Hotuba ya Mhe. Mbowe ina ubora kuzidi hotuba zote tangu mwaka 1995!

Makala Jr

JF-Expert Member
Aug 25, 2011
3,395
1,110
Hakika kwa kila mmoja aliyepata kushuhudia hotuba ya Mhe.Mbowe katika mkutano wa kumkaribisha aliyekuwa Waziri Mkuu wa awamu ya nne Mhe.Edward Ngoyai Lowassa ametoa hotuba bora sana. Kwa wale waliodhani kiwango cha elimu ni kipimo cha ustaarabu, hekima na uelewa basi leo Mhe.Mbowe amethibitisha kwamba anaweza. Hotuba imejaa ukweli, haja ya msamaha na mabadiliko, mwanzo mpya wa kifikra katika vichwa vya raia na mwongozo safi kwa wanachama wa CHADEMA na UKAWA. Hongera sana Kamanda Mbowe,nimekuelewa na umenifungua katika namna ya kucheza siasa.

Pia nimshukuru kipekee Mhe.Lowassa kwa kunitoa wasiwasi, ameanika ukweli wake kuhusu usafi wake na namna alivyobambikiziwa kashfa ya RICHMOND. PEOPLEEEES!
Nimesikiliza kwa makini sana, nimerudia tena na tena, nimewasiliana na rafiki zangu ambao mwanzo walisita kulainisha mioyo yao kumpokea ndugu Edward na mwisho wa siku nimeona niseme tu kuwa speech ya Mbowe iligusa mioyo ya watanzania na kukiri kuwa inaweza kuchukua tena zaidi ya karne kupata tena speech kama hiyo. Hakika Mbowe umekomaa kisiasa, matendo yako yanaonesha dhamira ya dhati ya ukombozi, umeweka mbele maslahi ya taifa kwelikweli.

Nilivutiwa zaidi pale aliposema kuwa "mwanachama aliyejiunga leo hana tofauti na yule aliyejiunga miaka 20 iliyopita...si chama cha kugawana vyeo bali kupeana majukumu kulingana na taaluma na uwezo wako"

Nisiongee mengi...tafuta ile speech uisikilize tena!
 
Safi sanaaaa

11221345_742060975904529_1389171789283824097_n.jpg
 
naomba utuwekee clip ya hiyo hotuba, wengine huku umeme walikuwa wamechukua
 
Hotuba ile kaandikiww na Apson Mwang'onda. Yeye mwenyewe hata kuongea hajui
 
I salute Mhe Mbowe.... the best political figure in Tanzania... akifuatiwa na Mhe Mbatia.".. nawahusudu hawa jamaa sana
na hajasoma hiyo hotuba yake but imepangilika sana....

ccm kazi wanayo mwaka huu
 
Back
Top Bottom