirisha nusu ya abiria waliosafirishwa na Precision. Ni mategemeo ya Watanzania kuiona ATCL kama fahari ya Taifa (The National Pride). Hata hivyo hali ya ATCL inatia simanzi sana kwa sisi wapenzi wa sekta ya umma katika maeneo nyeti kama usafiri wa anga.

47. MHESHIMIWA SPIKA SHIRIKA LETU LA NDEGE LIMEKUWA KATIKA WAKATI MGUMU SANA KWA KIPINDI KIREFU KUTOKANA NA UKATA NA UKOSEFU WA FEDHA KUTOKANA NA SERIKALI NA HALI NGUMU YA KIUCHUMI AMBAYO INALIKUMBA SHIRIKA HILO , NA HII INATOKANA NA SERIKALI KUTENGA KIASI KIDOGO SANA CHA FEDHA KUJIENDESHA. KITENDO CHA ATCL KUSAFIRISHA NUSU YA ABIRIA WALIOSAFIRISHWA NA KAMPUNI MOJA BINFSI NA ROBO TU YA ABIRIA WALIOSAFIRI KWA NDEGE NCHI NZIMA NI AIBU KWA SHIRIKA LETU LA NDEGE KWANI KAMA ABIRIA WANAONGEZEKA ILITEGEMEWA KUWA NI SHIRIKA LETU LA NDEGE LINGEWEZA KUJIONGEZEA FAIDA NA MAPATO ZAIDI KUTOKANA NA ONGEZEKO HILI LA WATEJA ,ILA BADALA YAKE SHIRIKA LETU LIMEKUWA LIKIWA NA WAKATI MGUMU ZAIDI KIFEDHA .






48. Mheshimiwa Spika, Kambi ya Upinzani inaitaka serikali kutoa majibu ya kina juu ya hali ya shirika letu la ndege na ni kwanini shirika hilo limeendelea kupata matatizo ya kifedha? Tatizo ni nini hasa, Menejiment, hujuma au kuna ufisadi?

49. Mheshimiwa Spika, Kuna taarifa kuwa katika mwaka 2007 kampuni ya ndege Tanzania iliendelea kujiimarisha kwa kukodi ndege nne ambazo kati ya hizo mbili ni za aina ya B737-200 na nyingine aina ya B737-700/800. Kambi ya Upinzani imepata taarifa kuwa ndege zote hizo ni mbovu na zilinunuliwa kifisadi. Sisi tunatoa ‘benefit of doubt’ kwa ATCL na hivyo tunataka maelezo kutoka serikalini kuhusiana na ununuzi wa ndege hizi na hasara ambayo ATCL imepata. Tunahitaji maelezo ya kina na majibu yasiyofinyangwa finyangwa.

50. MHESHIMIWA SPIKA, BAADA YA MCHAKATO WA KUBINAFSISHA ATC SERIKALI ILIUNDA KITU KINACHOITWA ATHCO ILI KUUZA MALI ZA ILIYOKUWA ATC. KATIKA MICHANGO MBALI MBALI YA WABUNGE KAMBI YA UPINZANI HUMU BUNGENI, TULIULIZIA KUHUSU NYUMBA ZA ATC ZILIZOUZWA AMA KUACHWA KINYEMELA KATIKA NCHI MBALIMBALI DUNIANI. TULIHOJI MWAKA 2006/2007 KUHUSIANA NA NYUMBA ZA ATC HUKO JOHANNESBURG, HARARE, LUSAKA, COMORO NA MALI KADHA WA KADHA HUKO OMAN NA RIADH SAUDIA. SERIKALI ILIKIRI KUWAPO KWA MALI HIZO NA KUAHIDI KUTOLEA MAJIBU. MPAKA SASA WATANZANIA HAWAJAPATA MAJIBU KUTOKA SERIKALINI. TUNATAKA KUJUA MALI ZA WATANZANIA HIZI NI NINI HATMA YAKE?

51. Mheshimiwa Spika, Upanuzi wa viwanja vya ndege ni eneo ambalo halijatiliwa mkazo wa kutosha na pia halipewi kipaumbele cha kutosha. Kutokana na kukua kwa kasi ya usafiri wa anga hapa nchini na ikizingatiwa kuwa sekta ya utalii inakua kwa kasi kubwa ,basi haina budi kuboresha viwanja vyetu vya ndege na kuviendesha kibiashara. Hili litawezesha kuvutia watalii wengi kuja nchini moja kwa moja kwani kwa sasa watalii wengi kutoka Ulaya na Marekani huwa wanaishia nchini Kenya kutokana na ubora wa viwanja vyao vya ndege ,na hata mashirika mengi ya kimataifa huwa safari zake zinaishia nchini Kenya na ndipo wanabadilisha ama wanaamua kubakia huko moja kwa moja.

52. Mheshmiwa Spika, Kambi ya Upinzani inapendekeza kuwa sasa ni wakati muafaka tukaamua kutumia terminal 1 kwa ajili ya wasafiri wa ndani na terminal 2 ikatumika kwa ajili ya wasafiri wa nje na hatua hii itawezesha mamlaka husika kuweza kukarabati kiwanja cha Julius Nyerere International Airport na hivyo kuweza kuvutia mashirika mengi ya kimataifa. Pia kama tukiweza kukarabati viwanja vyetu kwa sasa ni wakati muafaka sana kwani kutokana na mashindano ya mpira wa miguu kombe la dunia ambayo kwa mara ya kwanza yatafanyika Barani Afrika mwaka 2010. Lazima tuboreshe viwanja vyetu ili kuhakikisha kuwa timu nyingi zinakuja kuweka kambi nchini na ikizingatiwa kuwa kwa sasa tuna kiwanja cha mpira wa miguu cha kisasa nchini. Kambi ya upinzani inapenda kupata maelezo ya kina kuhusu utayari wa serikali kufaidika na Mashindano ya Kombe la Dunia yatakayofanyika nchini Afrika Kusini miaka miwili ijayo na sekta ya ‘aviation’ imejiandaa vipi.

53. Mheshimiwa Spika, Kambi ya Upinzani inapenda pia kusisitiza umuhimu wa viwanja vya ndege vya pembezoni mwa nchi. Uwanja wa Ndege wa Mwanza na ule wa Kigoma ni viwanja muhimu sana katika eneo la Maziwa makuu. Ni muhimu uwanja wa ndege wa Kigoma ukapewa kipaumbele pekee kwani uwanja huu ukitangazwa vizuri utakuwa ni ‘stop over’ ya ndege kutoka Congo na Burundi kwa ajili ya kuleta abiria Uwanja wa ndege wa Dar es Salaam na kwenda ughaibuni. Mamlaka ya Viwanja vya Ndege iliangalie suala hili kutoa kuweka mkakati wa pekee wa uendeshaji wa uwanja huu ili Taifa lifaidike lakini pia kampuni za ndege nchini nazo zifaidike.

54. Mheshimiwa Spika, Kuna hili suala la ukiritimba wa Kampuni ya Swissport katika viwanja vyetu na hasa uwanja wa ndege wa Dar es Salaam. Zama hizi kuwa na kampuni ya huduma moja katika uwanja ni hatari sana na wala sio tija. Kuna haja kubwa ya kuweka ushindani katika huduma hii katika viwanja vyote vya ndege nchini. Ninamtaka Waziri atengue mara moja ukiritimba huu na kuruhusu ushindani. Hili lifanyike haraka kwani hakuna mantiki hata kidogo kuwa na kampuni moja pekee katika huduma ya mizigo katika viwanja vya ndege.

7. MUHTASARI WA MAPENDEKEZO YA KAMBI YA UPINZANI KATIKA
MAENDELEO YA MIUNDOMBINU.

55. Mheshimiwa Spika, katika kuhitimisha hotuba yangu ninaomba kurejea mapendekezo mahususi ambayo ninayatoa kwa serikali, kwa niaba ya Kambi ya Upinzani, ili kuleta mabadiliko katika eneo la miundombinu ya Tanzania

- SERIKALI IZINGATIE TAARIFA YA HALI YA UMASIKINI KWAMBA SEKTA YA MIUNDOMBINU NA HASA SEKTA NDOGO YA HUDUMA ZA UCHUKUZI NI SEKTA YA KWANZA KIMKAKATI KATIKA KUKUZA UCHUMI WA NCHI ILI KUHUDUMIA NCHI JIRANI ZISIZO NA BANDARI. HIVYO, VIPAUMBELE VYA BARABARA ZIPI ZA KUJENGWA, VIWANJA VIPI VYA NDEGE VYA KUBORESHWA, BANDARI ZIPI KUIMARISHWA LAZIMA VIZINGATIE USHAURI HUO.
- SERIKALI ILETE BUNGENI MPANGO MBADALA WA UJENZI WA MIUNDOMBINU NA KUWA NA MJADALA MPANA WA BUNGE KUHUSU JINSI YA KUGHARAMIA MIUNDOMBINU YETU (FINANCING INFRASTRUCTURE IN TANZANIA FOR DEVELOPMENT). KWA KUSHAURIANA NA KAMATI YA BUNGE YA FEDHA NA UCHUMI NA PIA KAMATI YA BUNGE YA MIUNDOMBINU, SERIKALI IHARAKISHE MCHAKATO WA KUCHUKUA ‘SOVEREIGN BOND’ ILI KUGHARAMIA UJENZI WA MIUNDOMBINU NA KULETA TAARIFA BUNGENI KATIKA MKUTANO WA 13 WA BUNGE LA TISA.
- SERIKALI IAMUE KWA MAKUSUDI KABISA KUIFANYA BANDARI YA DAR ES SALAAM KUWA NI TRANSIT PORT KWA MIZIGO YOTE INAYOKWENDA NCHI ZA ZAMBIA NA MALAWI ( BANDARI YAKE IWE MBEYA), BURUNDI NA CONGO DRC (BANDARI YAKE IWE KIGOMA) NA RWANDA NA UGANDA (BANDARI YAKE IWE SHINYANGA – ISAKA).
- VIWANJA VYA NDEGE VYA MBEYA, MWANZA NA KIGOMA VIBORESHWE KWA HARAKA ILI KUKIDHI HAJA YA UKUAJI WA SEKTA YA UCHUKUZI NA MABADILIKO YATAKAYOLETWA NA MAAMUZI NILIYATAJA HAPO JUU. UWANJA WA NDEGE WA KIGOMA KATIKA SIKU CHACHE ZIJAZO NA KWA MIKAKATI MAALUMU UTAKUWA NI ‘HUB’ YA UKANDA WA MAZIWA MAKUU. UMUHIMU NI HUO HUO KWA MBEYA NA MWANZA.
- KATIKA HALI YA HARAKA SANA NA KWA VYOVYOTE VILE, BARABARA NA RELI KUELEKEA NGARA ZIJENGWE ILI KUHAKIKISHA KUWA UZALISHAJI WA NIKELI UTAKAPOANZA KULE KABANGA KUWE NA MIUNDOMBINU STAHILI NA HUDUMA HII YA MIUNDOMBINU ITAFUNGAMANISHA SEKTA YA MADINI NA SEKTA YA MIUNDOMBINU NA HIVYO TAIFA KUFAIDIKA NA RASILIMALI MADINI NA VILE VILE KUCHOCHEA MAENDELEO YA KIUCHUMI YA ENEO LA ZIWA MAGHARIBI.
- SERIKALI IFIKIRIE KUANZISHA WAKALA WA BARABARA ZA VIJIJINI KATIKA KILA MKOA (RURAL ROADS AGENCY) ILI KUWA NA JUKUMU LA KISHERIA KUJENGA NA KUKARABATI BARABARA ZA VIJIJINI NA KUONDOA JUKUMU HILO KATIKA MAMLAKA ZA SERIKALI ZA MITAA. HII ITAONGEZA UFANISI NA UTAALAMU NA PIA KUPUNGUZA KWA KIASI KIKUBWA GHARAMA ZA UJENZI WA BARABARA (ECONOMIES OF SCALE) BADALA YA SASA AMBAPO KILA HALMASHAURI KATIKA MKOA INAJIJENGEA BARABARA BILA KUWIANA NA MIPANGO YA MAENDELEO YA MIKOA. USHAURI HUU UNAIMARISHA D BY D BADALA YA KUUA KWANI BADO JUKUMU LA BARAZA LA MADIWANI LITAKUWAPO LAKINI WAKALA HUU UTAFANYA KAZI CHINI YA BODI YA BARABARA YA MKOA NA KAMATI YA USHAURI YA MKOA (RCC).
- KAMATI YA BUNGE YA MIUNDOMBINU KWA KUSHIRIKIANA NA KAMATI YA BUNGE YA UWEKEZAJI UMMA (PUBLIC INVESTMENTS COMMITTEE/ POAC) IFANYE TATHMINI YA UBINAFSISHAJI WA TRC NA ATC NA KUHAKIKI MALI ZA MASHIRIKA HAYA NA KULETA TAARIFA BUNGENI ILI KUWEZA KUOKOA BAADHI YA MALI ZA UMMA ZILIZOPOTEA KATIKA ZOEZI HILI KAMA NYUMBA ZA ATC ZILIZOKUWA KATIKA NCHI ZA AFRIKA KUSINI, ZAMBIA, COMORO, ZIMBABWE NA OMAN. VILE VILE MALI ZA TRC KAMA VILE GEREZANI RAILWAY SOCIAL CLUB NK. HII NI KUTOKANA NA ATHCO NA RAHCO KUUZA MALI HIZI KAMA WENDAWAZIMU.
- SERIKALI IACHE KWA SASA MPANGO WOWOTE WA UJENZI WA UWANJA WA NDEGE MPYA NA BADALA YAKE IFANYE MAREKEBISHO MAKUBWA KATIKA TERMINAL ONE YA SASA NA KUANZIA MWAKANI MWEZI JANUARI TERMINAL ONE ITUMIKE KWA NDEGE ZA NDANI NA TERMINAL 2 ITUMIKE KWA NDEGE ZA NJE.

- STESHENI ZA RELI ZOTE KATIKA MIJI MIKUBWA ZISIWE MALI YA TRL NA KAMA IPO HIVYO KATIKA MIKATABA NA IBADILISHWE ILI STESHENI HIZO ZIENDESHWE NA SEKTA BINAFSI ZA KITANZANIA KAMA VITUO VYA KIBIASHARA NA TRL WAPANGE KAMA ILIVYO KATIKA NCHI NYINGINE. HII ITAFANYA MAJENGO HAYA KUTUMIKA KWA UFANISI KWA HIVYO KUKUZA BIASHARA KATIKA MIJI YA DAR ES SALAAM, MOROGORO, DODOMA, TABORA NA KIGOMA KWA KUANZIA. TATHMINI YA KINA IFANYIKE KUHUSU SUALA HILI.
- SERIKALI ITENGUE MARA MOJA UKIRITIMBA WA SWISSPORT KATIKA HUDUMA ZA MIZIGO KATIKA VIWANJA VYA NDEGE VYA TANZANIA NA BADALA YAKE IRUHUSU USHINDANI WENYE TIJA. USHIRIKI WA WATANZANIA UPEWE KIPAUMBELE KATIKA BIASHARA HII.

8. HOJA ZA MAJIBU

56. Mheshimiwa Spika, Kambi ya Upinzania inahitaji majibu katika masuala yafuatayo kutoka Serikalini.

- SERIKALI ILETE TAARIFA BUNGENI KUHUSIANA NA MAPITIO YA MKATABA WA UKODISHWAJI WA UWANJA WA NDEGE WA KIA KWA KAMPUNI YA KADCO ILI TUJUE KAMA KATIKA MAREKEBISHO YA MKATABA MASLAHI YA TAIFA YAMEZINGATIWA. JE, MAPITIO HAYO TAYARI?
- SERIKALI ITOE MAELEZO YA KINA BUNGENI KUHUSIANA NA MASWALI YANAYOULIZWA NA UMMA JUU YA UKODISHWAJI WA NDEGE MBOVU NA ZA GHARAMA KUBWA UNAOFANYWA NA ATCL.
- SERIKALI ITOE MAJIBU ILIYONAYO KUHUSIANA NA MALI ZA ATC ZILIZOKO NJE YA NCHI.
- TANZANIA NA HASA SEKTA YA USAFIRI WA ANGA IMEJIPANGAJE KUHUSIANA NA FURSA ZITAKAZOLETWA NA KUFANYIKA KWA MASHINDANO YA KOMBE LA DUNIA LA MPIRA WA MIGUU HUKO NCHINI AFRIKA YA KUSINI?
- SERIKALI ITOE MAELEZO KUHUSIANA NA MAFAO YA WALIOKUWA NA WAFANYAKAZI WA AMI WAKATI WANAENDESHA BANDARI YA KIGOMA.

HITIMISHO

57. Mheshimiwa Spika, Kambi ya upinzani inatekeleza wajibu wake wa kidemokrasia wa kutoa maoni na hojaji ili Kambi ya chama kinachotawala ifanyie kazi kwa maslahi ya Taifa. Ninawatahadharisha wenzetu kuwa hali ya kisiasa ya nchi imebadilika sana na kwa kasi. Iwapo walio na serikali watashindwa kutekeleza mabadiliko muhimu ya kisera ili kuendena na upepo wa mabadiliko ya kiuchumi wananchi watawapumzisha. Sisi tunasubiri tupewe ridhaa na wananchi ili tutekeleze mipango hii ambayo wenzetu mmeshindwa kutekeleza. Mawazo mbadala tunayo, nguvu ya kutekeleza mawazo haya tunayo na tunaweza!

58. Mheshimiwa Spika, ninashukuru kwa nafasi hii uliyonipa na naomba kuwasilisha.

KABWE ZUBERI ZITTO (MB)
MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI BUNGENI
WIZARA YA MIUNDOMBINU
2 JULAI, 2008
 
Last edited:
. Mheshimiwa Spika, napenda pia kuwashukuru wananchi wa jimbo langu la Kigoma Kaskazini kwa ushirikiano mkubwa wanaonipa katika kazi zangu. Najua kuna changamoto nyingi sana zinazotukabili lakini tumeanza kuona mwanga kwani tayari mkataba wa ujenzi wa Barabara yetu ya Mwandiga – Manyovu na ile ya Kigoma - Kidahwe umesainiwa na ujenzi unatarajiwa kuanza mwaka huu. Tumekuwa Jimbo la Kwanza katika Mkoa wa Kigoma kupata barabara ya lami toka nchi yetu ipate uhuru!. Kufuatia ujenzi wa barabara hii ndugu zetu wa Kasulu Magharibi nao watafaidika na mradi huu kwani barabara hii pia itafika kwao. Kwa niaba ya wananchi wa Kigoma Kaskazini napenda kuishukuru Serikali kwa kutimiza wajibu wake bila kujali itikadi za kisiasa. Ninawataka wananchi wa Kigoma Kaskazini kuhakikisha kuwa wanajiandaa na mabadiliko ya kiuchumi yatakayotokana na ujenzi wa barabara hii na hivyo kushika Ardhi ya kutosha na kuongeza uzalishaji mashambani kwani soko la bidhaa zetu sasa litapanuka. Vilevile wakulima wa Kahawa wa kata za Kalinzi, Mukigo na Bitale waongeze uzalishaji na ubora wa Kahawa yetu uongezeke zaidi kwani sasa gharama za usafiri wa kahawa itapungua kufuatia ujenzi wa barabara hii.


Kauli hii imemkera sana Nsanzuguako na ameamua kumshambulia Zitto wazi wazi ndani ya bunge wakati akichangia hotuba ,na ameamua kumvaa na hata Zitto alipoomba muongozo wa Spika alipigwa danadana .

Ila ukweli ni kuwa hii ndio barabara pekee itajengwa Kigoma na hii ipo Jimboni kwa Zitto.
 
. Mheshimiwa Spika, napenda pia kuwashukuru wananchi wa jimbo langu la Kigoma Kaskazini kwa ushirikiano mkubwa wanaonipa katika kazi zangu. Najua kuna changamoto nyingi sana zinazotukabili lakini tumeanza kuona mwanga kwani tayari mkataba wa ujenzi wa Barabara yetu ya Mwandiga – Manyovu na ile ya Kigoma - Kidahwe umesainiwa na ujenzi unatarajiwa kuanza mwaka huu. Tumekuwa Jimbo la Kwanza katika Mkoa wa Kigoma kupata barabara ya lami toka nchi yetu ipate uhuru!. Kufuatia ujenzi wa barabara hii ndugu zetu wa Kasulu Magharibi nao watafaidika na mradi huu kwani barabara hii pia itafika kwao. Kwa niaba ya wananchi wa Kigoma Kaskazini napenda kuishukuru Serikali kwa kutimiza wajibu wake bila kujali itikadi za kisiasa. Ninawataka wananchi wa Kigoma Kaskazini kuhakikisha kuwa wanajiandaa na mabadiliko ya kiuchumi yatakayotokana na ujenzi wa barabara hii na hivyo kushika Ardhi ya kutosha na kuongeza uzalishaji mashambani kwani soko la bidhaa zetu sasa litapanuka. Vilevile wakulima wa Kahawa wa kata za Kalinzi, Mukigo na Bitale waongeze uzalishaji na ubora wa Kahawa yetu uongezeke zaidi kwani sasa gharama za usafiri wa kahawa itapungua kufuatia ujenzi wa barabara hii.


Kauli hii imemkera sana Nsanzuguako na ameamua kumshambulia Zitto wazi wazi ndani ya bunge wakati akichangia hotuba ,na ameamua kumvaa na hata Zitto alipoomba muongozo wa Spika alipigwa danadana .

Ila ukweli ni kuwa hii ndio barabara pekee itajengwa Kigoma na hii ipo Jimboni kwa Zitto.
Kwa kweli wakati mwingine ukiangalia bunge unapatwa na hasira sana.Binafsi nimesindwa kumwelewa Mh Nsazugwako alipoamua kumshambulia mbunge mwenzake tena kwa maneno ya kashfa kwa kusema mbunge wa miaka miwili hawezi kujenga barabara hii inaonyesha ni kwa jinsi gani wabunge wanavyowadharau wabunge majuniour.Sijui ni hasira ya kutolewa kwenye baraza la mawaziri mimi sijui.Ila kwa wenye macho na masikio watajua ni nani anawafaa kuwa kiongozi wao.Binafsi mefuatilia bunge na nimesoma tena hii hotuba ya kambi ya upinzani hapa JF.sijaona mahali wamesema tofauti na wananchi tunavyotaka nchi yetu iwe jamani.
 
