Hotuba ya Lukuvi bungeni kuthibitisha kauli yake kanisani, UKAWA kumchukulia hatua za kisheria

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,883
6,884
lukuvi+ukawa.jpg

Lukuvi aishukia Ukawa

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi amewashukia wajumbe wa Kundi la Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), waliogomea kuendelea na mchakato wa kutengeneza Katiba, akisema wanapanga kuivuruga nchi.

Lukuvi alikwenda bungeni mjini Dodoma kwa kazi maalumu ya kutoa ufafanuzi kuhusu kauli yake aliyoitoa kwenye Kanisa la Methodist kwamba hoja ya serikali tatu ikipita inaweza kulifanya jeshi kuchukua madaraka, ambayo imeibua hisia kali kutoka kwa wana Ukawa.

Akizungumza bila kuwapo wanachama wa Ukawa waliosusia Bunge kuanzia juzi, Lukuvi alikishutumu Chama cha Wananchi (CUF), kwamba kimekuwa kikijiita ni chama cha siasa wakati ni kundi la Uamsho ambalo linasumbua Zanzibar.

Alisema kauli za Ukawa kwamba Rais Jakaya Kikwete atapelekwa katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu The Hague, Uholanzi haiwezi kutokea badala yake watakwenda wao katika mahakama hiyo kwa kujihusisha na Uamsho.

Lukuvi amekiri bungeni aliyoyasema kanisani
Alisema ameamua kusema kile alichokichangia katika kanisa hilo wakati wa kusimikwa kwa Askofu Joseph Bundala kwa kuwa hana tabia ya unafiki na alitaka maneno hayo yarekodiwe kwenye kumbukumbu za Bunge.


“Nayasema yote haya kwa kuwa naamini huo ndiyo msimamo wangu na utakuwa msimamo ambao wakati wote utaendelea kuwa hivyo na ninawataka ndugu zangu kuacha unafiki,” alisema.

Alikanusha madai kwamba ni mchokozi badala yake akarusha tuhuma hizo kwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Shariff Hamad.

Alinukuu hotuba ya kiongozi huyo wa chama kikuu cha upinzani Zanzibar aliyoitoa mwezi uliopita katika Uwanja wa Kibandamaiti Zanzibar kwamba imekuwa ikipotosha hotuba ya Rais Kiwete kwa sehemu kubwa kuhusu mchakato mzima wa Katiba.

Lukuvi pia aliituhumu Ukawa kwamba imepanga kuigawa Tanzania katika vipande, kwamba Zanzibar itatawaliwa na CUF, Tanzania Bara na Chadema halafu CCM ipewe urais wa Muungano.

“Kutokana na hilo, nani ambaye hatakuwa na wasiwasi juu ya haya mambo? Nataka niwahakikishieni katika Katiba hii hakuna chombo chochote wala mtu yeyote atakayenizuia kusema ninachokiamini ilimradi nasema ukweli na ninayoyaamini,” alisema.

Alisema kama maneno yake yamewachukiza zaidi wapinzani, basi waendelee kugoma zaidi alichofanya kilikuwa kwenda kusimamia masilahi ya serikali mbili zenye masilahi kwa wananchi.

Lukuvi alisema wakati wote wananchi hawataki serikali tatu, bali wanataka maendeleo ikiwamo maji, barabara na vitu vingine lakini vyote viwe kwa kupitishwa kwa serikali mbili.

Lukuvi ampongeza Mrema - aahidi tuzo kwa Mrema kufuatilia mafao yake
Waziri huyo alitumia nafasi hiyo kumpongeza Mbunge wa Vunjo na Mwenyekiti wa Taifa wa Tanzania Labour Party (TLP), Augustino Mrema kuhusu mchango wake bungeni juzi ambao uliunga mkono muundo wa serikali mbili.

Lukuvi ambaye jana alimtaja Mrema kwa cheo cha Naibu Waziri Mkuu alichowahi kushika katika Serikali ya Awamu ya Pili, alisema mwanasiasa huyo ndiye mpinzani wa kweli ambaye anastahili kupongezwa na kila mtu kwenye Bunge hilo kwa kuwa anachokizungumza ni ukweli mtupu.

“Kutokana na hilo mheshimiwa Mrema, nakuhakikishia kuwa sasa masilahi yako nitayafukuzia kwa sababu umeongea mambo ya maana sana,” alisema Lukuvi.

Kwa muda mrefu Mrema amekuwa akifuatilia serikalini kile anachokiita ni mafao na stahiki zake katika kazi ya Unaibu Waziri Mkuu aliyoifanya wakati wa utawala wa Rais Mwinyi licha ya kwamba nafasi hiyo haikuwamo kwenye katiba.

UKAWA kumchukulia hatua za kisheria Lukuvi
Akizungumza katika mkutano wa Ukawa jana, Mwenyekiti Mwenza, Profesa Ibrahimu Lipumba alisema wanafanya taratibu za kumchukulia hatua za kisheria Lukuvi kwa matamko aliyoyatoa.


“Alipaswa kusema kama kweli aliyazungumza maneno yale au la na tungekuwa na uongozi unaowajibika baada ya kuyasema yale (kanisani), Rais angemwita na kumtaka ayathibitishe,” alisema.

Alisema Uamsho ni taasisi ambayo imeandikishwa kisheria na Serikali ya Zanzibar na kuongeza kuwa wakati inaandikishwa, Chama cha CUF hakikuwa madarakani.

“Serikali ya Umoja wa Kitaifa ilikuwa haijaanza Zanzibar, iliyouandikisha Uamsho ilikuwa Serikali ya CCM Zanzibar, sasa hawaulizi kwa nini waliiandikisha?” alihoji Profesa Lipumba.

Alisema Uamsho wamekuwa wakimshambulia hata Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad... “Huyu tutamshughulikia kisheria kwa yale matamko aliyoyatoa,” alisema Profesa Lipumba.

Hisani ya Mwananchi Publication

 
ukawa3-300x171.jpg

UKAWA: Haturudi bungeni


  • Wajipanga kufanya mikutano nchi nzima
  • Kusambaza CD za Lukuvi, kesho Zanzibar
WAJUMBE wa Bunge Maalumu, wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), wamesema hawatarudi bungeni na badala yake kuanzia kesho wataanza mikutano ya hadhara nchi nzima kuwaeleza wananchi juu ya hila za Chama Cha Mapinduzi (CCM) na washirika wake kutaka kuhodhi mchakato wa uandikaji wa Katiba mpya.
UKAWA wamesema katika mikutano hiyo watazisambaza ‘CD' zinazomuonesha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi, akiwa katika Kanisa la Methodist, mkoani Dodoma akiwaeleza waumini wakatae muundo wa serikali tatu.
Walisema kwenye CD hizo, Lukuvi, anaonekana akiwaambia wananchi iwapo wataridhia muundo wa serikali tatu, jeshi litachukua nchi na Zanzibar itaingia katika utawala wa Kiislamu.
Juzi wajumbe wa UKAWA walisusia kikao cha Bunge Maalumu kwa madai ya kuchoshwa kusikiliza matusi, ubaguzi na kauli za chuki zinazotolewa na wajumbe kutoka CCM bila viongozi wakubwa kukemea.
Jana wakizungumza na waandishi wa habari, viongozi wa UKAWA walisema hawatarejea bungeni mpaka watakapoketi kwenye vikao vya maridhiano ambavyo pia watakwenda na masharti yao mojawapo ni rasimu ya Tume ya Warioba ndiyo iwe msingi wa majadiliano.
Masharti mengine ni kukaa kwenye meza ya maridhiano na viongozi wa serikali na CCM, kusiwepo matusi, ubaguzi na kauli za chuki.
Mmoja wa viongozi wa UKAWA, Profesa Ibrahim Lipumba, alisema kuwa watazunguka nchi nzima kuwaeleza wananchi kilichotokea bungeni na namna CCM wanavyopenyeza rasimu yao kwa mlango wa nyuma.
"Sisi tupo tayari kwa mazungumzo kama tulivyoombwa na Mwenyekiti wa Bunge Maalumu, Samuel Sitta, lakini hatutakubali kubeba matakwa ya CCM, tunataka tujadili rasimu ya Tume ya Jaji Warioba ambayo ilikwenda kuwahoji wananchi," alisema.
Profesa Lipumba, alisema wameamua kususa vikao vya Bunge kwa sababu hawako tayari kushiriki kupitisha masuala yenye masilahi ya CCM yaliyopelekwa bungeni kwa mlango wa nyuma.
Alisema walitegemea wajumbe wangejikita kujadili rasimu iliyowasilishwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba kwa hoja lakini badala yake wameshuhudia matusi, ubaguzi, kauli za chuki ambazo zinachangia zaidi kuligawa taifa.
Lipumba alisema rasimu iliyopo mezani inataja serikali tatu hivyo kama wajumbe wa CCM wanataka kujadili serikali mbili, lazima Bunge livunjwe na iundwe tume nyingine itakayotoa rasimu ya serikali mbili.
"Wenzetu wanatushangaza sana yaani walivyokuwa wakijadili rasimu ile kama imetolewa na wapinzani, hii ni rasimu iliyotolewa na tume iliyoundwa na rais, sasa kama wenzetu hawaamini sisi tunakwenda kuwaeleza wananchi CCM isivyotaka kuandika Katiba yenye masilahi ya wananchi," alisema.
Lipumba pia alisema Chama cha Wananchi (CUF), kitaangalia hatua za kisheria za kumchukulia Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi, alivyokihusisha chama hicho na taasisi ya kidini ya UAMSHO.
Alisema si kweli kwamba CUF imekuwa ikishirikiana na taasisi hiyo ambayo mara kadhaa imekuwa ikihusishwa na mihadhara ya kidini yenye vurugu visiwani Zanzibar.
Naye James Mbatia, alisema maridhiano ndiyo yatakayosaidia mchakato wa Katiba kusonga mbele lakini kwa hali inavyoonekana CCM hawana dhamira ya kuandika Katiba yenye kujali masilahi ya wananchi.
Alisema wiki iliyopita TCD iliitisha mkutano wenye lengo la kutafuta maridhiano lakini CCM walituma wawakilishi wasio na nyadhifa za juu kama zilivyofanya pande nyingine.
Naye Mwenyekiti wa UKAWA, Freeman Mbowe, alisema wameamua kususa vikao vya Bunge kwakuwa wajumbe wengi kutoka CCM wameacha kujadili rasimu iliyowasilishwa na Tume ya Warioba ambayo ndiyo msingi wa majadiliano yao.
Alisema Tume ya Warioba iliwekwa kisheria na ilifanya kazi ya kuwahoji watu pamoja na kutumia nyaraka mbalimbali hadi kufikia kutoa rasimu isiyotakiwa na wajumbe wa CCM walioanza kujadili rasimu waliyopewa na chama chao.
"Kususia vikao vya Bunge ni miongoni mwa hatua za kutafuta haki, kuendelea kushiriki vikao hivi ni kuhalalisha na kubariki udhalimu wa CCM ambayo imeamua kukwamisha Katiba mpya.
"Matusi, ubaguzi, chuki haviwezi kutusaidia kupata Katiba mpya, UKAWA hatuko tayari kuendelea kushiriki majadiliano yenye mambo hayo….tunakwenda kwa wananchi kuwaeleza kile kinachofanywa na wajumbe humu bungeni," alisema.
Mbowe alisema si lazima Rais Jakaya Kikwete aondoke madarakani wakati Katiba mpya imepatikana bali mchakato huo unaweza kuendelezwa na rais mwingine lakini katika mazingira yanayokubalika na watu wote.

Hisani ya Tanzania Daima Publication
 
Mods pamoja na kwamba habari imeongelewa katika majukwaa kadhaa, tatizo huwa ni habari zisizo na kina na kuleta ufafanuzi kamili, napenda hii kwa vile imekuwa published kwenye vyombo vya habari na hivi wasomaji wanaweza kupata picha ya kile kilichoongelewa au kinachoendelea. Asanteni kwa ushirikiano.

CC; Paw,
PainKiller,
Fang,
Cookie
 
Hizo cd za lukuvi wasihishie kuzigawa znz tu,wazigawe pia na Arusha,kagera na kwengineko!! Ili na cc ndugu zetu wa huko waone tutakavyonyanyasika!! Wasiwe wanafiki kugawa upande mmoja!
 
Hizo cd za lukuvi wasihishie kuzigawa znz tu,wazigawe pia na Arusha,kagera na kwengineko!! Ili na cc ndugu zetu wa huko waone tutakavyonyanyasika!! Wasiwe wanafiki kugawa upande mmoja!

Wataanzia Zanzibar ambako wamedhalilishwa zaidi na pasi na shaka zitazambazwa nchi nzima.
 
