Hotuba ya JK kwa Taifa mwisho wa mwezi Februari 2010

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,474
39,987
Rais Kikwete ameanza kuhutubia Taifa katika utaratibu wa mwisho wa mwezi. Ameanza kuzungumzia suala la rushwa katika uchaguzi kama alivyozungumzia kule kwenye Mkutano wa TAKUKURU Mwanza.. more to come..
 
Ameelezea pia kuhusu baadhi ya vyama vya kisiasa na wadau wengine kugomea agizo la fedha za uchaguzi kukaguliwa
 
Hakuna sababu ya kumsikiliza kiongozi aliyeshindwa kuongoza. JK anawalea mafisadi, wahujumu wa uchumi na kila uchwao anakuja na hizi ngonjera zake.

Siku yake itafika wengi wamejaribu lakini historia duniani kote wameshindwa. Aliapa kulinda katiba ya Jamhuri na hivi sasa anachofanya ni kuwalinda wahujumu - Dowans, shirika la reli, BWM, BOT, Shirika la Reli, Shirika la simu kila upande left, right, top and bottom. Hizi ni ngonjera za udanganyifu wa kutaka kupata kura lakini ni fisi aliyevaa ngozi ya kondoo.
 
Rais Kikwete ameanza kuhutubia Taifa katika utaratibu wa mwisho wa mwezi. Ameanza kuzungumzia suala la rushwa katika uchaguzi kama alivyozungumzia kule kwenye Mkutano wa TAKUKURU Mwanza.. more to come..

Hivi huo utaratibu bado ulikuwepo ama ameuanzisha tena mwezi huu tunapokaribia uchaguzi mkuu?

Ni kweli wanachojali wao ni uchaguzi tu ndio maana rushwa inazungumziwa ya uchaguzi,viongozi wetu are never serious,rushwa ni tatizo alilotakiwa alishughulikie througout his first term na si eti kwenye uchaguzi wa second term,vituko tu!
 
mimi nadhani JK haishi katika muda tunaoishi maana miezi mingine ina mwisho mingine haina!
 
huyu mi naona kama anaweweseka na kuogopa watu watakavomwaga mihela kutaka kumng`oa.mbona yeye alilipia wajumbe kibao malazi wakati wa kupitishwa na CCM kule dodoma.au kasahau? aaah JK bwana huachi kunichekesha
 
yeye mwenyewe ameingia madarakani kwa mihela ya EPA sasa anajitunisha kifua kutunga sheria anamtungia nani?
 
Kuna chochote katika Govt ya CCM unaweza ahidiwa ukasema "acha tusubiri tuone"?????? Kila kitu ni siasa na masilahi ya wenye Chama.
 
mimi nadhani JK haishi katika muda tunaoishi maana miezi mingine ina mwisho mingine haina!

Kila move atakayokuwa ana make this time ni lazima iwe well calculated for the coming elections,sasa najiuliza ni kwanini kalivalia hili njuga?Je anataka sapoti ya wapiga kura ama anajijengea mazingira ya kudhibiti watu flani flani?Ama ni both?Ama je ni tofauti nyingine zaidi ya hizo mbili nilizozitaja?

Kwa kuanzia,tuondoe hilo neno mwisho wa mwezi,maana naona hiyo inatumika kama pazia tu,hii ni hotuba towards elections....Baada ya hapo sasa lets see ni kwanini anasema anachokisema,na kufanya anachokifanya.
Pia kama ulivyosema kuhusiana na miezi mingine kuwa na mwisho na mingine kutokuwa nayo,je hudhani kuwa ni maybe jet lag problems?lol
 
Mie nishamchoka huyu baba yani sio kama matarajio ya wengi walidhani atakuwa mkombozi wetu kumbe, tumeruka nanihii ka kukanyaga nanihii:(
 
Hakuna sababu ya kumsikiliza kiongozi aliyeshindwa kuongoza. JK anawalea mafisadi, wahujumu wa uchumi na kila uchwao anakuja na hizi ngonjera zake.

Siku yake itafika wengi wamejaribu lakini historia duniani kote wameshindwa. Aliapa kulinda katiba ya Jamhuri na hivi sasa anachofanya ni kuwalinda wahujumu - Dowans, shirika la reli, BWM, BOT, Shirika la Reli, Shirika la simu kila upande left, right, top and bottom. Hizi ni ngonjera za udanganyifu wa kutaka kupata kura lakini ni fisi aliyevaa ngozi ya kondoo.

Inamaana hakuna mtu aliyepelekwa mahakamani kwa sababu ya EPA ? BOT ? hakuna watu waliojiuzuru kwa ajili ya Richmond/Dowans ?

Katika mambo yote hujawahi kuona mafanikio ya serikali ya sasa ? Tanzania ni nchi inayokuwa kwa kasi sana kiuchumi afrika ya mashariki ukiacha rwanda
 
Mie nishamchoka huyu baba yani sio kama matarajio ya wengi walidhani atakuwa mkombozi wetu kumbe, tumeruka nanihii ka kukanyaga nanihii:(

Hata mungu hakuwa mkombozi wa wote ukombozi wako unao wewe mwenyewe yeye ni msimamizi tu usiwe mbinafsi wewe kujifikiria mwenyewe kama mipango ya serikali haiko sawa upande wako usilaumu fanya kazi kwa jitihada zako tafuta oppotunities zingine sio kukaa kungoja tu hata vipofu wanafanya kazi
 
Pamoja na mapungufu yake. Kwa hili Rais ameliezea vizuri na kwa kweli maudhui ya sheria yakifuatwa vizuri yatatatua mambo mengi sana...

Kwangu mimi ninayeamini mifumo zaidi ya kubwatuka maneno nadhani ... hili ni miongoni mwa yale ambayo atatakiwa kujivunia kwenye utawala wake.
 
Ili Matatizo ya Rushwa na Ufisadi yaishe ni lazima Rais wa nchi apatikane bila kuwa na rushwa au ahadi za kulipa fadhila pindi akishinda. Yaani Rais asipatikane ki-mtandao wa uhalifu wa uchumi kama huyu wa sasa. Huyu atakuwa na guts za kusema bila haya wala woga lakini huyu wa sasa hakupatikana hivyo, japo anatupotezea muda watanzania kimaendeleo ila tumwache amalize muda wake huenda atakuwa amajifunza na kusaidia ajaye apatikane nje ya mfumo aliopatia yeye. Akilifanya hilo atakuwa amelisaidia Taifa zaidi ya vipindi vyake vyote viwili kuchecheka tu Pale IKULU. Hivi sasa yeye asijiingize kwenye dili na kashfa kama aliemtangulia ili asiwe na mawazo ya kulindwa na ajaye ambapo itapelekea kuwa na pre-conceived preference ya walewale waliomuingiza madarakani ili Mtandao wa Uhalifu wa kuididimiza nchi uendelee.
 
Inamaana hakuna mtu aliyepelekwa mahakamani kwa sababu ya EPA ? BOT ? hakuna watu waliojiuzuru kwa ajili ya Richmond/Dowans ?

Katika mambo yote hujawahi kuona mafanikio ya serikali ya sasa ? Tanzania ni nchi inayokuwa kwa kasi sana kiuchumi afrika ya mashariki ukiacha rwanda

Kuna kilichojificha hapo?
 
mambo hayo kawaambie watoto wa darasa la 3 ...usitake kutia watu hasira hapa.
 
Back
Top Bottom