Hotuba imetulai...nimependezwa sana na mapendekezo ya upinzani hasa kwenye kufanya bandari ya Dar iwe "Transit Port" kwa nchi jirani. Bila ubishi wowote foleni itapungua sana pale bandarini sababu makontena yatakayokuwa yanatumiwa kwa undani ni yale yanayoishia Tanzania peke yake. Pia, nina imani wakazi wa Congo, Rwanda, Burundi, Zambia etc watavutiwa zaidi kuitumia bandari yetu iwapo Mizigo yao wataifuatana na kuishughulikia Mipakani mwa nchi zao na Tanzania badala ya kuwa Dar es salaam.

Sikulijua Hili: Barabara ya Mwandiga – Manyovu na Kigoma - Kidahwe ndizo Barabara za KWANZA kuweka Lami mkoani Kigoma..TANGU 1961..!!!

Hongera Upinzani...
 
Jenarali Ulimwengu anamfahamu vizuri sana huyu mbunge wa Kasulu mashariki. Kwa kifupi ni mtu aliyejaa wivu sana na a very dangerous person !
 
Kwa kweli wakati mwingine ukiangalia bunge unapatwa na hasira sana.Binafsi nimesindwa kumwelewa Mh Nsazugwako alipoamua kumshambulia mbunge mwenzake tena kwa maneno ya kashfa kwa kusema mbunge wa miaka miwili hawezi kujenga barabara hii inaonyesha ni kwa jinsi gani wabunge wanavyowadharau wabunge majuniour.Sijui ni hasira ya kutolewa kwenye baraza la mawaziri mimi sijui.Ila kwa wenye macho na masikio watajua ni nani anawafaa kuwa kiongozi wao.Binafsi mefuatilia bunge na nimesoma tena hii hotuba ya kambi ya upinzani hapa JF.sijaona mahali wamesema tofauti na wananchi tunavyotaka nchi yetu iwe jamani.


Maneno haya ya Mhe Nsazugwanko yanaonyesha jinsi wabunge wa CCM wanavyohamaki kufuatia mafanikio ya Upinzani. Wache waendelee kuhamaki; anayefaidika na hiyo barabara ni Wananchi wa Kigoma Kaskazini...na sio wa South Afrika wala Canada.
 
Hotuba imetulia kwa kweli.
Mmeona alivyo imulika hiyo ATC?hapo sasa kama kutakuwa hakuna majibu ya kuridhisha tunaomba wahusika wa hicho kitengo mtuleteee hapa hapa JF data ili tuweze kulipua uozu huku kwenye ndege maana sasa imekuwa kero hadi pesa ya mafuta hawana.Dah aibu sana.
 
kwakweli naomba wote muitikie hiki nisemacho tena kwa sauti kubwa UPINZANI OYEEEEEEEEEE!!!!!!

HII HOTUBA IMEKAMILIKA NA VILIVYOONGEWA VYOTE NI VYA MUHIMU KWA NCHI NA MSLAHI YA WATZ KWA UJUMLA KWANINI WATU HATUONI JAMANI? HIVI NDIO VICHWA VINAVYOTAKIWA KUTUONGOZA.

NDIO MAANA IKIFIKA ZAMU YA ZITTO AU SLAA BUNGENI ANAEPIGWA SWALI UNAMUHISI ANATETEMEKA KWAKUJUA ATAPIGWA MASWALI YA UKWELI NA AMBAYO HATA MAJIBU YAKE INAWEZEKANA ASIWE NAYO SAAAAAAAFIIIIIIIII.

SASA HIVI BUNGE LINALETA HATA RAHA KULISIKILIZA NA KUFUATILIA, KAMA KAWA SIKU MOJA KITAELEWEKA TUU.
 



Maneno haya ya Mhe Nsazugwanko yanaonyesha jinsi wabunge wa CCM wanavyohamaki kufuatia mafanikio ya Upinzani. Wache waendelee kuhamaki; anayefaidika na hiyo barabara ni Wananchi wa Kigoma Kaskazini...na sio wa South Afrika wala Canada.

mimi nilishasema tatizo lao wengi ni mambumbumbu yaana wana mamidomo ya kuongea tu lakini vichwa vyao ni nyumba za macho, wana upeo mdogo sana wa kufikiri halafu hawajui kuwa kila kukicha mambo hubadilika,wanafikiri waliumbwa waishi milele na ubunge wao
 
Eti hata Komba anajifanya kumshambulia Zitto leo ,wakati huyu anajua kutunga taarabu tuu kila siku.
 
