Hotuba ya JK siyo aina ya Hotuba inayohitajika

Gurtu

JF-Expert Member
May 15, 2010
1,237
1,500
Nadhani kuna matatizo makubwa kwa washauri wa JK. Kama rais (wa NEC) anazungumza vitu vidogo na vilaini kuna haja ya kukaa bungeni na kumsikiliza kweli?

Anapozungumzia ujenzi wa vyuo vikuu waziri wa Elimu atazungumzia nini wakati wa vikao vya bajeti? anapozungumzia ujenzi wa barabara waziri wa ujenzi atazungumzia nini.

Rais anatakiwa azungumzie mambo ya msingi ya yenye umuhimu zaidi. Kwa mfano alitakiwa kuzungumzia namna ya kuinua hali duni ya maisha ya watu (ingawa hotuba yake imetaja suala la makazi - sijui kaiba toka kwenye ilani ya CHADEMA). Kwanza akiri hali hiyo ikoje na atoe suluhisho na mpango wa utekelezaji. Tungemwelewa kama angesema alichosema Dr. Slaa yaani kupunguza bei ya vifaa vya ujenzi.

Kwa aina hii ya marais tutaendelea kuumia hadi mwisho. Saa ya ukombozi ni sasa. Hakuna kukataa tamaa.
 

Mzee Wa Rubisi

JF-Expert Member
Nov 6, 2010
1,759
1,500
Leo alichofanya kaunganisha majibu ya mwaswali ya mdaharo wake na waandishi ndo alichosema,asilimia 70 ya hotuma ya rais imejaa kuwa sifiwa watu,taasi,spika ambaye atakazi ajafanya lakini kasifiwa,mkuuu wa majeshi,polisi,mafisadi rowasa, kwa ujumla sikusikia jipya
 

Kigogo

JF-Expert Member
Dec 14, 2007
20,523
2,000
unategeme nini kwa rais asiye na vision !! hana cha kuongea ndo maana anaongelea vitu laini laini kwa kuwa akili yake ni laini laini
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom