Hotuba ya kamanda miliakwenye msiba wa denis arusha. Waombolezaji wamshangilia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hotuba ya kamanda miliakwenye msiba wa denis arusha. Waombolezaji wamshangilia

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Made aw kubofya, Jun 14, 2012.

 1. M

  Made aw kubofya Member

  #1
  Jun 14, 2012
  Joined: May 8, 2012
  Messages: 56
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimetoka kwenye mazishi ya mwanachama wa CDM kijana Denis Saitoti aliepata ajali Nairobi.
  Kamanda MIlia ametoa hotuba nzuri sana kwa niaba ya CDM. Amewaasa wanachi kuhakikisha wanatoa mchango wao kwenye katiba mpya.
   
 2. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #2
  Jun 14, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  tupe japo kwa kifupi Millya aliongea nini?
   
 3. s

  sharo Member

  #3
  Jun 14, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 18
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hatutaki siasa kwenye misiba mana mungu hatauliza ulikua chama gani duniani
   
 4. Maishamapya

  Maishamapya JF-Expert Member

  #4
  Jun 14, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,280
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Nini ambacho sio siasa?
   
 5. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #5
  Jun 14, 2012
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 722
  Trophy Points: 280
  asante kwa taarifa......ni bahati mbaya sana tumepoteza vijana wale wakingali bado taifa linawahitaji.....vifo vya vijana hawa ni vimeacha simanzi kubwa sana........lakini naomba niseme kitu kimoja....wiki moja kabla denis na mwenzake hawajapata ajali iliyochukua maisha yao...kuna picha moja waliweka kule facebook ikionyesha spidi ya gari ikiwa 180 net....yaani wamemaliza mzunguko mzima wa spid.....wadau wengi walitoa koment kuwaomba wasirudie mchezo huo maana ni hatari kwa maisha.mmoja wa wao alikoment kuwa wamezoea kwenda spidi...haikuchukua mda vijana wale walipata ajali na gari ile ile na kufariki dunia wote wawili........
  ninachotaka kusema hapa ni kwamba tuwe makini tukiwa na vyombo vya usafiri...spidi kubwa inauwa....polen wafiwa
   
 6. k

  kasimba123 JF-Expert Member

  #6
  Jun 14, 2012
  Joined: Apr 18, 2010
  Messages: 1,318
  Likes Received: 188
  Trophy Points: 160
  hehe Mungu alimpenda zaidi kauli ambayo sipendi kuisikia
   
 7. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #7
  Jun 14, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Mkuu Edson nakubaliana na wewe mia kwa mia.
  Ni lazima tuchukue tahadhari tunapoendesha haya magari, ukweli ni kwamba High Speed Kills, asiyetaka kukubaliana na ukweli huo, atajitanguliza mbele ya haki mwenyewe.
  Poleni sana familia za wafiwa pamoja na ndugu jamaa na marafiki.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 8. F

  FJM JF-Expert Member

  #8
  Jun 14, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Natoa pole kwa wafiwa na mungu amlaze mahali pema peponi Denis.

  Ningependa kuona vyama vyote vya siasa vinaacha kufanya siasa (kwa namna yoyote ile) kwenye misiba. Naona huu mtindo unaanza kuzoeleka lakini ni kinyume kabisa na mila/tamaduni za mtanzania. Msiba ubakie msiba.
   
 9. Communist

  Communist JF-Expert Member

  #9
  Jun 14, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 5,391
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Rip Kamanda.
   
 10. M

  Made aw kubofya Member

  #10
  Jun 14, 2012
  Joined: May 8, 2012
  Messages: 56
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Milia alisema hivi. Jina langu ni James OLe Millia,
  Kwa niaba yangu na kwa niaba ya chama cha demokrasia na maendeleo, tumeshtushwa sana na kifo cha gafla cha kijana Denis.
  "Binafsi Nimemfahamu Denis kwa muda mrefu, toka wakija na kaka yake kunisalimia nikiwa iringa, na hata nilipoingia kwenye siasa tumekuwa tukikutana sehemu mbalimbali na kwenye mihadhara tofautitofauti. Denis alikuwa msikivu, na wamekuwa wakishauriana mambo mengi. Denis ametutoka Wakati ambao Taifa hili linahitaji vijana Kama yeye kulikomboa.
  ndugu zangu tumkumbuke Denis kwa kufanya yale mazuri aliokuwa akifanya. Vijana we zangu nawaasa , pamoja na kuwa ajali hutokea bahati mbaya tujitahidi kujilinda kwani sio tu familia zetu zinatuhitaji, ila Taifa la Tanzania lina hitaji vijana.
  Naomba niwakumbushe pamoja na kuwa tunalia, misiache kutoa maoni yenu kwaajili ya katiba mpya itakayo majibu ya maisha bora kwetu na vizazi vijavyo. Bwana alitoa na bwana ametwaa. Jina lihimidiwe amen"
   
Loading...