Hotuba ya January Makamba kuadhimisha uhuru wa Tanganyika (Tanzania Bara kama alivyosema)

ICHONDI

JF-Expert Member
Dec 3, 2008
595
250
Nikiwa mmoja wa wale walioisikiliza hotuba ya mheshimiwa huyu kupitia blog mbalimbali kama za michuzi na vijimambo ninaomba kutoa maoni yangu machache
1. Mheshimiwa January Makamba alianza kwa kuonyesha kuwa ana uchungu sana wa gharama za kusafiri kuja nchini Marekani kwa tukio moja ambalo yeye alialikwa. Alipopata mualiko wa wana DMV, akapat asababu ya pili ya kuja nchini Marekani. Jambo ambalo limenigusa kwenye hili ni kuwa kwa ziara kama hii, mheshimwa huyu amekuja kwa gharama ya serekali au ya kwake mwenyewe au kwa wale waliomualika? Mimi ninaona hii ni ziara ya binafsi zaidi na sioni ni kwa jinsi gani inatakiwa kulipiwa na walipa kodi wa Tanzania. Kabla sijamhukumu January, ninegfurahi kujua ni nani amelipa gharama za ziara hii. Kama serekali ndio imelipia ziara hii, huu ni ufisadi na bila hiyana nasema January Makamba ni fisadi na madai yake kuwa anaona huruma kutumia gharama kuja kwa tukio moja ni ya kinafiki. Najua January ni member huku, namuomba aje hapa atuambie ni nani alilipia ziara yake hii

2. Mheshimiwa ameongea vizuri sana kuhusu maudhui ya uhuru na malengo yake. Amegusia waasisi wetu walifanya nini na vision yao kwa taifa hili ilikuwa nini. Ameongelea jinsi walivyojitahidi kujenga umoja, demekorasia na kupendana. Mheshimiwa huyu hakuzungumza lolote kama misingi hiyo imevurugwa au imeendelezwa na watawala wa chama chake. Hakuzungumzia mikakati ya chama chake akiwemo yeye mwenyewe ya kuua upinzani na kama hiyo ndio vision ya waasisi wetu kujenga utawala bora na demokrasia.


3. Lakini hata baada ya kuchambua vizuri malengo ya uhuru, mheshimwa huyu hakusema kama hatua tuliyofikia kama taifa kwa miaka 52 ya uhuru ni hatua ya kasi iliyo sawa, na kama mmoja wa viongozi walopo madarakani ni juhudi gani za makusudi zinafanywa na serekali na chama chake kufikia malengo ya uhuru kwa kasi zaidi

4. Kuna madai kuwa utawala wa Jakay aKikwete umerudisha nyuma taifa hili badala ya kwenda mbele. Sina uhakika sana na madai hayo kwa kuwa sijaona statistics, lakini kama ni kweli ,je mheshimiwa haoni kuwa madai yake kuwa kila utawala mpya umeendeleza kuyapatia ufumbuzi malengo ya uhuru? Kwa waliorudisha nyuma wawekwe kundi gani?


5. Mheshimwa January aliongelea mambo matatu ambayo yatashape future ya taifa la Taanzania. Ameongelea demographic, mapinduzi ya mawasiliano na kukua kwa tofauti ya kipato cha wenye nacho na wasio kuwa nacho. Nimependa uchambuzi wake huu, lakini kama kiongozi anayetawala sasa hakutoa majibu ya nini kifanyike sasa. Ameongelea takwimu zilizopo sasa na kuwa hizo ndio zitashape future ya Tanzanai in 50 years to come. Je si kuwa hizo data ni sasa na solution yake ni sasa, kwa mfano amasema rika la watu chini ya miaka 35 kuwa ni karibu asilimia 80 na kuwa kuna shida ya ajira kwa vyuo kuzalisha watu laki 8 wakati ajira ni elfu harobaini tu, ni tatizo kubwa ambalo litashape nchi hii. Mimi nadhani hilo tatizo ni la sasa, hivyo kusema kuwa viongozi wajao inabidi kulipatia ufumbuzi tatizo hilo ni kukosa umakini na weledui wa uongozi kwa kuwa solution yake ilitakiwa ianze miaka 20 iliyopita.

6. Kwa mheshimwa makamba, uwingi wa line za simu ndio kipimo cha kukua kwa mawasiliano. Kwa njia moja yuko sahihi, lakini ni kwa jinsi gani kama taifa linatap ukuaji huo ili kuimarisha uchumi. Kutoza kodi line za simu sio muafaka kwa kuwa ndio bado vuguvugu hili linapamba moto. Mawasiliano si blog tu na simu tu, ningemuelewa kama angeliongelea jinsi y akupanua uchumi kutokana na mapinduzi ya mawasiliano.
Kimsingi hotuba yake ilijaa matatizo zaidi ya majawabu. Kuorodhesha mlolongo wa matatizo na changamoto imekuwa ndio talking points za viongozi tulionao sasa Tanzania. Nimeamini kuwa ni mheshimwa huyu ambaye alikuwa anamuandikia mkuu wa nchi hotuba, kwa kuorodhesha malalamiko na kutoa majawabu mepesi yasiyo halisi. Kwa mfano sakata la EAC ni moja ya viashria tosha jinsi viongozi wetu wako makini kulalamika tu, badala ya kutafuta suluhisho. Kulikuwa na ugumu upi kwa JK kumpigia simu Kenyatta na Yoweri au Kagame na kuwaambia kile anachokiona, badala ya kutoa lawama na malalamiko bungeni?
Kimsingi nimekuwa disspaointed na hotuba ya January, lakini pia sikushangazwa kwa kuwa sikuwa na matarajio makubwa.
Kuna haja ya viongozi wetu kutumia mianya ya kuimarika kwa mawasiliano kuwasaidia watanzania kubadili fikra. Hotuba aliyoitoa makamba haikuizingatia audience, kuwa audience ile imesheheni watu wenye upeo mpana na wanaojua wajibu wa serekali na watawala. Ile ni hotuba inayofaa kuitoa kwenye mikutano ya ndani kwa viongozi wa CCM kwa kuwa haikuwa na jambo jipya, na haikutoa vision yake yeye binafsi kama kiongozi au serekali na chama anachokiwakilisha katika kumkomboa mtanzania ili afaidi matunda ya uhuru
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom