Hotuba ya mh. Kikweta ya mwisho wa Mwezi Feb. 2006 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hotuba ya mh. Kikweta ya mwisho wa Mwezi Feb. 2006

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by victor11, Jun 30, 2011.

 1. v

  victor11 Member

  #1
  Jun 30, 2011
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 68
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Ndugu Wananchi:Hali ya umeme nchini kwa hivi sasa ni mbaya zaidi kuliko ilivyokuwa tarehe 31 Januari, 2006. Mgao wa umeme niliosema siku ile kuwa unaweza kuanza wakati wowote umeanza na unaendelea kwa karibu wiki ya nne sasa. Tena, basi, mgao ulioanza kwa kuzima umeme kwa saa nane na nusu kwa siku sasa umeongezeka na kuwa saa 16. Hali imekuwa hivyo kutokana na kushuka zaidi kwa uzalishaji wa umeme kwenye vituo vyetu karibu vyote. Uzalishaji wa umeme umekuwa mdogo zaidi kwa sababu ya maji katika mabwawa yetu kupungua zaidi ya ilivyokuwa mwanzoni. Hivi majuzi nilitembelea mabwawa ya Mtera na Kihansi yanayotumika kuzalisha sehemu kubwa ya umeme tunaoutumia nchini. Hali ni mbaya sana. Bwawa la Mtera linalotegemewa kwa ajili ya kuhifadhi maji ya kuzalishia umeme Kidatu lina maji kidogo sana. Hakuna matarajio ya bwawa hilo kujaa kwa mvua za masika za mwaka huu, labda tupate mvua kubwa zisizokuwa za kawaida. Lakini, kwa mvua za kawaida itachukua misimu kadhaa ya mvua nzuri ndipo tuweze kufidia upungufu wa kina cha mita 11 uliopo sasa.Kama nilivyosema, hali ya mabwawa yote siyo nzuri na imesababisha kupungua sana kwa uzalishaji wa umeme kama ifuatavyo:- [TABLE="class: MsoTableGrid"]
  [TR]
  [TD]KITUO
  [/TD]
  [TD="width: 148"]UWEZO
  [/TD]
  [TD="width: 108"]

  TAREHE31/01/2006
  [/TD]
  [TD="width: 96"]

  TAREHE 26/2/2006
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 148"]Kidatu
  [/TD]
  [TD="width: 148"]Megawati 204
  [/TD]
  [TD="width: 108"]

  101​
  [/TD]
  [TD="width: 96"]

  26​
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 148"]Mtera
  [/TD]
  [TD="width: 148"]Megawati 80
  [/TD]
  [TD="width: 108"]

  29​
  [/TD]
  [TD="width: 96"]

  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 148"]Hale
  [/TD]
  [TD="width: 148"]Megawati 21
  [/TD]
  [TD="width: 108"]

  4.1​
  [/TD]
  [TD="width: 96"]

  4​
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 148"]Pangani Falls
  [/TD]
  [TD="width: 148"]Megawati 68
  [/TD]
  [TD="width: 108"]

  15.6​
  [/TD]
  [TD="width: 96"]

  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 148"]Nyumba ya Mungu
  [/TD]
  [TD="width: 148"]Megawati 8
  [/TD]
  [TD="width: 108"]

  2.5​
  [/TD]
  [TD="width: 96"]

  2.5​
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 148"]Kihansi
  [/TD]
  [TD="width: 148"]Megawati 180
  [/TD]
  [TD="width: 108"]

  15.3​
  [/TD]
  [TD="width: 96"]

  18​
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="width: 148"]JUMLA
  [/TD]
  [TD="width: 148"]Megawati 561
  [/TD]
  [TD="width: 108"]

  167.5​
  [/TD]
  [TD="width: 96"]

  50.5​
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]

