Hotuba ya Kambi ya Upinzani: Kwa nini Serikali haijailipa NSSF fedha iliyojengea UDOM

Nikupateje

JF-Expert Member
Dec 22, 2009
1,334
988
Katika hotuba ya kambi rasmi ya Upinzani, inayosomwa sasa hivi, wametaka serikali ijibu kwa nini NSSF na mifuko yote haijalipwa hata senti tano kwa kukopwa kwa kujengea UDOM.
 
"ni heri Dr. Willibrod Slaa ashinde na aingie Ikulu, kuliko Tundu Lissu kushinda ubunge na kuingia Bungeni"......Jakaya Mrisho Kikwete, Oct. 2010.
 
Jamani tuwekee hotuba nzima ya kambi ya UPINZANI kuhusu wizara ya vijana na ajira. Ninaona kambi ya upinzani imeiubua mambo mazito kama
1. Jinsi Serikali ilivyochachukua sheria ya mafao ya kujitoa
2. Serikali kutoanza kurejesha pesa ilizokopa NSSF kujengea UDOM na Machinga complex etc
 
Tatizo l.iko hata kwenye matumizi ya kawaida katika mifuko hii.nimeambiwa kuwa baadhi ya hii mifuko huwa inafanya matumizi ya anasa sana.mishahara wanayolipana ni mikubwa zaidi ya wachangiaji wa mifuko hiyo.pia posho wanazolipana katika vikao ni balaa.kwa mfano,kikao cha maafisa wa nssf kilichofanyika mjini mbeya mwaka huu kilitumia mamia ya mamilioni ya pesa.inasemekana kila mshiriki alikuwa analipwa jumla ya zaidi ya laki tatu na nusu kwa siku.kikao kilikuwa cha wiki mbili
 
Sina uhakika kama umewahi kuona majengo yaliyojengwa na NSSF Dodoma University, Kwa busara tu, kabla ya kuongelea malipo kwa kazi waliyofanya wakaangalie kama kazi iliyofanyika inastahili kulipwa. Majengo mengi yamweka nyufa kubwa hata miaka mitatu hayajafikisha, je ni haki kuwalipa au wao ndio wanatakiwa kwenda kurudia kazi hiyo kwa gharama zake.
 
Katika hotuba ya kambi rasmi ya Upinzani, inayosomwa sasa hivi, wametaka serikali ijibu kwa nini NSSF na mifuko yote haijalipwa hata senti tano kwa kukopwa kwa kujengea UDOM.

Madeni ya aina hiyo na kutumbua fedha za hifadhi za jamii kiholela ni moja ya sababu kubwa kabisa za mkakati wa kufuta fao la kujitoa ili kuondoa pressure! obviously kama hakuna mtu anayedai vile vile hakuna sababu ya serikali kurudisha fedha hizo!! hapo ndio unaiona nguvu ya umma ilivyo devine, sasa kaa la moto limewakwama kooni!
 
Mbona huyu waziri anasema hapa kwamba serikali ishaanza kuilipa UDOM na wana mawasiliano mazuri tu!
 
Mbona huyu waziri anasema hapa kwamba serikali ishaanza kuilipa UDOM na wana mawasiliano mazuri tu!

Tuache siasa, taaluma ya fedha na uwekezaji, haiwezi kutekelezwa na serikali hii dhaifu.Kuna miradi mikubwa ya uwekezaji wa majengo, kama udom, bunge nyumba za polisi, nk, ni miradi kimsingi ni capital intensive project, urudishaji wa pesa si wa siku moja unahitaji muda mrefu.Kwa taarifa ni kwamba hata mkataba wa kuanza kulipa na riba kati ya nssf na serikali ulikuwa haujasainiwa, ni kivipi waanze kulipa?taarifa ya ukaguzi ya cag ya mwezi wa tatu , imeeleza kuwa mkataba huo ulikuwa bado haujasainiwa, na walikuwa hawajaanza kulipa.hayo ya kuanaza kurudisha ni kauli za kisiasa , serikali isionekane kubweteka na kuhimiza uwekezaji ambao ni mzigo kwa nssf.Ni budi serikali iheshimu uwekezaji huu, na pia ijitahidi kutenga fedha ya kulipa kuliko maneno ya blabla.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom