Hotuba ya kinana; ccm kuipongeza zanu pf nchini zimbabwe

R.B

JF-Expert Member
May 10, 2012
6,296
2,571
[h=2][/h]





Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia kwenye mkutano mkuu wa ZANU PF

Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Abdulrahaman Kinana , amekipongeza Chama Cha ZANU PF Cha Zimbabwe kwa kusimama imara licha ya Changamoto mbalimbali zinazoikabili Zimbambwe ikiwemo vikwazo vya kiuchumi ambavyo vimewekwa dhidi ya nchi hiyo.


Amewataka wana ZANU PF kuendelea kuunga mkono chama chao na kuongeza mapambano dhidi ya maadui wote wanaotaka kurudisha nyuma jitihada za kupigania maslahi ya nchi yao.

Akisoma salamu za mshikamano za Chama Cha Mapinduzi kwenye mkutano Mkuu wa ZANU PF unaofanyika mjini Harare Ndg. Kinana aliwakikishia wana ZANU PF na wana Zimbabwe wote kuwa katika mapambano hayo CCM iko nyuma yao na kwamba haitaacha kupaza sauti dhidi ya vikwazo vya uchumi ilivyowekewa Zimbabwe.

Alisema vikwazo hivyo havina uhalali na kwa ujumla wake vinatoa adhabu isiyo ya haki kwa Wananchi wa Zimbabwe wasio na hatia.

Ndugu Kinana alimpongeza Rais Mugabe ujasiri na kwa msimamo wake usioyumba wa kupigania maslahi ya wana Zimbabwe licha ya vitimbi vya wapiga maendeleo.

Alisema ujasiri na msimamo wa Mugabe pamoja na Chama anachokiongoza Cha ZANU PF ndiyo uliowezesha Zimbabwe kusimama ilivyo hivi sasa kama Taifa huru na lisilikubali kuyumbishwa.

Alisema Mugabe na Chama chake wameonyesha kwa mfano kwamba kumbe watu wakisimama imara chini ya uongozi wa chama imara hakuna anayeweza kukwamisha nyendo zao za kimapinduzi zinazoendana na matakwa ya umma.

Akizungumzia ushindi wa kishindo wa ZANU PF kwenye uchaguzi Mkuu June mwaka jana Kinana alisema hicho ndicho kiashiria cha kukubalika kwa Chama na sera zake.

Alisema CCM inaipongeza ZANU PF kwa ushindi huo na kwamba wana CCM wanajisikia fahari sana wanapoona ZANU PF ikiendelea kukua na kuimarika.

Aidha Ndg. Kinana alimpongeza Rais Mugabe na kueleza kuwa CCM na Watanzania kwa ujumla wanafurahishwa na msimamo wa dhati alionyesha Rais Mugabe katika majukwaa mbalimbali ikiwemo mkutano wa wakuu wa nchi za SADC uliofanyika Victoria Falls wa kueleza umuhimu wa kutambua na kuheshimu mchango wa Mwalimu Nyerere katika ukombozi wa Afrika na hasa kusini mwa Afrika.

Hotuba ya Ndg. Kinana ilipokelewa kwa shangwe na furaha kubwa sana na wajumbe wa mkutano huo ambao mara kwa mara walishangalia kuashiria kuridhika na kauli za kimapinduzi na kidugu kutoka kwa wana CCM.

Ndugu Kinana na ujumbe wake wataondoka kesho kureke nyumbani. Ujumbe wa Katibu Mkuu kwenye mkutano ulimhusisha pia Mjumbe wa halmashauri Kuu ya Taifa CCM Ndg. Phares Magesa na afisa wa makao makuu ya CCM Ndg. Thobias Mwilapwa.
 
Mugabe amesimama kidete kwa ajili ya raslimali za wazimbabwe kuwanufaisha wazimbabwe huku Serikali ya CCM ikiwabeza na kuwatukana wawekezaji wazawa kwamba hawana uwezo na hawatakiwi kuwekeza kwenye gesi yao kwa kuwa mitaji yao ni ya kutosha kuuzia juisi na maandazi tu

Hotuba ya Kinana ni hotuba ya kinafiki

Anajua Mugabe amechukua hatua kuhusu madini na kutaka wazimbabwe wengi wawezeshwe kuwekeza huko badala ya wageni wakati CCM na serikali yake ikiwatukana

Msimamo wa Serikali ya ZANU-PF ni tofauti na Msimamo wa Serikali ya CCM katika maslahi ya umma
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom