Frey Cosseny
JF-Expert Member
- Feb 4, 2015
- 1,984
- 1,405
Mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), ambaye pia ni Rais wa Tanzania, Dk. John Magufuli amesema nchi za kiafrika si maasikini hivyo ziache kujitangaza kuwa ni duni mbele ya mataifa mengine.
“Tusikubali kusafirisha tu malighafi nje ya Afrika, hii inaatufanya tuwe tunasafirisha ajira. Nchi zetu si masikini, narudia tena nchi zetu si masikini tunao utajiri wa kutosha kwenye madini, mafuta na ardhi yenye rutuba .
Vitu vyote vinavyotufanya tuwe matajiri tunavyo, kwanini tushindwe kupiga hatua,” alisema Rais Magufuli.
Akizungumza baada ya kukabidhiwa uenyekiti wa jumuiya hiyo katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam leo, Rais Magufuli amesema mbali ya kuwa na rasilimali nyingi lakini bado Afrika inalalamika hali duni ya kiuchumi.
Rais Magufuli amesema Tunaagiza sukari, magari na mafuta katika nchi za mbali huku tukijua baadhi ya mataifa ya SADC yanaweza kuuza bidhaa hizo kwa bei nafuu. Ndio maana katika mwaka wangu wa uongozi nimeamua kuongozwa na kaulimbiu ya mazingira bora ya viwanda, ufanyaji biashara na kutengeneza ajira.
Vievile, fursa nyingi za kibiashara zinapelekwa katika mataifa ya mbali huku baadhi ya nchi zinazozalisha bidhaa nzuri ikiwemo magari na bidhaa nyingine za viwanda zikiachwa mbali ya kuwa na bidhaa bora na zilizo karibu.
Aidha, Rais Magufuli aliigeukia Sekretarieti ya SADC na kuitaka ieleze kwanini uchumi katika nchi wanachama wa jumuiya hiyo unashindwa kufikia viwango vya kukua. Kwanini kwa miaka 10 lengo la kuondokana na tatizo la kiuchumi halijafikiwa.
Awali Rais Magufuli akielezea changamoto zinazoikabili jumuiya hiyo na kushindwa kufikia baadhi ya makubaliano, Rais Magufuli alisema changamoto ya kwanza ni vurugu za kisiasa, kutokamilika ahadi za kubadili uchumi na ukosefu wa taarifa za fursa katika nchi wanachama.
“Bado hatujafanikiwa katika ukuaji wa uchumi, niseme kweli bado tunasuasua. Na tusipibadilika hatutaweza kufanikiwa katu. Bado tupo nyuma katika lengo letu la kiuchumi, uhaba wa taarifa unasababisha tunashindwa kujua wapi pa kuuza bidhaa zetu,” alisema Dr John Pombe Magufuli