Huyu mzee anapaswa kutambua kuwa "Ukubwa wa pua si wingi wa Kamasi". Haijalishi uzoefu bali uko pale umefanya nini hata kama ni mbunge wa mwaka mmoja. Kwa kweli binafsi Mhe. Zitto, Dr. Slaa/Upinzani wananitia moyo sana. Uchaguzi ujao tunatakiwa tukaribishe MOVEMENT FOR CHANGE.
 
Safi sana Mhe. Zitto, sisi vijana wenzenu pamoja na Mungu tuko pamoja. Najua unavyojua kujipanga, kile kiporo kuhusu Meremeta bado hakijaeleweka mkuu, ikiwezekana kiwekewe hoja binafsi kabisa ili kianikwe. Tuko pamoja
 
Sasa kama habari za barabara ya lami si kweli si Waziri ataonesha kuwa si kweli; tatizo la baadhi ya wabunge ni sense of entitlement... kana kwamba nchi ni ya kwao wao wenyewe.
 
Hongera sana Mh. zitto kwa hotuba iliyotulia. Ushauri wangu ni kwamba maswali uliyouliza ni ya msingi sana usikubali yapite hivihivi bila majibu ya kueleweka. Ile hotuba ya Mh. Dr Slaa ilikuwa nzuri hivihivi na maswali yake yalikuwa ya msingi lakini majibu yake mimi sikurizika nayo sasa naomba kwa hii ya zitto pia tujitahidi kuwabana mpaka majibu yawe ya uhakika. tusikubali ya funika kombe....................................!
 
Cha "kufurahisha" kuna watu watatwambia kwamba wapinzani hawajawa tayari kutawala, hwana sera, etc ebo!!
 
Cha "kufurahisha" kuna watu watatwambia kwamba wapinzani hawajawa tayari kutawala, hwana sera, etc ebo!!

Kwa kweli tu tayari.......... tulichosema leo ni 'policy statement' ya maendeleo ya miundombinu nchini. Tunaweza, yes we can.......
 
Zitto amejitahidi na hilo ndilo la kuweka vichwani mwetu... Kuhusu yule Nsazug****o; hatuna cha kukumbuka baala ya mazungumzo yake. hiyo ni ishara tosha kwamba baadhi ya wabunge wa CCM wangekua wanaa kimya tu!!! kwani huaibsha chama na wenzao wa maana.

Hivi huyu Nsa*******ko aliwahi kuongoza wapi vile?
 
Zitto,

..bandari ya DSM ni IN-EFFICIENT. nadhani tatizo hilo linapelekea reli zetu kukosa mizigo.

..kuna article nimesoma inazungumzia Wacongo kusafirisha shaba yao kupitia bandari za Afrika kusini. wako radhi wasafiri umbali mrefu kuliko uzembe ulioko bandari ya DSM.

..halafu tukumbuke kwamba kuna reli/bandari za Angola na Mozambique ambazo zimekuwa hazitumiki kutokana na vita.

..kutokana na vita kuisha, na oil boom, Angola sasa hivi ana pesa kama mwendawazimu. nina hakika atafungua reli na bandari zake kwa soko la Zambia na Watanzania lazima tujipange.

..kuna ramani inaonyesha reli toka Lubumbasi inaingia Zambia mpaka Kapiri-Mposhi. Hiyo inamaanisha unaweza kusafiri toka Lubumbashi mpaka Dar kwa reli.


Kitila Mkumbo,

..kama CHACHA WANGWE ni Makamu wa Mwenyekiti wa Chadema basi kwa kweli hamko tayari kuongoza nchi.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom