Hotuba ya mbowe mazishi ya Makani imebeba uzito stahiki unaofikirisha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hotuba ya mbowe mazishi ya Makani imebeba uzito stahiki unaofikirisha

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, Jun 14, 2012.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Jun 14, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160

  [​IMG]

  Mbowe apasua jipu kwenye mazishi ya Makani

  Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, amewaonya wanasiasa wanaopenda kutumia propaganda chafu za udini kwa manufaa ya muda mfupi ya kisiasa ya vyama vyao kwa gharama ya kuwagawanya Watanzania na kulibomoa taifa lao.

  Amesema kuwa amekuwa akishangazwa na unyenyekevu, ukaribu na ushirikiano unaooneshwa baina ya wanasiasa na viongozi mbalimbali wa kiserikali wakati wa misiba, lakini huonekana kusahahu kila kitu mara baada ya misiba na kuendekeza propaganda za udini na ukabila, badala ya kuweka mbele utaifa.

  Akizungumza wakati wa kutoa salaam za rambimrambi kwa niaba ya Chadema mara baada ya mazishi ya mmoja wa wanasiasa wa chama hicho, Bob Mkani Makani, jana katika kijijini Ukenyenge, wilayani Kishapu, Mbowe alisema marehemu alikuwa mtu mzuri aliyejitoa kwa hali na mali kwa ajili ya Watanzania.

  “Kwa ujumla niseme tu kuwa siwezi kutumia dakika tano hizi kumaliza kuzungumzia sifa za Bob, lakini niseme kuwa nimekuwa nashangazwa na unyenyekevu huu unaooneshwa wakati wa misiba pekee, wakati wa misiba kunakuwa na ukaribu na ushirikiano wa hali ya juu, lakini tunakuwa wepesi sana tunasahau punde tu…baada ya msiba tunarudi kunyukana tena kwa kutumia na kutanguliza propaganda mbalimbali zikiwemo za udini,” alisema na kuongeza:

  “Mathalani leo wengine hapa walijua Bob ni Mkristo, kumbe Bob ni Mwislamu, lakini tumekuwa tunatumia propaganda nyepesi za udini tunaharibu historia makusudi kwa maslahi yetu mafupi ya kisiasa bila kujua kuwa wakati huo huo tunalibomoa taifa letu katika misingi ya udini.”

  “Leo tumekaa wote hapa, watu wa dini mbalimbali, tuna viongozi wetu hapa wa dini mbalimbali, tumekaa pamoja kabisa tumevumiliana, wapo watu wa makabila mbalimbali…hakuna tatizo lolote kabisa, kwa sababu sisi hatupaswi kutambulishwa kwa makabila wala dini zetu bali tunatambulishwa kwa utaifa na Utanzania wetu basi,” aliongeza.

  “Napenda kutoa hii rai leo kwa viongozi wa dini zote walioko mahali hapa, kwa viongozi wote wa vyama vya siasa na kwa viongozi wa serikali, vyama hivi vya siasa ni vitu vya kupita, tusibomoe utaifa wetu kwa bendera za vyama vyetu. Vyama vyote hivi Chadema na CCM vitapita, lakini Watanzania na nchi yao watabaki,” alisema Mbowe huku waombolezaji wakishindwa kujizuia kumpigia makofi mengi.

  Mbowe alisema kuwa Hayati Bob alijitoa kwa hali na mali kwa ajili ya Watanzania akitolea mfano namna alivyojitolea nyumba yake maeneo ya Sea View, Dar es Salaam kuwa mahali pa vikao vya mwanzo kabisa kuanzisha chama hicho cha siasa.

  “Wakati watu wengi wakiogopa kujihusisha na vyama vya upinzani Bob hakujali, kwa sababu Bob was a guy of courage (mtu jasiri). Hakuogopa. Akadiriki kuruhusu nyumbani kwake kuwa mahali pa vikao. Mzee wenu amewatumikia Watanzania kupitia Chadema kwa miaka 21 mfululizo bila malipo. Leo hapa tujiulize wangapi tunaweza kufanya hivyo,” alisema.

  Mzee Bob Makani alizikwa jana katika Kijiji cha Ukenyenge, Tarafa ya Negezi, wilayani Kishapu, eneo la makaburi alipozikwa Baba yake, marehemu Ali Makani na ndugu zake wengine.​
   
 2. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #2
  Jun 14, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Binafsi nakubaliana na kauli ya Mbowe, kwani ukweli mara zote huzungukwa na kupanda propaganda, ya moyoni yanayomwumiza ameyaanika, kwani ni dalili ya propaganda tofauti na wanavyoonekana misibani, hapa napata picha kuwa viongozi na wanasiasa unafiki una kipaumbele kuliko ukweli.
   
 3. m

  mamajack JF-Expert Member

  #3
  Jun 14, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 1,162
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  long live mr mbowe!!!!ur real a leader.
   
 4. samstevie

  samstevie JF-Expert Member

  #4
  Jun 14, 2012
  Joined: Nov 11, 2011
  Messages: 202
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Thanks Mr. Mbowe I must appreciate this.
   
 5. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #5
  Jun 14, 2012
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,849
  Likes Received: 473
  Trophy Points: 180
  Nani anabisha kuwa Mbowe si jembe???
   
 6. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #6
  Jun 14, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Maneno mazito kabisa, na wenye masikio wasikie! R.I.P wa kwetu Mzee Bob
   
 7. MESTOD

  MESTOD JF-Expert Member

  #7
  Jun 14, 2012
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 4,641
  Likes Received: 142
  Trophy Points: 160
  Hivi mzee wa usingizi alikuwepo? Kumbe naye ni mwanzilishi wa cdm. Njaa mbaya sana, itachukuwa muda kuamini kuwa kumbe mzee wa usingizi anafahamu mchanganyiko wa watu waloanzisha cdm bado naye anatoka mapovu kukomalia issue za udini chadema.
  Nimeipenda hii kauli ya mbowe, bendera za vyama vyetu visibomoe msingi wa utaifa wetu.
   
 8. Oluoch

  Oluoch Senior Member

  #8
  Jun 14, 2012
  Joined: Aug 30, 2010
  Messages: 134
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni hotuba iliyokidhi vigezo,tena yenye kuonesha ukomavu wa kisiasa na uzalendo
   
 9. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #9
  Jun 14, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Hili ndilo jibu kwa Mukama Katibu mkuu wa CCM aliyeanza ukabila bale kwenye maombolezo ya Makani
   
 10. Amiliki

  Amiliki JF-Expert Member

  #10
  Jun 14, 2012
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 2,087
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Duh! Mbowe huwa namkubali si kwa bure tu! Huyu jamaa ni Jembe la Uhakika!
   
 11. BornTown

  BornTown JF-Expert Member

  #11
  Jun 14, 2012
  Joined: May 7, 2008
  Messages: 1,716
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160

  “Mathalani leo wengine hapa walijua Bob ni Mkristo, kumbe Bob ni Mwislamu, lakini tumekuwa tunatumia propaganda nyepesi za udini tunaharibu historia makusudi kwa maslahi yetu mafupi ya kisiasa bila kujua kuwa wakati huo huo tunalibomoa taifa letu katika misingi ya udini.”

  “Leo tumekaa wote hapa, watu wa dini mbalimbali, tuna viongozi wetu hapa wa dini mbalimbali, tumekaa pamoja kabisa tumevumiliana, wapo watu wa makabila mbalimbali…hakuna tatizo lolote kabisa, kwa sababu sisi hatupaswi kutambulishwa kwa makabila wala dini zetu bali tunatambulishwa kwa utaifa na Utanzania wetu basi,” aliongeza.

  “Napenda kutoa hii rai leo kwa viongozi wa dini zote walioko mahali hapa, kwa viongozi wote wa vyama vya siasa na kwa viongozi wa serikali, vyama hivi vya siasa ni vitu vya kupita, tusibomoe utaifa wetu kwa bendera za vyama vyetu. Vyama vyote hivi Chadema na CCM vitapita, lakini Watanzania na nchi yao watabaki,” alisema Mbowe huku waombolezaji wakishindwa kujizuia kumpigia makofi mengi.

  Mbowe alisema kuwa Hayati Bob alijitoa kwa hali na mali kwa ajili ya Watanzania akitolea mfano namna alivyojitolea nyumba yake maeneo ya Sea View, Dar es Salaam kuwa mahali pa vikao vya mwanzo kabisa kuanzisha chama hicho cha siasa“
  .
  [/QUOTE]


  Mbowe kanifurahisha sana, hii ni msg nzito sana
   
 12. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #12
  Jun 14, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Magwanda bwana, hukua anachukuwa misaada kutoka vyama vya siasa vya kidini huku Mbunge wake anasema anataka Taifa la kanda ya kaskazini, huku anasimaa kudanganya watu wamuone kuwa yeye sio mdini wala mkabila. Huu ndio unafik wa kisiasa.

  Angeanza kwa kuachana misaada ya kisiasa kutoka vyama vya kidini. Angeanza kwa kukemea kanisa lililowatenga waumini kwa kuwa tu waliipigia kura CCM. Angeanza kwa kumkemea na kumchukulia hatua za kinidhamu Nassari ambae anataka Taifa la kaskazini. Angeanza kwa kuwa na uwiano sawa wa wabunge wa kupendekezwa badala ya asilimia kubwa ni Wakristo na waliotoka Kaskazini.

  Mbowe huu mimi nauita unafik.
   
 13. Endeleaaa

  Endeleaaa JF-Expert Member

  #13
  Jun 14, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 1,229
  Likes Received: 320
  Trophy Points: 180
  Watanzania tulifanya makosa sana 2005, tulipochagua Gamba badala ya Gwanda
   
 14. b

  blue arrow JF-Expert Member

  #14
  Jun 14, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 271
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Big up mheshimiwa mbowe; may God be with you anywhere you go
  you are really a good leader.
   
 15. M

  Megawatt B JF-Expert Member

  #15
  Jun 14, 2012
  Joined: Aug 23, 2011
  Messages: 260
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Acha hizo, mbona alishakemea siku nyingi. wewe hukusikia anmwambia Nasary "this is childish"
   
 16. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #16
  Jun 14, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  "vyama hivi vya siasa ni vitu vya kupita, tusibomoe utaifa wetu kwa bendera za vyama vyetu. Vyama vyote hivi Chadema na CCM vitapita, lakini Watanzania na nchi yao watabaki,”

  Ni kauli ya busara sana hii.
   
 17. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #17
  Jun 14, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,986
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  Wakuu mnaona sasa watu na cheap propoganda kumbe hata waanzilishi wa CHADEMA si wote walikuwa Wachaga wala Wakristo, (Mzee Bob Makani na Mzee Mtei waanzilishi wa CHADEMA) hii ni aibu kwa wote wa siasa za udini na kabila!!! Kumbe Mzee Bob hakuwa Mkristo wala Mchaga, yeye alikuwa Msukuma na Mwislamu safi, watokee kina siasa uchwala za dini na ukabila sasa!!!!!

   
 18. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #18
  Jun 14, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Sasa kusema "childish" ndio kachukuwa hatua stahiki? unanifurahisha kweli kweli, hiyo si kumsifia tu, maana mtoto anaweza fanya lolote akaachiwa tu, si mtoto! Sasa Nassari ni mtoto?

  Na kuchukuwa misaada vyama vya siasa vya kidini? na kuchaguwa wabunge wa upendeleo asilimia kubwa (zaidi ya 80%) wakristo na waliotoka Kaskazini? kama si udini na ubaguzi wa ukabila ni nini? aache unafik.

  Ukiona mtu anajitangaza na kujipamba kwenye jambo fulani, basi mtazame sana huyo, "guilty conscious" inamuhangaisha.
   
 19. Comi

  Comi JF-Expert Member

  #19
  Jun 14, 2012
  Joined: Oct 2, 2011
  Messages: 3,347
  Likes Received: 478
  Trophy Points: 180
  mda huu siyo jembe tena ila ni sururu maana inatoboa hata bomba la chuma
   
 20. KALYOVATIPI

  KALYOVATIPI JF-Expert Member

  #20
  Jun 14, 2012
  Joined: Aug 11, 2011
  Messages: 1,419
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 0
  Ni zaidi ya jembe ni mfano wa greda au trekta
   
Loading...