Hotuba ya Mbowe mkoani Iringa; Asema CHADEMA inachokozwa, ataja bendera ya CCM

CCM hovyo sana utakuta huo mwenge wao unaaenda kwenye tassisi binafsi wa mibendera yao ya kijani ila watu wanapotezea .

Ofisi za umma mezani wameweka ilani utadhani ni ofisi za CCM bado watu wanapotezea tu.
 
Nafikiri Chademqa sometimes wa ignore vitu vidogo vidogo wajikite kwenye main issues

Vibendera tu ndivyo kuvigeuza main issue ya media attention?
Mfano Kesho utakuta vichwa vya habari magazetini vinasema magari ya Chadema yashushwa bendera na Polisi !!! Habari ya Mbowe kahutubia nini hawaandiki

Wangeyashusha chap chap bila mtafaruku ili media zijikite zaidi kwenye alichosema Mbowe

Washaharibu vichwa vya habari vya magazeti Kesho

Vizuri Chadema kwenye siasa kujua main issue ni ipi na minor ni ipi?
Swala la kufanya hivyo vibendera kuwa main issue hawajitetendei haki wenyewe
Ujinga ni kuona kawaida kwa bendera za chadema kushusha ila sio kawaida kwa bendera za ccm kutapakaa Kila Kona ya Nchi!!. Police ccm Wana utindio wa ubongo.
 
Tatizo kubwa tulilo nalo nchini ni kwamba sehemu kubwa sana ya wananchi hawafahamu maana ya Demokrasia ya Vyama vingi. Tatizo hili linajithihirisha zaidi kwenye Taasisi mbali mbali ikiwemo Mahakama, Polisi, tume za uchaguzi, Msajili wa vyama na hata ndani ya vyama vya upinzani na zaidi ndani ya chama tawala. Hii ni shida kubwa tuliyo nayo Tanzania.
 
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyoandaliwa na Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha) mkoani Iringa

Sehemu ya kauli za Mbowe katika hotuba yake:
"Tumekataa kuwa chama cha tamaa za fedha na uongozi, hata watu tuliokuwa nao walipojaribu kuwa na tamaa hizo, tuliwaachia waondoke."

"Kila mmoja ana mchango katika Chadema, na asitokee mtu kusema ni kazi ya Mbowe, ni kazi ya kila mmoja wetu waliopo hai na waliotangulia mbele za haki. Kadiri watakavyotumia nguvu dhidi ya CHADEMA wajue kuwa wanazidi kutuimarisha zaidi na zaidi"

"Nguvu yetu ya umma tuliyokuwa nayo, tumeheshimishwa na kuaminiwa kwa nguvu hii, wenzetu wanaheshimishwa na nguvu ya dola.

“Nilipokuwa njiani nakuja Iringa nilipata taarifa kuwa kuna kamanda ametoa gizo bendera za Chadema zishushwe, nikiwa njiani nakaribia nikaona bendera nyingi za CCM, nikisema tunaandama kulalamika kitendo hicho watasema nani mchokozi?

“Tumevumilia sana, nawaomba tuendelee kuvumilia, kiongozi wa kisiasa hasa kwa nafasi kama yangu kuna wakati unatakiwa kufanya maamuzi magumu.

“Kabla sijakamatwa nilimuandikia Rais Samia barua mbili nikiomba tukutane naye, sikuweza kukutana naye muda ule kabla ya kuingia gerezani licha ya kuwa alijibu barua yetu ya kuridhia kukutana nasi vyama vya upinzani.

“Niliomba kukutana na Rais aliyepita (kabla ya Samia) lakini haikuwezekana.

“Nilikutana na Magufuli katika matukio mengine lakini siyo kikao cha kazi, wakati kila mmoja alikuwa anamuogopa, mimi nilitaka kumwamba ukweli.

“Nilisema nitamwambia lakini hakunipa hiyo nafasi.

“Rais wa mwisho ambaye tulikaa naye kikao cha kazi ni Kikwete, tumetafuta nafasi ya kuonana na viongozi kwa kuwa tunajua Wanachadema mioyoni mwenu mmebeba nini.

“Ndiyo maana nilipopata nafasi ya kuonana na Rais siku ileile nilipotoka sikutaka kufikiria mara mbili.

“Namshukuru Rais kwa kunipa nafasi hiyo ya kukutana naye, kwa kuwa mimi mwenyewe nilikuwa najiuliza nitoke kwa nafasi ipi baada ya kutoka gerezani.

“Nashukuru mazungumzo yetu yalienda vizuri, nampa hongera kwa kutamua nafasi ya Chadema kama chama kikuu cha upinzani.

“Rais Samia amekuwa Rais wa kwanza tangu kupata uhuru kwa nchi hii kusimama na chama cha upinzani kuzungumza Pamoja lengo likiwa moja kuondoa maumivu katika taifa hili.

“Aliniambia nimueleze Chadema tuna shida gani, nikamwambia sijaenda kumwambia shida, muhimu kwanza ni kujenga msingi wa uvumbuzi wa haki za Watanzania.

“Nilimuomba mama tuzungumze kuhusu haki, kwa kuwa kuendelea kuhubiri amani amani wakati watu wetu wanapigwa risasi si sawa.

“Namshukuru, Waswahili tunasema ‘Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni’

“Nikamwambia mama tuyafanya haya kwa vitendo na siyo maneno, akasema nia yake ni ya kweli. Nikamwambia kuwa Chadema hatujawahi kuwa na nia mbaya, tunataka Serikali iwajibike na wananchi wawe na neema ya kweli, watuachie sisi nafasi yetu kama wapinzani, tuijenge demokrasia, mambo yafanyike kwa uwazi na siyo kwa ukandamizaji.

“Tukakubaliana tutaweka taratibu. Niwaulize Wanachadema kuwa nilikosea wapi?

"Watanzania wana hofu hasa Wanachadema wana hofu sana, ningekuwa ni mjinga kwa kiwango cha lami, kama nafasi tunayoitafuta ya kuweka mambo sawa nisiitumie.

“Tunataka wanachama wa vyama vyote wafanye kazi yao kwa haki, vyombo vya dola vifanye haki.

“Hiki kinachofanyika (polisi Iringa kushusha bendera za Chadema) sicho tulichokubaliana na mama.

“Taharuki iliyojitokeza kwa mimi kwenda Ikulu ni kielelezi kwa jinsi hali ilivyo ya kutoaminiana kama taifa. Mchakato wa kutafuta amani ya taifa siyo jambo la siku moja.

“Wengine wanahisi mimi kwenda kuzungumza na mama Ikulu labda Chadema watakuja kutuambia kuacha habari za Katika. Chadema siyo Mbowe.

“Wengine wanaiambia nikitaka nieleweke nielezea kila kitu nilichozungumza na Rais, haiwezekani, kila jambo lina muda wake, hata Makamu Mwenyekiti alivyokutana na Rais hakuzungumza kila kitu.

“Unatakiwa kuhifadhi chakula, sina nia ya kuwalisha chakula kibichi, lazima ufanye mambo taratibu.

“Mimi nimekaa kwenye chama hiki kwa miaka 30 ya shuruba, ningekuwa nina haraka nisingefika hapa. Wiki moja ijayo tutakaa kikao cha kamati kuu, baada ya hapo tutaendelea kupakua chakula kidogo kidogo kwa uhitaji utakavyokuwa.

“Nikiwa gerezani nilijulishwa mambo kadhaa yanayoendelea kuhusu Chadema ikiwemo makongamano…

“Bila kujenga uwezo wetu wa ndani tutakuwa tunagombanishwa, hatutakiwi kutegemea ruzuku.

“Ningewachangia lakini tangu nimetok gerezani sina simu wala kompyuta, wakubwa hawajanirudishia.
Kweshnei!
 
Ukweli ni kuwa Mbowe ni mwanasiasa mkongwe na anajua kuchanga karata
 
Nafikiri Chademqa sometimes wa ignore vitu vidogo vidogo wajikite kwenye main issues

Vibendera tu ndivyo kuvigeuza main issue ya media attention?
Mfano Kesho utakuta vichwa vya habari magazetini vinasema magari ya Chadema yashushwa bendera na Polisi !!! Habari ya Mbowe kahutubia nini hawaandiki

Wangeyashusha chap chap bila mtafaruku ili media zijikite zaidi kwenye alichosema Mbowe

Washaharibu vichwa vya habari vya magazeti Kesho

Vizuri Chadema kwenye siasa kujua main issue ni ipi na minor ni ipi?
Swala la kufanya hivyo vibendera kuwa main issue hawajitetendei haki wenyewe
Aliyetakiwa ku ignore hilo swala la bendera ni jeshi la polisi kwasababu wao ndio waliotumia kodi na rasilimali za nchi kwenye mambo yasiyo na msingi.dunia ya leo wanaangaika na bendera za chama zisizoleta impact yoyote.Chadema wanachotaka ni haki kwasababu hawajavunja sheria yoyote mambo yakuandikwa kwenye magazeti hilo sio la msingi maana mitandao iko kila kona sasa hivi.
 
Aliyetakiwa ku ignore hilo swala la bendera ni jeshi la polisi kwasababu wao ndio waliotumia kodi na rasilimali za nchi kwenye mambo yasiyo na msingi.dunia ya leo wanaangaika na bendera za chama zisizoleta impact yoyote.Chadema wanachotaka ni haki kwasababu hawajavunja sheria yoyote mambo yakuandikwa kwenye magazeti hilo sio la msingi maana mitandao iko kila kona sasa hivi.
We poyoyo kweli. Chadema wanaijua haki zaidi ya kujaza matumbo?

Sent from my Infinix X688B using JamiiForums mobile app
 
Kwaleo sijaelewa kitu kwamara yakwanza toka namfahamu mbowe Leo ndo sijamwelewa ngoja tusubirie hotuba baada ya kikao chakamati kuu
Usiishi kwa kutegemea kupewa,kupata,kisikia au kuona unachokitegemea tu.Tegemea chochote,wakati wowote na mahali popote.Ndiyo ukubwa.
 
Back
Top Bottom