HOTUBA ya Kambi ya Upinzani Bungeni, Maliasili na Utalii na Peter Msigwa (FULL TEXT)

Checklist:
1. Je, umeona taarifa yoyote mpya kwenye hotuba ya Msigwa?

2. Je, umeona utatuzi wowote wa changamoto za kitaifa kwenye hotuba hiyo?

3. Je, kusomwa kwa hotuba kama hii kunaweza kubadilisha nini nchini?

4. Je, hotuba hii isingesomwa kuna jambo lolote lingeharibika?

5. Je, hotuba hiyo imemuwezesha mwananchi kujua kama kiwango cha fedha zilizotengwa kwenye wizara husika kinatosha?

6. Je, hotuba hiyo imekuwezesha kujua meneo gani yanatakiwa kupewa vipaumbele na wizara hiyo katika mwaka huu wa fedha?

Isome kwa makini with objectivity utajijibu mwenyewe. Kama una urojo kichwani mwako shauri yako!
 
Isome kwa makini with objectivity utajijibu mwenyewe. Kama una urojo kichwani mwako shauri yako!

Ukiona umeshindwa kujibu ujue hamna kitu.

Mimi nimeisoma, nimeisikiliza ndio nikatengeneza hiyo checklist kuwasaidia vijana wasilaghaike...
 
Nimependa sana uchangiaji wa Dr Mbassa wa cdm jinsi alivyojikita ktk mambo ya msingi jimboni kwake na namna anavyojieleza, huo ndo upinzani cyo kutukana watu na kuonyesha dharau kama Taifa lisilo na viongizi. Naomba wabunge wengine muigemfano huo.. Kwani mkiheshimiana hamtajulikana kama ni wapinzani?
 
Msigwa alipiga mikwara kuwa hotuba yake itakuwa babkubwa, itatetemesha, itakuwa kombora.

Hali hiyo ni tofauti na hotuba yenyewe ambayo ililazimika kubadilishwa baada ya kuvuja na kusambaa kwenye mitandao.

hotuba hiyo imekuwa TUPU. Haina chochote cha kusisimua.

Kombora moja tu la Dr.Nchimbi limeisambaratisha hotuba nzima na Msigwa ameonekana akiwa na sura ya kuona aibu.

Jitihada za tundu Lissu kutaka kumuokoa Msigwa hazikuzaa matunda.

Kiujumla Msigwa leo ametia aibu kubwa.

Kwa kuelewa zaidi utupu wa hotuba ya Msigwa angalia hii checklist:

1. Je, umeona taarifa yoyote mpya kwenye hotuba ya Msigwa?

2. Je, umeona utatuzi wowote wa changamoto za kitaifa kwenye hotuba hiyo?

3. Je, kusomwa kwa hotuba kama hii kunaweza kubadilisha nini nchini?

4. Je, hotuba hii isingesomwa kuna jambo lolote lingeharibika?

5. Je, hotuba hiyo imemuwezesha mwananchi kujua kama kiwango cha fedha zilizotengwa kwenye wizara husika kinatosha?

6. Je, hotuba hiyo imekuwezesha kujua meneo gani yanatakiwa kupewa vipaumbele na wizara hiyo katika mwaka huu wa fedha?
 
Meli iliyobeba meno haimilikiwi na Kinana.

Kinana ni shareholder wa shipping agency. Hii ni kampuni inayoihudumia meli sio kuimiliki.

Kampuni hii haihusiki na ukaguzi wa mizigo inayosafirishwa na meli.

Watuhumiwa wa kesi ya meno ya tembo walifikishwa mahakamani mwaka 2009.

Msigwa anajua yote haya ila anapotosha kwa makusudi ili kuwalaghai watu.

Pole kaka, naona tangu asubuhi umepagawa mkuu ZeMarcopolo. Sasa umeamua kunukuu maneno ya Nchimbi wakati akichangia na ukatafuta conclusion. Soma hotuba sehemu hiyo inayomhusu Katibu Mkuu wenu Kinana katika hizo tuhuma za ujangili, uchangie topic hapa kwa uelewa.
 
Mtahaha sana mwaka huu,kikubwa wananchi wameyasikia yaliyokusudiwa kusemwa na mh msigwa,nyie endeleni kulindana na kuteteana while nchi inazidi kuliwa na rasilimali zinazidi kuisha tu.....angalia kwa karibu ukoo wako wote unanufaika na ujangiri wa kinana? kama sio,unachotetea ni hicho kitumbua chako ama chama chako?

kuweni na woga na aibu kwa jamii nzima,hii nchi c ya ccm wala cdm ni yetu sote na chama kinachotupigani tupate haki hyo ni cdm ndo maana tunaiunga mkono
 
Mchango wa Dkt. Nchimbi ni sawa na mwanafunzi aliyepata paper nje ya chumba cha mtihani, akakariri akaingia kwenye chumba cha mtihani akakuta mtihani si wenyewe, lakini kwa sababu amekariri au kukaririshwa majibu, yeye akaendelea kutumia majibu yale yale ya paper 'fake' kumbe paper imebadilishwa.

Serikali na wabunge wa CCM wameingizwa mkenge. Waende wakajipange, mechi imemalizwa mapema. Walikariri hotuba waliyopewa jana asubuhi...wakapeana na majibu. Wakapangana nani atasema nini, wakati gani..

Kama Mike Tyson vs Frank Bruno. Dakika ya tatu...game is over.
 
Hotuba imejaa mipasho.

Ufafanuzi wa ishu ya tembo umetolewa na Msigwa ameona aibu kusema uongo wa kupotosha.

Taarifa za Wakala wa Usajili wa Biashara na Makampuni (BRELA) zinaonyesha kwamba Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana anamiliki robo tatu ya hisa za Sharaf Shipping Co. Ltd., wakati robo iliyobaki ya hisa hizo inamilikiwa na mtu aitwaye Rahma Hussein. Kwa mujibu wa taarifa ilizonazo Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Rahma Hussein ni mkewe Abdulrahman Kinana!

Huu nao ni uongo?? Au unataka tuamini Uongo wa Dr. Nchimbi?? Kama Mch. Msigwa kasema uongo si wamchukulie hatua???
 
Pole kaka, naona tangu asubuhi umepagawa mkuu ZeMarcopolo. Sasa umeamua kunukuu maneno ya Nchimbi wakati akichangia na ukatafuta conclusion. Soma hotuba sehemu hiyo inayomhusu Katibu Mkuu wenu Kinana katika hizo tuhuma za ujangili, uchangie topic hapa kwa uelewa.
Weka hapa hotuba ya dakika kumi ya nchimbi ambayo imejibu uzushi wa msigwa, muwe mnafanyia utafiti kile mnachoambiwa ona mnavyoingia choo cha kike vibaya
 
Tulikosea pale tulipodhani kuchagua wanaharakati kungetusaidia, sasa wamebadilisha hotuba ya wizara inakuwa sawa na barua ya mualiko wa sendoff

Msigwa katia aibu kubwa leo.

Bora angesoma tu hotuba yake kama wabunge wengine, sasa yeye kajitaaaaaaaaaaaaaaaaamba kumbe hana kitu kipya.

halafu kumbe hotuba yenyewe kaandikiwa yeye kazi yake kusoma tu, hata anavyoongea havijui!
 
  • Thanks
Reactions: Luv
Back
Top Bottom