  Kutokana na kupungua kupita kiasi kwa umeme unaotokana na nguvu ya maji, mfumo wa umeme nchini sasa unategemea na, kwa kweli, unahimiliwa na umeme unaotokana na gesi asilia ya Songosongo na mafuta ya dizeli. Kituo cha Songas kinachotumia gesi kinatoa megawati 190 na cha IPTL kinachotumia dizeli kinatoa megawati 100. Bahati mbaya sana, wiki iliyopita transfoma ya Kampuni ya Songas inayoendesha mashine mbili zinazozalisha megawati 75 ilipata hitilafu na kusababisha umeme huo kukosekana. Hitilafu hiyo imefanya hali ya upatikanaji umeme ambayo tayari ni mbaya kuwa mbaya zaidi. Matokeo yake ni makali ya mgao kuongezeka. Matengenezo ya transfoma hiyo yanaendelea na huenda baada ya siku si nyingi itatengemaa na kuleta nafuu tunayoihitaji sana. Ndugu Wananchi:Serikali kwa kushirikiana na TANESCO na wadau wengine tumekuwa tunachukua hatua mbalimbali kwa lengo la kupunguza makali ya tatizo la mgao wa umeme. Wakati huo huo tumekuwa na malengo ya muda wa kati na muda mrefu ya kupata jawabu la kudumu kwa matatizo ya umeme nchini. Kwa nia ya kupunguza makali ya mgao wa umeme tunafanya mipango ya kupata jenereta za kukodi kutoka nje ili kuziba pengo ililopo. Mazungumzo yanaendelea kati ya TANESCO na makampuni yaliyojitokeza kutaka kukodisha jenereta hizo kwa TANESCO. Kwa upande wetu Serikali tuko tayari kwa hali na mali kuiwezesha TANESCO kukodi jenereta hizo.Ndugu Wananchi: Kwa upande wa kutafuta ufumbuzi wa kudumu wa tatizo la umeme nchini, ipo mikakati mbalimbali ambayo kimsingi inalenga kupunguza kutegemea mno umeme unaotokana na nguvu ya maji. Hii ni mara ya tatu sasa tatizo la aina hii linatukuta. Bahati nzuri nchi yetu imejaliwa kuwa na gesi ya kutosha huko Songosongo na Mtwara. Pia tuna rasilimali kubwa ya makaa ya mawe huko Kiwira na Mchuchuma. Hivyo basi, tumeamua kuanza kuchukua hatua za dhati za kuongeza kiasi cha umeme nchini unaotokana na gesi asilia na makaa ya mawe. Katika hatua za muda wa kati, tunakusudia kuongeza jenereta ya kuzalisha umeme wa megawati 60 utokanao na gesi katika Kituo cha Umeme cha Ubungo na megawati 45 huko Tegeta. Wakati huo huo tunaanza mipango ya kuzalisha megawati 200 za umeme kwa kutumia makaa ya mawe ya Kiwira. Pia, tumeanza mikakati ya kujenga kituo kikubwa cha kuzalisha megawati 300 za umeme huko Kinyerezi, wilayani Ilala kwa kutumia gesi ya Songosongo. Ndugu Wananchi: Mikakati na mipango yote hii ni ya gharama kubwa, lakini Serikali imeamua kufanya kila iwezalo kuiwezesha TANESCO kuifanikisha. Tuko tayari kutumia fedha zetu na kuomba kwa washirika wetu wa maendeleo kutusaidia. Bahati nzuri Waholanzi walishakubali kutusaidia kugharamia mradi wa megawati 45 za pale Tegeta. Hivi majuzi tena Shirika la Fedha la Kimataifa limekubali tutumie fedha za msamaha wa madeni kununulia mitambo ya kuzalisha umeme kwa kutumia gesi. Pia wametukubalia kutumia fedha hizo kugharamia kukodisha mitambo ya kuzalisha umeme wa dharura na kununulia chakula cha njaa. Napenda kutumia nafasi hii kuwashukuru sana marafiki zetu wa Uholanzi na Shirika la Fedha la Kimataifa kwa msaada wao huo na moyo wao wa upendo. Msaada huo umetolewa wakati ambapo unahitajika kweli kweli.
  www.tanzania.go.tz/Presidential Library/Presidential Speeches
   
 2. Revolutionary

  Revolutionary JF-Expert Member

  #2
  Jun 30, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 457
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Ndio utajua kwamba tuna rais au hatuna!
   
 3. v

  victor11 Member

  #3
  Jun 30, 2011
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 68
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  I decided to this cut with members just for you to see how we are moved arround like a piece of wood.
  So imaging since then todate we are still hearing stories of megawat but nothing substatial is happening.
   
 4. kongomboli

  kongomboli Senior Member

  #4
  Jun 30, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 154
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Yani mshkaji kaelezea vilevile kama wkt anaingia ikulu 2005,maneno yaleyale na michakato ya muda mfupi na muda mrefu.Me nadhan muda mwafaka ndo huu wa kumwagiza RA akatuletee mitambo bora zaidi.ZIDUMU FIKRA ZA MWENYEKITI!
   
 5. Ndallo

  Ndallo JF-Expert Member

  #5
  Jun 30, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 7,129
  Likes Received: 1,083
  Trophy Points: 280
  Raisi wa nchi hii natumaini atakapoingia uzeeni baada ya kumaliza kipindi chake natumaini wajukuu zake watamfurahia sana kwa umakini wake wa HADISI! HADISI! HADISI NJOO UONGO NJOO! UTAMU KOLEA!
   
 6. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #6
  Jun 30, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Mkuu wakaya kaenda kutafuta wahisani ktk hili teh! IFIKAPO 2013 HAKUTAKUA NA MGAO WA UMEME! Thubutu!
   
 7. Kimilidzo

  Kimilidzo JF-Expert Member

  #7
  Jun 30, 2011
  Joined: Jan 3, 2011
  Messages: 1,346
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 135
  Hii nchi iko mikononi mwa msanii...

  Ukitulia hapo ukafuatilia mahesabu ya megawatt aliyoyapiga mshkaji unaweza kudhani ukirudi home leo baada ya kazi utakuta kuna mwanga. Halafu hizo porojo zote si hata Ngeleja kazieleza juzi tu hapa...

  Mbaya zaidi msanii ( Rais) hajaja na suluhisho la kudumu zaidi ya kuzidi kutegemea umeme wa kuunga unga...

  Na mbaya zaidi yake anaona kama kutumia fedha zetu kumaliza tatizo la umeme ni dhambi ndio maana katoa hii kauli ''Tuko tayari kutumia fedha zetu na kuomba kwa washirika wetu wa maendeleo kutusaidia...
   
 8. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #8
  Jun 30, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 163
  Trophy Points: 160
  Kikwete OYE..CCM OYE...!
   
Loading...