Hotuba ya JK kuuaga mwaka; msitarajie mabadiliko! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hotuba ya JK kuuaga mwaka; msitarajie mabadiliko!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Dec 31, 2009.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Dec 31, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Katika hotuba yake ya kuuaga mwaka huu na kuukaribisha mwaka mpya Rais Kikwete anatarajiwa kutuambia mafanikio ya utawala wake na kujaribu kutuliza hofu yoyote kuelekea uchaguzi mkuu. Hotuba yake hiyo itakuwa ni ya kuhalalisha mambo mbalimbali na wakati huo huo itakaa kikampenikampeni.

  Mambo ambayo hatuwezi kutarajia ni Rais Kikwete kusafisha Benki Kuu; baada ya kushindwa kufanya hivyo wakati wa Gavana Ballali na hata baada yake ni wazi kuwa ufisafi mkubwa utaendelea kufanyika kwenye Benki hiyo kwani nadharia inayomuongoza Rais Kikwete na uongozi wake ni kuwa tatizo la Benki Kuu ni "watu". Hivyo, wataendelea kubadilisha watu na kulaumu watu wakati tatizo hasa ni la mfumo.

  Hivyo, tusitarajie mabadiliko yoyote kwenye taasisi hiyo nyeti na habari za matumizi haya kama ilivyokuwa suala la EPA litapokolewa na Rais Kikwete kwa "mshtuko" huku akitarajiwa kuagiza "uchunguzi" kufanyika.

  Lakini kubwa zaidi katika hotuba yake hiyo Rais Kikwete atazungumza katika kujitengenezea nafasi ya kugombea tena huku akiahidi mambo ambayo ni wazi hawezi kuyatekeleza ndani ya mwaka huu mmoja uliobakia. Hivyo, atatumia nafasi hii kuhalalisha nia yake ya kugombea tena.


  Ninachosema ni kuwa kwa vile tayari tumeshaelewa kuwa Rais Kikwete hawezi kusimamia mabadiliko ya mfumo uliomuingiza madarakani, uliomsimamia na kumsimamisha na ambao bila ya shaka sana waweza kumrudisha madarakani ni bora tuanze kujiuliza kama katika akili zetu timamu tuna sababu yoyote ya kutarajia mabadiliko.

  Vinginevyo, hotuba hii kama zile nyingine itajaa manung'uniko, maelezo ya kila tunachokijua, mipango na "nia" ya kufanya x,y' itakuwa ni hotuba ambayo watakoifurahia zaidi ni wale wenye kunufaika moja kwa moja na utawala huu.

  Kwa maoni yangu, tumshukuru Rais Kikwete kwa kutuonesha kiongozi ajaye wa Tanzania asiweje, na asituahidi nini; tumshukuru kwa kutuonesha kuwa uongozi wa kweli si maneno matamu na matabasamu yenye hamu; kwamba uongozi wa kweli ni ule wenye kuthubutu kutenda yale yaliyo juu na zaidi ya yanayotarajiwa.

  Ninamshukuru Mungu kwa uongozi wa Rais Kikwete kwa muhula wake huu mmoja. Na kama nilivyosema mahali pengine, ni matumaini yangu atafikia ule uamuzi ambao tunautarajia kuwa hatasimama kama mgombea kwa tiketi ya CCM mwaka huu ujao.

  Natumaini naye kama Rais Mkapa na Mwinyi atakuwa tayari kula pensheni yake ya Urais na kufurahia maisha ya kustaafu.

  Heri ya Mwaka Mpya!
   
 2. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #2
  Dec 31, 2009
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,504
  Likes Received: 2,744
  Trophy Points: 280
  Atazungumza kitu ambacho waTZ wanataka kusikia.
   
 3. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #3
  Dec 31, 2009
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 221
  Trophy Points: 160
  Mimi binafsi sintakuwa na muda wa kusikuliza hotuba yake na nilishaacha siku nyingi tu, sababu hakuna jipya atakalonimbia leo. Majibu ya maswala muhimu tunayotaka kujua hatma yake mkuu wetu wa kaya anayapaka mafuta badala ya kuyatolea ufumbuzi.
   
 4. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #4
  Dec 31, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Ataanza na ndugu zangu watanzania....... halafu kitakachoendelea kitasababisha nizime tv yangu kwani hakutakuwa na mpya kama ulivyosema MM.

  Nitasoma hotuba yek gazetini kesho leo sina muda wala mood ya kumsikiliza
   
 5. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #5
  Dec 31, 2009
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,504
  Likes Received: 2,744
  Trophy Points: 280
  Atatumia muda mwingi kuzungumzia Msiba wa Taifa!!!
   
 6. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #6
  Dec 31, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,576
  Likes Received: 18,546
  Trophy Points: 280
  Hata Ningekuwa mimi JK, of course I can't promise anything in times of such destitutes. JK is a human being too, please give him a break! Msiba, Mafuriko, moshi unaomfukia CCM, forces za kumtetea akiwemo Mrema na Mnajimu bado tuu tunamsakama?.

  Watanzania huungana wakati wa shida na raha, naomba tuungane nae kipindi hiki cha msiba wa taifa na majanga kwa kumfariji badala ya kuendelea kumlima, yatapita na kazi iendelee mpaka October 2010.
   
 7. tovuti

  tovuti Senior Member

  #7
  Dec 31, 2009
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 160
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kawawa kafa, kishapata sababu, atajifanya ana majonzi makubwa, anashindwa kuhutubia
   
 8. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #8
  Dec 31, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,576
  Likes Received: 18,546
  Trophy Points: 280
  .
  Kama hutasikiliza, hutajua anasmaanisha nini, bali unawategemea zaidi waandishi wanaokusikiliza na kuandika walivyoelewa wao.
  Kwa kusikiliza huku unaona, unaweza kupima yafuatayo
  - genuinity kama anayosema ni genuine ama anajisemea tuu ili mradi kusema.
  - sincerity, kama anayosema yametoka moyoni kweli.
  -originality, kama anayosema ni ya kwake ama kaandikiwa na yeye anakuja kuyakasuku tuu.
  -humility, utaona kama kweli ameguswa ana anakuja kufuniuka kombe tuu.
  -Tuna Msiba wa Taifa, is he touched ama ni kutimiza wajibu tuu,
  - firmness-utaweza jua kama he mean what he says, or just uters words by his mouth
  -strength, kama ni imara kweli, ama anazungumza with fire in his eyes and the the fear is his weapon in his heart ili kubeg symphathy ya Watanzania.

  hayo na mengine mengi utaweza kuyaona wewe kwa kumtazama na kumsikiliza, hakuna mwandishi wowote wa kukuandikia.
   
 9. R

  Ronaldinho Member

  #9
  Dec 31, 2009
  Joined: Aug 7, 2009
  Messages: 69
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Presidents failures can not be separated from his advicers,jamaa mara kadha wa kadha amekuwa akizungumzia mambo ya kiuchumi,siasa na jamii kama mtu asiyefikiri kwa umakini,siwezi mtupia yeye tu lawama,wanafanya nini wasaidizi wake?for all those years hawajaona kuwa jamaa anastahili mabadiliko?honestly more than msiba wa kawaa,mafuriko,mahuzuniko..sitegemei jipya toka kwake
   
 10. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #10
  Dec 31, 2009
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  well, true .......... but these advisers are a reflection of what person the president is.
   
 11. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #11
  Dec 31, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Hakutakuwa na jipya zaidi ya kampeni na salamu za pole kwa Babu yangu Kawawa maana hatakuwa na majibu ya msingi yanayolikabili taifa kwa sasa
   
 12. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #12
  Dec 31, 2009
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Nakubaliana na wewe na kwa jinsi alivyo msanii kwenye hotuba hiyo atasanii ile mbaya.
   
 13. Kubwajinga

  Kubwajinga JF-Expert Member

  #13
  Dec 31, 2009
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,190
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Hotuba ya JK ya kuaga mwaka ingefaa akaitoa akiwa USA alikoishi na kufanya kazi kwa muda mwingi katika mwaka huu.

  Binafsi ningefurahi sana kama angemalizia hotuba yake kwa kusema;
  "Ndugu wananchi, kazi mliyonituma imenishinda kwa hiyo naomba nijiuzulu"
   
Loading...