Hotuba ya kamanda Mwema na yanayotekelezwa na askari wake yanafananA?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hotuba ya kamanda Mwema na yanayotekelezwa na askari wake yanafananA??

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Hhm, Nov 15, 2011.

 1. H

  Hhm Member

  #1
  Nov 15, 2011
  Joined: Apr 28, 2010
  Messages: 69
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 15
  Ndg zangu wana Jf nimekuwa nikitafakari vurugu zinazotokea kati ya jeshi la polisi na wanainchi kila panapokuwa na ama maandamano au mpango wa maandamano kwa kile kinachoitwa kufikisha ujumbe serekalini na ulimwenguni kero sugu....

  Hivi ni nani mwenye ushahidi hata sikumoja palipotokea maandamano na waandamanaji wakaachwa bila kubugudhiwa na polisi halafu wakavuruga amani ya nchi??? Kwa upande wangu mara zote maandamano yanayosababisha vifo na hata ulemavu lazima utasikia polisi waliingilia maandamano hayo na kuanza kurusha mabomu kwa lengo lakuwatawanya waandamanaji.

  Nikirejea kauli ya kamanda Mwema kuwa jeshi la polisi lipo kwa ajili ya kulinda amani na Mali za watanzania sidhani kama kweli endapo ingelikuwa hivyo kama tungepoteza ndugu zetu na wengine kupata ulemavu nk

  Unajuwa Polisi ni mwanadamu na sisi watanzania ni wanadamu pia, hakika ndugu zangu mtakubaliana na mimi kuwa mtoto ukimuonya kwa viboko kila siku anakuzoea na hofu ya viboko inaondoka matokeo yake anakuwa sugu na asiyeshikika tena...kitendo cha jeshi la polisi kutumia maguvu kila iitwapo leo inaipeleka nchi tusipotaka kufika....juzi mbeya polisi wanapiga mabomu watu wananawa uso na maji na huku wakisonga mbele kwa hasira...ambapo hapo awali mtu akisikia mabomu anakimbia.....sasa hivi jeshi la polisi halioni kuwa sasa si wakati wakutumia maguvu zaidi na ni vyema kutumia busara na mbinu nyingine kuepusha machafuko nchini???....

  Hebu acheni watu waandamane kwa kwa amani msiwarushie mabomu tuone hizo vurugu polisi wanazosema kuwa wanahisi zitatokea... Kwa historia niliyonayo siku zote police are the source of vurugu....kama siyo wao kuingilia tusingefika kote huku....

  Jamani tusidanganyane vita siyo swala la mchezo tusipoangalia nchi itaingia kwenye machafuko kwasababu ya uzembe wa math wachache tu....

  Ukweli ni kwamba sidhani kama kazi ya jeshi la polisi ni kuvuruga amani....wala katika nchi isipokuwa ni kinyume chake...sasa inapofika wakati wanainchi tunaona kuwa jeshi la polisi ni adui na si mtetezi wetu tena ndipo mwanzo wa machafuko jina.

  Pia jambo lingine ambalo kwakweli ni hatari sana tena sana ni pale wanasiasa na wanainchi wanapofikia mahali na kuamini kuwa jeshi la polisi linathamini zaidi chama fulani cha kisiasa na kukandamiza chama kingine hii haina tofauti na kuingiza udini katika dola jambo ambalo ni hatari sana kwa mustakabali wa taifa letu....

  Jeshi la polisi lipo kwa ajili yakulinda wanainchi na Mali.zao, sasa kama ni hivyo basi kwa maneno mengine jeshi la polisi ni rafiki wa raiya wa nchi yake, inasikitisha sana pale inapoonekana kuwa jeshi hilo lipo kwa ajili yakutetea serikali iliyopo madarakani na kukandamiza wanainchi ambao wanateseka kila siku wakiwemo.polisi haohao....

  Wana Jf naomba mchango wamawazo katika hili
   
 2. Ulukolokwitanga

  Ulukolokwitanga JF-Expert Member

  #2
  Nov 15, 2011
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 8,418
  Likes Received: 3,905
  Trophy Points: 280
  Amani inayoongelewa hapa Tanzania ni kuwa na wananchi waoga. Wananchi wakijua haki zao hakuna amani ndio maana mabomu na risasi za moto zinatumika. Maskini Said Mwema hana legacy yoyote ya kuacha mara atakapoachia madaraka siku mtwasi mwenzie JK atakapotoka ikulu na baada ya hapo safari ya The Hague haiepukiki kwa huyu jamaa kwani inaonyesha amedhamiria kuua watu wengi sana hadi 2015
   
Loading...