Kimenuka! Hivi kweli katika hali ya kawaida watu wanaweza kufanya mizahaa ya namna hii? Kura ya wazi na siri ulishaona wapi dunian licha ya maendeleo ya sci&tech. Huu ni unafiki ubinafsi na Ccm hawana dhamira ya kuandika katiba mpya!
 
Muda mwingine si elimu peke yake inayosaidia,bali hata umri na busara pia uwa ni msaada tosha!tunapoelekea siko kwenyewe kabisa
 
CCM na rushwa said:
Lukuvi ambaye jana alimtaja Mrema kwa cheo cha Naibu Waziri Mkuu alichowahi kushika katika Serikali ya Awamu ya Pili, alisema mwanasiasa huyo ndiye mpinzani wa kweli ambaye anastahili kupongezwa na kila mtu kwenye Bunge hilo kwa kuwa anachokizungumza ni ukweli mtupu.


"Kutokana na hilo mheshimiwa Mrema, nakuhakikishia kuwa sasa masilahi yako nitayafukuzia kwa sababu umeongea mambo ya maana sana," alisema Lukuvi.


Kwa muda mrefu Mrema amekuwa akifuatilia serikalini kile anachokiita ni mafao na stahiki zake katika kazi ya Unaibu Waziri Mkuu aliyoifanya wakati wa utawala wa Rais Mwinyi licha ya kwamba nafasi hiyo haikuwamo kwenye katiba.
Hii sasa kiboko, rushwa hadi Bungeni! Kwa CCM, rushwa ni kama hewa ya oxygen...bila rushwa ni kaburi tu lachungulia.
 
Hii sasa ni hatari. Mrema huyuhuyu aliyekuwa anabebwa kama maiti?
 
mchakato wa upatikanaji katiba mpya umehodhiwa na wanasiasa hasa wa chama twawala,wewe lukuvi,wassira,nape,olesendeka.mtaishi milele?wapeni wananchi kile wanachokitaka,nyinyi hamtaishi milele,lakini tanzania yetu itakuwepo milele na milele.
 
Jana nilipokua nafuatilia bunge mwenyekiti wa bunge alimpa nafasi waziri wa nchi sera uratibu na bunge ndg Lukuvi nafasi ya alichokiita kujibu alichosema prof Limbumpa baada ya hicho alichokiita majibu kwa Lipumba, mh Lukuvi alimsifia sana Mrema kwa mchango wake uliomfurahisha bila shaka na kuwafurahisha wakubwa wa ccm mpaka akafikia kumuahidi kwamba atahakikisha Mrema anapata mafao yake ,maswali ya kujiuliza
1. je ni haki ya Mrema kupata hicho Lukuvi anachookiita mafao au ni rushwa baada ya kuwafurahisha kwa mchango wake bungeni
2.kama ni haki yake inahitaji kujipendekeza kwao ndio upate haki yako?
3. hii inatufundisha nini kwamba mpaka tujipendekeze kwa ccm ndio tunaweza kupata haki yetu?
4. kwanini Watanzania tunaruhusu mambo ya kijinga haya yatokee katika nchi yetu kwanini tunaruhusu waziri atumie ofisi ya umma na rasilimali za umma kwa manufaa ya chama chao na serikali iliyoko madarakani
5.ni wangapi wataanza kujipendekeza kwa ccm na serikali yake ili wapate wanachokitaka je tutajenga demokrasia kwa njia hizi?
inakera sana
 
Inasikitisha sana yaan haya maneno ya Lukuvi yameidhalilisha Zanzibar kuliko kuidhalilisha, lakin pia la kushangaza ccm wanaotoka zanzibar nawo hawakuonyesha hisia zozote juu ya kauli hii ya kichochezi ya kibaguzi ya kidini, jambo baya zaidi Lukuvi ameenda mbali zaidi kuhusisha na uamsho, wakati ata hawo uamsho wenyewe hawajapatwa na hatia yeyote ikijihusisha na chama cha siasa, juzi tu kesi yao iliisha hakuwa na hatia na kesi ishafutwa sasa Lukuvi anapata nguvu wapi juu ya maneno yk haya ya kibaguzi, ccm hawana hoja ni vyema Kukuvi akashughulikiwa kisheria
 
Back
Top Bottom